.[/FONT]
3. UCHAGUZI WA MEYA MANISPAA YA ARUSHA
Kwa kuzingatia kwamba umekuwepo upotoshaji mkubwa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha, na hata kusababisha malalamiko mengi na vurugu, Kamati Kuu inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:-
Kwanza:
· Matokeo ya Udiwani Manispaa ya Arusha yalikuwa ifuatavyo: Madiwani wa Kata: CCM 10, CHADEMA 8 na TLP 1 Jumla viti 19.
· Madiwani Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.
· Wabunge Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.
Matokeo ya jumla: CCM Viti 16, CHADEMA 14 na TLP 1. Jumla Viti 31.
Pili:
Siku ya kupiga kura (tarehe 18/12/2010) Mkutano ulipoanza wajumbe 14 wa CHADEMA hawakuwepo. Waliofika ni wajumbe 16 wa CCM na 1 wa TLP, jumla wajumbe 17 ambao ni zaidi ya nusu ya wajumbe wanaotakiwa ili mkutano uwe halali kwa mujibu wa sheria.
Katika mazingira haya Msimamizi wa Uchaguzi aliendesha uchaguzi ambapo Ndugu Gaudence Vicent Lyimo wa CCM alipata kura 17, hivyo kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Umeya na Ndugu Michael Kivuyo wa TLP alipata kura 17 na kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Naibu Meya.
Kwa hiyo wanaosema uchaguzi huo haukuwa halali ama hawajui sheria au wanajiingiza tu katika ushabiki wa kisiasa.
Tatu:
CHADEMA wanadai katika wale wajumbe 16 wa CCM, mmoja wao (Mhe. Mary Chatanda) hakuwa mjumbe halali kwa kuwa katika kugombea Ubunge wa Viti Maalum aligombea kupitia Mkoa wa Tanga.
CHADEMA, kupitia Msimamizi wa Uchaguzi waliomba ufafanuzi wa kisheria kutoka Tume ya Uchaguzi, Katibu wa Bunge na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Ofisi zote hizo tatu zilitoa jibu kwamba Mhe. Mary Chatanda alikuwa mjumbe halali wa kikao hicho, na kwamba Wabunge Viti Maalum ni Wabunge wa Kitaifa na vyama vyao ndivyo vinawapangia Halmashauri za kufanyia kazi. Mhe. Mary Chatanda anaishi Arusha akifanyakazi kama Katibu wa CCM wa Mkoa huo hivyo CCM ilimpangia hapo hapo Arusha ndipo afanyie kazi za Halmashauri kama Diwani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa iliarifiwa kuhusu uamuzi huu kama sheria inavyotaka.
Ni ufafanuzi huo huo ndio CHADEMA waliutumia kushinda kiti cha Halmashauri ya Hai baada ya kuwapangia kufanyakazi katika Halmashauri hiyo Wabunge 2 wa Viti Maalum na ambao si wakaazi wa Wilaya hiyo. Kura hizo mbili ndizo ziliwapa CHADEMA ushindi; na CCM tumekubali matokeo kwa kuwa kwa kufanya hivyo CHADEMA hawakuvunja sheria.
Uhalali wa Mhe. Mary Chatanda kupiga kura Manispaa ya Arusha ni sawa sawa na uhalali wa Wabunge wawili wa Viti Maalum wa CHADEMA walivyopiga kura Hai.
Jambo hili CHADEMA wanalijua vizuri lakini wanapotosha umma kwa makusudi wakitumia vyombo vya habari ambavyo bila kufanya utafiti navyo vimekuwa vinashabikia suala hili.
Kwa kifupi Kamati Kuu inasisitiza kwamba Uchaguzi wa Meya wa Arusha ulifuata sheria kwa ukamilifu, na washindi walishinda kihalali na hakuna sababu ya kurudia kufanya uchaguzi mwingine. Iwapo kuna watu hawaridhiki na mchakato wa uchaguzi huo wanayo nafasi ya kupinga katika vyombo vya sheria bila ya kufanya fujo wala kuleta uvunjifu wa amani kama ule uliotokea tarehe 5/1/2011 kule Arusha.
Bila bias kidogo wamejieleza kwa busara na kufafanua mambo bila jazba....Wale vijana wa ccm jana waliniudhi sana.
Utadhani walitoka chooni!!!!
Ila hii kamati kuu bado hawajaonyesha nia ya kuwakomboa wananchi na mzigo wa umeme uliopo....
Hawa tatizo kubwa wanakosa washauri wa kuwaambia wananchi wanataka nini!!!!
Kama wangemaliza tatizo la mgawo wa umeme na ku maintain garama za umeme na gas nadhani wananchi wasingelalamika wala kuona tatizo la kuheshimu hukumu ya mahakama ya kimataifa ya biashara..
Sasa kuna haja gani ya kutumia hela zetu kulipa wezi ambao mpaka sasa umeme hatuna na garama zinapanda kila siku??
Hili ndilo litakalosababisha maandamano nchi nzima.