Tanesco Mngesubiri Watu Wajiandae Waende Makazini Angalau, Mnakata Umeme Mtu Akiwa na Mapovu Bafuni Wazee...?

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
1,959
2,179
Hata salamu sitoi.

Kiukweli hii sio sawa aisee mmeamua kutushindisha bila ya umeme na kutulaza bila ya umeme sawa haina shida, ila kwa asubuhi angalau mgekuwa mnakata japo saa 2 kamili wazee.

Kuna sehemu zina baridi na watu wanatumia heater kuoga, sasa mtu ameshajipaka sabuni hata hajaanza kuondoa povu mnakata umeme, kweli...? Hii sio sawa.

Kuweni wastaarabu kidogo ratiba yenu kama skosei inasema umeme mnakata kuanzia saa 2 kamili sasa unakuta saa 1 na nusu sharp mnatukatia umeme, wakati mtu yupo bafuni anajiandaa ili aende kwenye majukumu ya kila siku ya ujenzi wa Taifa letu, kwa hili wazee naomba mlitazame kwa kina sio sawa hata kidogo, narudia.

SIO SAWA HATA KIDOGO WAZEE.
 
" Mimi ni mtu mzima Nina akili ndiyo maana nimetoka,
mambo ya kuniletea ushauri kwenye bata unanifanyia makosa " 😳😳😳😳😳
 
Jina umechagua mwenyewe.

Anyways.. ukioga afu ukaenda kazini wakakata Umeme unaenda kufanya Nini?
Generator ipo kiongozi...! Lakini istoshe sio kila kazi inahitaji umeme kiongozi vipi kama mtu ni dereva wa Uber, Bajaj au bodaboda n.k...?
 
Watanzania acheni kuendekeza usingizi kwani mshahara wake ni ndoto tu, amkeni mapema kabla ya muda wa kuondoka umeme!
Mzee kama nimeamka saa 1 na nahitajika kuingia ofisini saa 2 na ofisi ipo ndani ya eneo ninaloishi kwa nini niamke saa 11...?

Jaribu kuepuka KUFIKIRI kwa kutumia makalio bwege wee...!
 
Back
Top Bottom