Tangazo la ajira Jeshi la Polisi 2014/2015

Mshahara ni kufuata elimu yako...na zaidi kuna 15% ya kutumikia profession yako, kuna 15% ya kupanga mitaani kulipia nyumba. Ukija utayajua mengi, hadi wala rushwa utawajua, na utatambua kwanini polisi wanalaumiwa sana lakini wala hawachukii wala kujoshitukia.[/QUOTE
mwenye degree anakunja sh ngapi kwa mwezi
 
Mshahara ni kufuata elimu yako...na zaidi kuna 15% ya kutumikia profession yako, kuna 15% ya kupanga mitaani kulipia nyumba. Ukija utayajua mengi, hadi wala rushwa utawajua, na utatambua kwanini polisi wanalaumiwa sana lakini wala hawachukii wala kujoshitukia.

mwenye degree anakunja sh ngap kwa mwezi?
 
hata kama ni graduate kwenda uafisa ni baada ya miaka 2 hadi 3,so kipindi hicho huna rank yoyote wewe ni police constable tu kama wengine hivyo shughuli zote za kipolisi lazima ufanye

Hivi police constable sio cheo?
 
Jeshi sio baya but viongoz wake ndio wenye matatizo,ndugu yangu ameuguliwa na mama yake na amezaliwa pekeake ila alinyimwa. Uhamisho ili asogezwe apate kumuuguza mzazi,likizo alibaniwa mpaka alifisi,ikabidi aache kazi ndani ya sana 24,ingawa mpaka sasa anaipenda. Kazi ila ilibidi aache,viongoz. Hawana msaada kwa walio chini yao, ushahidi huo ninao kabisa. Na mwenyewe aliandika barua mpaka kwa IGP aliemaliza muda asaidiwe ila kimya, anaipenda sana kazi yake. Inauma sanaaa
 
mi nitajieni mshahara tu kwa graduate mwenye degree nijue kama natuma maombi au la...ilo la rushwa halinihusu
 
Kwa hiyo kama umemaliza mwaka Jana na Una miaka 25 hauruhusiwi ku apply
 
Ajira kwa Wahitimu Elimu ya Juu Mwaka 2014
Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza azma hii waombaji watajaza kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo.

Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM

Waombaji wawe na taaluma zifuatazo:

Shahada: Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala katika Utumishi wa Umma, Uchumi, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji[BaLE], Sheria, Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa Habari, Uandishi wa Habari za Michezo, Mawasiliano ya Umma, TV & Redio Production, Michezo, Ugavi[BA in Procurement & Supplies], Mawasiliano ya Redio[Bsc in Radio Communication], Mazingira[BA in Environmental Disaster Mgt], Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining Engineering], Uchoraji[BA in Fine Arts], Fedha na Benki[Finance & Banking], Daktari[Medical Doctor] na Daktari wa Meno[Dental Surgeon], Mkemia, Bailojia[Molecular Biology].

Stashahada: Utunzaji Kumbukumbu, Katibu Muhutasi[Personal Secretaries], Mawasiliano ya Redio, Matengenezo ya Kompyuta, Fax na Photocopy Machines, Mafundi Mitambo wa Meli, Mafundi Umeme wa Magari, Ugavi[Procurement & Supplies], TV na Video Production, Manahodha, Tabibu[Clinical Officer], Tabibu wa Meno[Dental Therapist], Mzoeza Viungo[Psysiotherapist/Occupational Therapist], Fundi Sanifu Mionzi[Radiographer] na Fundi Sanifu Macho[Optometrist].

Astashahada: Uzamiaji, Mpishi, Fundi Pikipiki, Fundi Ushonaji na Muuguzi Msaidizi[Enrolled Nurse].

MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika
picha yake “Ppt Size” kwenye fomu.
2. Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote
yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari[Leaving
& Academic], cheti/vyeti vya taaluma[Academic Transcript].
3. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
3. Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2013/2014 tu.
4. Awe na tabia njema.
5. Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
6. Awe na afya njema[kimwili na kiakili]
7. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
8. Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu].
9. Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
10. Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.
11. Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini.
12. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi.
13. Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje.
fomu ya ajira elimu ya juu (1).pdf



Sifa za muombaji. Kigezo #4 na #9 havikupaswa kuwepo
 
Ni 741,000/- ukiachana 15% ya kutumikia profession yko, 15% kodi ya kupanga (kama huishi quoters), au 10% kama utakuwa FFU, au 15% ukipangwa upelelezi. Toa na 180,000/- lession ya kila tar15. Nimekuibia japo mshahara ni siri. Haya uamuzi niwenu.
Kipimo cha mtanzania mpiga kelele ni kumpa nafasi au pesa, yoote mnayoongea humu,mkiingia huku mnakaa kimyaa!
 
Basic salary TGS D 567,000

Kaka usipotoshe watu, hiyo ilikuwa ya 2012/13...2013/14 ilikuwa 674,000/- na mwaka huu 2014/15 imeongezeka 10% = 741,000/- mwakani tunaingia uchaguzi mkuu..najua magamba yatajipendekeza yataongeza pakubwa. Endeleeni kupiga porojo zamkumbo mitandaoni.
 
hapa kama ulitafuta credit miaka 3 form four lazima ikupite hii....huwezi kugota kwenye 25 utakuwa above dat....shiiiida
 
Ni 741,000/- ukiachana 15% ya kutumikia profession yko, 15% kodi ya kupanga (kama huishi quoters), au 10% kama utakuwa FFU, au 15% ukipangwa upelelezi. Toa na 180,000/- lession ya kila tar15. Nimekuibia japo mshahara ni siri. Haya uamuzi niwenu.
Kipimo cha mtanzania mpiga kelele ni kumpa nafasi au pesa, yoote mnayoongea humu,mkiingia huku mnakaa kimyaa!

poti mkisha maliza mafunzo kwa profesional ya ubaharia unapangwa wap kazi?
 
Ngoja tuone maana ndio system ya siku hizi kuajiri watoto wadogo ili wawabuluze tu kwani wanajua mtu ambaye ni fresh from xl bado hajawa na utamaduni wa kuajiriwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom