Tanzania isitishe uhusiano wa Kibalozi na Utawala dhalimu wa Muammar al-Gaddafi

Sasa hivi hakuna ujasiri tena wa kimsimamo. Mtindo uliopo sasa nikuvizia kusubiri tamko la AU na sisi tujichomeke humohumo. Hakukuwa na lolote kwa Ivory Coast wala Madagaska mpaka ulipotolewa msimamo wa AU ndiyo unamuona Membe anaibuka nalo. We exist without loci Tumekuwa bendera fuata upepo.
 
Jamani, Tanzania hatuna tena sauti ya kutetea wanaokandamizwa? Yaani tumepoteza kabisa hata msimamo wetu wa "kila binadamu anastahili haki ya kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake"?

Leo hii Botswana ndio wanaongoza na sitoshangaa Namibia watafuatia wakati sisi viongozi wetu wanacheka cheka na huyu kichaa wa Libya. Of course I know serikali yetu haina uwezo au ujasiri huo hasa baada ya kupokea favors nyingi toka kwa Gaddafi lakini kweli tumeuza na utu wetu kwa sababu kuombaomba kwa viongozi wetu?


aibu na fedheha!!

Huna hoja!
 
Kaka; huyo jamaa kwa baadhi yetu ni kama nabii. Kumzungumzia kwa suala hilo unagusa moja kwa moja imani za watu. Unajua aliyoyafanya nchi hii? Alivyojenga majumba ya ibada na mamisaada kibao kwa kutazamana kwanza usoni? Nachelea usijeambiwa mdini wewe; jiandae kupambana na hoja za aina hiyo.

Nchini kwake kafanya makubwa lakini mafisi wanangoja mkono udondoke. Na hao wananchi wapuuzi wanaokimbilia visima vya mafuta kwa niaba ya mabwana zao ni vyema wateketezwe kabisa. Mungu anapenda watetezi wa haki. Dunia ya sasa mwenye haki ni mwenye madaraka, nguvu za uchumi, mwenye kauli. Gaddafi anavyo na atapambana na kuwashinda wapuuzi nchi za magharibi na vibaraka wao zenye uchu wa nchi iliyojengwa kwa damu. VIVA GADAFI

Sisi tunakufa kidogo kidogo kwa kuwaendekeza mafisadi. Watakapoamka wananchi na kuwachinja mafisadi kelele zitapigwa bado. SULUHU HAIJI BALI KWA NCHA YA UPANGA. VIVA MAPINDUZI YA KULINDA HAKI NA MASLAHI YA WATU NA NCHI ZAO.
 
Ghaddafi ndiye mfadhili wao wa chaguzi za kidhalimu hapa tz, wana ubavu wa kumlaani?
 
Mwkjj udhalimu wa gadafi ni upi? ungeanza na chanzo cha mgogoro kisha ukamakizia na hayo madai yako.
Kinacho tokea libya si sawa na kilichojiri misri na tunisia kuna kitu nyuma yake, kitu kilichotengenezwa na wababe ambacho kimekutia upofu wewe mimi na yule tuamini wanavyotaka wao.
Matokeo ya vurugu yanayo jiri sasa si ukaidi wa gadafi bali damu ile ni sababu ya wanaotaka dunia iwe wanavyotaka wao.
Niaibu kubwa kwa watu kulaumu utawala wa gadafi kwa kigezo cha so called demokrasia ya magharibi na kufumbia mazuri yote aliyofanyia nchi yake na afrika kwa ujumla ukizingatia nchi ngapi za afrika zenye demokrasi na hamna lolote.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Nadhani tungewapisha walibya waje Tanzania chini ya utawala tuliokuwa nao na sie tuende kwa Gaddafi, nchi ambayo watu hawalipii umeme, maji wala matibabu mshahara kima cha chini dola mia tano!Ukioa unapewa allowance ya kuanzia maisha, wasio kuwa na ajira wanapewa allowances.

Wale wanaoipinga serikali wana lao "mafuta" na hili linajulikana! Ningeichukulia kauli yako ni ombwe ingelikuwa unazungumzia balozi za nchi vamizi mashariki ya kati leo miaka mingapi wanaendelea kuuwa wakina mama na watoto wasiokuwa na hatia?

Tafakari mkuu..........................
 
yaani kwa vile kaleta misaada ambayo sasa inaonekana imejaa damu ndio baadhi ya watu wanasema tumkumbatie tu? Utumwa gani huu wa kifikra ambao tunao sasa? Wanajeshi wake wanakimbia na ndege kukataa kuwalipua wananchi wao hapa watu wanasema "tuoneshe udhalimu wa Ghadaffi" Utii au upendo wa aina gani huu?

Mzee Mwanakijiji, 'penye uzia, penyeza rupia'. Gadaffi kapenyeza rupia kila kona ya Afrika, kuanzia AU mpaka nchi moja moja. Sisi Tanzania, ametujengea U-Dom!, ametutolea fedha za kampeni ya chama chetu!, anaifadhili first family kwa hili na lile!, ametuzawadiwa zile benzi nyeusi S-Class 100 pale Tamesa!, ndizo zinazowabeba waheshimiwa wetu wote!. Amejenga misikiti lukuki ya kisasa!. anatupa misaada ya mifweza kibao, kila tunapoomba!. Mtu mwenye wema kama huu, tukimshutumu itakuwa ni ukosefu wa shukrani, au ukosefu wa fadhila ambao nao ni dhambi.

Kama watu wa Libya wanapata huduma za afya bure!.elimu ya bure mpaka chuo kikuu!, hakuna kulipa kodi yoyote!, raia wake wanalipwa mishahara kila mwezi hata wasio na kazi!. Sasa watu kama hawa, wanaandamana kwa nini?.

Tanzania inaungana na Ghadafi kuwalaani waandamani ambao kwa mujibu wa mtoto wa Ghadafi, ni wabwia unga, waliopewa fedha na nchi za Magharibi ili waandamane.

Kama Walibya pamoja na raha zote hizo bado wanaandamana, jee sisi Watanzania, pamoja na shida zote hizi zinazosababishwa na CCM, tutapata wapi audacity ya kumlaani Ghadafi!.

Tuungane tumuombee kwake kutulie, after all ni shemeji yetu kwa yule ma-mdogo wetu aliyempora Komandoo!.

Sisi ni watu wa shukrani, Long Live Ghadafi!, Long live Partnership na Tanzania kwa maendeleo ya taifa na kuongeza idadi ya nyumba za ibada tena mpaka zifikie hadhi ya Taj Mahal!.
 
Mkuu unaweza kutetea wanaokandamizwa bila kuvunja diplomatic relations. Mimi nadhani uhusiano wetu wa kibalozi uko na wananchi wa Libya not individuals. If not, then it should be so. La muhimu hapa ni kwa serikali yetu kutujuza hali ya Watanzania walioko huko Libya and what is being done to evacuate them. Thats is the most important thing we want to know.

Whether or not Tanzania kusitisha diplomatic relations with Libya haitasaidia. In fact, ita affect hata Watanzania ambao bado wapo huko. So far hakuna taifa kubwa ambalo limevunja uhusiano wa kibalozi na Libya probably for those reasons.

Nakubali serikali yetu haina uwezo au ujasiri huo hasa baada ya kupokea favors nyingi toka kwa Gaddafi, but why they did not do so in relation to Egypt?
Tanzania hatuna ofisi za ubalozi wetu nchini Libya!.
 
tusitishe pia na marekani,si wanaua huko Iraq na Afhanistan kwa kisingizio cha ugaidi kumbe wana shida na mafuta,tuna uhakika gani sicho wanachokitaka huko Libya kwa visingizio vya kijinga,au hao huko Iraq na Afhanistan si binadamu,wa Libya ndo binadamu?

Colleague,

You be right or not!

Wewe ulichokiona ni Wa-Marekani kuchukua mafuta sehemu hizo. Lakini kwa upande mwingine wa shilingi-sio haki Gaddafi kutawala Libya miaka yote hiyo lakini pia sio haki kujiesabia urais wa milele na kuandaa kupokezana urais huo kifamilia ktk nchi kama Libya. Policies za utawala wa Libya zimeonekana kusambaa hata East Africa, mfano Uganda. Pia kunammoja wetu ktk thread hii ameogopa asiitwe mdini but the fact is ...Gaddafi amejenga misikiti mingi hapa Tanzania kwa malengo anayoyajua yeye na wanaomkaribisha kufanya hivyo.

Tanzania ina historia ya kukemea udharimu na zaidi haki za binadamu zinapokiukwa. Kama hatuwezikufanya hivyo sasa ni dhairi ujasiri na utanzania wetu umepotea mikononi mwa serikali iliyopo madarakani.
 
Kwa nini hatukuanza na marekani na uingereza pale walipovamia irak bila ridhaa ya baraza kuu la umoja wa kimataaifa? Au tunataka tuwasaidie wapate tena nafasi ya kupeleka majesh yao na kuchota mafuta kama irak?
 
Viongozi wetu ni dhalimu kuliko Gadafi. Kama pamoja na ushahidi uliowazi kuhusu wizi wa dowans bado wanashinikiza kumlipa, Gadafi anakuwa kama malaika nikimlinganisha na hawa wa kwetu!
nimeipenda hii mkuu ni kweli kabisaa
 
Nadhani Mkuu Mwanakijiji upo sawa kwa hili, nahisi si Tanzania tu, hata mataifa na jumuiya za kimataifa nazo zimepoteza ile dhana ya kuilinda dunia na watu na majanga ya vita na dhulma kama ilivyokubaliwa katika UN charter ya mwaka 1945, nchini Marekani.

Mataifa mengi yanayojilabu na utawala bora na haki za binaadamu,ikiwamo Tanzania yamesaini mkataba huu, pamoja na maazimio mengine ya UN, ya kulinda uhuru na haki ya kuishi ya raia.

Bahati mbaya mengi ya mataifa hao ni wavunjaji wakubwa wa mikataba ya umoja wa mataifa ya kulinda haki na uhuru wa watu kuishi. Kuna binaadamu wanakufa bure bila ya sababu katika ukanda wa Gaza, wacha Tanzania hata hayo mataifa yanayouona uhuni wa Ghaddafi leo, hawayaoni hayo ya Gaza ua wanajipofua makusudi kujifanya hawaoni. Kuna watu wanakufa kule Afghanistan, hakuna anayesema uhuni.

Kuna watu walikufa hapa hapa Tanzania, tena waliuliwa na dola (Mauwaji ya Januari 26/27/2001 Pemba), hakuna jumuiya ya kimataifa iliyotoa walau onyo kwa Tanzania, na Tanzani yenyewe haijawachukulia hatua walifanya unyama ule mpaka leo, wala hakuna aliyewajibika kwa khiari yake.....Leo Ghaddafi ndo mbaya?????
 
Vilevile Tanzania isiste pia kusitisha uhusiano wake na mataifa ya Magharibi!! Hivi uovu wa Gaddaf na ule wa mataifa ya Magaribi ni upi una nafuu kwa Afrika...? Je mbona pia hatujasitisha uhusiano wetu na Cuba toka enzi zile? sidhani kama ni vema kwa taifa lolote linalojitawala kuimbishwa nyimbo tusizozitambua... mwisho wa siku ni aibu kwa vizazi vijavo... tutahukumiwa kwa akili zetu! Naomba nisiwe miongoni mwa waimbao nyimbo zinazoimbwa na wengine bila kujulikana! (mpaka leo silaha za sumu hazijapatikana Iraq na raia kule wanaendelea kuuawa! Mpaka leo Libya watu wanaandamana kwa amani huku wakibeba bunduki na kutaka kuing'oa serikali wasiyoitaka.... Sipendi na sitaki kufananisha bundi na njiwa!
 
Mwkjj udhalimu wa gadafi ni upi? ungeanza na chanzo cha mgogoro kisha ukamakizia na hayo madai yako.
Kinacho tokea libya si sawa na kilichojiri misri na tunisia kuna kitu nyuma yake, kitu kilichotengenezwa na wababe ambacho kimekutia upofu wewe mimi na yule tuamini wanavyotaka wao.
Matokeo ya vurugu yanayo jiri sasa si ukaidi wa gadafi bali damu ile ni sababu ya wanaotaka dunia iwe wanavyotaka wao.
Niaibu kubwa kwa watu kulaumu utawala wa gadafi kwa kigezo cha so called demokrasia ya magharibi na kufumbia mazuri yote aliyofanyia nchi yake na afrika kwa ujumla ukizingatia nchi ngapi za afrika zenye demokrasi na hamna lolote.
Wanajua sababu ni nini wote wanaolaumu utawala wa Libya, je ni mikataba mingapi ilifanyika na Libya ikauziwa silaha na hao wanaosema leo hawautambui utawala wa Gaddaf?

Mwl. Nyerere alipata kusema namnukuu "....akija mtu mjinga, akakuambia jambo la kijinga... na wewe ukalikubali... ATAKUDHARAU SANA!!" mwisho wa kunukuu.
 
MBONA HUTUELEZI UDHALIMU WA GADAFI???????
dunia ya sasa hivi ni ULIMWENGU-MASLAHI...unajua na ndio maana umeikimbia nchi yako na kwenda kuishi ughaibuni.
eleza udhalimu wa GADAFI uone tutakavyokushukia

swali nzuri sana udhalimu wa Gadaff uko wapi au na sisi tunafata mkumbo wa wazungu wenye nia na lengo la kuzidi kulinyonya bara letu.
 
Jamani, Tanzania hatuna tena sauti ya kutetea wanaokandamizwa? Yaani tumepoteza kabisa hata msimamo wetu wa "kila binadamu anastahili haki ya kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake"?

Leo hii Botswana ndio wanaongoza na sitoshangaa Namibia watafuatia wakati sisi viongozi wetu wanacheka cheka na huyu kichaa wa Libya. Of course I know serikali yetu haina uwezo au ujasiri huo hasa baada ya kupokea favors nyingi toka kwa Gaddafi lakini kweli tumeuza na utu wetu kwa sababu kuombaomba kwa viongozi wetu?


aibu na fedheha!!

Nadhani ni fedheha si tu kwa haya ya Ghadaffi, yapo mengi yakuongelewa kuhusu misimamo wa taifa letu kwa masuala kama ya Zimbabwe , Ivory coast n.k, ni suala la kuogopa kutoa kauli mpaka tujifiche nyuma ya AU au UN. Tumepoteza 'leadership' kwasababu ya umatonya.

Wale wanaosema kuna kila kitu na ni bure Libya, mbona Oman, Baharain na Saudia nao wanaandamana? Bahrain ndiko kabisa hata ukitaka ticket ya kwenda kujirusha duniani, mashaalah ipo.
Uhuru ni zaidi ya elimu, afya bure na pesa za ndoa. Unaweza kuwa na vyote lakini kama huna uhuru wa kujieleza, kushiriki na
kuthaminiwa bado fedha hazikusaidii na huna uhuru. Kama watu wanadhani Ghadaffi ni poa kwa kutumia helikopta na magrunedi kusaga watu wake, ahh! basi asilalamike mtu yakitokea ya Arusha na siku tutakapopondwa zaidi na FFU, kwasababu machungu tuliyonayo ndiyo waliyonayo Walibya kwa namna tofauti(ninamaana si elimu afya na pesa za ndoa bure, yaweza kuwa uhuru wa kujieleza na kuamua au kushiriki)

Hiivi mtu anayepewa hicho kima cha chini cha 'dolla 500' anajisikiaje Seif Ghadaffi anapokuwa visiwani Hawaii na kuwaalika akina
Beyonce, Mariah C, Usher n.k kutumbuika kwa pesa ile ile ya rasilimali za Libya?
Kwanini nchi iongozwe na watoto saba wa Ghadaffi na wapwa zake? Hapa Tz watu wameshaanza kupiga kelele kwanini mtoto X naye anataka kuwa sehemu ya chama na serikali, sembuse Walibya walioishi na hali hiyo miaka 40.!!!
Kwanini 'Diplomat' wamemuasi Ghadaffi kama raia wa kawaida tu mambo yao ni tambarare!
Utu wa mtu ni zaidi ya elimu bure, afya na pesa za ndoa, uhuru ni zaidi ya kupewa bure.

Kwa wale walio na kumbu kumbu, wakati Tanzania ina msisimamo ya dhati, kwa uchache Tanzania ingetoa kauli juu ya migogoro inayoendelea. Siku hizi misimamo yetu inategemea nani anajaza kibaba. Tunachokiona Botswana ndivyo ilikuwa Tz. Si lazima kulaani lakini ni lazima nchi itoe kauli, na si kuvizia nyuma ya migongo ya watu. Ni ukweli usio na kificho kuwa sisi kama taifa tumepoteza thamani ya utu na misimamo yetu ili kukidhi matakwa ya wakubwa nyuma ya migongo ya jumuiya za kimataifa.
Ndiyo maana imefika mahali hatujiamini na kuanza kujiuliza kama ni vema kuwapa pole marafiki zetu Wajapan.
 
Hakuna uchaguzi Libya kwa miaka 40 na ushee.
Ametangaza vita vya makombora dhidi ya raia wa Linda wasio kubaliana naye kisiasa.

MBONA HUTUELEZI UDHALIMU WA GADAFI???????
dunia ya sasa hivi ni ULIMWENGU-MASLAHI...unajua na ndio maana umeikimbia nchi yako na kwenda kuishi ughaibuni.
eleza udhalimu wa GADAFI uone tutakavyokushukia
 
Wengine humu mlikuwa bado kuzaliwa.
Gadaffi alimpa Iddi Amini msaada wa Askari kibao kuvamia nchi yetu 1978.
Baada ya vita kuisha Walikuwako Wafungwa kibao wa kivita kutoka Libya Nyerere akamwambia aje achukue watu wake.

Gaddafi ana pochi na watu wengi wanahusudu pochi yake lakini Gaddafi si mtu ni mnyama aina ya Iddi Amin.



Wanajua sababu ni nini wote wanaolaumu utawala wa Libya, je ni mikataba mingapi ilifanyika na Libya ikauziwa silaha na hao wanaosema leo hawautambui utawala wa Gaddaf?

Mwl. Nyerere alipata kusema namnukuu "....akija mtu mjinga, akakuambia jambo la kijinga... na wewe ukalikubali... ATAKUDHARAU SANA!!" mwisho wa kunukuu.
 
yaani kwa vile kaleta misaada ambayo sasa inaonekana imejaa damu ndio baadhi ya watu wanasema tumkumbatie tu? Utumwa gani huu wa kifikra ambao tunao sasa? Wanajeshi wake wanakimbia na ndege kukataa kuwalipua wananchi wao hapa watu wanasema "tuoneshe udhalimu wa Ghadaffi" Utii au upendo wa aina gani huu?

Mzee Mwanakijiji lazima ukumbuke kuwa tunaishi kwenye real world, not ideal one. Mimi siungi mkono anayofanya Gadaffi lakini sitaunga mkono kusema Tanzania itangaze kufuta uhusiano na serikali ya Gadaffi.

Unajua udhalimu unaofanywa na US dunia hii? unajua udhalimu inaofanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wake? unajua udhalimu unaofanywa na democratic dictatorships dhidi ya watu wao? Mbona tunawakumbatia tu? Where are our morals?

And why should we show our morals kwa kunyooshea udhalinu wa nje na kuchekelea wa ndani?

Naona ni bora tuwe kimya. Kwa sasa Tanzania kama nchi haina uwezo wa kusema lolote mbele ya watu.
 
Back
Top Bottom