Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
popcorn zangu zishaisha.....mshiko sina duh!!ngoja nikaushe tu hivi hivi
Tukikubali hata kinadharia kuwa chombo cha utendaji kinaweza kuanzisha na kuendesha uchunguzi dhidi ya mbunge au kundi la wabunge tutakuwa tumekubali jambo la hatari sana. Itakuwaje huko mbeleni polisi au uwt wakiona wanajadiliwa vikali bungeni wakaanzisha uchunguzi ambao utawazuia wabunge wakali kushiriki mjadala bungeni? Na vipi kama kura ya kutokuwa na imani na WM inatarajiwa kupigwa na mara wabunge kadhaa wanasombwa kusaidia uchunguzi na kuondoa wingi wa kura zinazohitajika? Tukiwakubalia kwa wabunge nani atawazuia ikija kwa majaji?
Mkuu huko sahihi, ila lazima tuliangalie hili, je ni tabia yetu kufanya hivi tunapowaona wengine wanafanya makosa? ebu ji -examine, wewe mwenyewe, ni mara ngapi huwa unaona uovu katika jamii, na mara ngapi huwa unaripoti katika mamlaka zinazohusika,
Kama siyo tabia zetu, au culture yetu, unataka Zitto aitoe wapi, tena wa Kigoma huyu, au double standard? ina-aaply kwa viongozi , na sio hata raia, ambao kesho watakuwa viongozi??
Ni mara ngapi tunaona majirani zetu wanakunywa gongo, wanavta bangi, watotot wa vijiweni, madaladala kukatisha ruti, watu kutizamiana kwenye mitihani na ku-copiana assignment n.k
Huoni unapomsema huyu mkuu unajisema na wewe na kwa mara hii, tena kwa nadra sana tunadumisha msemo wa Julius kuwa hivi ndivyo tulivyo
Zitto kutokutoa taarifa anadumisha mila na jadi yetu na kwa mara hii usiseme KWA NINI HUKUSEMA, TOA USHAURI SI NYINGINE ASEME!
aU VIONGOZI Hawa wanatoka sayari ya mars na si nji hii hii ya akina Kalunde!
You deserve to be a director of TAKUKURU nothing else! Hosea and his team are wrong,Susuviri is right!
Usipotoshe. Uchunguji ni wa muda mrefu. Umekuwa public hivi karibuni tu. TAKUKURU kimsingi chombo cha dola chini ya Ofisi ya Rais (Head of State). Head of State yupo juu ya mihimili yote mitatu. Rais kama Head of the Executive ndio mhimili mmoja. Lakini kama Mkuu wa Nchi ni mlinzi wa Katiba na sheria zilizotungwa kwa mujibu wa Katiba. Mbona Tume ya Maadili ya Viongozi inaendesha zoezi la kuchunguza mali za wabunge kwa kutuita na kutuhoji hamna kelele.
Msitetee uhalifu. Acheni tuhojiwe na kama tuna makosa tuwajibike. Hakuna visasi hapa!
Kama Zitto amethubutu kuandika hapa ukumbini kwamba "Mimi najua" kuhusiana na Wabunge kugushi risiti za kuonyesha kwamba wameenda kuhudhuria vikao ya Bunge Dodoma kwa magari yao binafsi kumbe wamepanda mabasi basi ni bora atupe ushahidi wote badala ya kupigia debe tu akina Mwakyembe waburuzwe mahakamani na yeye maovu mengine yanayofanywa na Wabunge kuliibia Taifa ambayo anayafahamu fika anataka kuyaficha. Kama na yeye alihusika na kugushi hizo risiti basi naye ajitaje kwamba pia alihusika na wizi.
Ukishakuwa Mheshimiwa lazima unyenyekee heshima ambayo wananchi wako wamekupa "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko" na ufanye kazi kwa uadilifu mkubwa na kulinda maslahi ya wale waliokupa dhamana ya kutetea maslahi yao na ya nchi yao. Ndiyo maana kuna umuhimu mkubwa wa Mheshimiwa Zitto kutueleza kwa kirefu jinsi alivyolijua hili na haoa Wabunge wanaogushi risiti na kuliibia Taifa ni akina nani. Vinginevyo itakuwa ni upigaji wa debe tu ambalo hana evidence ya aina yoyote ya kusupport kauli yake na pia hufai kuwa mheshimiwa kama maovu unayoyajua yakifanywa na Wabunge wenzio katika kuliibia Taifa unayafumbia macho.
Waberoya point hapa ni kupinga ufisadi sio swala la kufany kazi takukuru.
Muheshiwa Zitto ni mmoja kati ya WABUNGE walio mstaliu wa mbele kupinga Ufisadi.Madai aliyoyatoa ni mazito sana hasa ukizingatia yeye ni mmoja kati ya hao wabunge.
Kama utakumbuka wabunge wa Uingereza walijiuzulu kwa tuhuma tu hata zikiwa bado hazijasibitishwa.
Zitto kama mpambanaji alitakiwa asibishe madai yake haya kwa kupeleka pale Takukuru majina ya hao wanaofoji risti kujipatoia mihela ya bure nao ni ufisadi kama ufisadi mwingine mkuu
Kama huna cha kuandika kaa kimya.....! Umesikia kwenye vijiwe vya kahawa?
Naona wewe mwenzangu husomi magazeti wala huangalii TV. Hata hii hii asubuhi ya leo kwenye taarifa ya habari TBC wamesema hivyo kuwa kuakidi wito wa chombo cha dola ni kosa la jiani na adhabu yake ukikutwa na hatia ni jela miaka mitatu.
Sasa TBC ni vijiweni? Ndugu fanya research wacha longolongo.
U have no clue unabakia Nasikia, inasemekana, inasikika......! great thinker wa JF! looooh
Naona wewe mwenzangu husomi magazeti wala huangalii TV. Hata hii hii asubuhi ya leo kwenye taarifa ya habari TBC wamesema hivyo kuwa kuakidi wito wa chombo cha dola ni kosa la jiani na adhabu yake ukikutwa na hatia ni jela miaka mitatu.
Sasa TBC ni vijiweni? Ndugu fanya research wacha longolongo.
Kwanza nilazima tujiulize: je upo utaratibu uliowekwa kisheria kutumika kabla ya kuleta mashtaka dhidi ya mbunge?(haijalishi ni nani na anaweza kuwa mjukuu wa shetani!). Pili, kama upo unafuatwa wakati wote? Kama la nani anatakiwa kulalamika? Kama haupo basi matendo ya takukuru yanahalalishwa. Lakini kama tunakubali kuwa chombo cha serikali kinaweza kuja bungeni na kuchukua wabunge kadhaa (waweza kuwa rostam, selelii, chenge au kilango 4 all i care) wakidai kuwa wanaendesha uchunguzi na kuwa ati hakuna aliyejuu ya sheria basi demokrasia imetushinda. Na hapana rais hayuko juu ya mihimili mitatu. Tukikubali hilo basi tuna mfalme.

,Kwanza nilazima tujiulize: je upo utaratibu uliowekwa kisheria kutumika kabla ya kuleta mashtaka dhidi ya mbunge?(haijalishi ni nani na anaweza kuwa mjukuu wa shetani!). Pili, kama upo unafuatwa wakati wote? Kama la nani anatakiwa kulalamika? Kama haupo basi matendo ya takukuru yanahalalishwa. Lakini kama tunakubali kuwa chombo cha serikali kinaweza kuja bungeni na kuchukua wabunge kadhaa (waweza kuwa rostam, selelii, chenge au kilango 4 all i care) wakidai kuwa wanaendesha uchunguzi na kuwa ati hakuna aliyejuu ya sheria basi demokrasia imetushinda. Na hapana rais hayuko juu ya mihimili mitatu. Tukikubali hilo basi tuna mfalme.
Kwanza nilazima tujiulize: je upo utaratibu uliowekwa kisheria kutumika kabla ya kuleta mashtaka dhidi ya mbunge?(haijalishi ni nani na anaweza kuwa mjukuu wa shetani!). Pili, kama upo unafuatwa wakati wote? Kama la nani anatakiwa kulalamika? Kama haupo basi matendo ya takukuru yanahalalishwa. Lakini kama tunakubali kuwa chombo cha serikali kinaweza kuja bungeni na kuchukua wabunge kadhaa (waweza kuwa rostam, selelii, chenge au kilango 4 all i care) wakidai kuwa wanaendesha uchunguzi na kuwa ati hakuna aliyejuu ya sheria basi demokrasia imetushinda. Na hapana rais hayuko juu ya mihimili mitatu. Tukikubali hilo basi tuna mfalme.
Kaka unajua Mramba alihojiwa na kufikishwa mahakamani akiwa Mbunge? Unajua stori ya yule mbunge wa Morogoro aliyeburuzwa na Landrover la Polisi kwa madai ya Maji? Hawa nani alikuja hapa kuwatetea na kusema tawi la utendaji lisiingilie Bunge?
Kuna tatizo la msingi katika Taifa letu na katika mfumo wa Bunge. Fanya tafiti zako, ni Bunge la Tanzania tu duniani ndilo halina utaratibu wa kudhibiti mienendo ya Wabunge. Nchi nyingine wana mtu anaitwa Kamishna wa mienendo (Office of the Commissioner for standards). Huyu huchunguza mienendo na ile ambayo ni ya kijinai huenda katika jinai na ile ya kimaadili (hili la posho ninadhani ni la kimaadili) linakwenda kamati ya Maadili na kisha Bunge kutoa adhabu.
Mwaka 2004 Sheria ya maadili ilirekebishwa ili Bunge lipitishe 'code of conduct' kwa wabunge. Mpaka leo hatujapitisha. Mwaka 2008 niliwasilisha muswada binafsi ili kuunda code na kisha kuunda ofisi ya Kamishna huyu. Mpaka leo Ofisi ya Spika imekalia muswada huu na kukataa kuupeleka kuwa gazzetted ili ujadiliwe Bungeni.
Hivi MwanaKijiji unajua wabunge wanasafiri kwa mabasi kutoka Dar kuja Dodoma na wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?
Tunafanya makosa, halafu hakuna code wala mamlaka ya kutuchunguza halafu tuachiwe. Hapana. Mwanakijiji wewe kwa heshima yako hupaswi kutetea uvunjifu wa maadili.
Waache TAKUKURU wafanye kazi yao. Lazima Wabunge tujue kuwa hatupo juu ya sheria na kwamba tupo accountable na answerable kwa vitendo vyetu (for actions and inactions).
Mkuu nilivyokuelewa hapa ni kuwa TAKUKURU HAWANA KAZI YA KUFANYA, na wabunge wanaokubali kuhojiwa nao hawana kazi ya kufanya pia.