TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie!

ha ha ha .... TAKUKURU wanawafanyia interview wabunge! hiyo ni interrogation mkuu.

Kumbe umenipata; huo ndio ukweli kuwa tunaamua kutoelewa mambo yaliyo wazi kwa bias zetu kwa makusudi. Hi ndungu yangu waandishi wa habari wanapomhoji mbunge na kuweka "kiti moto" je wanafanya interview au interrogation? Hebu tuwe objective katika kauli zetu.

Kuulizwa kuhusu ulipwaji marambili malipo na kuthibitisha kama sahihi na majina yaliyopo kwenye hati za malipo ni ya mbunge mhusika, ni interview. Interrogation ni pale ambapo maelezo yako yanaweza kutumiwa kwenye mahakama ya sheria,na huwa unapewa caution ya hilo.

Mwizi asiyekuwa mzoefu ukimuuliza amebeba nini au anatoka/kwenda au umwambie unaitwa Polisi utashangaa atakavyo hamaki. Hawa wabunge wetu wanajifunza ufisadi ukubwani eventually wamegeuka kuwa wezi.

Ufisadi hua uko kwenye damu......... unachukua malipo double double Aibu .. Poor armatures!
 
Acha kuchemka, Spika 6 mwenyewe ameshawaunga mkono wabunge wenzake kwamba hiyo ni takrima tu, halafu unategemea ataunda Kamati au kutumia Kamati ya Maadili kuwahoji wenzake? Na kama akitaka kuwahoji sasa hivi kuna mtu amewakataza? Spika 6 afanye kazi yake, TAKUKURU nayo ifanye kazi yake! Then life goes on! Kama ni rushwa au la it is subject to interpretation by the court na sio kwenye magazeti!

Wewe nawe,kwa hiyo Spika Sitta kuwaunga mkono wabunge ndo ipelekee TAKUKURU wafanye kazi ya Polisi??,ya kuwashughulikia watu wanaopokea posho mara mbili..Ni vema ungejibu swali kwanza kama kitendo cha wabunge kupokea posho mara mbili(kutoka sehemu 2 tofauti) ni RUSHWA ama badala ya kukurupuka tuuu na kuanza KUBWABWAJA hapa..I shu hapa ni kwamba TAKUKURU wamechemka mbaya mno.FULL STOP
 
nilijisemeaga awali kuwa Ufisadi ni Jadi yetu na Asilimia kubwa ya Watanzania ni Mafisadi kwa namna yao, nikaambiwa nimerukkwa akili!
 
Unaamini Zitto yeye yuko msafi na hafanyi kama anavyodai wengine wanavyofanya?

Unajua siku zoe akina Julius ndio maana huwa tunapotza direction, kwasababu badala yakujadili hoja mnaanza kuwashambulia watu na kupersonalize. Zitto amempinga MKJJ kwa Hoja na wewe kama hukubaliani na Zitto njoo na hoja. Nashauri mkuu rudi kwenye mada, tuendelee kuona wapi tumekosea
 
...wanasafiri kwa mabasi kutoka Dar kuja Dodoma na wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?
...

mheshimiwa,

hizi ni tuhuma nzito sana. na kwa vile umesema "unajua" napenda kuamini umeshuhudia hili likitendeka na si mara moja bali mara nyingi kwani maelezo yako hapo juu yanaashiria kwamba huko kutiliana saini ni tabia iliyojengeka.

kwanini umekaa kimya katika hili? au katika hoja yako binafsi ulizungumzia hili na kuwataja wahusika? kama hujafanya hivyo
naamini nawe utakuwa mshiriki kwa kukaa kimya hata kama hujashiriki kwa vitendo.
 
Tukikubali hata kinadharia kuwa chombo cha utendaji kinaweza kuanzisha na kuendesha uchunguzi dhidi ya mbunge au kundi la wabunge tutakuwa tumekubali jambo la hatari sana. Itakuwaje huko mbeleni polisi au uwt wakiona wanajadiliwa vikali bungeni wakaanzisha uchunguzi ambao utawazuia wabunge wakali kushiriki mjadala bungeni? Na vipi kama kura ya kutokuwa na imani na WM inatarajiwa kupigwa na mara wabunge kadhaa wanasombwa kusaidia uchunguzi na kuondoa wingi wa kura zinazohitajika? Tukiwakubalia kwa wabunge nani atawazuia ikija kwa majaji?

Mwanakijiji nadhani kama hakutakuwa na chombo nje ya Bunge ambacho kitakuwa na mamlaka ya kuweza kuwachunguza wabunge mbalimbali wanaokiuka maadili na hata uvunjaji wa sheria kutasababisha ujengaji wa taifa ambalo halifuati misingi ya kisheria na haki kwa wote. Hii pia itaondoa nidhamu na uwajibikaji kwa viongozi wetu na hatimaye wananchi kwa ujumla. Mambo hayo yote yanaweza pia kusababisha mfumuko wa matabaka ya kijamii kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa amani na maendeleo ya nchi. Kinachotakiwa ni kuwekwa taratibu sahihi ambazo zitahakikisha wabunge au majaji hawalengwi na chunguzi ambazo zina muelekeo wa kuwanyamazisha, kuwanyanyasa au kuwavunjia haki zao za msingi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nafasi zao katika jamii za uwakilishi wa wananchi na utungaji wa sheria. Hakuna yeyote ambaye yuko juu ya Sheria, kama Dr. Mwakyembe na wabunge wengine walivunja sheria katika upataji wa malipo na ikathibitishwa kuwa walifanya hilo jambo kinyume cha sheria, nadhani ni sahihi kabisa kwa wao kuchunguzwa, kuhojiwa na hata kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
Usipotoshe. Uchunguji ni wa muda mrefu. Umekuwa public hivi karibuni tu. TAKUKURU kimsingi chombo cha dola chini ya Ofisi ya Rais (Head of State). Head of State yupo juu ya mihimili yote mitatu. Rais kama Head of the Executive ndio mhimili mmoja. Lakini kama Mkuu wa Nchi ni mlinzi wa Katiba na sheria zilizotungwa kwa mujibu wa Katiba. Mbona Tume ya Maadili ya Viongozi inaendesha zoezi la kuchunguza mali za wabunge kwa kutuita na kutuhoji hamna kelele.

Msitetee uhalifu. Acheni tuhojiwe na kama tuna makosa tuwajibike. Hakuna visasi hapa!
Huu uchunguzi wa muda mrefu wa kuchunguza Shekilango or who ever kapewa posho mara mbili ambayo sijui ni laki mbili au millioni mbili, wakati huo huo takukuru wanashindwa kufuatilia mambo ya mabillioni na yenye madhara ya muda mrefu na kuuwa uchumi kama kukosa barabara au umeme, pantoon mbovu mbovu nk nk.
Hili suala la posho mara mbili ni ukiangalia na amount involve ni more of administrative than rushwa, ni rushwa gani ambayo mtu anasainishwa na ipo public?
Rushwa ni kama zile mafisadi wanakupa then wanaficha ushahidi wa kukupa mpaka mambo yaende kinyume na walivyo tarajia.
Lakini hili la posho , ambapo vitabu vya mahesabu vinapitiwa na wakaguzi , na kesho na kesho kutwa mtu mwingine ataviona utaiita ni rushwa?
Hili lilikuwa linatakiwa kushughulikiwa na mashirika husika wakishirikiana na ofisi ya bunge na kuwataka wahusika kama inabidi warudishe na serikali itoa waraka kuwakumbusha wahusika walipaji na wapokeaji wasifanye hivyo, linapo ingiza forgery then Polisi ndio wanatakiwa kuingilia.
Ama sivyo kuna tatizo kubwa saana la kutafsiri nini ni rushwa, impact ya tatizo hilo katika society, na kiasi kilicho husika.
 
Wewe umejuaje wanafanya haya yote? Ni mmoja wapo?

Mkuu nakumbuka tulipokuwa tunafanya mitihani, unauwezo wa kuona walioingia na madesa, wanatazamia n.k, kujua kuwa fulani au watu fulani wanafanya makosa haimaanishi nawe unahusika, this is childish! na swali kama hili sidhani anaweza kuuliza mtu kama wewe unless ulikuwa unatania, if you were serious! then you should examine yourself time for nonsense questions like this is over!

Athari zake ni hizi wasikokuelewa na wasiojisimamia, wanaopenda kujikombakomba ndiyo hizi pumba hapa chini. Wala haingii akilini from no where mtu anaanza kumshambulia Zitto!, mlikuwa serikali ya Kayombo nini nyie??

Haya makundi yenu ndiyo yanawaaibisha, JF ni huru, na ukiwa huru wa mawazo utakuwa huru kusema kwa uhuru, makundi si mahali pake hapa, maana ubishi wa bila sababu haujaleta manufaa, urafiki huu ndiyo umewazaa akina JK kuwachagua washikaji kwenye position nyingi! yet we are blaming them bad leaders


ebu ona pumba hizi!

Zitto ndo zake hizo. Anadhani kuwa anaelewa kuliko watu wote duniani. He gat some issues.

Hili ni Tatizo pia! Wengi tumeisha liona .......

Masanilo na Mwafrika ebu acheni kufuta mkumbo nyie, jamani ebu jisimamieni, I see no wrong kwa hoja ya Zitto, na pia hakuna tatizo kwa hoja ya MKJJ, ni hoja inabidi kujibiwa kwa hoja.

My take;

MKJJ yuko right if and only if hawa wabunge kweli huwa wanapigana na mafisadi, kwa mtazamo wangu sijaona m'bunge yeyote wa CCM ambaye ni threat kwa chama chake mwenyewe huyo hamna, natemea mate chini si Kilango, wala Mwakyembe na kudhihirisha hawana heshima wala hawaogopwi, ndiyo hao wanahojiwa kijinga jinga kama wamachinga, siyo wabunge hawa!
 
MASANILO "Ungewahi basi kwenye mipasho naona umepotea vile vile!"
Yani kwasababu nimekwambia uende kwenye mipasho, ndo unasema ni wahi vile vile! unajua maana yake? unajua ulichokisema hap? yani umemaanisha kuwa wewe tayari upo kwenye mipasho, kwaiyo nami nije!...ndo maana ya neno "vilevile" kwenye sentensi yako.

Acha watu tujadili hoja. Zitto katoa hoja dhidi ya hoja ya Mwanakijiji...tunapaswa kuchangia kwa hoja...ama tunaunga mkono kwa kutoa hoja, au tunapinga kwa kutoa hoja! sio mambo ya MASANILO ya kutuletea mipasho humu ya ohh!!eeeh!...jenga hoja! huwezi ondoka jukwaa la siasa.

Punguza mapovu basi mkuu .... goosh
 
Serikali yaibua hoja ya 'posho mbili' kuua kashfa ya Richmond

Na Waandishi Wetu

kikwetecapaign.jpg


Ofisi ya Rais Kikwete inadaiwa kushinikiza kuibuliwa hoja ya 'posho mbili' kufifisha kashfa ya Richmond kuendelea kuhojiwa bungeni.

SERIKALI imeshutumiwa kwa kuibua hoja ya 'posho mbili' kwa wabunge ili kuzima kashfa ya Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development (LLC) iliyobuni mkataba wa kifisadi kati yake na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Shutuma hizo zinakuja baada ya vyombo vya habari mbalimbali kutangaza jana msuguano uliojitokeza kati ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliyetoa hoja kusitishwa kwa wabunge kuhojiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusisitiza kuwa zoezi hilo litaendelea kwa sababu ni agizo kutoka katika Ofisi ya Rais, Ikulu.

Takukuru imekuwa ikiwahoji baadhi ya wabunge, wengi wao wakitajwa kuwa ni miongoni mwa wanaojipambanua katika kupiga vita ufisadi, kwa madai ya kupokea posho mara mbili, kufuatia malalamiko ya baadhi ya idara na taasisi kuwa kamati za Bunge zinadai posho mara mbili.

Sambamba na hoja ya 'posho mbili' za wabunge kwa kazi moja, kuendelea kujadiliwa katika nyanja mbalimbali za kijamii, pia mjadala mkali umekuwa ukiendelea katika mtandao maarufu wa 'wanajamii'.

Mchangiaji mmoja, Richard Mabala alisema anashangaa kuona serikali imeamua kuchagua kupambana na baadhi ya wabunge wakati suala la 'posho mbili' ni utamaduni wa miaka mingi bungeni.

"Mwaka juzi nilipotumwa kazi na wafadhili kuonana na kamati moja ya Bunge, vivyo hivyo walitengewa vijisenti vyao, wakiwemo mawaziri na mawaziri wastaafu ndani ya Bunge, mashirika ya jamii na wafadhili," ameandika.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa hiyo ya Richmond, juzi alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kusema kuwa kitendo hicho cha Takukuru ni cha kisasi na kuwa kamwe hatokubali kuhojiwa.

Jana Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Haji Duni alisema serikali inaogopa matokeo ya sakata la Richmond na inataka kutumia suala la wabunge kupokea posho mara mbili kama njia ya kutokea, baada ya kukwama kutekeleza maazimio ya Bunge kwa zaidi ya miezi sita sasa.

"Waziri Mkuu Mizengo Pinda na serikali yake anaogopa Richmond, anakazania wabunge wahojiwe kwa kuwa anaona hapo ndio mahali pa kutokea, wanajaribu kukwepa hoja ya msingi," alisema.

Alisema ikiwa serikali ina sura mbili moja ikiwa ya ufisadi na ndio sababu inachelea kuchukua hatua za wazi zilizopendekezwa na kamati ya Bunge kuhusu watendaji wake.

"Kama serikali ina sura mbili, moja ya kifisadi; ingekuwa makini ingewachukulia hatua wote kama ilivyopendekezwa na Bunge. Sasa inashangaza kwa kushupalia posho za wabunge na kuwahoji ikitafuta pa kutokea," alisema Duni na kuongeza:

"Kama serikali ipo makini kwa nini haijasema wazi ni nani waliorejesha fedha za EPA? Si kweli kama posho za wabunge ndiyo suala kubwa kwa sasa. Serikali iache unafiki kwani, kama posho si wabunge pekee hata watendaji wa serikali wanakula mara mbili."

Alisema, Pinda anajipapatua, huo ni unafiki wa serikali kutaka kufunika hoja ya Richmond na kwamba, kama wana umakini mbona waliorejesha fedha za EPA hawatajwi mpaka leo. Kama Takukuru wapo 'serious' (makini) kwa nini hawakulisemea hilo mwanzo wanasubiri wakati huu wa mkutano wa Bunge."

Aliongeza kuwa lililo mbele ni Bunge kuachiwa lifanye kazi yake na wabunge wafanye kazi yao na iwapo serikali kupitia Takukuru inahitaji kuwahoji basi isubiri kumalizika kwa mkutano wa Bunge.

Kauli hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF iliungwa mkono na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) aliyesema kuwa ingawa hana tatizo na Takukuru kutekeleza wajibu wake, lakini hofu yake ni wakati gani inatekeleza wajibu huo na kama Bunge ambalo pia lina kanuni zinazoweza kufanyia kazi madai hayo limeshindwa kufanya hivyo.

"Ingawa sheria za nchi hazikatazi mtu kuhojiwa wakati wowote, lakini kila jambo lina wakati wake. Kama Takukuru imefanya hivyo ili kudhoofisha nguvu za wabunge kutetea maslahi ya taifa, basi wajue hakuna mtu yeyote anayeweza kulizuia Bunge kufanya kazi yake," alisema Hamad na kuongeza:

"Bunge lisizuiwe kufanya kazi yake. Hata kama litawavuruga wachache bado tutasimamia haki kwani waliobaki pia ni nguvu ya umma, kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi na wana nguvu na uwezo ule ule".

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewasihi wabunge wenzake kukubali kuhojiwa na Takukuru kama njia pekee ya kujisafisha mbele ya umma kuhusu tuhuma za kulipwa posho mara mbili kwa kazi moja.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake bungeni mjini Dodoma jana, alihadharisha kuwa endapo umakini na busara haitatumika katika suala hilo, kashfa hiyo inaweza kuliondolea Bunge heshima ambayo chombo hicho kimejijengea kwa wananchi.

“Sisi wabunge tunapopinga kuhojiwa na chombo cha dola tunatoa taswira mbaya kwa jamii…tunaweza kuharibu hii sifa tuonekane kuna mambo tunayafanya halafu tunajificha na kinga ya Bunge…kinga inatulinda kutoa maoni na michango yetu ndani ya Bunge tusishtakiwe,”alisema Zitto.

Katika mtazamo tofauti Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema anayachukulia mabishano hayo sawa na ya vibaka wawili wanaogombana kila mmoja akitaka kumuwahi mwenzake.

“Takukuru ni questionable (wanatuhumiwa) na wabunge nao pia ni ‘questionable’. Sasa imekuwa ni sawa na vibaka wawili ambao wanapambana na sasa inategemea ni kibaka yupi atamuwahi mwenzake.” alisema Mbatia.

Alifafanua kuwa katika mazingira ya sasa wabunge, wanatuhuma na wanapaswa kuchunguzwa na suala la Richmond nalo linapaswa kuchukua nafasi yake, hivyo Takukuru wasizuiwe kufanya kazi zao kama Bunge nalo lisivyotakiwa kuingiliwa.

Naye Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaye pia ni kijana aliyeinukia kwa kasi kisiasa nchini katika miaka ya karibuni, Nape Nnauye, alisema anatilia shaka uhalali wa Takukuru kutekeleza kazi yao wakati huu wa Mkutano wa Bunge, hasa ikizingatiwa hoja nzito zinazotarajiwa kujadiliwa.

"Mazingira ya sasa tuna sakata la Richmond na bado halijaisha na mmoja wa wanaotuhumiwa ni Mkurugenzi wa Takukuru. Hata kama operesheni yao ni 'genuine' (halali) tunaweza tukafikiri ni kuzuia wabunge wasitekeleze wajibu wao," alisema Nnauye.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Malya alielezea kitendo hicho cha Takukuru kuwa ni cha kuwadhalilisha wabunge na kuongeza kama ni suala la kutolewa posho mara mbili kwa wabunge, Bunge kupitia kamati yake ya maadili lingeweza kujadili na kutoa ripoti.

"Tunaamini wabunge wetu wamekuwa wakijadili kwa uwazi mambo yote kwa maslahi ya umma. Suala hilo pia wangeweza kulifanyia kazi. Kitendo cha Takukuru kwenda kuwafuatilia mimi naona ni cha kuwashushia hadhi," alionya Usu.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dk Edward Hosea, ametia ngumu akitaka uchunguzi dhidi ya wabunge uendelee akisema : "Hakuna mtu aliye juu ya sheria."

Kauli hiyo ya kwanza ya Dk Hosea tangu kuanza uchunguzi huo ambao sasa umefikia hatua ya juu zaidi, inakuja kipindi ambacho tayari kumeibuka msuguano kati ya mihimili miwili ya dola, ambayo ni Bunge na Serikali.

"No one is above the Law..., no matter who are you (Hakuna aliye juu ya sheria, bila kujali wewe ni nani)," alisema Hosea na kuongeza:

"Sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba, kwa hiyo hatuangalii nani ni nani zaidi ya sheria na katiba".

Mapema mwaka huu Dk Hosea alionya wabunge kwamba, wakianza mchezo wa kuumbuana hawatasalimika, kwani kumekuwa na taarifa na ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wao wa kuchukua posho mara mbili.

Akionyesha kutimiza azma hiyo, Hosea alisema hapendi malumbano na wanasiasa kwani yeye si mwanasiasa mwenye jukwaa kama Bunge, ila atasimamia sheria.

"Wanaweza kusema mambo mengi, mimi si mwanasiasa sipendi malumbano na wanasiasa, wao wana audience (hadhara) mimi sina, wana Bunge na wanaweza kukaa bungeni na kuzungumza chochote," alifafanua Hosea na kusisitiza:

"Lakini kwa kifupi ni kwamba, msimamo wa Takukuru uko wazi, ni kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba basi, hakuna jambo jingine".

Alipoulizwa endapo uchunguzi huo una msukumo na nguvu za aina yoyote nje ya sheria na utendaji kazi wa kawaida wa Takukuru, alijibu: "Nasisitiza, sipendi malumbano na wanasiasa, wanaweza kusema mengi, lakini tunasimamia sheria tu".

Msuguano huo unaondelea kati ya mihimili hiyo miwili ya dola, pamoja na mambo mengine unaweza kuliingiza Bunge la Tanzania katika kashfa mbaya ya matumizi mabaya ya fedha za umma kama ilivyokuwa kwa Bunge la Uingereza.

Tayari hadi sasa, wabunge wengi wakiwa ni kutoka Kamati ya Nishati na Madini wakiongozwa na Shellukindo mwenyewe, wamekwishahojiwa kutokana na tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata, karibu wajumbe wote 21 kutoka Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma wamekwishaitwa kuhojiwa huku mwenyekiti wao Zitto akiwa njiani.

Baadhi ya wabunge kama James Lembeli wa Kahama na Dk Mwakyembe, walikwishaitwa kuhojiwa lakini hadi sasa hawajafanyiwa hivyo, huku mbunge huyo wa Kyela akiweka bayana kwamba, hayuko tayari kuhojiwa na Takukuru vinginevyo apelekwe mahakamani.

Baadhi ya wananchi waliliambia gazeti hili kwamba, hawaoni sababu ya wabunge kulalamikia kitendo cha Takukuru.

"Mjadala wa bunge hauwezi kuzuia mambo mengine yasifanyike... kama wabunge watashindwa kwa sababu tu ya kuhojiwa basi kazi yao watakuwa hawaijui. Na pengine hili litakuwa ni changamoto kwao," alisema Hamis Athuman.


Imeandaliwa na Exuper Kachenje, Leon Bahati na Ramadhan Semtawa
 
Mimi najua.

Mkuu kama unajua mbona umekuwa kimya kuhusu hilo? Nafikiri itakuwa vyema kama ukiwaumbua bungeni ili wananchi wakajua ukweli, lakini utakaponyamaza basi wengi wetu tutafikiri unalea UCHAFU.

Wataje popote pale maana umesema unawajua, hivyo tunaamini una ushahidi. Mwaga kuku kwenye mtama mwingi......ooh sorry mwaga mtama kwenye kuku wengi.
 
Tatizo lako una kaujeri jeuri flani hivi. You need to have a spirit of humbleness in you if you want to go further in your political career.

Mimi nimekuuliza wewe unajuaje hao wabunge wanafanya kama ulivyodai wanafanya. Wewe ukanijibu unajua. Kunijibu kuwa unajua hujajibu swali langu. Jibu swali, wewe umejuaje wanafanya hivyo? Siyo swali gumu hili.

And does it matter if you are clean or not? Of course it does. You can't be throwing all these stones while you live in a glass house.

And don't get it twisted. I know good and well that two wrongs don't make a right.

My dear friend Julius aka Nyani, we do have disagreements, lakini hapa lazima nikupe tano!
Kwa kusoma hoja za mh Zitto, naona kama kaingia humu kutetea kitu ambacho hajakifanyia reflection. Na ninakubaliana na wewe kuwa amekuwa jeuri kukujibu Najua. That is childish.

Na ninaona kashindwa kuendelea na discussion maana sasa amejiweka katika wakati mgumu, kwani kesho waandishi, polisi, TAKUKURU anayewatetea wanaweza kumfanyia 'interview' aeleze njia hizi anazijuaje.

Sorry Mh Zitto, hujaonyesha busara katika hili, you still have a lot to learn, and do so humbly.

But getting back to the point of TAKUKURU kuchunguza Bunge, mi sikubaliani nalo, kwani TAKUKURU iko chini ya Rais kwa hiyo mhimili moja utakuwaje na mamlaka juu ya nyingine wakati kuna mhimili mwingine wa kisheria yaani mahakama ambayo ndo kazi yake - to uphold the law of the land. Hii ishu ya kupokea posho mara mbili naweza kusema maximum ni misdemeanor, na si kazi ya TAKUKURU ambao BTW waliishafisha Richmond na serikali na waka-declare kuwa hakuna rushwa wakati mabilioni yalichotwa.

Let us all take perspective on this na siyo kubakia kuongea as if there is no context to this issue.

Tusikubali hii ishu kupindishwa by mistake, or on purpose....
 
Zitto kama unajua kwa nini umekaa kimya sasa ndio unaongea?Kwanini usingewasaidia TAKUKURU kitambo kuwa kunawabunge wanafoji risiti?

My dear friend Julius aka Nyani, we do have disagreements, lakini hapa lazima nikupe tano!

Kwa kusoma hoja za mh Zitto, naona kama kaingia humu kutetea kitu ambacho hajakifanyia reflection. Na ninakubaliana na wewe kuwa amekuwa jeuri kukujibu Najua. That is childish.

Na ninaona kashindwa kuendelea na discussion maana sasa amejiweka katika wakati mgumu, kwani kesho waandishi, polisi, TAKUKURU anayewatetea wanaweza kumfanyia 'interview' aeleze njia hizi anazijuaje.

Sorry Mh Zitto, hujaonyesha busara katika hili, you still have a lot to learn, and do so humbly.

But getting back to the point of TAKUKURU kuchunguza Bunge, mi sikubaliani nalo, kwani TAKUKURU iko chini ya Rais kwa hiyo mhimili moja utakuwaje na mamlaka juu ya nyingine wakati kuna mhimili mwingine wa kisheria yaani mahakama ambayo ndo kazi yake - to uphold the law of the land. Hii ishu ya kupokea posho mara mbili naweza kusema maximum ni misdemeanor, na si kazi ya TAKUKURU ambao BTW waliishafisha Richmond na serikali na waka-declare kuwa hakuna rushwa wakati mabilioni yalichotwa.

Let us all take perspective on this na siyo kubakia kuongea as if there is no context to this issue.

Tusikubali hii ishu kupindishwa by mistake, or on purpose....

You deserve to be a director of TAKUKURU nothing else! Hosea and his team are wrong,Susuviri is right!
 
You deserve to be a director of TAKUKURU nothing else! Hosea an all team of TAKUKURU are wrong,Susuviri is right!
Mkuu, Mungu aniepusha kuifanyia kazi serikali ya CCM! Lakini mabadiliko yanakuja naamini tutakuja kupata mkurugenzi mzuri na tutashinda vita hivi dhidi ya ufisadi, lakini ili hilo litokee inabidi tuing'oe CCM na sisemi hivyo kama mshabiki wa chama chochote bali kama mtu anayeitakia mema Tanzania.
 
Huu uchunguzi wa muda mrefu wa kuchunguza Shekilango or who ever kapewa posho mara mbili ambayo sijui ni laki mbili au millioni mbili, wakati huo huo takukuru wanashindwa kufuatilia mambo ya mabillioni na yenye madhara ya muda mrefu na kuuwa uchumi kama kukosa barabara au umeme, pantoon mbovu mbovu nk nk.
Hili suala la posho mara mbili ni ukiangalia na amount involve ni more of administrative than rushwa, ni rushwa gani ambayo mtu anasainishwa na ipo public?
Rushwa ni kama zile mafisadi wanakupa then wanaficha ushahidi wa kukupa mpaka mambo yaende kinyume na walivyo tarajia.
Lakini hili la posho , ambapo vitabu vya mahesabu vinapitiwa na wakaguzi , na kesho na kesho kutwa mtu mwingine ataviona utaiita ni rushwa?
Hili lilikuwa linatakiwa kushughulikiwa na mashirika husika wakishirikiana na ofisi ya bunge na kuwataka wahusika kama inabidi warudishe na serikali itoa waraka kuwakumbusha wahusika walipaji na wapokeaji wasifanye hivyo, linapo ingiza forgery then Polisi ndio wanatakiwa kuingilia.
Ama sivyo kuna tatizo kubwa saana la kutafsiri nini ni rushwa, impact ya tatizo hilo katika society, na kiasi kilicho husika.

Mkuu nilivyokuelewa hapa ni kuwa TAKUKURU HAWANA KAZI YA KUFANYA, na wabunge wanaokubali kuhojiwa nao hawana kazi ya kufanya pia.

Unajua wabunge hawa lazima wajilaumu sasa, hii maiti ya TAKUKURU wameibeba beba sana bungeni, leo inaanza kunuka , inawanukia wao wanaanza kulia sasa.

My take ni kuwa hawa wabunge hamna kitu, yaani walaini mno , siyo wakali, wala hawana heshima katika jamii achilia mbali ndani ya bunge lenyewe

mpaka TAKUKURU wanawaendea kuna uwezekano mkubwa ishu si posho tu, inawezekana wana virushwa rushwa vingine visivyojulikana, na ndio maana wanaingilika kirahisi!

You can not convince me ishu ya posho mara mbili wahojiwe na TAKUKURU!

Wabunge; Hii mizigo kama Takukuru, uwt, Tanroads n.k, wananchi wanapopiga kelele ebu fanyeni juu chini muangalie facts na kuchukua hatua mbadala, hii aibu kwenu, achilia mbali huko mlikochaguliwa!
 
Yote haya ni kupunguza kasi ya kuifatilia Richmond...

Kasi ya kufuatilia Richmond inapunguzwa vipi?
1. Ripoti imekwisha andikwa, kujadiliwa na Bunge na maamuzi kutolewa.
2. Waziri Mkuu amekwisha jiuzulu.
3. Mawaziri wawili wa Nishati na Madini wamekwisha jiuzulu.
4. AG amekwisha staafu.
5. PS wa Nishati na Madini amekwisha staafu.
6. Hosea amekwisha pewa onyo.
7. Bunge bado lina nafasi ya kujadili kama halijaridhika.

Hapa nadhani wanaotaka kulipiza visasi ni kundi la wabunge ambao hawaridhiki mpaka labla watu wote hapo juu watolewe roho. Hapa hatuko China au Iran. Hapa ni Tanzania ambapo tumeamua kufuata sheria katika misingi ya kistaarabu na maadili yanayozingatia haki za Binaadamu.

Inasikitisha kuona kuwa hata wenye wanaodhaniwa kuwa wenye busara wanamezwa na jazba za mapenzi kwa mtu.

Spika amekwisha sema kuwa kuchota posho mara mbili ni jambo dogo na la kawaida tu na hakuna rushwa katika hilo. Sasa kama Spika wao kisha sema hivyo wao wana wasiwasi gani? Waende tu kutetea hoja yao na si kupigia kelele nje ya vyombo vya dola.

Wakati nakubaliana na Zitto kwa yote, lakini sikubaliani naye kuwa hili ni suala la maadili. Huu ni wizi dhahiri wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa sababu kitendo chao cha kudai posho hizo, na sio kwamba walipewa tu kwa ridhaa ya Wizara na mashirika husika, ni ushahidi wazi kuwa walidanganya walipaji kuwa walikuwa hawajapata posho hizo toka Bungeni.

Tena nimepata fununu kutoka kwa Mbunge mmoja kuwa kuna wakati kamati hizo ziliweza kutembelea mashirika mawili kwa siku moja. La kwanza asubhi na la pili mchana. Katika siku kama hiyo walilipwa posho mbili, moja kwa kila taasisi. Ukiongeza na ile ya Bunge, inakuwa wanapata posho mara tatu kwa siku. Yote haya wanafanya huku wakijua kuwa ni makosa. Hii huwezi kusema ni kosa la kimmadili bali ni udanganyifu dhahiri
 
Mimi nafikiri mwakyembe ahojiwe...TAKUKURU can be evil but ni legal entity..yeye kama leader lazima afuate sheria..kufuata sheria zilizopo..takukuru siyo hosea! bana!
Mbona hawa jamaa sasa kila kitu wanasingizia kwamba wanafuatwa..je yeye pekee aliyetakiwa kuhojiwa?
 
Hivi jamani kuhojiwa kuna ubaya gani? Kama uko salama au sio salaama unalalamika nini? kwani kuna ubaya wa mtoto wako kukuuliza au kujua kuwa eti baba baiskeli ya hapa nyumbani ni ya uizi au sio ya wizi. Kwani inakuaje kwa baba kukasirika eti kuwa usinihoji we mtoto au kaka. kwani ukihojiwa ndio umekuwa mwizi? kwani TAKAKURU ndio mahakama? Kama wataonekana wanamakosa na wao wanaona wameonewa, jamani si kuna mahakama ambayo itawasafisha hawa wabunge wetu!! kwa hiyo wakati wa uchaguzi sisi wapiga kura tusiwahoji wabunge wetu jinsi wanavyofanya kazi. Maana tutaambiwa tuwapeleke mahakamani. Sisi ni wapiga kura tu na hatuna ubavu kama hao TAKAKURU.

Hivi nashindwa kufahamu, ivi hawa wabunge walilazimisha wapewe hizo posho mara mbili??? Hao waliotoa posho kwa nini waliwapa hao wabunge posho mara mbili. Kama wabunge waliwalazimisha watoa posho na kwamba kuna sheria kuwa wasipewe posho mara mbili na kwamba watoa posho walilalamika basi wabunge wanamakosa. Na kama ni jadi kuwa wabunge wapewe posho mara mbili basi sio kosa. kama hao watoa posho hawakulalamika na TAKAKURU imegundua basi watoa posho lazima nao watiwe hatiani ni wezi watupu hao.

Sasa kwa nini Mwakyembe analalamika kuwa hataki kuhojiwa kama ni jadi kupokea posho mara mbili. Au yeye hakulazimisha apewe posho mara mbili.
Binafsi nahisi Sita yuko ndani ya huo mtego.Huenda mafisadi wamegundua jinsi ya kumng`oa Sitta kwa staili kama hiyo
 
Back
Top Bottom