Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.
Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).
Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.
Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?
Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?