Tangazo la ajira Jeshi la Polisi 2014/2015

Jamani hapo labda niweke wazi kidogo kuhusu ishu ya umri katika jeshi la polisi..1.vijana wanaotakiwa ni kuanzia miaka 18-25 kama tangazo linavyoonesha kwa kuwa kwa umri wa level iyo bado hawajachangamana sana na mtaani katika kuadapt new behaviours..kwaiyo ndio mana sasa hivi jeshi la polisi limebadilisha mfumo wa kuajiri kwa kufuata watu katika education institutions ili kuweza kuwa na historia nzuri ya waajiriwa wote.2.mtu anapoajiriwa na umri wa level iyo ni kuwa anakuwa hazina ya jeshi kwa muda mrefu mpaka umri wa kustaafu pasipo kuja kukaa muda mfupi kazini.lakini pia mtu wa umri huu bado anafundishika mambo mbalimbali na pia anaweza kusoma fani nyingine ndani ya ajira na kuweza kuwa na muda mrefu wa kulitumikia jeshi ndani ya fani nyingine..Napenda kutoa rai yangu kuwa wale wanaodhani jeshi la polisi sio zuri sio kweli waangie kikubwa ukumbuke kujiendeleza kielimu,nidhamu,na kuzingatia maadili mema ya kazi.kuhusu maslahi sitaki sana maswali mana kazi ya jeshi kwanza inaanzia moyoni na maana kuwa na moyo wa kutumika katika national service..nawatakia kila la heri wale wote watakaochaguliwa kujiunga na jeshi la polisi.kumbuka kuna vitengo vingi sio lazima uende lindo tena kwa wale wenye fani zao mambo sio mabaya.acha kusikiliza maoni na maneno ya mtaani.utafute ukweli.
 
Wadau,

Tangazo la ajira kwa wahitimu wa elimu ya juu (diploma,degree,etc. 2014 tu). Kwa wanaohitaji watembelee blog ya jeshi la police www.policeforce.go.tz kwa maeleza zaidi ya professional zinazohitajika na vigezo au viambatanishi wakati wa kuomba, pamoja na jinsi ya kudownload form husika. Mwisho wa application ni 31.08.2014.

ANGALIZO: Tunataka vijana wenye weledi waje huku, usije kwakuwa umekosa ajira. Uje utusaidie kulibadili jeshi upunguze haya malalamiko na laana za raia juu yetu kwa mambo wasioyaelewa kuhusu kazi hii ya lawama. Uje na moyo wote na uvumilivu wako na utayari kufanya kazi yyte ya polisi ndani ya vikosi vyetu. Lamwisho...unapokuja usimsikilize mtu..wengi utawasikia wakibeza na kukuvunja moyo lakini utakutana nao kwny interview. Binadamu ni waajabu...hayo yalitokea enzi zetu wakati tunaingia na degree zetu!

KARIBUNI SANA TUJENGE NCHI!
 
na mshahara utaangalia kiwango cha elimu au ndo yale mambo ya polisi ni polisi tuu?
 
Mshahara ni kufuata elimu yako...na zaidi kuna 15% ya kutumikia profession yako, kuna 15% ya kupanga mitaani kulipia nyumba. Ukija utayajua mengi, hadi wala rushwa utawajua, na utatambua kwanini polisi wanalaumiwa sana lakini wala hawachukii wala kujoshitukia.
 
Hayahaya vijana changamkieni hiyo fursa wake mliojaza uwanja wa Taifa kwa nafasi za watu 70 uwanja mpana ndio huo tena mshindwe kucheza na golokipa kila la kheri.
 
Polisi hata uwe na MASTERS bado utakuwa na upeo wa kijinga tu.Hawa polisi wakishavaa magwanda ufahamu wote huwapotea.
 
Baba aliniusia. Mwanangu fanya kazi zote lakini usije ukafanya kazi ya polisi. Hii ni baada ya baba kuona dhulma wanazofanya polisi dhidi ya watu wenye haki.
Umewahi kuona polisi akikata roho anavyoteseka ????ni kiashirio cha dhambi nyingi wanazokua nazo. kula na majambazi. wezi. wauaji. kumgeuzia kibao mwenye haki etc. Watangazie wasio jua madhambi yenu sio mimi na wanangu.
 
Baba aliniusia. Mwanangu fanya kazi zote lakini usije ukafanya kazi ya polisi. Hii ni baada ya baba kuona dhulma wanazofanya polisi dhidi ya watu wenye haki.
Umewahi kuona polisi akikata roho anavyoteseka ????ni kiashirio cha dhambi nyingi wanazokua nazo. kula na majambazi. wezi. wauaji. kumgeuzia kibao mwenye haki etc. Watangazie wasio jua madhambi yenu sio mimi na wanangu.

Hahahahaa..anahangaikaje mkuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom