Tanzania ina watu milioni 43, Zanzibar hawazidi milioni 5 kwa nini tugawane kwa kulingana?

pole mwenzetu, kwa maneno ya zanzibar tunasema umechelewa kibweni kwa kuitaka mtoni.

wazanzibar siku zote hawatayumba juu ya kile wanachokiamini, kuminywa na nguvu zinazotumika kuwatisha zamani waliogopa, na mbinu ya wagawe uwatawale ambayo ilikuwa ikitumika ndio iliochelewesha moto huu

ila kwa sasa hakuna la kuwarejesha nyuma. na weshang'amua janja ya nyani, kazi mnao mtapayukwa sana mwaka

na tukuimbieni

zee la nyeti wacha kupiga misere
yamekushinda wache wajilie vya wenyewe

Mh, ivi ni kweli Umma wa Watanganyika wanauhitaji Muungano au? ivi kwanini wazanzibari mnapenda kuaminisha kwamba umma wa watanganyika wanapenda Muungano? Walah hawaupendi na kamwe hawataupenda kwani nothing gained by individual people from Tanganyika.
 
Mh, ivi ni kweli Umma wa Watanganyika wanauhitaji Muungano au? ivi kwanini wazanzibari mnapenda kuaminisha kwamba umma wa watanganyika wanapenda Muungano? Walah hawaupendi na kamwe hawataupenda kwani nothing gained by individual people from Tanganyika.


wenye kuandaa muswada wa katiba mpya tanganyika, wenye kuzuia mambo ya muungano ni Tanganyika, wenye kutaka kuweka hadidu za rejea ni Tanganyika. kisha mseme na nyny muungano hamuutaki ?

wazanzibari wao wanaandaliwa tu chakula kwenye sahani ati wale, na wao wamekataa kwa maana mlo huu wao kamwe hawali kutokana na mila na silka zao
 
Hio kutumia Tanzania Mainland na Tanzania Zanzibar ni muendelezo wa ujanja wa kuimeza Zanzibar kabisa. Mimi nawashangaa hata Wazanzibari wanaotaka kujadili Mswada wa Katiba ya Muungano wakati la kufanya ni kujadili Katiba yetu ya Zanzibar.

Kujadili Katiba ya Muungano ni kuuhalalisha Muungano wenyewe ambao kwetu wengi tunaona ni kiinimacho cha watawala kuisambaratisha Zanzibar.

Nonda ndugu yangu, sahau kuhusu serikali moja, the worst it can get to be ni serikali tatu lakini la msingi kila mtu na lake na kama ni federal government hilo ni baadae.

Kwamba Muungano una utata wala halitaki mjadala maana hata muasisi wake aliona hivyo hivyo:

"Without any question, the manner and the implications of the union between Tanganyika and Zanzibar is the most misunderstood aspect of Tanzania's political development. It may not matter very much when foreigners get confused, but unfortunately there are many times when Tanzanians themselves appear to misunderstand it."

Former Tanzanian President Julius Nyerere. - Dar es Salaam Government Printer, July 1970. p. 3.

Kuhusu Dr. Shein tuwaulize nyinyi mliomleta lakini sisi tunajua tunachokitaka.

GNU mpaka sasa ni ya CCM lakini nayo haina muda kubadilika kuwa ni ya Wazanzibari (fuatilia mjadala wa jana Bwawani Hotel na ukishindwa ntakutumia clips)

Siri iliopo ni kubwa lakini sisi tumeitambua - kuimeza Zanzibar na kuifuta kwenye ramani ya dunia.

OVER OUR DEAD BODIES

Nilichokiona katika mjadala wa jana bwawani ni umbumbumbu mtupu wa wachangiaji na kudhihirisha kuwa hata baadhi ya viongozi wa zanzibar hawajui chochote. Ivi kuna mzanzibari ambaye hawakilishwi Bungeni-ufahamu wangu ni kwamba kila mzanzibari anawakilishwa bungeni (Pia kuna wabunge maalum ambao ni wawakilishi wa SMZ/GNU) na wabunge wake ndio waliotoa hoja ya kutaka upande wa zanzibar nao kuwe na centre ya kutoa maoni. Sasa anapotokea mchangiaji na kusema zanzibar haijahusishwa ana maana gani? Kwanini tubabaishane lakini na talaka halali, Please Jeykey and your convoy, let these people go alone with their isles, we are tired of being insulted ever to night!
 
Inaonekana hujui unazungumza nini na sidhani kama umesikiliza huo mjadala wa Bwawani jana au wa Haille Selasie leo.

Kuwaita watu na vingozi wao mbumbumbu ni kuwakosea adabu na si ustaarabu. Lakini labda kweli mbumbumbu maana tusingekubali "kutawaliwa" na Tanganyika kwa miaka 47 iliopita.

Kwenu nyinyi lolote kwa sasa ni mshangao maana Wazanzibari sasa wanaelewa adui wao nani - mkoloni TANGANYIKA. Mlizoea kutubambikia mambo ndani ya serikali yenu ya Tanganyika mkidai eti ni Tanzania, tumewashtukia.

Hivyo endeleeni kuchonga lakini saa ya ukombozi ni sasa.

Walichozungumza hao unawaita wewe mbumbumbu ni ukiukwaji wa taratibu katika kuandaa mswada, hayo mengine nayaita mbwembwe zako za uandishi tu.

Hio talaka, wengi wetu tuliitaka jana lakini bado haijachelewa. talaka.jpg
 
Mh, ivi ni kweli Umma wa Watanganyika wanauhitaji Muungano au? ivi kwanini wazanzibari mnapenda kuaminisha kwamba umma wa watanganyika wanapenda Muungano? Walah hawaupendi na kamwe hawataupenda kwani nothing gained by individual people from Tanganyika.


Wasivyovitaka tunaviona kwani wanasema na kuchukua hatuwa. Si mnagombana na ufisadi nyie, si mnagombana na ugumu wa maisha nyie ,si mnagombana na utawala wa CCM nyie, sasa lini Lema, Slaa ,Mbowe, Mnyika walisema kuwa hawautaki Muungano?
 
Nilichokiona katika mjadala wa jana bwawani ni umbumbumbu mtupu wa wachangiaji na kudhihirisha kuwa hata baadhi ya viongozi wa zanzibar hawajui chochote. Ivi kuna mzanzibari ambaye hawakilishwi Bungeni-ufahamu wangu ni kwamba kila mzanzibari anawakilishwa bungeni (Pia kuna wabunge maalum ambao ni wawakilishi wa SMZ/GNU) na wabunge wake ndio waliotoa hoja ya kutaka upande wa zanzibar nao kuwe na centre ya kutoa maoni. Sasa anapotokea mchangiaji na kusema zanzibar haijahusishwa ana maana gani? Kwanini tubabaishane lakini na talaka halali, Please Jeykey and your convoy, let these people go alone with their isles, we are tired of being insulted ever to night!


Unajuwa kijana kule kwetu mtu aliepita kiwango cha umbumbumbu tunamwita TOHO na wewe ni mmoja wao. Unaposema Wazanzibari wamewaklilishwa una maana gani? Unataka kutwambia kuwa lile bunge ni la Tanzania au ni la Tanganyika? Tukianzia na huo unaoita uwakilishi mle ndani mna mawaziri wote wa Tanganyika na Bunge linaongozwa na Waziri Mkuu wa Tanganyika. Mambo mawili ya kujiuliza jee kwanini Mawaziri wa wote wa Zanzibar wasiwepo? na kwanini kiongozi wa hilo bunge awe Waziri Mkuu wa Tanganyika? Ukishapata jawabu ndio uangalie jee hao Wazanzibari ni mabumbumbu kusema kuwa hawakushirikishwa na sio kuwakilishwa?
Kama unakumbuka Spika wa Bunge alisema kuwa Wazanzibari wangewakilishwa kwenye kutowa maoni (sawa na Bungeni). Halafu unakurupuka na kuwaita Wazanzibari mambumbumbu au ni wewe toho wa kutojuwa nini Wazanzibari wanasema? Rasimu ya mchakato wa kubadilisha Katiba haukuandikwa Bungeni (naomba ufahamu hilo) na badala yake imeletwa Bungeni kutaka kupitishwa na kati ya wanaopinga ni Wakubwa wako wa CHADEMA sasa kama ilitayarishwa Bungeni unakodai kuwa Wazanzibari wanawakilishwa inakuwaje kuwa hata wabunge wenyewe wanaipinga?
Bunge halitayarishi rasimu bali inapitisha na hadi ssasa hiyo rasimihaijapitishwa na bunge ambako wewe unadai Wazanzibari wanawakilishwa. Jambo la kujiuliza hiyo rasimu imetoka wapi na kupelekwa Bungeni na nani alieitayarisha hiyo rasimu? Na hapo ndipo Wazanzibari wanaposema hawajashirikishwa na ushahidi ni kuwa mwanasheria Mkuu wa Zanzibar haiuji hiyo rasimu.
Tatizo lenu mkimuona joti anaigiza mnafikiri Wazanzibari wako hivyo , poleni sana msichezee moto wa kumbi!
 
Sina la kuongeza hapo Ngekewa maana kweli huyu jamaa ni TOHO hasa. Tatizo lake na wenziwe wenye fikra kama yeye, ni ile ya dharau walionayo juu ya Zanzibar.

Kama hajui, huu Muungano umedumu kwa miaka 47 kutokana na Chama Dola cha CCM na matumizi mabaya ya hizo nguvu za Dola. Baada ya kuona Wazanzibari wameamka na kuungana kudai haki yao, wameanza kulalama kama mtu alietubukia mtoni.

Iliobaki kwao ni kudai Tanganyika yao lakini Zanzibar hioooooooooooooo inaondoka.
 
Makaimati said:
Sina la kuongeza hapo Ngekewa maana kweli huyu jamaa ni TOHO hasa. Tatizo lake na wenziwe wenye fikra kama yeye, ni ile ya dharau walionayo juu ya Zanzibar.

Kama hajui, huu Muungano umedumu kwa miaka 47 kutokana na Chama Dola cha CCM na matumizi mabaya ya hizo nguvu za Dola. Baada ya kuona Wazanzibari wameamka na kuungana kudai haki yao, wameanza kulalama kama mtu alietubukia mtoni.

Iliobaki kwao ni kudai Tanganyika yao lakini Zanzibar hioooooooooooooo inaondoka.

Makaimati,Ngekewa,

..mtu anayedai haki hana nia ya kuondoka.

..kile kitendo cha Zanzibar kudai hiki na kile ndani ya muungano maana yake ni moja, kwamba Zanzibar haina nia ya kujitoa ktk muungano.

..Zanzibar wana uwezo wa ku-recall viongozi wao walioko ktk serikali ya muungano, pamoja na kuzuia wabunge wao kushiriki vikao vya bunge la muungano, na huo ukawa mwisho wa muungano huu.

NB:

..wakati G-55 walipopeleka hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, wa-Zanzibar[CCM,CUF] mlikaa pembeni na kuwaacha wahangaike peke yao.
 
Naomba kuuliza, kama Zanzibar haijashirikiswa, je kuna maana gani kuwa na mwaziri kutoka zanzibar? na makamu wa Rais kutoka zanzibar? please wazanzibar kama mnataka kuondoka si msema tu, hakuna atakaye walazimisha, huu ni utoto wa ajabu saana. Tuna bunge amablo uwakilishi wa zanzibar ni kila watu 300 wana mbunge, leoi wanasema hawajashirikishwa? na je mnawalipa hao wabunge wa Zanzibar? kama si mzigo kwa wananchi wa bara peke yao
 
Kwani hujui kwamba Zanzibar Serikali ni ya CCM kama ilivyo ya Tanganyika ambayo nyinyi kwa ujanja wenu mnaiita ya Tanzania.

Kitendo cha kufanya mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ni hatua za GNU za kufikia huko kwani hata hao CCM sasa wameanza kuona ukweli na wanabadilika (refer mjadala jana na juzi Bwawani na Haileselasie)

La kudai Zanzibar halina u CUF wala u CCM kwa taarifa yako.

"..wakati G-55 walipopeleka hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, wa-Zanzibar[CCM,CUF] mlikaa pembeni na kuwaacha wahangaike peke yao."

Hivyo siku hizo CUF ilikuwako? Hebu refresh my mind sir.
 
Sasa ni wakati muaafaka wabara kudai haki nao, nafikiri mnajua kuwa hairuhusiwi mtanzania bara kunua ardhi Zanzibar kwa kisingizio eti ardhi ya Zanzibar haitoshi. Sasa nauliza je mbona sijasikia Mtanzania yeyote kukatzwa kunua ardhi Ukerewe? au ardhi ya Ukerewe ni kubwa inatosha? sasa ni wakati muaafaka kuwashioka sharubu hawa wazenji, wasitufanye wajinga sisi, kama wanataka waarabu warudi sawa, waende
 
Wewe YOMBAYOMBA kwa kweli ni CCM imara maana hizo ndio lugha walizotumia kina Nyerere kumtisha Karume na kumghilibu mpaka Tanganyika ikaivamia Zanzibar kiulaini na imekuwa ikiikalia kwa mabavu kwa miaka 47 sasa.

Hivyo vitisho vimetumika sana mpaka siku moja Nyerere amewahi kuwaambia viongozi wa Zanzibar hivi:

"Viongozi wa siasa huko zanzibar hawana la kuwambia wananchi wao, isipokuwa Hizbu imefanya hivi na Sultani amefanya lile"

Haya maneno hata hao CCM hawayasikii tena na wanaungana kudai Zanzibar yao huru.

Mambo ya ardhi ya Zanzibar tuwachie wenyewe maana nyinyi mmezoea kuigawa kwa mafisadi ambao wanaondoka na mali zenu kila siku.

Dawa yenu ni kudai Tanganyika yenu na mtuwachie Zanzibar yetu.
 
Makaimati,

Hebu nitajie kiongozi hata mmoja wa Tanzania bara alikuja kujenga nyumba Zanzibar? nami kama nakuodheshea viongozi wa Zanzibar waliojenga Dar es salaam,
1) Mwinyi
2) Jumbe
3) Komandoo
3) Mwakanjuki
Niendeleeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Si vema kuwaambia wachangia hoja kuwa wanatumia "tumbo kufikiri", hayo ni matusi kabisa na sidhani kama ni utu na inaonyesha wewe hujalelewa na values nzuri...sidhani kama kujibu hoja mpaka utukane, kwani ukitumia lugha proper hutasikilizwa? The fact that you start with insults doesn't show you use your head...and you are shaming yourself. Plus this issue is a very critical issue, huwezi kulinganisha na UN wala EAC...We are talking about justice within the union...in the use of our resources. Equitable distribution of governance and resources. How can you ignore such carnal issues? My friend, next time be civil...

Paundwe serikali tatu,
 
Hivi Zanzibar ina ubavu wa kuchangia gharama za serikali ya muungano kwa 50%? nafikiri mmeshiba futali sasa
 
Katika hao uliotaja, ni Komandoo Dr. Salmin Amour ndio kwao Zanzibar na hao wote wengine ni ndugu zenu waliokuja kujenga Zanzibar

Please check your facts Yombayomba.
 
Irelevant! Tena kwanini mnaing'ang'ania Zanzibar kwa maguvu ya Dola yenu ya Tanganyika?
 
Kwani nani anamhitajia mwenzake. Ni nyinyi Tanganyika na ajenda zenu za siri hizo. Tumeshiba futari sisi kabla hamjatuvamia na kutudidimiza kiuchumi. Kama mmeona Zanzibar ni mzigo, kwanini mmeing'angania kwa miaka 47 sasa?
 
Back
Top Bottom