Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Hivi sasa siyo tena habari, kuona maeneo kadhaa ya nchi, yakiwa yako gizani, kutokana na mgao wa umeme, ambao ni "endless" bila ya TANESCO kutoa taarifa za mapema, kuwa kutakuwa na mgao wa umeme katika maeneo hayo husika!
Nyinyi watu wa TANESCO hebu jaribuni kufikiria, hizo hasara kubwa mnazotusababishia sisi wananchi, kutokana na kukata kwenu umeme kusiko na ratiba maalum.
Hebu nyinyi watu wa TANESCO, jaribuni kuvaa viatu vyetu sisi wananchi na kufikiria mitaji mingapi ya mabilioni ya pesa, inayoangamia Kila siku, kutokana na kukata kata kwenu umeme, kusiko na ratiba maalum?
Shirika lenu ni la kutoa huduma, hivyo pale ambapo wananchi, haturidhishwi na huduma zenu, sisi wananchi, inatubidi tulalamike.
Kwani mnashindwa nini kutoa ratiba ya ukataji wa umeme katika maeneo husika?
Nyinyi TANESCO mshukuruni sana Mungu, shirika lenu lipo Tanzania, lenye wananchi wasiojua haki zao za msingi na wapole wa kupitiliza.
Mimi naamini kuwa kama shirika lenu, lingekuwa lipo kwenye nchi nyingine, ambako wananchi wake wanajitambua na kuzijua haki zao za msingi wateja, shirika lenu, lingefilisika, kutokana na madai ya wateja wenu, kufidiwa kutokana na uzembe wenu wa kuwakatia umeme, bila ratiba maalum!
Hivi siyo nyinyi TANESCO, mwaka Jana tu, mlikuwa mkituambia sisi wananchi, kuwa mgao wa umeme uliokuwa ukiendelea hapa nchini, unatokana na mabwawa hayo yanayozalisha umeme kukauka?
Sasa Mungu naye kawaheleleza, amemwaga mvua ya El-Nino ya kufa mtu, hadi mabwawa yetu yote yamejaa hadi kutapika!
Msivyo na haya machoni kwenu, mmebadilisha "story" sasa hivi mmekuja na kutueleza kuwa, mgao huu wa umeme, unatokana na miundombinu ya TANESCO kuwa ni chakavu!
Nyinyi TANESCO mmeungana na chama tawala cha CCM, kututesa sisi wananchi, Kwa kutoa ahadi zosizotekelezeka Kila leo za alifu lela ulela, ya kuwa, suala la kukatika umeme, litakuwa historia ndani ya nchi yetu!
Hizo "sound" mmekuwa mkitoa, tokea mimi nasoma shule ya msingi, miaka mingi sana ya nyuma!
Nadhani sisi wananchi tunapaswa sasa kusema, enough is enough, tuwapige chini nyinyi TANESCO na "wabia" wenu wa CCM, katika chaguzi zijazo, kutokana na kuwa nyinyi ni waongo sugu, mnaopenda kutoa matumaini Kwa wananchi, ambayo hayapo!
Nimewasikia mara kadhaa, nyinyi TANESCO mkijigamba kuwa, mradi wa umeme wa Bwawa la Nyerere, ukikamilika, basi hili suala la kukatika katika, umeme katika nchi hii, litakuwa ni suala la historia!
Hiyo siyo ahadi ya kwanza, kutolewa na kiongozi wa CCM, kutokana na kero ya kukatika umeme, kwa kuwa nakumbuka zaidi ya miaka 10 ya nyuma, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati wa wakati huo, alinukuliwa na vyombo vya habari akinena, kuwa mradi mkubwa wa Bomba la gesi kutoka Mtwara, ukikamilika, basi tuhesabu kuwa mateso yanayotokana na kero ya kukatika Kwa umeme, itakuwa ni historia katika nchi yetu!
Hivyo "vichekesho" tushaanza kuvizoea sisi wananchi kwenye masikio yetu, kutokana na viongozi wetu, kutuona sisi wananchi wa nchi hii ni wajinga na malofa tunaoweza kudanganywa miaka yote!