Tamko la Chama Cha Walimu(CWT)

walimu hawatakaa walipwe haki zao woga na uduni wa kufikiri umewatawala!hakuna mgomo unaweza kuruhusiwa na mahakama hata siku moja! mkiamua kupiga kunji piga mwanzo mwisho habari ya mahakamani achaneni nayo! CWT na Mukoba wameshafyata mkia na kuagiza walimu warudi kazini tena naishauri serikali iwashitaki kwa kuitisha mgomo mbuzi! mnatia aibu walimu!wafanyakazi hakuna haja kuitisha mambo ya mahakama tukilianzisha tulianzishe kavukavu mahakama ni huko mbele ya safari,. yaani mnategemea serikali na mahakama viwaruhusu kugoma au kuandamana>????
 
Chama Cha Walimu Tanzania-CWT-kimetangaza kusitisha rasmi mgomo wa walimu na hivyo kuwataka walimu wote nchini kurejea kazini mara moja kuanzia leo ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku kama kawaida.

Akitoa tamko la CWT kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kukiagiza Chama hicho kitoe maelekezo kwa wanachama wake kurudi kazini, Rais wa Chama hicho GRATIAN MUKOBA amesema walimu wanarudi kazini wakiwa wamekata tamaa kutokana na hukumu hiyo.

Amefafanua kuwa walimu wanaporudi kazini bila kuwa na mawazo yaliyotulia, utendaji wao utaathirika hivyo Chama kinatoa wito kwa Serikali kukutana na CWT kwa haraka ili kuendeleza majadiliano ya Madai mapya ya Walimu.

Kuhusu kulipa fidia ya hasara waliyoipata wanafunzi, Chama hicho kimesema kinasubiri taarifa rasmi ya Serikali kuhusu hasara hiyo kwa kuwa hakina uwezo wa kufahamu hasara waliyoipata wanafunzi.

Kwa mujibu wa Mwalimu MUKOBA wenye uwezo wa kuwasilisha hasara hiyo ni mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Serikali.

Hapo jana Chama hicho kilipongeza kauli ya Rais JAKAYA KIKWETE yakusema Serikali inajali na kuthamini mchango wa Walimu nchini"

Mytake:

Mara kwa mara nimekuwa nikiwaona viongozi wa CWT ni wasaliti na katu hawatawatoa walimu katika lindi la matatizo yao ambayo ni ya msingi mkubwa. Naamini wanaendekeza njaa maana wanayofanya hayaingii akilini kabisa.
Hebi jionee tamko lao baada ya mahakama kusitisha mgomo halafu utarajie serikali itasikiliza madai yao. Kama wangetaka suluhu kwa amani kusingekuwa na haja ya kugoma huko ni kama kumtishia nyau mkubwa.

Walimu mna kazi kweli.



 
hivi ilikuwaje wakachagua RAIS kama HUYU BOYA,NDO MAANA WAZIDI KUDHARAULIKA,WAJIHESABU WAO NI KAMA DARAJA TU AU NGAZI,HUYO JAMAA KAWADHALILISHA KWELI YAANI UKALI WOTE ULE AMEGEUKA KUWA KARATASI KTK MOTO!HATA HIVYO POLENI SANA WALIMU WANGU MJIFUNZE KUCHAGUA VIONGOZI KAMA DK ULIMBOKA JAPO NI WACHACHE,ILA SERIKALI IMESHASEMA HAIWAPENDI HATA MR DHAIFU ALISEMA HAITAJI KURA ZENU SO WHT.
 
Kwa maoni yangu, rais wa chama cha waalimu ndg. Gratias Mkoba na kaimu katibu mkuu mwl. Oluoch wanapaswa kujihuzuru kwa kuandaa mgomo ambao kwa tafsiri yangu ulikuwa ni kiini macho, hawakuwa na dhamira ya dhati ya kuwataka waalimu wagome kwa kuishinikiza serikali kuwapa waalimu madai yao. Nina sababu zifuatazo kwa kusema haya:

1. kama viongozi waandaji wa mgomo, sikutegemea kukiukwa kwa masharti ya mgomo na hivyo kuufanya mgomo ni halari kisheria. Kitendo cha kutoa masaa 48 siku ambazo si za kazi, upigaji kura bila kuwepo afisa wa kazi, na makosa mengine yaliyoufanya mgomo uwe batili binafsi siamini kama hawakujuwa sheria ila walifanya makusudi kwa sababu zao binafsi. Naamini kabisa wanasheria wapo, wangeweza kuwatumia kwa ishu seriou kama hii kama wao ni wajinga wa sheria. Wametuzalilisha waalimu kwa kutafsiriwa kuwa mambo yetu ni ya ovyo ovyo.

2. kuwadanganya na kuwaaminisha waalim, ambao ni wanachama wao kuwa mgomo ni halari, umefuata misingi na taratibu zote za kisheri, na kwamba wasiwe na wasi wasi, kila wakati walipohojiwa katika vyombo vya habari unaonyesha kuwa viongozi hawa ni waongo na si watendaji. Waalimu watashindwa tena kuitikia matamko yao ya migomo kwa kuwa hawatakuwa na uhakika na maneno yao. wakiendelea kutuongoza kamwe mgomo wowote utakaotangazwa hautafanikiwa.

3. Uongozi wa juu wa CWT chini ya mr. Mkoba haukufanya maandalizi ya mgomo ipasavyo kwa kuwashirikisha wanachama wake wote ambao ndio wagomaji. Hakuna elimu ya uamusho iliyotolewa kwa wanachama na ndiyo maana mwitikio wa mgomo haujaweza kutikisa sana. Najuwa wadau wa elimu, hasa waalimu wenzangu mnasababu nyingine nyingi za kumfanya huyu mtu ajihuzuru.

Naomba tuziweke zitusaidie kumtoa huu jamaa, hana lolote juu ya maslahi ya waalimu.
 
kuna mambo mawili aliyo hofu
  1. msitu wa magwe pande
  2. baadhi ya walimu kuto kuunga mkono huo mgomo eg Walimu wa Kigoma
 
Siui mende kwa nyundo maana nitaumia mimi'hapo pole pole,wakija kushtuka wapo nje ya Game wote CCM na Vibaraka wao hao akina Mukoba
 
kwishney waendelee hivyo hivyo wacha wafe nayo na uwoga wao, kuna mijitu minafiki sana wanataka watu wengine wapiganie na wao wafaidi tu tena serikali ingewakata 30% kila mwalimu ili kufidia hasara mwezi huu wa nane
 
Sasa mkisha fika shule si mfundishe tu hao watoto,kama mliamua kugoma mngejipanga mfanye mgomo wa ukweli au huo wa awamu ya pili mgome mgomo wa kutikisa serikali ila kwa sasa muwafundishe tu.

utafundishaje wakati kichwa hakijatulia?? si unajua ili akili itulie lazima mambo ya mbumba na kifamilia yawe yametulia sasa huku unawaza kodi ya meza, na mahitaji mengine muhimu lazima kichwa kipate moto na matokeo yake ndio hayo.. 50+0=500 :redface:
 
Kwa maoni yangu, rais wa chama cha waalimu ndg. Gratias Mkoba na kaimu katibu mkuu mwl. Oluoch wanapaswa kujihuzuru kwa kuandaa mgomo ambao kwa tafsiri yangu ulikuwa ni kiini macho, hawakuwa na dhamira ya dhati ya kuwataka waalimu wagome kwa kuishinikiza serikali kuwapa waalimu madai yao. Nina sababu zifuatazo kwa kusema haya: 1. kama viongozi waandaji wa mgomo, sikutegemea kukiukwa kwa masharti ya mgomo na hivyo kuufanya mgomo ni halari kisheria. Kitendo cha kutoa masaa 48 siku ambazo si za kazi, upigaji kura bila kuwepo afisa wa kazi, na makosa mengine yaliyoufanya mgomo uwe batili binafsi siamini kama hawakujuwa sheria ila walifanya makusudi kwa sababu zao binafsi. Naamini kabisa wanasheria wapo, wangeweza kuwatumia kwa ishu seriou kama hii kama wao ni wajinga wa sheria. Wametuzalilisha waalimu kwa kutafsiriwa kuwa mambo yetu ni ya ovyo ovyo. 2. kuwadanganya na kuwaaminisha waalim, ambao ni wanachama wao kuwa mgomo ni halari, umefuata misingi na taratibu zote za kisheri, na kwamba wasiwe na wasi wasi, kila wakati walipohojiwa katika vyombo vya habari unaonyesha kuwa viongozi hawa ni waongo na si watendaji. Waalimu watashindwa tena kuitikia matamko yao ya migomo kwa kuwa hawatakuwa na uhakika na maneno yao. wakiendelea kutuongoza kamwe mgomo wowote utakaotangazwa hautafanikiwa. 3. Uongozi wa juu wa CWT chini ya mr. Mkoba haukufanya maandalizi ya mgomo ipasavyo kwa kuwashirikisha wanachama wake wote ambao ndio wagomaji. Hakuna elimu ya uamusho iliyotolewa kwa wanachama na ndiyo maana mwitikio wa mgomo haujaweza kutikisa sana. Najuwa wadau wa elimu, hasa waalimu wenzangu mnasababu nyingine nyingi za kumfanya huyu mtu ajihuzuru. Naomba tuziweke zitusaidie kumtoa huu jamaa, hana lolote juu ya maslahi ya waalimu.
Na wewe ni mwalimu???? kama jibu ni ndio, nawaonea huruma sana wanafunzi wetu......... no wonder wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika.
 
Hawa matapeli wanaojiita viongozi wa CWT watueleze wametumia kiasi pesa za chama kuhamisisha mgomo? Walijua tangu awali wanachofanya ni tisha toto hawakuwa na nia ya kweli zaidi ya kujinufaisha; hawa viongozi ni lazima wachunguzwe, haiwezekani eti baada ya mahakama kusitisha mgomo wao wamekimbilia kutoa taarifa walimu warudi kazini, jee hiyo haki wameshaipata?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hawa viongozi CWT ni al munafiquu.
Wamewashawishi waalimu wetu kugoma, ona sasa wamepewa barua za kujieleza ili washughurikiwe kinidhamu. WAMEWASAIDIA NINI SASA?
Walijijua sana hawana uwezo wa kimsimamo fisi maji hawa.
 
Na wewe ni mwalimu???? kama jibu ni ndio, nawaonea huruma sana wanafunzi wetu......... no wonder wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika.

Walimu wanatakiwa ajira zao zipitiwe upya, kuna mtu aliwahi kushauri wanafunzi wakifanya mtihani walimu nao wafanye mtihani huohuo pia!!"kwa ishu seriou kama hii" hilo neno sikulielewa
 
Tena Mwalimu wa Kiswahili mkuu!!!! Nafikiri lazima atakuwa kafoji vyeti huyu

Mwalimu wa kiswahili?????!!!! Khaaaaaaaaa!!!!!!! Naomba isiwe kweli jamani........ mwalimu wa kiswahili anaandika kiswahili namna hii??!!! tuna tatizo kubwa zaidi ya nilivyokuwa nafikiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom