TANESCO yatangaza mgawo wa umeme

Thanks Zitto nimekusoma hapo juu, lakini kama bado una muda kidogo wa kuwepo hapa JF basi nakuulize kidogo. Mnapokaa na Ngeleja ktk mazungumzo yenu mabli mbali mnaona kweli ana uwezo wa kufanya chochote ktk hii wizara ya nishati na madini? Na je ni nini anachosema yeye kuwa ni tatizo??
 
Sheria ya Umeme ya mwaka 2007 (tuliipitisha bungeni 2008) inaruhusu makampuni ya binafsi kuzalisha umeme na kusambaza umeme (upande wa kuzalisha tayari IPTL na Songas wanashiriki).

Tatizo la umeme wa Tanzania ni Transmission. Uwezo wetu wa kusambaza umeme ni mdogo sana na tuna gridi moja tu. Uwekezaji katika gridi hauwezi kuwa kwa sekta binafsi (serikali ilitika kuliberalise transmission pia, nakumbuka mimi na mzee cheyo tulikataa kata kata na tukafanikiwa). Serikali ilipaswa kuwa imejenga gridi mpya ya North-West gridi ili kusafirisha umeme kwenda kanda ya Ziwa mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera na Mara. Mahitaji ya umeme wa mikoa hii kwa sasa kama migodi yote ikipata umeme wa gridi ni 240MW. Kwa sasa ni mgodi mmoja tu wa Bulyanhulu ndio unapata umeme wa gridi na usio na uhakika. Hii inapelekea serikali kupaata hasara mbili.
  1. TANESCO wanakosa soko la uhakika la zaidi ya 120 MW ambapo wangeweza kuingiza zaidi ya 120bn usd kwa mwaka na hivyo kupata fedha za kusambaza umeme vijijini na mijini. Pia hii inakosesha uchumi faida ya backward linkages kati ya sekta ya nishati na sekta ya madini (backward linkage is such that a sector that gets a lot of inputs from within the country will have strong backward linkages relative to sectors that import most of their inputs from oversees). Madhara haya tunayaona hapa chini kwenye hasara ya pili;
  2. Serikali inatoa misamaha ya kodi ya mafuta kwa kampuni za madini ili zizalishe umeme wake wenyewe (importing inputs). Kwa mujibu wa ripoti ya Bomani Tanzania ilisamehe jumla ya 191bn Tshs katika kipindi cha 2005/06 - 2007/08. Hii pia ina madhara katika urari wa biashara na hata thamani ya shilingi ya Tanzania pale uzalishaji unapokuwa unaongezeka katika sekta ya madini.
Uwekezaji wa transmission line ni uwekezaji mkubwa sana lakini unawezekana. Zinahitajika kama 700m usd kujenga grid hii mpya. Hapa serikali ndipo inapotakiwa kufanya kazi sawasawa.

Lakini kuna hatua za dharura zilizotakiwa kufanywa. Mojawapo ni kuwa na mtambo wa 60MW Mwanza ambao utapunguza mzigo kwenye gridi. Zabuni zilitangazwa na TANESCO toka mwezi Aprili na wazabuni kujitokeza lakini mtambo huu utaweza kufungwa na kuanza kazi mwaka 2011. Hii inatokana na taratibu za ujenzi wa mitambo kwenye viwanda. Baada ya kupata mzabuni, itabidi kuanza sasa ujenzi wa mitambo nk.

Kwa mwono wangu, matatizo ya sasa ya mgawo hayatachukua muda mrefu sana kwani mvua zitanyesha na mitambo kurekebishwa. Hata hivyo bado tutakuwa na tatizo kubwa la kanda ya Ziwa maana hata mabwawa yazalishe at 100%, kama gridi imezidiwa haitaweza kusafirisha umeme kwenda huko. Mtambo wa 60MW Mwanza ndipo unapopata umuhimu wake kwa sasa.

Kuwalaumu TANESCO sidhani kama ni sawa. Hili ni Shirika ambalo limeharibiwa sana na mikataba mibovu ambayo sio TANESCO wenyewe waliingia. Hili ni Shirika ambalo NetGroup Solution waliliingiza kaburini na ndio kwanza limetoka.

TANESCO wamejitahidi sana kwa kadiri ya uwezo wao kushugulikia suala hili kwani wao wenyewe wanajua kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwani wanatakiwa kubreak even mwaka 2010 ili waweze kuanza kulipa mkopo waliochukua katika taasisi za fedha. Hivyo migawo hii inawaumiza na ninajua wanaumia.

Tatizo ni commitment ya serikali katika suala hili. TANESCO waliomba 312bn kwenye bajeti ili kushughulikia masuala haya ya umeme hawakupewa kitu. Tuzingatie kuwa tuna nakisi ya 155MW za umeme kutokana na IPTL kusimama kuzalisha mpaka kesi iishe na kesi bado haijaisha.

Suala la umeme lapaswa kuangaliwa katika mapana sana. Ni kweli kuwa asilimia 12 tu ya nyumba ndio zina umeme, lakini umeme sio kwa jili ya kuwasha nyumbani tu. Umeme kwenye uzalishaji wa uchumi ni muhimu sana ili walaji wa kawaida waweze kufidiwa kwa kupata umeme wa gharama nafuu.

Ninaamini kabisa kuwa kama tukiamua kuisaidia TANESCO tunaweza kulifanya Shirika hili 'champion' wa nchi yetu. Potential zote zipo. Dhamira hakuna.
Ndugu yangu Zitto Amesema ukweli, Lakini mawazo yenu yote haya na kuweka mbele masuala ya Taifa hili wote wameshindwa kutatua tatizo hili?? je hiyo agency ambayo imeundwa na serikali kwa ajili ya kurekebisha na kusambaza umeme vijijini itaweza kufanya kitu kwa hali hii?? Mimi naona Tanesco washindwa hata kuvumbua na kutatua tatizo hili?? Je sasa kama tumefika hapa hata kwa kauli ya rais kuwa hatuwezi kuwa na mgao wa umeme lakini tumekuwa nao?? Bado kuna tatizo juu ya nini kifanyike ndani ya mawazo haya yote?? Je mawazo yako wamefuata kwa kiasi gani??
 
Hili tatizo la umeme linachukua miongo mingapi kulitatua? Maana tokea niko shule ya vidudu mpaka sasa na approach miaka 40 bado lipo tu....why?

Nakwambia mimi nashindwa kuelewa lakini ni Mzee mwinyi, mkapa ndo wametufikisha hapo kwa mikataba ya hovyo hovyo.
 
Ahsante Mhe. Zitto kwa kutuweka sawa.

Hata hivyo, jawabu ni kuwa na Serikali isiyo na mafisadi na inayoepuka mikataba mibovu. Serikali itakayothubutu kutathmini upya Mikataba iliyoingiwa na mafisadi na inayotunyonya kwa hali ya juu. Hii ni lazima ifutwe, na ikiwezekana mafisadi waliotuingiza ktk mikataba hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.

Tusipodhibiti mafisadi, hata transmission lines kuhakikisha Tanzania Magharibi na Lake Zone wanapata umeme wa National Grid zitakwamishwa. Pesa zote zitaingia mifukoni mwao ili vitambi vyao viendelee kukua. Lazima vita dhidi ya mafisadi iendelee. Hakuna kulala.

Kwa mpango wa muda mrefu (Long-Term Plan), ni lazima Serikali ifufue Mradi wa Stieglars' Gorge katika Mto Rufiji ambao miaka ya 1974 mpaka 1979 ulitathminiwa na Norad (Norway) lakini ukasahaulika tulipokumbwa na maamuzi ya Mwalimu Nyerere kukataa miradi ya IMF na World Bank. Maporomoko ya Stieglars' Gorge yana maji mengi sana kwa mwaka mzima, na unaweza kuyaona hayo maji pale Mkapa Bridge unapokwenda Mkuranga yakiingia baharini bila kutuzalishia umeme.
 
Last edited:
Sheria ya Umeme ya mwaka 2007 (tuliipitisha bungeni 2008) inaruhusu makampuni ya binafsi kuzalisha umeme na kusambaza umeme (upande wa kuzalisha tayari IPTL na Songas wanashiriki).

Tatizo la umeme wa Tanzania ni Transmission. Uwezo wetu wa kusambaza umeme ni mdogo sana na tuna gridi moja tu. Uwekezaji katika gridi hauwezi kuwa kwa sekta binafsi (serikali ilitika kuliberalise transmission pia, nakumbuka mimi na mzee cheyo tulikataa kata kata na tukafanikiwa). Serikali ilipaswa kuwa imejenga gridi mpya ya North-West gridi ili kusafirisha umeme kwenda kanda ya Ziwa mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera na Mara. Mahitaji ya umeme wa mikoa hii kwa sasa kama migodi yote ikipata umeme wa gridi ni 240MW. Kwa sasa ni mgodi mmoja tu wa Bulyanhulu ndio unapata umeme wa gridi na usio na uhakika. Hii inapelekea serikali kupaata hasara mbili.
  1. TANESCO wanakosa soko la uhakika la zaidi ya 120 MW ambapo wangeweza kuingiza zaidi ya 120bn usd kwa mwaka na hivyo kupata fedha za kusambaza umeme vijijini na mijini. Pia hii inakosesha uchumi faida ya backward linkages kati ya sekta ya nishati na sekta ya madini (backward linkage is such that a sector that gets a lot of inputs from within the country will have strong backward linkages relative to sectors that import most of their inputs from oversees). Madhara haya tunayaona hapa chini kwenye hasara ya pili;
  2. Serikali inatoa misamaha ya kodi ya mafuta kwa kampuni za madini ili zizalishe umeme wake wenyewe (importing inputs). Kwa mujibu wa ripoti ya Bomani Tanzania ilisamehe jumla ya 191bn Tshs katika kipindi cha 2005/06 - 2007/08. Hii pia ina madhara katika urari wa biashara na hata thamani ya shilingi ya Tanzania pale uzalishaji unapokuwa unaongezeka katika sekta ya madini.
Uwekezaji wa transmission line ni uwekezaji mkubwa sana lakini unawezekana. Zinahitajika kama 700m usd kujenga grid hii mpya. Hapa serikali ndipo inapotakiwa kufanya kazi sawasawa.

Lakini kuna hatua za dharura zilizotakiwa kufanywa. Mojawapo ni kuwa na mtambo wa 60MW Mwanza ambao utapunguza mzigo kwenye gridi. Zabuni zilitangazwa na TANESCO toka mwezi Aprili na wazabuni kujitokeza lakini mtambo huu utaweza kufungwa na kuanza kazi mwaka 2011. Hii inatokana na taratibu za ujenzi wa mitambo kwenye viwanda. Baada ya kupata mzabuni, itabidi kuanza sasa ujenzi wa mitambo nk.

Kwa mwono wangu, matatizo ya sasa ya mgawo hayatachukua muda mrefu sana kwani mvua zitanyesha na mitambo kurekebishwa. Hata hivyo bado tutakuwa na tatizo kubwa la kanda ya Ziwa maana hata mabwawa yazalishe at 100%, kama gridi imezidiwa haitaweza kusafirisha umeme kwenda huko. Mtambo wa 60MW Mwanza ndipo unapopata umuhimu wake kwa sasa.

Kuwalaumu TANESCO sidhani kama ni sawa. Hili ni Shirika ambalo limeharibiwa sana na mikataba mibovu ambayo sio TANESCO wenyewe waliingia. Hili ni Shirika ambalo NetGroup Solution waliliingiza kaburini na ndio kwanza limetoka.

TANESCO wamejitahidi sana kwa kadiri ya uwezo wao kushugulikia suala hili kwani wao wenyewe wanajua kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwani wanatakiwa kubreak even mwaka 2010 ili waweze kuanza kulipa mkopo waliochukua katika taasisi za fedha. Hivyo migawo hii inawaumiza na ninajua wanaumia.

Tatizo ni commitment ya serikali katika suala hili. TANESCO waliomba 312bn kwenye bajeti ili kushughulikia masuala haya ya umeme hawakupewa kitu. Tuzingatie kuwa tuna nakisi ya 155MW za umeme kutokana na IPTL kusimama kuzalisha mpaka kesi iishe na kesi bado haijaisha.

Suala la umeme lapaswa kuangaliwa katika mapana sana. Ni kweli kuwa asilimia 12 tu ya nyumba ndio zina umeme, lakini umeme sio kwa jili ya kuwasha nyumbani tu. Umeme kwenye uzalishaji wa uchumi ni muhimu sana ili walaji wa kawaida waweze kufidiwa kwa kupata umeme wa gharama nafuu.

Ninaamini kabisa kuwa kama tukiamua kuisaidia TANESCO tunaweza kulifanya Shirika hili 'champion' wa nchi yetu. Potential zote zipo. Dhamira hakuna.

Kwa kuongezea, kwa nini serikali imeingia kwenye mikataba na IPTL, RICHMOND etc. kwa mfano pesa za richmond za mkataba $172million ( three years contract) zingeweza kununua mitambo mipya 3 ya 100MW toka GE/ROLL ROYCE/ DRESSALAND/SIEMENS etc. bahati nzuri nafanya kazi kati ya hizo kampuni hapa Ohio, gharama ya mtambo (equipment only ya 100 MW ni 30-35million) ukiongeza installation cost , shipping etc ambayo ni 25-75% ya cost ya equipment. utaona kwamba mtambo mmoja ni kati ya 50-60 million mpaka kuwashwa. juzi juzi tu Tanesco wametangaza tender ya 100MW kwa gharama ya $120million, hizi pesa zingetosha kununua mitambo 2 ya 100MW. miezi kama miwili niliongea na classmate wangu tuliyekuwa naye Colombia university ambaye anafanya kazi roll-royce internation kaniambia kuna jamaa wanaitwa noor oil ya waharabu na wahindi wamepeleka bid ya hiyo tender kwa kutumia jina la roll royce kwa haraka haraka nikamwambia huyo classmate wangu kwamba mbona hawa jamaa ni wale wa richmond wanakuja kwa sura nyingine, kwa hiyo tunasubiri tender itoke kwa kweli safari hii tutatumia international lawyer kuwafikisha hawa noor na tanesco kwenye international court ya corruption. haiwezekani mtambo wa 100mw ambao gharama yake ni 50-60million wanunue kwa 120million.
 
Josh Michael,

Umenikumbusha kitu Rais kikwete aliwahi kusema mgao wa umeme utakuwa historia, je anaweza kurudia maneno hayo???
 
Mkuu nimepata matumaini kwamba mme wabaini hao waarabu na wahindi wa richmond wanakuja kwa jina tofauti. Naomba muwe makini ili tuwadhibiti. Hawa tanesco hapo ndo utajua ni wezi na ufisadi tu kama mitambo inapatikana kwa $60m na wao wana tangaza tender kwa $120m huu si wizi??
 
Yaani ndio hapo mimi napatwa na kigugumizi cha kufa mtu yaani huwa nashikwa na hasira kabisa kuona vitu vya ajabu kama Tanzania
 
Kwa kuongezea, kwa nini serikali imeingia kwenye mikataba na IPTL, RICHMOND etc. kwa mfano pesa za richmond za mkataba $172million ( three years contract) zingeweza kununua mitambo mipya 3 ya 100MW toka GE/ROLL ROYCE/ DRESSALAND/SIEMENS etc. bahati nzuri nafanya kazi kati ya hizo kampuni hapa Ohio, gharama ya mtambo (equipment only ya 100 MW ni 30-35million) ukiongeza installation cost , shipping etc ambayo ni 25-75% ya cost ya equipment. utaona kwamba mtambo mmoja ni kati ya 50-60 million mpaka kuwashwa. juzi juzi tu Tanesco wametangaza tender ya 100MW kwa gharama ya $120million, hizi pesa zingetosha kununua mitambo 2 ya 100MW. miezi kama miwili niliongea na classmate wangu tuliyekuwa naye Colombia university ambaye anafanya kazi roll-royce internation kaniambia kuna jamaa wanaitwa noor oil ya waharabu na wahindi wamepeleka bid ya hiyo tender kwa kutumia jina la roll royce kwa haraka haraka nikamwambia huyo classmate wangu kwamba mbona hawa jamaa ni wale wa richmond wanakuja kwa sura nyingine, kwa hiyo tunasubiri tender itoke kwa kweli safari hii tutatumia international lawyer kuwafikisha hawa noor na tanesco kwenye international court ya corruption. haiwezekani mtambo wa 100mw ambao gharama yake ni 50-60million wanunue kwa 120million.

Shukran kwa maelezo mazuri sana. Tender ya TANESCO ilitangazwa katika magazeti ya kimataifa kwa kampuni zinazojenga mitambo na sio middlemen. Hivyo hao NOIT hata wafanyeje hawawezi kupata. Sasa na wewe nawe kwa nini hukushauri kampuni unayofanyia kazi ibid?

TANESCO hawakutangaza bei ya kununua. Wao walisema wanataka mtambo mmoja wa 100MW na mwingine 60MW. Bei itatokana na wazabuni waliomba, atakaetoa bei nzuri na mtambo imara ndie anapaswa kupata. Bei bado na sio taratibu za tenda kusema ninanunua kwa bei hii, sasa zabuni haitakuwa na maana.

Hebu niambie, katika hiyo kampuni yako inachukua muda gani kuanzia order mpaka commissioning?

Mwisho - umezungumzia fedha za Richmond zingeweza kununua mitambo kadhaa. Lakini hatukulipa hizi fedha kwa Richmond. Tuliwapa advance ya 30m usd halafu tukakatana katika charges. Mpaka mkataba wa Dowans unavunjwa tulikuwa tunawadai 8m usd zilizobaki.

Kama katika vitambulisho - serikali haikai na 172m usd na kusema mkataba huu pesa hizi, hapana. Serikali haina pesa zilizokaa kwa kuchotwa. Huwa zinalipwa kidogokidogo kutokana na makusanyo ya kodi, Hivyo mkataba wa Richmond ulikuwa umesambazwa over 2 years na zile 172m usd zilikuwa zilipwe over 2 years kutokana na kiwango cha umeme tulichokuwa tunanunua. Nadhani umenielewa!
 
Mkuu nimepata matumaini kwamba mme wabaini hao waarabu na wahindi wa richmond wanakuja kwa jina tofauti. Naomba muwe makini ili tuwadhibiti. Hawa tanesco hapo ndo utajua ni wezi na ufisadi tu kama mitambo inapatikana kwa $60m na wao wana tangaza tender kwa $120m huu si wizi??

Sahihisho dogo tu - Noor Oil (NOIT) ni kampuni nyingine ambayo inamilikiwa na raia wa Qatar na Russia (katika kampuni hii CCM wana hisa 5%). Kampuni hii inajadiliana na serikali kujenga bomba la mafuta kwenda Mwanza na Kigoma.
Nadhani ndugu yangu amechanganya habar hii ya bomba la mafuta kwani Richmond waliwahi kupewa zabuni hii wakashindwa na wakanyanganywa mwaka 2004. Kwa hiyo tusiwachanganyi hawa.

Taarifa ya kwamba wameomba kusupply mitambo ya umeme TANESCO ni lazima tuzifanyie kazi maana watakuwa wanacheza umiddle men ambao umezuiwa na sheria. Asante kwa taarifa ngoja nizichimbe
 
Shukran kwa maelezo mazuri sana. Tender ya TANESCO ilitangazwa katika magazeti ya kimataifa kwa kampuni zinazojenga mitambo na sio middlemen. Hivyo hao NOIT hata wafanyeje hawawezi kupata. Sasa na wewe nawe kwa nini hukushauri kampuni unayofanyia kazi ibid?

TANESCO hawakutangaza bei ya kununua. Wao walisema wanataka mtambo mmoja wa 100MW na mwingine 60MW. Bei itatokana na wazabuni waliomba, atakaetoa bei nzuri na mtambo imara ndie anapaswa kupata. Bei bado na sio taratibu za tenda kusema ninanunua kwa bei hii, sasa zabuni haitakuwa na maana.

Hebu niambie, katika hiyo kampuni yako inachukua muda gani kuanzia order mpaka commissioning?

Mwisho - umezungumzia fedha za Richmond zingeweza kununua mitambo kadhaa. Lakini hatukulipa hizi fedha kwa Richmond. Tuliwapa advance ya 30m usd halafu tukakatana katika charges. Mpaka mkataba wa Dowans unavunjwa tulikuwa tunawadai 8m usd zilizobaki.

Kama katika vitambulisho - serikali haikai na 172m usd na kusema mkataba huu pesa hizi, hapana. Serikali haina pesa zilizokaa kwa kuchotwa. Huwa zinalipwa kidogokidogo kutokana na makusanyo ya kodi, Hivyo mkataba wa Richmond ulikuwa umesambazwa over 2 years na zile 172m usd zilikuwa zilipwe over 2 years kutokana na kiwango cha umeme tulichokuwa tunanunua. Nadhani umenielewa!

Kutengeneza 100MW mpaka commissioning inachukuwa miezi 3-12 inategemea na order zilizopo. Pia kwa taarifa zako nilikuwa na President wa GE Gas turbine division, kwa sasa hivi wanazo mitambo za 100MW kama mitano (Lm6000=50mw wanazo 6) na LM100=100MW miwili kuna kampuni ambazo walicancel order baada ya financial crisis. Pia Roll Royce wanazao kama 7 ziko Oklahoma mpya kabisa zinasubiri kufanyia testing tu. mtambo mpya tunaweza kukaa nayo miaka 30-40.

======================================================================
TANESCO yaomba bilioni 312/- serikalini

2nd June 2009

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashidi.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limewasilisha maombi serikalini kutaka lipewe Sh. bilioni 312 katika mwaka huu wa fedha wa 2009/2010 ili liweze kukamilisha ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme wa dharura katika miji mbalimbali nchini kabla ya mwisho wa Juni mwakani. Hatua hiyo ya Tanesco ilibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk. Idris Rashidi, mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ilipokutana na menejimenti ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam jana. "Tanesco imeomba kiasi kisichopungua Sh. bilioni 312 katika mwaka huu wa 2009/10 ili kukamilisha miradi hii ya dharura. Inashauri fedha hizo zitolewe kwa wakati ili kazi iweze kumalizika kabla ya mwisho wa Juni 2010," alisema Dk. Rashidi. Hata hivyo, alisema maombi yao makubwa kwa sasa, ni kupatiwa Euro 24989159 (Sh. bilioni 44.23) kwa ajili ya kununulia majenereta mapya 12 yatakayotumika kuzalisha umeme katika miji ya Kasulu na Kibondo iliyoko mkoani Kigoma, Loliondo (Arusha) na Sumbawanga (Rukwa) na kusisitiza kuwa iwapo serikali itatoa fedha hizo haraka katika kipindi hicho, hadi ifikapo Juni mwakani watakuwa wamefunga jenereta zote.
Alisema ili kudhibiti upungufu wa umeme unaotarajia kutokea katika kipindi cha mwaka huu wa 2009/10, Tanesco wametangaza kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa Megawati 100 jijini Dar es Salaam. Dk. Rashidi alisema gharama za ujenzi wa kituo hicho zinakadiriwa kuwa dola za Marekani milioni 120 (Sh. bilioni 161) na kuongeza kuwa serikali imeombwa kutoa fedha hizo ili kuiwezesha Tanesco kukijenga. Alisema kituo kingine cha kuzalisha umeme wa kutumia mafuta wa Megawati 60, kinatarajiwa kujengwa mkoani Mwanza, ambacho alisema si tu kwamba, kitaongeza upatikanaji wa umeme, lakini kitaongeza umeme wa uhakika katika Kanda ya Ziwa, ambako hivi sasa mitambo iliyopo yenye uwezo wa Kilovoti 220 imezidiwa nguvu.
Dk. Rashidi alisema kituo hicho hivi sasa kimezidiwa uwezo kwa asilimia 10 na kwamba, njia nyingine ya kuzalisha umeme kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga, inatarajiwa kujengwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2014, ambapo gharama za ujenzi wake zinatarajiwa kufika dola za Marekani milioni 80 (Sh. bilioni 107). Awali, alisema katika mwaka wa fedha wa 2008/09 Bunge liliidhinisha zitolewe fedha kwa ajili ya kununua majenereta 17 yatakayotumika kuzalisha umeme katika miji ya Kigoma, Loliondo, Kasulu na Kibondo na Sumbawanga. Alisema mchakato wake ulikamilika Januari 2009, ambapo kampuni ya M/s Zwart Techniek ilipewa kazi hiyo kwa kipindi cha miezi 15 kwa mkataba wenye thamani ya Euro 33,618,863 (Sh. bilioni 59.5). Hata hivyo, alisema ni Euro 8,629,704 ndizo zilizotolewa na serikali.
 
Last edited:
Kutengeneza 100MW mpaka commissioning inachukuwa miezi 3-12 inategemea na order zilizopo. Pia kwa taarifa zako nilikuwa na President wa GE Gas turbine division, kwa sasa hivi wanazo mitambo za 100MW kama mitano (Lm6000=50mw wanazo 6) na LM100=100MW miwili kuna kampuni ambazo walicancel order baada ya financial crisis. Pia Roll Royce wanazao kama 7 ziko Oklahoma mpya kabisa zinasubiri kufanyia testing tu. mtambo mpya tunaweza kukaa nayo miaka 30-40.

Safi sana. Ninawajulisha TANESCO ili tuone jinsi ya kutatua tatizo la Mwanza kwanza. PM address details zako na za huyo President wenu. Nakutana na TANESCO next week kwenye kamati kupitia hesabu zao na kupata maelezo ya madhara ya ule mgawo wa mwanzo. Naomba hizo details haraka tafadhali tuokoe nchi yetu.

Katika hali ya kawaida inachukua mwaka, katika hii ambayo watu wamecancel order inachukua muda gani kufunga na kuwasha?
 
Sahihisho dogo tu - Noor Oil (NOIT) ni kampuni nyingine ambayo inamilikiwa na raia wa Qatar na Russia (katika kampuni hii CCM wana hisa 5%). Kampuni hii inajadiliana na serikali kujenga bomba la mafuta kwenda Mwanza na Kigoma.
Nadhani ndugu yangu amechanganya habar hii ya bomba la mafuta kwani Richmond waliwahi kupewa zabuni hii wakashindwa na wakanyanganywa mwaka 2004. Kwa hiyo tusiwachanganyi hawa.

Taarifa ya kwamba wameomba kusupply mitambo ya umeme TANESCO ni lazima tuzifanyie kazi maana watakuwa wanacheza umiddle men ambao umezuiwa na sheria. Asante kwa taarifa ngoja nizichimbe

the U.S. firm Richmond and Canada’s Energem, a consortium made up of Qatar’s Noor Oil and the Russian firms Stroytransgas and Zakneftegaz owned by the Armenian Senik Gevorgyian has said it intends to build an oil pipeline stretching from Dar Es Salaam to the cities of Mwanza and Kigoma, as well as a refinery with a capacity of 200,000 bpd.
 
Kutengeneza 100MW mpaka commissioning inachukuwa miezi 3-12 inategemea na order zilizopo. Pia kwa taarifa zako nilikuwa na President wa GE Gas turbine division, kwa sasa hivi wanazo mitambo za 100MW kama mitano (Lm6000=50mw wanazo 6) na LM100=100MW miwili kuna kampuni ambazo walicancel order baada ya financial crisis. Pia Roll Royce wanazao kama 7 ziko Oklahoma mpya kabisa zinasubiri kufanyia testing tu. mtambo mpya tunaweza kukaa nayo miaka 30-40.

======================================================================
TANESCO yaomba bilioni 312/- serikalini

2nd June 2009

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashidi.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limewasilisha maombi serikalini kutaka lipewe Sh. bilioni 312 katika mwaka huu wa fedha wa 2009/2010 ili liweze kukamilisha ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme wa dharura katika miji mbalimbali nchini kabla ya mwisho wa Juni mwakani. Hatua hiyo ya Tanesco ilibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk. Idris Rashidi, mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ilipokutana na menejimenti ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam jana. “Tanesco imeomba kiasi kisichopungua Sh. bilioni 312 katika mwaka huu wa 2009/10 ili kukamilisha miradi hii ya dharura. Inashauri fedha hizo zitolewe kwa wakati ili kazi iweze kumalizika kabla ya mwisho wa Juni 2010,” alisema Dk. Rashidi. Hata hivyo, alisema maombi yao makubwa kwa sasa, ni kupatiwa Euro 24989159 (Sh. bilioni 44.23) kwa ajili ya kununulia majenereta mapya 12 yatakayotumika kuzalisha umeme katika miji ya Kasulu na Kibondo iliyoko mkoani Kigoma, Loliondo (Arusha) na Sumbawanga (Rukwa) na kusisitiza kuwa iwapo serikali itatoa fedha hizo haraka katika kipindi hicho, hadi ifikapo Juni mwakani watakuwa wamefunga jenereta zote.
Alisema ili kudhibiti upungufu wa umeme unaotarajia kutokea katika kipindi cha mwaka huu wa 2009/10, Tanesco wametangaza kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa Megawati 100 jijini Dar es Salaam. Dk. Rashidi alisema gharama za ujenzi wa kituo hicho zinakadiriwa kuwa dola za Marekani milioni 120 (Sh. bilioni 161) na kuongeza kuwa serikali imeombwa kutoa fedha hizo ili kuiwezesha Tanesco kukijenga. Alisema kituo kingine cha kuzalisha umeme wa kutumia mafuta wa Megawati 60, kinatarajiwa kujengwa mkoani Mwanza, ambacho alisema si tu kwamba, kitaongeza upatikanaji wa umeme, lakini kitaongeza umeme wa uhakika katika Kanda ya Ziwa, ambako hivi sasa mitambo iliyopo yenye uwezo wa Kilovoti 220 imezidiwa nguvu.
Dk. Rashidi alisema kituo hicho hivi sasa kimezidiwa uwezo kwa asilimia 10 na kwamba, njia nyingine ya kuzalisha umeme kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga, inatarajiwa kujengwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2014, ambapo gharama za ujenzi wake zinatarajiwa kufika dola za Marekani milioni 80 (Sh. bilioni 107). Awali, alisema katika mwaka wa fedha wa 2008/09 Bunge liliidhinisha zitolewe fedha kwa ajili ya kununua majenereta 17 yatakayotumika kuzalisha umeme katika miji ya Kigoma, Loliondo, Kasulu na Kibondo na Sumbawanga. Alisema mchakato wake ulikamilika Januari 2009, ambapo kampuni ya M/s Zwart Techniek ilipewa kazi hiyo kwa kipindi cha miezi 15 kwa mkataba wenye thamani ya Euro 33,618,863 (Sh. bilioni 59.5). Hata hivyo, alisema ni Euro 8,629,704 ndizo zilizotolewa na serikali.

Kituo ndio kina gharama hizo na sio mitambo. Katika tenda dokumenti bei haitajwi kwani wanaomba kusupply hutaja bei zao na mnunuzi huchagua amba bei ya chini na mtambo bora au mtambo bora na bei ikawa juu. Umenipata? Hiyo 120m usd ni gharama za mradi mzima!
 
Safi sana. Ninawajulisha TANESCO ili tuone jinsi ya kutatua tatizo la Mwanza kwanza. PM address details zako na za huyo President wenu. Nakutana na TANESCO next week kwenye kamati kupitia hesabu zao na kupata maelezo ya madhara ya ule mgawo wa mwanzo. Naomba hizo details haraka tafadhali tuokoe nchi yetu.

Katika hali ya kawaida inachukua mwaka, katika hii ambayo watu wamecancel order inachukua muda gani kufunga na kuwasha?

Kama GE wanazo tayari itachukuwa mwezi mmoja au miwili kufungwa na kuwashwa.
 
the U.S. firm Richmond and Canada’s Energem, a consortium made up of Qatar’s Noor Oil and the Russian firms Stroytransgas and Zakneftegaz owned by the Armenian Senik Gevorgyian has said it intends to build an oil pipeline stretching from Dar Es Salaam to the cities of Mwanza and Kigoma, as well as a refinery with a capacity of 200,000 bpd.

Richmond ndugu yangu hawamo. Huyu mwandishi alichanganya tu. Wao ndio walipewa mwaka 2004 wakashindwa.NOIT sasa ni Qatarians, Russians and CCM!

Thanks alot for very prompt responses and your sources backing your arguments. Impressed!
 
wakati mwingine bongo kunatia hasira kweli, huu umasikini wa umeme kukatika katika sijui hili tatizo kama litaisha.
 
Safi sana. Ninawajulisha TANESCO ili tuone jinsi ya kutatua tatizo la Mwanza kwanza. PM address details zako na za huyo President wenu. Nakutana na TANESCO next week kwenye kamati kupitia hesabu zao na kupata maelezo ya madhara ya ule mgawo wa mwanzo. Naomba hizo details haraka tafadhali tuokoe nchi yetu.

Katika hali ya kawaida inachukua mwaka, katika hii ambayo watu wamecancel order inachukua muda gani kufunga na kuwasha?

Just for curioristy, Zitto umekuwa msemaji wa TANESCO?
Maana nilitegemea kama mwenyekiti wa kamati uwaweke kwenye kitimoto kwa nini tunapata migao ya umeme kila wakati, na uwaulize wana mpango gani kututoa kwenye hali hiyo. Majibu ya historia hayana maana. Kama Netgroup au akina Baruany Luhanga waliboa hiyo imepita. Menejimenti ya sasa hivi wanatakiwa kuwajibika kwa sababu waliichukua hiyo kazi wakijua kuna walioharibu huko nyuma. Tuache kuwatafutia excuse watu. Sasa hivi hapa ukiharibikiwa luku wanakufungia luku mpya halafu unaanza kufuatilia ili uingie kwenye system na uweze kununua umeme. Just imagine mteja inabidi afuatilie ili aingizwe kwenye system aweze kununua umeme. Wao TANESCO hawajali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom