Elections 2010 Tamko rasmi la Dr. Slaa kuhusu CCM kustisha midahalo TBC

You sound a bit like a comedian broda!...!

Hapo nimecheka mpaka basi, maana unatusaidia kushangaa malimwengu ya MAKAMBA!
Ndugu yangu huyo mtu wenu nadhani anatokea sayari mpya ya Kleptomaniac!...huh!
Wewe MTU WA PWANI UNAONEKANA NI MWANAMAGEUZI KABISA ILA UNAHOFIA MACHO NA MANENO YA WAYAHUDI!
Achana nao hao SISIEM broda, hamia hii ng'ambo ya pili ili upambanue mambo kwa akili!...huh!

nna wasi wasi kuna mambo chama wameyaona na nnaamini hawataki wayaanike hadharani for sake of our chama sio mbaya.

mm si mnafiki kama wanachadema nikiona kuna jambo kwenye chama changu hayako sawa nnasema

mm ni mtu huru
 
That's why I like you mtu wa pwani ... ila punguza matusi mzee wangu.
Naona siku hizi una hasira sana na Dr Slaa, sijui kakukosea nini wewe binafsi.
 
Nadhani CCM ina hoja, sema tu tumekataa kusikiliza "' Stephen Convey" Anasema "Seek first to understand before beeing understood";

Sasa mumeamua kukurupuka tena bila ku-seek tu understand - CHADEMA you real have problems you guys.
 
Kama ingelikuwa uwezo wa kukariri ngonjera na kutapika mbele za watu kwa staili ya mdahalo ndio kigezo cha kuwa kiongozi wa watu basi kiongozi wa kwanza angekuwa Shehe Mtopea, Rev. Mtikila n.k Ila Uongozi una vigezo vingi kama vile uadilifu, ukweli, elimu, kukubalika na watu , mapenzi yako kwa watu. JEE TUKIANDAA MDAHALO SUALA LAKO LA NDOA LIKIULIZWA UTALIJIBU!!!!! . Tusubiri Oktoba 31 ndio siku ya mdahalo mzuri.

Tutalinda kura zetu mchezo wenu wa wizi tumeshautengenezea mkakati. HAPO NDIPO MTAJUA ATHARI ZA UCHAKACHUAJI POLENI
 
nadhani ccm ina hoja, sema tu tumekataa kusikiliza "' stephen convey" anasema "seek first to understand before beeing understood";

sasa mumeamua kukurupuka tena bila ku-seek tu understand - chadema you real have problems you guys.

jina lako ni problem "kasheshe"
 
Kweli binadamu ataendelea kuwa dhaifu daima....

Tanzania ya sasa ambao tunasema technology iko chini unatuletea rais wa darasa la saba (makamu wa rais) ... no CHADEMA no CHADEMA you are playing with us... you are not serious either... no no no.
 
nna wasi wasi kuna mambo chama wameyaona na nnaamini hawataki wayaanike hadharani for sake of our chama sio mbaya.
mm si mnafiki kama wanachadema nikiona kuna jambo kwenye chama changu hayako sawa nnasema
mm ni mtu huru

Mtu wa pwani, it is simple... assume ww ni mgombea wa CCM, ambaye hata sio mbunge wa kipindi kilichopita (Incumbent MP); kawaida kwenye mdahalo you need to be in the same level... thus huwezi kuambiwa hujaleta maji wakati haukuwa mbunge... hope you get it... Leo hii tunamhukumu Kikwete kwenye kura za Urais kwa kuwa alikuwepo 5 years ago... and he needs to defend kwa nini alishindwa x, y, z... the other thing is ... Mdahalo needs not to zomea au etc... angalia kipindi cha Adam Simbeye... TBC1 hoja tupu hakuna makofi au kuzomea etc...

Hoja kama hizi zinanikumbusha upuuzi mmoja unaitwa tume huru... na definition ya kwamba tume huru ni ile yenye composition ya representation ya vyama... to me tume huru ni ile yenye wataalamu tupu and we don't need to know unatoka chama gani.

So I could have been happy TBC1 waandae vipindi vyao,,, maswali yaulizwe but hakuna haja ya kuwa kama vile kuna representation ya vyama kwa wale walioko benchi.. i think they don't even needs to put on their party uniforms.
 
Kweli binadamu ataendelea kuwa dhaifu daima....

Tanzania ya sasa ambao tunasema technology iko chini unatuletea rais wa darasa la saba (makamu wa rais) ... no CHADEMA no CHADEMA you are playing with us... you are not serious either... no no no.

Kwani katiba inasema awe ana kisomo kiasi gani? kwani katiba ikoje?
 
Kwani katiba inasema awe ana kisomo kiasi gani? kwani katiba ikoje?

Swali lako nitalijibu baada ya ww kujibu kwa nini dereva wa Serikali anatakiwa kuwa form six!!! na dereva huyo say ni wa halimashauri ya Kibondo.

Please no constitution in the world has limited us to use common sense....
 
Ha ha haaa! Kasheshe bwana!

Mwaka huu mtanyolewa tu, tena bila maji.
 
Swali lako nitalijibu baada ya ww kujibu kwa nini dereva wa Serikali anatakiwa kuwa form six!!! na dereva huyo say ni wa halimashauri ya Kibondo.

Please no constitution in the world has limited us to use common sense....
Swali halijibiwi kwa swali. Toa jibu usichanganye mada hapa. Mimi sijauliza sheria inasemaje kuhusu ajira ya dreva na elimu yake, nimeuliza kuwa je katiba katika hili la mgombea mwenza ime set level ya education iwe darasa la ngapi? Wacha kukimbia swali kama kilaza bwana Kasheshe
 
Kimsingi ni fedheha. lakini kwa kuwa hawana hoja mpya kwa watanzania; ndo maana wameona ni vyema kusepa.
 
Kasheshe,
Mkuu wangu utanisaidia sana kuelewa kwa nini dereva wa gari la serikali anatakiwa kuwa form six..Mimi simo ktk ubishi wenu isipokuwa tu nachofahamu mimi CCM wameacha kujihusisha na midahalo kwa sababu itamlazimisha JK kupambana na Dr.Slaa mwishoni. Wakiweza kuepuka hilo sasa hivi itasaidia kukwaza mawazo ya wananchi kusema JK amekwepa....

Na bahati mbaya wengi wanatazama hapa karibu zaidi na kuweka sababu lakini dunia ya leo midahalo ni LAZIMA kwa wagombea wake na ndio hayo maswala ya elimu (ktk kuelimika)ya wagombea inapoweza kupimwa vizuri ktk mzani.
 
Swali lako nitalijibu baada ya ww kujibu kwa nini dereva wa Serikali anatakiwa kuwa form six!!! na dereva huyo say ni wa halimashauri ya Kibondo.

Please no constitution in the world has limited us to use common sense....

Mkuu Kasheshe,

Kila kazi ina sifa za muombaji ambazo huwa zinaainishwa kwenye tangazo la nafasi ya kazi. Pia tangazo hilo hutoa majukumu ya mtu huyo iwapo atapewa hiyo nafasi. Sifa za waombaji wa nafasi hiyo huandaliwa na mtoa ajira. So, serikali ya CCM ndiyo ambayo iliona kwamba dereva anatakiwa awe na elimu ya kidato cha sita.

Serikali hiyo hiyo ya CCM imekuwa ikigoma kubadilisha katiba. Katiba ndio inatoa sifa za mwombaji wa kazi ya Urais, Ubunge, Udiwani, n.k. Pia Katiba hiyo hiyo ndio inaainisha majukumu ya Mbunge na Bunge, pia majukumu ya Rais. Kwenye kipengele cha elimu, sifa ya muombaji wanasema anatakiwa AWE ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA, bila kujali kama alimaliza darasa la 7 au alisoma ngumbalo. Ndiyo maana ukipitia majina ya wagombea Ubunge wa CCM wengine hawakumaliza hata darasa la 7.

Hapo wa kulaumiwa ni nani? Kama CCM inaona kwamba Makamu wa Rais hawezi kuwa na elimu ya darasa la 7, wakubali kubadilisha katiba.

Kama unakumbuka vizuri kuna kipindi kulikuwa na hoja kwamba mgombea Urais angalau awe na elimu ya Chuo Kikuu, ndipo hapo Mrema alipokimbilia kwenda kusoma ile degree yake akaenda kutunukiwa nyumbani kwake Sinza. Baada ya hapo sijasikia tena mjadala wa swala la elimu ya mgombea Ubunge au Urais.

Common sense ingeanzia kwenye Serikali ya CCM kukubali kubadilisha Katiba. Katiba ndio mama wa yote, anything ambacho ni Unconstitutional, ni batili hata kama kina common sense. Pia kumbuka kuna common sense nyingine haziko common kwa wote. Ndio maana kwa wengine ushoga ni haki ya msingi na wengine wanasema NO, mwisho wa siku wataenda kwenye Katiba ili waweze ku-determine kama ni constitutional or unconstitutional.
 
This is a PLUS to CHADEMA. Thus, the weakness should be used in explaining the true colours of ccm to wananchi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom