Tanzania ni nchi ambayo raia wake hawana shida wala taabu yoyote.

Mimi sitetei lakini Watanzania wana akili!! Serikali haiwezi kulalamikiwa kwenye swala la mafuta kwasababu hizi bei ni za kimataifa na hata sisi hapa USA bei inapanda!!. Vita vya Libya vinachangia kwa kiasi kikubwa sana na viongozi wa Africa wanatakiwa kumpa offer Ghadaffi aondoke.
vipi bei ya sukari kupanda inasababishwa na nani mfano kiwanda kiko kagera lakini sukari inauzwa tzs 2200 lakini kutoka kwenye kiwanda mpaka eneo lingine ni km 600 halafu sukari inauzwa tzs 2000...
 
Mimi sitetei lakini Watanzania wana akili!! Serikali haiwezi kulalamikiwa kwenye swala la mafuta kwasababu hizi bei ni za kimataifa na hata sisi hapa USA bei inapanda!!. Vita vya Libya vinachangia kwa kiasi kikubwa sana na viongozi wa Africa wanatakiwa kumpa offer Ghadaffi aondoke.

Heshima mbele mkuu! Kama akili ya watanzania ni kukaa kimya huku wakinyanyasika hiyo akili nadhani yafaa kukarabatiwa haraka mnooo. Kinacho takiwa ni kupaa kutetea haki bila woga wowote maana ni haki ya kila mtanzania kutumia rasilimali zetu kupata maisha ya neema na rehema. Guys... where are we!!!
 
vipi bei ya sukari kupanda inasababishwa na nani mfano kiwanda kiko kagera lakini sukari inauzwa tzs 2200 lakini kutoka kwenye kiwanda mpaka eneo lingine ni km 600 halafu sukari inauzwa tzs 2000...[/QUOT

Ha ha ha!!! Probably Pinda has answers for this!
 
Juzi tumeona majirani zetu wa Kenya na Uganda wakiandamana kupinga mfumuko wa bei, kupanda kwa bei ya mafuta na ugumu wa maisha kwa ujumla.
Tanzania tumekaa kimya, mafuta yanapanda bei kila uchao, umeme nao unapanda bila kuchoka. Vyakula havikamatiki kwa jinsi vilivyo panda bei.
Je haya nayaona kauzu mimi tu au hata nyie wenzangu mnaona?
Kwanini tusiandamane kuonyesha uchungu wetu?
Vigogo kwao maisha mazuri viyoyozi hadi kwenye mabanda ya mbwa wao.

mi napenda sana mfumko wa bei na maisha kupanda bei viendelee tena geometric wise na sio arithmetic wise. kwani sisi watz tumekuwa mno waoga wa mabadiliko. ccm oye....maisha bora kwa kila mtz
 
Mimi sitetei lakini Watanzania wana akili!! Serikali haiwezi kulalamikiwa kwenye swala la mafuta kwasababu hizi bei ni za kimataifa na hata sisi hapa USA bei inapanda!!. Vita vya Libya vinachangia kwa kiasi kikubwa sana na viongozi wa Africa wanatakiwa kumpa offer Ghadaffi aondoke.

Mbona Kenya wameandamana serikali imeshusha bei ya mafuta?
 
juzi tumeona majirani zetu wa kenya na uganda wakiandamana kupinga mfumuko wa bei, kupanda kwa bei ya mafuta na ugumu wa maisha kwa ujumla.
Tanzania tumekaa kimya, mafuta yanapanda bei kila uchao, umeme nao unapanda bila kuchoka. Vyakula havikamatiki kwa jinsi vilivyo panda bei.
Je haya nayaona kauzu mimi tu au hata nyie wenzangu mnaona?
Kwanini tusiandamane kuonyesha uchungu wetu?
Vigogo kwao maisha mazuri viyoyozi hadi kwenye mabanda ya mbwa wao.

kila mbuz atakula kwa urefu wa kamba yake:mkulo
 
Ooooh hata hutu USA bei zimepanda!! nani kakuuliza habari za USA sisi tunajadili mambo ya TZ bwana usituchanganye na ulimbukeni wako wa USA,achana na sisi kabisa usharo baro wako peleka uso kitabu,huko utakutana na wenzio JF ni sehemu ya watu wenye misimamo,SEE ya.
 
Mkuu mwanzisha mada katoa mfaono wa nchi zingine mbona hujapinga?
Inaonyesha una hasira sana na ndg wa USA, nadhani umejaa wivu na chuki tu.
Lazima ukubali maoni ya wengine, usidhani kuponda tu kila kitu ndo umetatua. Utajijaza upepo tu! Try to think beyond your emotions, it will help u.
 
Ukitaka kuwatawala watu kiulaini wanyime ELIMU na vyanzo muhimu vya habari,yaani SOURCE OF INFORMATION.
Katika East Africa sisi Tanzania ndo tunaonekana wengi wetu hatujaenda shule,hakuna kisomo,wengi ni waloishia std 7,f4 za kata na f6 chache za serikali lakini they didn't make to University.

Kwa mtaji huu wa kutokuwa na shule ya kutosha wengi wa Wa-TZ hawana mtazamo wa kiundani wa namna ya kuchambua maswala mbalimbali ya KISIASA,KIUCHUMI na KIJAMII. Ndo maana linalotokea kwa WA-TZ ni twende tu(22kms),huku wakibembelezwa na vibwagizo,ngonjera na longolongo za Chama Cha Magamba/Majambazi kuwa ni nchi ya utulivu,amani,upendo na mshikamano.

Kuna mwandishi mmoja kwenye gazeti la The East African wiki iliyopita alisema kuwa haya maandamano ya KUPINGA KUPANDA KWA BEI ZA MAFUTA NA VYAKULA YATAIKUMBA E.A yote. Lakini mimi nikasema kwa TZ si rahisi. Kwa wenzetu Uganda na Kenya,they can,but not for the poor Tanzanians!

Hii nchi yetu ni nchi ya watu waliokata tamaa. Jaribu kufikiria tu matukio kama ya BABU WA LOLIONDO. Kuwa nchi nzima kuanzia Rais,Mawaziri,M/Katibu wakuu,Wakuu wa (M)/(W) kuacha kushughulikia mambo ya msingi ni kukimbilia kwenda kunywa kikombe cha Babu. Kwangu mimi this is a shame to all Tanzanians. Yaani sote tunaonekana mazezeta kuanzia Rais mpaka mwana kijiji wa mwisho kabisa kule kijijini ambaye hajui a,be wala che.

Unategemea nini kwa watu waliokunywa mvinyo wa Babu? Kuwa waandamane eti kupinga Kupanda kwa Gharama za Maisha kwa maana ya Bei za Mafuta ya mitambo,umeme na Chakula kuwa bei juu? Sahau!
 
Watanzania tuna kipaji cha kuongea sanaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!

no action

Nakumbuka wakti fulani nilikuwa na rafiki zangu wa Kikurya kule Sirari kwenye mpaka kati ya Kenya na Tanzania. Tulikuwa tunaingia upande wa Kenya kuchukua au kupeleka bidhaa fulani fulani kwa kuzivusha na kuziuza upande wa Tanzo kama wao wanavyotamka.

Sasa wakti mwingine ilikuwa inatokea kukamatwa na askari wa Kenya. Hawa jamaa yaani Polisi Kenya walikuwa na principle moja kuwa,UKIMKAMATA MTANZANIA USIMSIKILIZE MAANA ANA KISWAHILI MREEFU. Ukimsikiliza tu basi utamwachia kwasababu ataongea uongo mwingi na hongo au rushwa itatembea hadi umwachie.

Ndivyo tulivyo Wa-tz wengi wakiwemo wana-siasa wetu. Porojo nyingi utekelezaji 0 pc.

Bado kazi ipo.
 
Back
Top Bottom