Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012

Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka ,

Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja

Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.


Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!

Imetolewa na
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

huu ni ujumbe kutoka kwa Dr ulimboka stephen kutoka ICU!!!!
THE HERO ULIMBOKA.jpg
 
Tume itamchunzaje David (Abeid) toka ikulu??haiwezekani watapindisha tu ndio hao hao...walishajipanga kumuadhibu na kumuua Ulimboka!haitawasaidia kamwe!serikali dhaifu na waliotumwa hawana fikra nao dhaifu tu!na vibaraka!!
 
Mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?Kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?Hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?
 
Kumpiga Ulimbolk hakutatengeneza ile CT Scan kamwe!wala hawatatatua wagonjwa kulala chini,au wa 3 kitanda kimoja,vipimo kupata hospitali binafsi na kuleta tena hospitali za rufaa.....wala kuleta panado hospitali......wapinguze safari,posho semina na posho za wabunge wapeleke hospitali na sekta nyeti zingine na miundombinu sio kuua wazalendo wanaoiamsha serikali!!!!eti liwalo na liwe!shame sana hii serikali ya kidhalimu!!!ya kura za kununua na pesa za waarabu
 
Wauze magari ya Nape, Fisadi KOVa, na Ridhiwani kununulia Vitanda vya watoto wkenye wodi Muhimbili
 
David Abeid bado anaishi? inakuaje kama kweli kuna peoples power how long shall they kiil our prophets while we stand aside and look? hivi tunaakili sisi, lazima wanza kudondoshwa mmoja baada ya mwingine kuanzia leo,
 
Common, lets come to our senses...vita vya panzi furaha ya kunguru. Ubabe sio dawa ya matatizo popote pale duniani.
 
TZ naona kila mtu amekuwa msanii na mwanasiasa, hili tamko la madaktari wanajifanya wanagoma kutetea wagonjwa wakati kikubwa wanadai pesa.
Madaktari hawa hawa ndo wamesababisha vifo au ulemavu wa kudumu kwa mamia ya waTZ kwa uzembe wao au kutojali kwao harafu leo wanaleta picha kuonyesha wako na wananchi, wengine ndo wezi wa dawa hospitalini.
Hii ni mchemko tu, ngojeni ndo mtajua madai yenu na jeuri yenu si chochote.
 
safi sana madaktari unganeni kiukweli sisi tulioko uraiani tunaendelea kuwalewesha wanchi madai yenu na wanawaunga mkono...
 
Yupo Mbunge mmoja alikurupuka, akidai madaktari wanatumika kisiasa, kuonyesha kuwa Tanzania haitawaliki
 
Watawala wetu wengi hawataki kusikia ukweli. Ndo maana huhamaki sana wananchi wanapojua au kusema ukweli. Dhama za kutishana nafikiri zilikwisha muda mrefu. Badiikeni.
 
Tamko lenu nimelipenda HONGERENI SANA Madaktari ila ingekuwa vema kama pia mngetumia kuda wenu kuwaelewesha wananchi walio wengi juu ya madai yenu haya ili wakayaelewa na kuunga mkono jitihada zenu otherwise wengi wanafikiria mnadai maslahi yenu 'binafsi' ndio maana hata humu ndani wapo wanaopingana nanyi.
 
Hongereni sana madaktari. Nashauri mgomo huu udumishwe na manurse wagome. Kufanya hivyo serikali italeta fedha za EPA, madini huko uswisi, rada n.k na ukombozi wenu utadumu daima katika historia ya nchi hii.
 
  • Thanks
Reactions: 654
TZ naona kila mtu amekuwa msanii na mwanasiasa, hili tamko la madaktari wanajifanya wanagoma kutetea wagonjwa wakati kikubwa wanadai pesa.
Madaktari hawa hawa ndo wamesababisha vifo au ulemavu wa kudumu kwa mamia ya waTZ kwa uzembe wao au kutojali kwao harafu leo wanaleta picha kuonyesha wako na wananchi, wengine ndo wezi wa dawa hospitalini.
Hii ni mchemko tu, ngojeni ndo mtajua madai yenu na jeuri yenu si chochote.

*****...umemaliza kuharisha tukupe maji
 
Mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?Kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?Hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?
kichwa chenye memory ya 1kb hakiwezi kuwaelewa ma dr.
 
it is too late to kill the messenger!!the message has spread!!
 
Kamanda Msangi aliyemkamata na kumtesa Dr Ulimboka yupo katika jopo la kuchunguza nini kilimtokea Dr Ulimboka. Alipofika kumuhoji Dr Ulimboka alimwambia 'Nirudishie simu na waleti yangu'. Kamanda Msangi taratibu akatoka wodini kichwa chini.
 
Back
Top Bottom