Tanesco; Hivi kuna mgao wa umeme kimya kimya?

Jamani wanajamii, hivi kwa nini tanesco wasitutangazie sisi wakazi wa Marangu, Mwika na Rombo kuwa kuna mgao wa umeme? Hii ni wiki ya tatu sasa karibia kila siku umeme unakatika kwa zaidi ya masaa 6 hadi 12. Je, hii ni hitilafu au ndo mgao wenyewe?

hili ni dili, wanazima umeme kwa makusudi bila sababu
 
ckuiz tanesco wamekua na tabia ya kukata umeme mara kwa mara sa cjui ndo mgao wakimya kimya au vp?
 
Si huko tu ndugu yangu kwani kuna tatizo kubwa sana hata maeneo ya geita. Umeme unakatika mara kwa mara na wakati mwingine kwa muda mrefu tu! Ni tatizo ambalo limekuwepo kwa muda sasa kwanini zaidi ya mwezi mzima. TANESCO hawatatangaza kwa sababu tatizo haliko Dar es Salaam. Hivi ndivyo Tanzania yetu ilivyo kwani haki za mteja haziheshimiwi kwa namna yoyote ile na ndo maana huwasikii hao TANESCO wakisema chochote.
Dar es salaam pia wanakatakata bila mpangilio,kwahiyo ni kotekote.
 
moshi mjini toka asubuh mpaka sa hizi hakuna umeme, juzi mchana na usiku kucha kulikuwa hakuna umeme na hali hii inakaribia kufikisha mwezi sasa, nadhani kuna mh. Ameleta majenereta anataka afanye biashara fastafasta
 
KIGAMBONI .....mji teule!!!! Balaaa tupu!! Tangia jana asubuhi mapaka sahiv navyo post hapa..ni giza,maji tabu,cmu kuchaji shida...
 
...heshima mbele ma-kamanda...
J'mosi ya leo kama inavyofahamika ni siku ambayo tulikuwa tunaisubiri kwa hamu na shahuku kubwa... wanachama,wapenzi na makamanda wote wa CDM,popote pale ktk aridhi hii ya Tanganyika tulikuwa tumekaa mkao wa kushudia uzinduzi wa kampeni za mgombea wetu wa CDM LIVE kutoka Arumeru...wakuu kama badiko linavyo-someka hapo juu,jiji la CHADEMA(Mwanza) hivi sasa liko gizani tangu asubui saa 3:30...wanachama,wapenzi na Watanganyika wote wenye matumaini mkubwa na chama hiki kilichobeba matumaini ya ukombozi wa kweli wa wanyonge,tuko ktk si-ntofaham tukijiuliza je tutaweza vipi kuöna huo uzinduzi wa ukombozi wa nduguzetu wa Arumeru?...any way si kitu sana coz hatutawaöna live lakini "CHADEMA IKO NA ITABAKI LIVE MIYONI MWETU"...KILA LA KHERI MUNGU AWATANGULIE...PiiiiiiiiPoooooozzzz
 
Hiyo wanajisumbua tu ujumbe wa kutojionea unaenea haraka zaidi kuliko , watu mpaka sasa miyoni mwao wanaona umati mkubwa huku hotuba nzuri zeneye ujasiri zikilindima
 
TUONDOLEE UCHIZI WAKO! Mbona mi nipo morogoro na hakuna uchaguzi na umeme hakuna?
WW usiwe mvivu wa kufikiri!! Tumia hata upeo wa mtoto mdogo kufikiria hata kwa sekunde 2 tu.
Star Tv walitangaza kurusha matangazo ya ufunguzi wa kampen kule Arumeru, watanzaina sehemu mbalimbali wanatega macho yao kwenye tv zao ili waone kinachojir, tanesco wanakata umeme tutaonaje?
Tatizo lako ww nalifahamu, ila najitolea kukusaidia
 
...heshima mbele ma-kamanda...
J'mosi ya leo kama inavyofahamika ni siku ambayo tulikuwa tunaisubiri kwa hamu na shahuku kubwa... wanachama,wapenzi na makamanda wote wa CDM,popote pale ktk aridhi hii ya Tanganyika tulikuwa tumekaa mkao wa kushudia uzinduzi wa kampeni za mgombea wetu wa CDM LIVE kutoka Arumeru...wakuu kama badiko linavyo-someka hapo juu,jiji la CHADEMA(Mwanza) hivi sasa liko gizani tangu asubui saa 3:30...wanachama,wapenzi na Watanganyika wote wenye matumaini mkubwa na chama hiki kilichobeba matumaini ya ukombozi wa kweli wa wanyonge,tuko ktk si-ntofaham tukijiuliza je tutaweza vipi kuöna huo uzinduzi wa ukombozi wa nduguzetu wa Arumeru?...any way si kitu sana coz hatutawaöna live lakini "CHADEMA IKO NA ITABAKI LIVE MIYONI MWETU"...KILA LA KHERI MUNGU AWATANGULIE...PiiiiiiiiPoooooozzzz

Na matangazo ya Tanesco hujasoma kuwa kuna ukarabati unafanyika? au umeshindwa kupiga namba yao na kuuliza nini kinaendelea. Piga namba hii, wacha kelele: 0222194400
 
Hii imenisikitisha sana, nimewahi kurudi home ili nipate uhondo nikiwa nimetulia, lakini hakuna umeme, ngoje nifatilie online angalau nipate highlights.
 
...heshima mbele ma-kamanda...
J'mosi ya leo kama inavyofahamika ni siku ambayo tulikuwa tunaisubiri kwa hamu na shahuku kubwa... wanachama,wapenzi na makamanda wote wa CDM,popote pale ktk aridhi hii ya Tanganyika tulikuwa tumekaa mkao wa kushudia uzinduzi wa kampeni za mgombea wetu wa CDM LIVE kutoka Arumeru...wakuu kama badiko linavyo-someka hapo juu,jiji la CHADEMA(Mwanza) hivi sasa liko gizani tangu asubui saa 3:30...wanachama,wapenzi na Watanganyika wote wenye matumaini mkubwa na chama hiki kilichobeba matumaini ya ukombozi wa kweli wa wanyonge,tuko ktk si-ntofaham tukijiuliza je tutaweza vipi kuöna huo uzinduzi wa ukombozi wa nduguzetu wa Arumeru?...any way si kitu sana coz hatutawaöna live lakini "CHADEMA IKO NA ITABAKI LIVE MIYONI MWETU"...KILA LA KHERI MUNGU AWATANGULIE...PiiiiiiiiPoooooozzzz
inahusiana vipi na kampeni za Arumeru? kwani Star Tv hawana generator? hivi wewe kazi yako ni kufagilia CHADEMA ? huna kazi nyingine ? familia yako inaishi je au wewe kula kulala nini?
 
Hivi kuna uhusiano wowote umeme kukatika Mwanza, Morogoro, na sehemu zingine za Tanzania na uchaguzi wa Arumeru? Hivi mgao wa umeme Tanzania umeanza leo?
 
Back
Top Bottom