hili la kufanyia mikutano ya chama ikulu ni sawa na matumizi ya magari ya serikali wakati wa kampeni yaliyokemewa na msajili wa vyama vya siasa. nadhani sasa ni wakai mzuri wa kumwomba mh. tendwa akemee na hili pia.
halafu nimeona wameitisha maandamano ya mshikamano na mikutano ya hadhara nchi nzima kuwashukuru wanachi kwa kukipigia kura chama. mikutano ya namna hiyo na maandamanano ya vyama vya upinzani yamepigwa marufuku mara kadhaa na jeshi la polisi likiwamo tukio la arusha la hivi karibuni kutokana na taarifa za kiintelijensia kuwa kuna dalili za uvunjifu wa amani. hivi haya ya ccm hakuna taarifa za kiintelijensia kama hizo? afande mwema yuko wapi afafanue hapa please.
ama kweli kutawala wanachi wapole kama watanzania raha sana!
JF Great thinkers vipi tena? CC ya CCM wamekuja na hoja na utetezi mzito wenye nguvu! nyinyi mnabaki kuponda picha zao na ukumbi waliofanyia kikao chao! sasa huu sio uungwana! kama mna hoja tofauti na wao toeni hapa tuzione wacheni kutuyumbisha na kupost upuuzi kila wakati! mnatupotezea muda hapa kuzisoma post za kipuuzi zisizo na source wala logic!
Sorry wana jf, Kwenye mistari ya hili tamko sijaona karipio la udini! Au kw CC ya ccm hii antagonism ya viongozi wa dini is not a big deal but an important propagandistic weaponry aspect?
Kila tunaposema kwamba Rais Rostam Aziz anaogopwa bala ndani ya CCM watu hamsikii!!!! Na mbele ya huyu mtu Watanzania tusitegemee jema lolote lile.Sasa naanza kuamini R.A & co. wanaendesha hii nchi.
Sorry wana jf, Kwenye mistari ya hili tamko sijaona karipio la udini! Au kw CC ya ccm hii antagonism ya viongozi wa dini is not a big deal but an important propagandistic weaponry aspect?
Mle ndani watakaokuwa wamekuelewa mle japo kidogo ni Mzee Makamba peke yake ambaye ndio mara moja moja hugusa Biblia na kuchagua japo kimstari panapo haja.Ipo hadithi ninayoipenda kusoma kwa kuirudia rudia sana ndani ya biblia,ambayo ilihusu watoto wawili wa Isaka, yaani Esau na Jacob.
Esau aliiuza Ile baraka ya mzaliwa wa kwanza kwa mdogo wake Jacob kwa bakuli la dengu. Na jinsi maneno yanavyoumba, wakati baba mtu anataka kutoa baraka ile ambayo alimuandalia Esau, Jacob aliiba kitu kilichomuuzi sana Esau mpaka akafikia hatua ya kutaka kumuua mdogo wake Jacob.
Pamoja na mema yote ambayo CCM imefanya kwa miongo kadhaa, miaka michache iliyopita, kwa ridhaa yao wenyewe, kama alivyofanya Esau, wameamua kuuza mbaraka wa mzaliwa wa kwanza kwa bakuli la dengu.
Chonde chonde msije kukurupuka na kutafuta mchawi na kusahau kuwa mmeamua kuiuza baraka kwa tamaa ya mali na madaraka bila kujari matakwa ya wananchi.
Kuona jambo ambalo limekiukwa na kulinyamazia ndiko kunakopelekea mambo mengi yaende shaghalabagala nchini mwetu. Kuanzia kwenye ukiukaji wa sheria mabarabarani, ujenzi holela wa makazi na viwanda, na hata kuingia mikataba kama hii ya Dowans kwa kutokuwa makini kwa yale yaliyoandikwa kwenye mikataba hiyo.JF Great thinkers vipi tena? CC ya CCM wamekuja na hoja na utetezi mzito wenye nguvu! nyinyi mnabaki kuponda picha zao na ukumbi waliofanyia kikao chao! sasa huu sio uungwana! kama mna hoja tofauti na wao toeni hapa tuzione wacheni kutuyumbisha na kupost upuuzi kila wakati! mnatupotezea muda hapa kuzisoma post za kipuuzi zisizo na source wala logic!
Mbona hawakujadili jinsi watakavyotekeleza zile ahadi za JK wakati wa kampeni? Katiba? Hali ya uchumi wa nchi? Huduma za jamii zilizodorora?
Hicho kikao utadhani cha Democratic Party, yaani chama kisicho madarakani na kilichofutika kwenye ramani ya siasa.
CCM is a dying horse. There's nothing good that can be expected from these guys and their demise is imminent. Time will tellInaonekana CCM wana kiburi sana, hizi taarifa wapeane kwenye chama chao. Wananchi wa Tanzania wanategemea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa tamko kuhusu Vurugu za Arusha , malipo kwa Dowans nk. mambo yao ya kichama wapeane huko huko kwao. Serikali inafanya makosa kwa kutegemea Wanaharakati kufanya kazi ambayo wametumwa na wananchi, hivi wanafahamu maana ya Serikali kweli au ni kanyaga twende tu?