dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Salaam Wakuu,
UKEKETAJI NI NINI?
Ukeketaji ni ukataji wa sehemu za siri za mwanamke. Ukataji huo unahusisha maeneo nyeti. Au ni kitendo chochote kinachojeruhi uke kutokana na sababu ambazo sio za kimatibabu.
Ukeketaji unaumiza wanawake na wasichana kimaungo na kiakili na hakuna faida yoyote ya kitabibu wakati wa kitendo hicho.
Historia ya ukeketaji imeendelea kuwepo kwa takribani karne 21 sasa. Serikali na Taasisi mbalimbali zinajitahidi kuhakikisha zinatokomeza ukeketaji nchini.
UKEKETAJI UNASABABISHWA NA NINI?
i). Kichocheo kikuu cha vitendo vya ukeketaji hapa nchini ni mila na desturi za baadhi ya makabila katika jamii za kumvusha rika mtoto wa kike kutoka usichana na kuwa mwanamke kamili.
ii). Jamii inayokeketa huamini kuwa msichana aliyekeketwa anakuwa tayari kuolewa, sababu hii imepelekea ongezeko la mimba na ndoa za utotoni.
iii). Sababu nyingine ni mila ya kutambika ikiwa pamoja na kutii masharti ya mizimu ya baadhi ya jamii kuamini kuwa ukeketaji huondoa mikosi katika familia.
iv). Vilevile, zipo sababu za kiuchumi ambapo ngariba na wazee wa mila hulipwa fedha au vitu ili kutimiza azma hiyo. Kadhalika, wazazi wa watoto wanaokeketwa huwa na matarajio ya kuwaoza mabinti zao kwa lengo la kupata kipato kupitia mahari inayotolewa.
UKEKETAJI UNA MADHARA GANI?
i). Ukeketaji una madhara makubwa kwa wanawake na watoto wa kike ikiwa ni pamoja na athari za kisaikolojia kama msongo wa mawazo kwani vitendo hivyo hufanywa bila ridhaa ya wahusika.
ii). Madhara ya kiafya yanayoweza kueandana na kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua na baadhi yao kupelekea kupoteza maisha.
iii). Madhara mengine ya kiafya ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa na Virusi vya UKIMWI ikiwa vifaa vinavyotumika kukeketa havitatakaswa vyema.
iv). Madhara mengine ya ukeketaji ni pamoja na maumivu makali wakati wa ukeketaji kwa kuwa hakuna utaalamu unaotumika kupunguza maumivu wakati wa zoezi lote la ukeketaji.
v). Aidha, ukeketaji unaweza kusababisha ugonjwa wa fistula yaani kutokwa na haja ndogo bila kujizuia mara baada ya kujifungua.
Mikoa yenye viwango vikubwa vya ukeketaji ikijumuisha Mikoa ya Manyara (58%), Dodoma (47%), Arusha (41%), Mara (32%) na Singida (31%); hii ni kwa mujibu wa Utafiti wa Kidemografia na Afya Tanzania (Tanzania Demographic and Health Survey) wa mwaka 2015/16.
Bado kuna uwekezaji mdogo katika kukomesha Ukeketaji na ulinzi na usalama wa wanawake, matokeo yake kiwango cha ukatili na ukeketaji vinaendelea kuongezeka.
Ukeketaji bado ni changamoto kubwa katika jamii zinazokeketa. Kwa mujibu wa Utafiti wa Kidemografia na Afya Tanzania (Tanzania Demographic and Health Survey) wa mwaka 2015/16 ulibaini kuwa, mwanamke 1 kati ya 10 hapa nchini Tanzania amekeketwa.
Aidha, utafiti huo pia ulibaini kuwa kiwango cha ukeketaji kwa wanawake na watoto kinaongezeka kulingana na umri. Asilimia 19 ya wanawake wenye umri wa miaka kati ya 45 hadi 49 walikuwa wamekeketwa ukilinganisha na asilimia 5 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19.
Vile vile, utafiti huo ulibainisha kuwa wanawake wenye elimu ya sekondari wana uelewa mkubwa zaidi kuhusu athari za ukatili kwa asilimia 97 ukilinganisha na wanawake ambao hawakufikia ngazi ya elimu ya sekondari kwa asilimia 71.
Taarifa hiyo imeeleza pia kuwa wasichana wanaozaliwa au kulelewa na mama aliyekeketwa nao pia hukeketwa.
Taarifa hiyo ilibainisha pia kuwa asilimia 86 ya wanawake waliokeketwa hawakubaliani na kitendo hicho na wanatamani kisiwepo kabisa.
Chanzo cha Takwimu: UNFPA