Elections 2010 Tamko rasmi la Dr. Slaa kuhusu CCM kustisha midahalo TBC

Mdahalo ni ngumu. Mathalani Jimbo fulani miaka mitano iliyopita shida kuu ilikuwa ni maji, hadi sasa hukuweza kuwaletea maji, unarudi unawaahidi wakikuchagua tatizo la maji litakuwa historia, Je unafikiri hao wanaoelezwa hivyo wakipewa fursa ya kuuliza maswali majibu yatapatikana?

LAKINI MBONA HILI HALIWASUMBUI CCM HATA SIKU MOJA. Hujamsikia Mh Kikwete anaahidi upya kabisa kama vile hakuwahi kuahidi! Wanaweza wakarudia ahadi zile zile na wakapamba kidogo kwamba mambo yote yalikuwa kwenye mchakato naam kipindi cha pili ni utekelezaji! Hawa ni vilaza tu, hata hawajui madhara ya kujitangaza kujitoa kwenye midahalo
 
Kama ingelikuwa uwezo wa kukariri ngonjera na kutapika mbele za watu kwa staili ya mdahalo ndio kigezo cha kuwa kiongozi wa watu basi kiongozi wa kwanza angekuwa Shehe Mtopea, Rev. Mtikila n.k Ila Uongozi una vigezo vingi kama vile uadilifu, ukweli, elimu, kukubalika na watu , mapenzi yako kwa watu. JEE TUKIANDAA MDAHALO SUALA LAKO LA NDOA LIKIULIZWA UTALIJIBU!!!!! . Tusubiri Oktoba 31 ndio siku ya mdahalo mzuri.
Chadema wako tayari muda wowote na hilo swali lako lilishajibiwa mbona...tatizo tukuuliza ni kweli una kifafa+HIV sijui utajibu au utacheka cheka tu...
 
dsbanner.jpg

Mgombea wa urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dr. Wilibrod Slaa amesema; Uamuzi wa CCM kukataza wagombea wake kushiriki midahalo ya kisiasa ni aibu kwa mwelekeo wa demokrasia nchini. Kiongozi anayetaka nafasi ya kisiasa anayekwepa nafasi ya kuzungumza na wananchi anaotaka kuwaongoza na anataka kuwahubiria tu ni mwoga na hafai kuwa kiongozi wao. Chadema tuko tayari wakati wowote na mahali popote kujadiliana na mtu yeyote wa chama chochote.

My take: Kwanini uogope kukutana na wananchi unaowaomba kura?

Dr. Wilbrod Slaa 2010
Wakati mwingine kufanya mdahalo na mtu hana uzoefu wowote wa uongozi na mwenye uzoefu inakuwa ni kujishusha chini
 
Wakati mwingine kufanya mdahalo na mtu hana uzoefu wowote wa uongozi na mwenye uzoefu inakuwa ni kujishusha chini
Uzoefu huanzia wapi....tena kwa maoni yangu ndiyo sehemu ya kuchukulia pointi...au hawa kujiandaa, kupanga watu wakupiga simu na kuuliza maswali kama wavyofanya kwa kikwete alipo kuwa akiulizwa maswali ya moja kwa moja kupitia TBC...
 
Tatizo huwezi kufananisha siasa za maerekani na hapa bongo, vyama vya huko angalau vina uwiano sawa
sasa huku huyu katawala miaka 30 huyu mwingine loo,. jitahidini tu, hamna hadhi ya kufanya midahalo na ccm kwa sasa
 
Nadhani CCM ina hoja, sema tu tumekataa kusikiliza "' Stephen Convey" Anasema "Seek first to understand before beeing understood";

Sasa mumeamua kukurupuka tena bila ku-seek tu understand - CHADEMA you real have problems you guys.

listen to yourself brother ,you're trimping !
you cant ignore the importance and the power of debate
 
Wakati mwingine kufanya mdahalo na mtu hana uzoefu wowote wa uongozi na mwenye uzoefu inakuwa ni kujishusha chini

is debate for those who run for the office.
If you're best good for you , don't run away .....wicked and weak are those who afraid
 
Tatizo huwezi kufananisha siasa za maerekani na hapa bongo, vyama vya huko angalau vina uwiano sawa
sasa huku huyu katawala miaka 30 huyu mwingine loo,. jitahidini tu, hamna hadhi ya kufanya midahalo na ccm kwa sasa

Wewe naona unachanganya habari. Kwani anayekwenda kwenye mdahalo ni chama au mgombea? Yule Mama wa Ubungo ana uzoefu gani na ilihali ndio anagombea ubunge kwa mara ya kwanza? Mama Buriani ana uzoefu katika kugombea ubunge zaidi ya ule wa viti maalum ambao ni wa kubebwa? Chama kutawala miaka mingi haimaanishi kwamba wanachama wake nao wanakuwa wazoefu. Mbona kuna vijana wengi tu wamewaangusha wazee kwenye kura za maoni ndani ya CCM? Kama swala ni uzoefu basi Mzee Malecela, Mungai, Makweta na wengineo wangeshinda maana wamekuwa serikalini na bungeni tangu miaka ya 70 mwanzoni.

Kuweni wakweli kwamba mnaogopa maswali, mnataka mwende kuhubiria watu bila kuulizwa maswali. Halafu baadaye mkae vikao vya ndani kupanga mikakati ya kuchakachua matokeo ili mshinde. Mwaka huu ngoma nzito.

Sehemu zote ambazo JK ameulizwa maswali ameshindwa kujibu na kama kuna sehemu amewajibu, kesho yake kibao kilibadilika. Sasa amebaki na sera moja ya kumwaga ahadi za uongo kwa kuwa mwaka 2005 alikuwa anauza sura tu, mwaka huu amegundua watu hawaangalii tena sura yake, wanataka mtendaji atakaye tekeleza ahadi zake kwa vitendo na siyo porojo na kucheka cheka tu.
 
Sidhani kama unazungumza kisomi, anyway nakumbuka 1995 midahalo ilikuwapo, tatizo la CCM siyo kuwa hawana uzoefu kinaongozwa na wazee wasiotaka mabadiliko wao wanataka kutumia mbinu zile zile za tangu TANU bila kujaribu mpya, kama na wewe unaungana nao nitakuwa na wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri.
 
kwahhiyo kwenu nyinyi mdahalo ndio kila kitu?
 
unazungu mzia usomi mkuu, sidhani kama unanafasi hapa, kama mimi nsihitaji mdahalo na ninafanya kampeni zangu na sera zangu zina uzika unalazimisha mdahalo wa nini? kwani ni lazima?
 
kwahhiyo kwenu nyinyi mdahalo ndio kila kitu?

Mkuu wangu mbona unaanza kuhamisha goli? Wewe si ulisema kwamba CCM haiwezi kufanya mdahalo na vyama ambavyo havina uzoefu? Kuna mahali nilisema kwamba kwa wapinzani mdahalo ni kila kitu?

Kama wapinzani wangekuwa wanategemea mdahalo tu, wangekuwa wamebweteka bila kupiga kampeni ili wasubiri mdahalo.

Lengo la mdahalo, ni kupima hoja za wagombea namna watakavyoshughulikia matatizo ya jimbo husika. Mfano, jimbo lina shida ya walimu, maji, soko la mazao, huduma za afya, na mengineyo. Je, hao wagombea wakichaguliwa watafanya nini?

Wewe unatetea mfumo wa watu waende kwenye mkutano wa Kampeni, wahubiriwe sera bila kuuliza hizo sera zitatekelezwa vipi? Mfano mtu anasema nitaboresha elimu, how? Kikwete, juzi akiwa Handeni kasema ataboresha malisho ya mifugo, how?

Hizo sera zako kama zinauzika na zinakubalika, kwanini uogope kwenda kwenye mdahalo? Naona mkuu unaanza kuji-contradict wewe mwenyewe, maana naona mara unarukia hili ukibanwa unahama unakimbilia angle nyingine.

The bottom line ni kwamba mdahalo utawa-expose wagombea wa CCM na ndio maana Makamba amesema NO. Hiyo ilikuwa ni baada ya Mama wa Ubungo kuchemsha halafu yule mgombea wenu wa Vunjo nae alionekana kuchemsha. Ili kuzuwia michemsho, Makamba ndo akaja na hiyo mpya kwamba hakuna kushiriki mdahalo. Kama sera za CCM zinauzika na zinakubalika, si mkaziuze kwenye mdahalo, mnaogopa nini?
 
Nadhani waliuona ule mdahalo wa arusha mjini wakafyata jinsi mgombea wa chadema alivyokuwa amejipanga. Subirini kidogo mtasikia zengwe jingine tena linakuja kuwa chadema ni kikundi cha uasi kutokana na mavazi yao ya magwanda
 
Takwimu zinaonyesha wabunge ambao walikuwa mabubu Bungeni ndio walitekeleza vizuri ilani zao na wanarudishwa bungeni... this says what about debate... that it really doesn't matter a lot to Tanzanians.
 
unazungu mzia usomi mkuu, sidhani kama unanafasi hapa, kama mimi nsihitaji mdahalo na ninafanya kampeni zangu na sera zangu zina uzika unalazimisha mdahalo wa nini? kwani ni lazima?

Mdahalo siyo lazima, lakini unapokwepa kwenda kwenye mdahalo maana yake ni kwamba hujiamini, hivyo unaogopa kuwa exposed. Pia kutoshiriki mdahalo ni kuwanyima fursa wapiga kura kuweza kujua mgombea yupi ambaye ni bora kuliko wengine.

Najua hapa kwetu Tanzania hatujafikia kwenye stage ya ku-rate midahalo, lakini mwisho wa mdahalo lazima watu watakuambia mgombea fulani ali-shine na mgombea fulani alipwaya, au alishindwa kujieleza kwa ufasaha namna atakavyoshughulikia kero za wananchi jimboni mwake.
 
Common sense ingeanzia kwenye Serikali ya CCM kukubali kubadilisha Katiba. Katiba ndio mama wa yote, anything ambacho ni Unconstitutional, ni batili hata kama kina common sense. Pia kumbuka kuna common sense nyingine haziko common kwa wote. Ndio maana kwa wengine ushoga ni haki ya msingi na wengine wanasema NO, mwisho wa siku wataenda kwenye Katiba ili waweze ku-determine kama ni constitutional or unconstitutional.

Niko na wewe ndugu,

Lakini kama Serikali ya CCM imechemka na chama makini kama CHADEMA... no.... tuna matatizo waTanzania, hakuna namna yoyote ya ku-justify standard seven kuwa Rais wa Nchi.... please understand makamu wa Rais ni Rais.... STOP and THINK guys.

NI UPUUUZI CHADEMA WAMEFANYA TENA WA MCHANA KABISA...
 
Takwimu zinaonyesha wabunge ambao walikuwa mabubu Bungeni ndio walitekeleza vizuri ilani zao na wanarudishwa bungeni... this says what about debate... that it really doesn't matter a lot to Tanzanians.

No relation at all ,maswali ya debate hayaitaji genus kujibu .
Of course ni haki ya mwananchi kuuliza maswali na the one run for the office ana wajibu wa kutoa maelezo.
Sote tunajua CCM wanachoogopa ni kuulizwa kuhusu utekelezaji wa ahadi za nyuma .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom