Tanzania ina watu milioni 43, Zanzibar hawazidi milioni 5 kwa nini tugawane kwa kulingana?

Makaimati,

Hivi una habari mjomba wenu Bakhersa anadai eti mama yake Mnyamwezi na baba yeke Mpemba? nyinyi ni ndumila kuwili, mnatikisa kiberiti tukija juu mnafyata, hivi nani anawadanganya kuwa bara inaitaka Zanzibar? kama si nyinyi wenyewe kutaka muungane?
 
Hivi Yombyomba umeishiwa na hoja? Sisi tunazungumza ya huu "MUUNGANO", wewe unakuja na habari za Bakhresa.

Jadili hoja, mmelikoroga, mtalinywa.
 
Mkaimati,

Hii ndo yenu wa Zenji mkiambiwa ukweli manywea na kuabadilisha agenda za majadiliano, so mmezoea chenu ni chenu cha wezenu ni chetu, hizi ni tabia za kike
 
Nonda kwa kweli mimi siioni Tanganyika. Hiyo power of Attorney labda alipewa Nyerere as a natural person and not a legal person. Hayo mambo yasiyo ya Muungano ambayo unasema ni ya TAnganyika yanaamuliwa na Bunge gani au na Baraza gani la Mawaziri? Mbona wakati wa kujadili hotuba za Wizara ambazo si za muungano wabunge toka Zanzibar hawatoki nje ili mambo yasiyo ya muungano yajadiliwe na Watanganyika peke yao? Huwa nashangaa ati wabunge toka Zanzibar wanakuwa kwenye kamati za Bunge za Nishati na Madini, Utalii, Ujenzi na Miundombinu na wanapiga kelele kwelikweli wakati haya Mambo si ya Muungano kwa Mujibu wa Katiba. Ni bora wasingekuwa wanashiriki katika mambo hayo ningeamini kuwa japo kwa mbaaali Watanganyika wanaaamua mambo yao kivyao, lakini loooo Wazanbibar Baraza la Wawakilishi LAO Bunge la Muungano LAO imekaaaje? Paomoja na hayo mchakato wa Kutunga Katiba Mpya/Kurekebisha Katiba unatupa nafasi mujarabu ya kuuangalia Muungano wetu kwa jicho la pili ili tuachane na mazonge yanayouzunguka huu Muungano ambao kwangu ni tata.

Kimbunga, Kuna Serikali mbili tanzania moja ya Tanzania na moja ya Zanzibar iwapo unataka tuzungumze nadharia. Kwenye vitendo halisia ni kuwa hii Serikali ya Tanzania inatumikia maslahi ya upande mmoja tu (Tanganyika) hali kadhalika Bunge linashughulikia upande mmoja tu Tanganyika. Nikupe mifano mimiwili ambayo unaweza kunipa ufafanuzi wake iwapo unao

Moja ni Muundo wa Bunge ,nani kiongozi wa Bunge siku zote nikimaanisha kutoka upande gani. Na nani wanaokaa katika viti vya Mawaziri (tuondoe waziri wa Mambo ya nje na ndani ambao Zanzibar haina Wizara hizo)?
Jambo la pili kwanini Rais wetu kila siku anapohutubia Bunge huwa hazungumzii mambo ya upande wa pili yaani Zanzibar?
Katika sheria za kimataifa matukio ya kila siku yanageuka na kuwa ni sheria hivyo hili la kuwa Bunge na Rais wake wanashughulikia mambo ya Tanganyika yana apply kuwa ni sheria (kuwa Bunge ni la Tanganyika)
Hili la Wazanzibari kuwapo kwenye mambo yasiyo wahusu katika Bunge hakuwafanyi wanawakilisha mambo ya Zanzibar kwani Zanzibar ina Baraza lake la kutunga sheria na Serikali ya Zanzibar inawajibishwa huko sio Bungeni. Hali hii ipo pia kwa Makamo wa Rais ambaye anafanya kazi zisizomuhusu na ndiyo maana Shein aliona bora kushuka na kuwa Rais wa Zanzibar kuliko kugombana na conscious yake. Huu ni ujanja wa kuwafanya Wazanzibari wadanganyike lakini ukweli wenyew Wazanzibari si mbumbumbu kama inavyofikiriwa!
 
Makaimati,

Hivi una habari mjomba wenu Bakhersa anadai eti mama yake Mnyamwezi na baba yeke Mpemba? nyinyi ni ndumila kuwili, mnatikisa kiberiti tukija juu mnafyata, hivi nani anawadanganya kuwa bara inaitaka Zanzibar? kama si nyinyi wenyewe kutaka muungane?

Hilo la Bakhresa halina uhusiano na matakwa ya Wazanzibari> Bakhresa ana hiyari yake nanyi mnahiyari yenu juu yake. Nafikiri hamna uwezo wa kumfanya chochote kwani anaweza kuondosha miradi yake au akawa kama mwekezaji. Mna wawekezaji wa kiwango cha Wachina wakiuza vikombe mtamdharau Bakhresa anaeekupeni karibu nusu ya mapato ya kodi kuliko wafanya biashara wenu.
Hivyo wewe unashangaa kuwepo Mnyamwezi na Mzanzibari? Kamuulize Abuod Jumbe, Ali Hassan Mwinyi, Hassan Nassoro Moyo, Marehemu Saidi Natepe, Seif Bakari na wengi.

Hata hivyo ishu hapa ni kuwa kama ni Muungano basi uwe wa haki na usawa kama hamuwezi basi na tuuuvunje.
 
Kilichotokea Zbr siku tatu zilizopita ktk mijadala ya kukusanya maoni kuhusu Mapitio ya Muswada wa Katiba, 2011 wote tumejionea. Nadhani hapa the best way kwa kuwa tukiulizwa sisi wenye nchi iwapo tunautaka muungano au la jibu litakuwa - hatuutaki! Labda hao viongozi ambao nadhani ni uoga na unafiki wa kutotaka kuonekana muungano umewafia mikononi mwao ndio wanaukumbatia muungano. Tuanze kujadili the best way ya kila upande kuanza kivyake! Tujadili ni namna gani ya kupeana talaka, na namna gani tunaweka mahusiano yetu ya kidiplomasia, kijamii, kiuchumi n.k.

Hakukuwa hata na sababu ya kutuma ujumbe wa kina mzee Sitta Zbr, for what? kwa kuwa kama maoni ya katiba kutoka upande wa Zanzibar yangeweza kupatikana thru Wizara inayoshughulikia Muungano, Wabunge zaidi ya 70 kutoka Zbr ktk Bunge la Tanzania, Wabunge 5 kutoka BLW Zbr waliopo ktk Bunge la Tanzania etc. Tunajikomba nini hadi kuraruriwa Muswada mbele ya macho ya watu wazima kama kina Sitta???? Viongozi wetu wasikie, pleeeease JK na timu yako vunjeni huu muungano hakuna atakayewalaumu. Hata mapenzi yakianza ni matamu sana lakini mkishachokana hufikia mwisho hata mbinu gani zikitumika, mapenzi yakiisha - yameisha! Ndoa yetu ktk muungano imefikia tamati, lets break the knots. We need back our beloved Tanganyika!
 
Nakubaliana nawe kuwa kweli tumefika to the point of no return kwani tunapoanza kuona vitendo yva pande zetu ndiyo sahihi hata kama sio sahihi eti tu kulindana basi hatuwezi tena kulijadili hili.
Naomba nitofautiane nawe na mtizamo wako kuwa kulikuwa hakuna haja ya kuupeleka mswada Zanzibar ETI kuna wabunge wa Zanzibar kwenye Bunge. Hivyo ndugu yangu uko serious na hili au ndio umekereka na vitendo vya Wazanzibari? Kwa muono wako basi hakuna hajan ya haya yote kwani Watanganyika wanawakilishwa na Wabunge zaidi ya 250 basi maoni yao yangepatikana kwenye Bunge sawa na maoni yatakayotoka Zanzibar kama unavyofikiria.
Viongozi waliomo madarakani ndio wanaofanya watu wafanye vitendo unavyofikiria kuwa ni utovu wa nidhamu. Wao akiwamo Sitta ndio wanaoidharau Zanzibar na ndio zao la vitendo vinvyofanywa. Nashangaa kwa hili la Wazanzibari inaonekana ni kitendo kibaya lakini kile cha maandamano yanayosababisha vifo kinaitwa ukombozi> Ukweli siku zote haufichiki na Wazanzibari wameamuwa kuwa wakweli wa nafsi zao sio kudanganya!
 
Hivi kwanini nyie waarabu koko mnalialia kuhusu Muungano? C mpitishe azimio kwenye baraza la wawakilishi kuuvunja,at the same time mnawaambia wabunge wenu kwenye Bunge la URT warudi Zenji..watu wenu waliojaa Bugurun,Vingunguti,Magomeni,Ilala n.k..warudi,wakina Simai,Babu Ali,Ali Omari,Said jecha na wote
 
Hilo la Bakhresa halina uhusiano na matakwa ya Wazanzibari> Bakhresa ana hiyari yake nanyi mnahiyari yenu juu yake. Nafikiri hamna uwezo wa kumfanya chochote kwani anaweza kuondosha miradi yake au akawa kama mwekezaji. Mna wawekezaji wa kiwango cha Wachina wakiuza vikombe mtamdharau Bakhresa anaeekupeni karibu nusu ya mapato ya kodi kuliko wafanya biashara wenu.
Hivyo wewe unashangaa kuwepo Mnyamwezi na Mzanzibari? Kamuulize Abuod Jumbe, Ali Hassan Mwinyi, Hassan Nassoro Moyo, Marehemu Saidi Natepe, Seif Bakari na wengi.

Hata hivyo ishu hapa ni kuwa kama ni Muungano basi uwe wa haki na usawa kama hamuwezi basi na tuuuvunje.

Hivi unajua hicho kipande chenu cha ardhi(Zanzibar) miaka 20 ijayo kitazama kutokana na tabia nchi ambayo itasababisha maji kuongezeka na chote kuzama,jaribu kuwaheshmu watanganyika wanaowatunza na kuwapa ardhi,cdhan kama muungano ukivunjika mtatosha huko kwenu..ee Mungu 2letee Tanganyika ye2..
 
Issue ni state sovereignty,si idadi ya watu jamani...Znz hata ingekua na watu laki moja,the fact that ina utaifa wake tangu awali inatosha kabisa...kuna nchi zina watu pungufu ya Znz,lakini zipo huru na ni wanachama wa UN...tumewanyanyasa sana wazanzibar ktk utaifa wao, ni kama koloni letu dogo,tulipofikia tuwaache na wao waamue sasa...
 
Mojawapo ya mambo yaliyonichefua kwenye muswada wa katiba ni pamoja na Part III hasa section 5 na 6. S.6 inasema kuwa wajumbe wa tume watatoka pande zote za muungano kwa idadi sawa (yaani kama wajumbe ni kumi basi Zanzibar watoke 5 na Bara watoke 5), ukienda mbele zaidi unaona kuwa maamuzi ya watu wa Bara yanaamuliwa na Wazanzibari.
Bunge letu lina wabunge takribani 360, kati ya hao zaidi ya 75 wanatoka Zanzibar (kama asilimia 20 hivi) sasa hili suala la katiba kwa nini tusitumie uwiano wa wabunge au hata uwiano wa watu, je kwa nini serikali yetu inabembeleza sana huu muungano?

Nadhani inabidi hii ipingwe kwa nguvu zote na wabunge wa bara maana huku si kuimarisha muungano bali kuendekeza upendeleo ambao nisingependa kuutaja hapa

Ukweli ni kwamba population ya wazanzibari including wapemba haijafika hata 1.5m. Iloikatiba mpya itende haki kwa muuungano, representation bungeni lazima iwe ya ki-uwiano. 1.5/43 x 100 = 3.5%. Wao walipaswa kuwa 3.5% tu hata hivyo natambua kuwa kuna factor nyingine za kisiasa zinazofanya wawe karibia asilimia 20; siasa hizo si za haki kwani inwezekana mbungo mmoja kule Zennji akawa anawakilisa watu wasiozidi elfu 30. This is bad. Katiba lzima iliangalie hili suala la muungano upya.
 
Wewe Yombayomba hujielewi hata kidogo. Sasa anaekimbia hoja mimi au wewe. Tunazungumza issue za maana unaleta mambo binafsi ya Bakhresa.

Nadhani huna hoja tena na siwezi kujadiliana na mtu kama wewe ambae sasa unakimbilia matusi sasa.

Simply put, "Muungano" huu hatuutaki, period
 
Haya ndio maneno ya kumwambia Yombayomba na wenzake wenye mawazo kama yake ya kuwa Zanzibar ni kama Wilaya ya Kahama.

Zanzibar na Tanganyika ndio zilizoungana kuunda Tanzania, zote zikiwa nchi huru.

Baada ya kuigeuza koloni la Tanganyika kwa miaka 47, sasa kelele za nini Wazanzibari wanapodai haki zao?

Hebu Mdau nisaidie kuwafahamisha hawa kina Yombayomba.
 
Hilo la kudai Tanganyika ndio kazi yenu na sio habari ya Zanzibar kuzama kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ukweli ni kwamba, iliotuzamisha ni Tanganyika ilioikalia Zanzibar kooni na kuidumaza kiuchumi na kuifanya kuwa tegemezi.

Kabla ya kuungana na nyinyi Zanzibar ilikuwa inajitegemea kwa kila kitu mpaka tukisaidia nchi nyengine

Kutokana na fitna zenu ndipo mlipofaulu kutugawa na kutusambaratisha kama Taifa.

Sasa tunadai haki yetu mnakuja juu. Tunasema "saa ya ukombozi ni sasa", daini Tanganyika yenu kama mna ubavu.

Wacheni kung'ang'ania visivyo vyenu, Zanzibar ina wenyewe.
 
Wacha matusi kijana, jadili hoja iliopo ukumbini.

Zanzibar ni Kisiwa kilichobarikiwa na kuwa na watu wa asili mbali mbali kama vile Waarabu, Wahindi, Wachina n.k na wakiishi kwa amani na upendo mpaka mlipokuja nyinyi na fitna zenu mkatuvuruga. Mmeona hivi sasa tunaungana kudai haki zetu ndio mnachonga sana.

Hayo ulioyataja yote yatakuja kwa wakati wake na usifanye haraka ukajitia presha bure.

Zanzibar Zindabad.
 
Ukweli ni kwamba population ya wazanzibari including wapemba haijafika hata 1.5m. Iloikatiba mpya itende haki kwa muuungano, representation bungeni lazima iwe ya ki-uwiano. 1.5/43 x 100 = 3.5%. Wao walipaswa kuwa 3.5% tu hata hivyo natambua kuwa kuna factor nyingine za kisiasa zinazofanya wawe karibia asilimia 20; siasa hizo si za haki kwani inwezekana mbungo mmoja kule Zennji akawa anawakilisa watu wasiozidi elfu 30. This is bad. Katiba lzima iliangalie hili suala la muungano upya.

Mkuu.
Mimi nafikiri ni vizuri liwepo bunge la Tanganyika, bunge la Zanzibar na bunge dogo la muungano lenye model kama ya bunge la EAC.
Kwenye bunge la Tanganyika tuchague idadi yoyote ya wabunge tunayotaka na bunge la Zanzibar wachague idadi wanayopenda kuwa nayo..lakini bunge la muungano liwe dogo na idadi sawa la wabunge..bunge la EAC lina wabunge 9 kutoka kila nchi mwananchama.

La muhimu ni kuweka muundo wa muungano makini, wa haki na usawa. Hili litaondosha manung'uniko. sasa hivi muungano ni hovyo tu, kila kitu kimefichwa fichwa na ubabe mwingi au tuseme muungano tunauendesha kwa matakwa binafsi na kidekteta.
 
Hivi unajua hicho kipande chenu cha ardhi(Zanzibar) miaka 20 ijayo kitazama kutokana na tabia nchi ambayo itasababisha maji kuongezeka na chote kuzama,jaribu kuwaheshmu watanganyika wanaowatunza na kuwapa ardhi,cdhan kama muungano ukivunjika mtatosha huko kwenu..ee Mungu 2letee Tanganyika ye2..

Mdharau kwao mtumwa! Na tungojee hapo tutakapozama lakini hizi tabu za sasa zituepuke. Hao walioko huko hawakutumwa nasi kuja huko bali waliamuwa kwa utashi wao na wao wenyewe wataamuwa> Sisi tulioko huku tunataka tuishi kwa uhuru na usawa!
 
Ukweli ni kwamba population ya wazanzibari including wapemba haijafika hata 1.5m. Iloikatiba mpya itende haki kwa muuungano, representation bungeni lazima iwe ya ki-uwiano. 1.5/43 x 100 = 3.5%. Wao walipaswa kuwa 3.5% tu hata hivyo natambua kuwa kuna factor nyingine za kisiasa zinazofanya wawe karibia asilimia 20; siasa hizo si za haki kwani inwezekana mbungo mmoja kule Zennji akawa anawakilisa watu wasiozidi elfu 30. This is bad. Katiba lzima iliangalie hili suala la muungano upya.

Kwani Mbunge kutoka Zanzibar anafanya nini kwenye Bunge la Tanganyika? Sioni maana ya Hesabu ya X ngapi au % ngapi Bungeni. Bunge ni la Tanganyika basi haipaswi kuwepo wabunge kutoka Zanzibar. Wabunge hao wanawawakilisha nani wakati Bunge ni la kutengeneza sheria za Tanganyika tu?
 
Mimi nadhani huu si wakati tena wa kujadili masuala ya idadi ya Wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri bali ni kukubali kuwa mfumo huu mzima wa Muungano hauna maslahi kwa Watanganyika na Wazanzibari.

Muungano huu umedumu kwa muda wote wa miaka 47 kutokana na utashi wa viongozi wa CCM wa pande zote mbili za "Muungano". Kwa maana nyengine, Muungano huu umekosa uhalali wa kisiasa na kisheria.

La msingi ni ndugu zetu wa Tanganyika wadai nchi yao maana sisi Wazanzibari ndio tumeanza hivyo.

Baada ya hapo, kama wananchi wa pande mbili hizi (wakiona kama kuna haja hio), wanaweza kutafuta njia ya kushirikiana kwa mfumo wowote watakaoona unafaa. La muhimu ni kuhakikisha kuwa muungano au ushirikiano wowote utaokubalika utatokana na maslahi ya pande mbili kwa misingi ya kuheshimiana.

Napenda kuwashauri wadau nyote, kuwa sisi wananchi wa pande hizi mbili kwa vyovyote vile, tusikubali kugombanishwa wala kuchezewa akili na wanasiasa ambao wanapata faida kupitia migongo yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom