Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
- Thread starter
- #81
Sidhani kama huo ndiyo ulikuwa umuhimu wa kikao hiki cha juu kabisa katika CCM, na kikao cha kwanza kwa mwaka mpya 2011.
Mara nyingi umuhimu wa tamko au waraka wo wote, unaonekana kwa kiasi gani muda au nafasi imetumika kujadili hilo suala. Ukiangalia na kuchambua tamko hili la CCM CC, utaona kuwa kwa mpangilio, wametumia:
Maneno 472 kuzungumzia Chadema na u-Meya Arusha
Maneno 193 kuzungumzia Sherehe za CCM
Maneno 171 kuzungumzia vurugu na vifo vya Arusha
Maneno 115 kuzungumzia umoja wa vyama vya ukombozi
Maneno 104 kuzungumzia malipo ya Dowans (bila kutaja tatizo la umeme nchini)
Maneno 100 kuzungumzia semina ya wabunge wa CCM. (Agizo kwa wabunge lilitolewa siku 3 KABLA ya kamati Kuu kukaa)
Maneno 65 kuzungumzia migomo/mitafaruku vyuoni.
Nini ambavyo havikuzungumziwa wala kutajwa hata neno moja:
Utekelezaji wa ahadi za JK na CCM kwa mwaka 2011 na miaka ijayo
Katiba
Uchumi wa nchi
Elimu
Afya
Barabara, Reli, Umeme na Miundombinu yote
Usalama wa Raia na Nchi.
mkuu uchambuzi umetulia