TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie!

Zitto,
TAKUKURU wako right kabisa, lakini wanachofanya hawafanyi at a right time, timing yao ndio inayoleta walakini na mvutano, baada ya Hosea kuona anajadililiwa yeye anafanya counter attack ili apunguze makali ya mumjadili. Muhimu Hosea awajibike kama maagizo ya bunge yanavyotaka na baadaye kuhojiwa kuenedelee kwa kufuata taratibu na ile wawe fair kwa kiasi kinachotakiwa waanze na mawaziri, manaibu, wabumbe, makatibu wakuu na washuke chini zaidi, natoa hoja.

Hapana, Mkuu. Takukuru hawako right. Basi itafika wakati itabidi Takukuru wakawahoji wabunge kwa kulala bungeni au kutohudhuria vikao vya bunge!

Wana kazi muhimu lakini hii si mojawapo.

Amandla.......
 
FM,
Tunayo tume ya MAADILI ya VIONGOZI wa UMMA. Hakuna inachokifanya. Hata hiyo anayotaka Zitto iundwe haitafanya lolote. Wanasiasa wetu wameoza nje ndani.
 
Wakuu tufikie mahali ukweli ubakie kua ukweli. Tuondoe tabia ya kuhurumiana na kuona hili linamfaa flani na flani halimfai. Kwakweli intergrity ya hawa watu inaogopesha na lazima wachukulihe hatua. Huwezi ukatuibia ati tusikukamate kwakua ulitusaidia kumkimbiza mwizi, tena mwizi mwenyewe sisi ndo tulimuona na tukaanza kupiga mayowe it was just of your advantage kwamba ulikua karibu ukamkimbiza.

Kwanini tusihoji uadilifu wako kama unaweza kutudai mara mbili kwa kitu kimoja? je umedai mara ngapi namna hiyo? Taifa linaathirika kiasi gani kwa uovu huo mkubwa? Unaposema walikupa je ulipopewa uliamriwa ukikataa utauwawa? There is a very serious issue here and PCCB should inverstigate.

Tusitumie mapambano ya ufisadi kama mwavuli wakutetea ufedhuli wetu. Wawajibike kwa mema na mabaya yao.

Tunazihitaji sana hizo hela kwaajili ya kujenga vituo vya afya kule kyela anakotoka Mwakyembe
 
Mkuu, umeona hii ishu ya posho mbili ndiyo ina athiri Taifa kwa kiasi kikubwa kuliko Richmond, Dowans, IPTL, rada na grand scale corruption nyingine zote????
Please, you can't be serious! Yaani PCCB wameacha kazi zote za kukusanya evidence na kushirikiana na SFO ya UK eti kumhoji Mwakyembe? Au watawahoji na wabunge wengine wote na kutengeneza paperload kwa miaka 2 ijayo wakiwa busy wanafuatilia wabunge na posho zao?
Don't try to create a mountain out of a molehill!
 
Tatizo lako una kaujeri jeuri flani hivi. You need to have a spirit of humbleness in you if you want to go further in your political career.

Mimi nimekuuliza wewe unajuaje hao wabunge wanafanya kama ulivyodai wanafanya. Wewe ukanijibu unajua. Kunijibu kuwa unajua hujajibu swali langu. Jibu swali, wewe umejuaje wanafanya hivyo? Siyo swali gumu hili.

And does it matter if you are clean or not? Of course it does. You can't be throwing all these stones while you live in a glass house.

And don't get it twisted. I know good and well that two wrongs don't make a right.

Spinning!!!!

Who are you to question Zitto on this?? I think what Zitto intended here was just to reveal to us how the MPs are not different from any other citizen of Tanzania.

I can assure you haya mambo hayapo tu huko kwenye public sector yako pia huku private. Wangapi wanagushi risiti za malazi, chakula, mafuta etc?? Nafikiri tukiendelea hivi Tanzania itakuwa the most corrut country in Africa/world!

We are corrupt in the mind and it begins from our early childhood! Nikiwa pale UDSM nakumbuka kuna aina ya corruption ilikuwa ikiendelea pale especially kwenye masuala ya Accommodation ambapo some people had privilege(just because they had "connections" with the DARUSO leaders) ya kuwa na zaidi ya 4rooms while other dont get even a single bed!! In turn hawa wenye connection would sell the extra rooms at ridiculous amounts of money! I hope it is still happenning! Sasa unategemea mtu aliyekulia katika style hiyo ya maisha atafanya nini akiwa Mbunge/Waziri/Mwajiriwa ktk mashirika binafsi etc?? Huu ni upuuzi. We are corrupt in every way!?

Rushwa ni jambo hatari sana na ili kuliondoa lazima tuanzie katika ngazi za chini mpaka za juu kabisa. Mimi naiunga mkono TAKUKURU 100%, do your job and don't entertain no one at all!!!

Hii nchi inahitaji mabadiliko na hayaji hivihivi!!..................
 
FM,
Tunayo tume ya MAADILI ya VIONGOZI wa UMMA. Hakuna inachokifanya. Hata hiyo anayotaka Zitto iundwe haitafanya lolote. Wanasiasa wetu wameoza nje ndani.

Nakubaliana na wewe. Lakini nadhani tatizo si wanasiasa bali ni sisi wananchi ndiyo tunaowapa kiburi. Kama tunampokea kwa vifijo na maandamano mwanasiasa ambaye ameonekana kuwa amefanya uovu, tunategemea nini? Ndiyo maana tunahitaji Media iliyo jasiri na vyombo vilivyo nje ya mfumo huu kuwaaibisha hawa wakuu na kuwafungua macho wapiga kura. Tukidai kwa dhati Tume iwajibike, itafanya hivyo. Bahati mbaya wengi wetu tumeridhika na hali iliyopo.

Amandla........
 
Kaka unajua Mramba alihojiwa na kufikishwa mahakamani akiwa Mbunge? Unajua stori ya yule mbunge wa Morogoro aliyeburuzwa na Landrover la Polisi kwa madai ya Maji? Hawa nani alikuja hapa kuwatetea na kusema tawi la utendaji lisiingilie Bunge?

Kuna tatizo la msingi katika Taifa letu na katika mfumo wa Bunge. Fanya tafiti zako, ni Bunge la Tanzania tu duniani ndilo halina utaratibu wa kudhibiti mienendo ya Wabunge. Nchi nyingine wana mtu anaitwa Kamishna wa mienendo (Office of the Commissioner for standards). Huyu huchunguza mienendo na ile ambayo ni ya kijinai huenda katika jinai na ile ya kimaadili (hili la posho ninadhani ni la kimaadili) linakwenda kamati ya Maadili na kisha Bunge kutoa adhabu.

Mwaka 2004 Sheria ya maadili ilirekebishwa ili Bunge lipitishe 'code of conduct' kwa wabunge. Mpaka leo hatujapitisha. Mwaka 2008 niliwasilisha muswada binafsi ili kuunda code na kisha kuunda ofisi ya Kamishna huyu. Mpaka leo Ofisi ya Spika imekalia muswada huu na kukataa kuupeleka kuwa gazzetted ili ujadiliwe Bungeni.

Hivi MwanaKijiji unajua wabunge wanasafiri kwa mabasi kutoka Dar kuja Dodoma na wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?

Tunafanya makosa, halafu hakuna code wala mamlaka ya kutuchunguza halafu tuachiwe. Hapana. Mwanakijiji wewe kwa heshima yako hupaswi kutetea uvunjifu wa maadili.

Waache TAKUKURU wafanye kazi yao. Lazima Wabunge tujue kuwa hatupo juu ya sheria na kwamba tupo accountable na answerable kwa vitendo vyetu (for actions and inactions).

dont mixed up issues here... Mramba alishitakiwa na kuhojiwa kwa makosa yake binafsi lakini hawa wabunge wanatuhumiwa kwa kazi ambayo ilikuwa ni ya kibunge ambayo ina kinga. na pia hili limetokea wakati bunge linataka serikali imwajibishe hosea...why now?
 
Swali nililouliza ni jepesi mno. Nimeuliza yeye kajuaje baadhi ya wabunge hufanya hivyo? Nikupe mfano, angeweza tu kusema kuwa nimeambiwa, nimeshuhudia, nimewahi kufanya, n.k....lakini siyo kunjibu "najua". Heck..I didn't ask if you know, I asked you how do you know?

Wewe Julius mbona unamshupalia sana Mh. Zitto? Je ulipokuwa shule au chuo hukujua mambo/mbinu ambazo wanafunzi wenzio wanafanya kuhusu jambo fulani ambalo linamaslahi kwao hata kama ni kwa siri? Kwa mfano binu ya wanafunzi kuingia na desa kwenye chumba cha mtihani. Sasa utauliza nimejuaje kwamba kuna wanafunzi wanaingia na desa kwenya mtihani? Probably commonsense is not common to all
 
Haki tupu niko nawewe 100% Takukuru kufanya kazi ya kufichua maovu ni sawa kabisa lakini timing inatia wasi wasi, kama mtakumbuka Hosea alimjibu Mh. Raphael Chegeni alipomhoji kuhusu uadilifu wake kwenye semina kwa Wabunge semeina iliyoandaliwa na Takukuru na kuwalipa posho kuwa "Mnaniandama mimi wakati yenu ya kuchukua posho mara mbili mbili tunayamezea, mkitaka tuumbuane tutaumbuana" kwa hiyo hapa kinachofanyika si kazi ya kawaida bali kukomoana na kuumbuana! Hivi tunamuweka mtu kazini, tena sehemu nyeti kama hiyo ili awaumbue wanaotaka kumuumbua?? Na kuwasitiri wataomfurahisha hata kama ni Mafisadi?? Eeeh mtu hatari
 
Mkuu, wewe usimtetee Mh Zitto,mwache aje ajitetee, lakini ukiangalia tokea amekuwa challenged na Julius aka my dear friend Nyani, naona Mh kakimbia kabisa hii thread ameshaona amejiingiza katika mtego. NIngekuwa na access ya namba ya mbunge hata Mwakyembe ningemtumia nakala ili aibue hii public discussion aliyoanzisha Zitto na ahojiwe kwamba amejuaje.. alafu tuone kama atajibu kwa jeuri "Najua".
 
Rushwa ni jambo hatari sana na ili kuliondoa lazima tuanzie katika ngazi za chini mpaka za juu kabisa. Mimi naiunga mkono TAKUKURU 100%, do your job and don't entertain no one at all!!!.......

Ni kweli kabisa maneno yako, Ila, kwenye sheria, mtoaji rushwa na mpokeaji rushwa wote ni wahalifu. Sasa kama hii ya wabunge kupokea posho mbili ni "rushwa", hao wakurugenzi wakuu wa mashirika ya umma ambayo yanatoa posho wameshavikwa pingu?.....

TAKUKURU wanasema wameanzia uchunguzi kwenye hayo mashirika na kujiridhisha kuwa yalitoa posho au "rushwa" kwa wabunge. Sasa kama tayari wamesha establish hivyo. Ni kwanini hakuna hata mkurugenzi mkuu mmoja aliyefikishwa kwa pilato?

Huu wote ni mchezo wa kitoto...na mijinga ndiyo iliwayo. Hosea anataka kulinda kitumbua chake kwa intimidation, its not you (watanzania) at the heart of his motivation on this.

First things fisrt, kwanza HOSEA OUT!...then interrogation za wabunge ziendelee kwa mujibu wa sheria.
 
dont mixed up issues here... Mramba alishitakiwa na kuhojiwa kwa makosa yake binafsi lakini hawa wabunge wanatuhumiwa kwa kazi ambayo ilikuwa ni ya kibunge ambayo ina kinga. na pia hili limetokea wakati bunge linataka serikali imwajibishe hosea...why now?
"Posho" hizi sio kazi ya kibunge. Kwani Hosea ndiye TAKUKURU? Baadhi yetu tunaona wamechelewa kulishughulikia suala hili wewe unauliza....why now?
 
Haki tupu niko nawewe 100% Takukuru kufanya kazi ya kufichua maovu ni sawa kabisa lakini timing inatia wasi wasi, kama mtakumbuka Hosea alimjibu Mh. Raphael Chegeni alipomhoji kuhusu uadilifu wake kwenye semina kwa Wabunge semeina iliyoandaliwa na Takukuru na kuwalipa posho kuwa "Mnaniandama mimi wakati yenu ya kuchukua posho mara mbili mbili tunayamezea, mkitaka tuumbuane tutaumbuana" kwa hiyo hapa kinachofanyika si kazi ya kawaida bali kukomoana na kuumbuana! Hivi tunamuweka mtu kazini, tena sehemu nyeti kama hiyo ili awaumbue wanaotaka kumuumbua?? Na kuwasitiri wataomfurahisha hata kama ni Mafisadi?? Eeeh mtu hatari

Kudos kwa kutukumbushia malumbano haya, kama iko on the record basi Mwanakijiji is right - HOSEA has to resign immediately, kwani ametumia madaraka yake vibaya ili kulipiza kisasi binafsi! Sijui wanaomtetea Hosea wanafnya hivyo on what basis?
 
Zitto, hivi ni kweli suala la mzozo wa posho za wabunge unaoendelea ni RUSHWA? Je, sual hili la posho ni muhimu sana kwa sasa kuliko suala la Richmond na TRL? Wabunge watakuwa ktk madaraka yao mpaka mwakani, kwanini suala hili lianzishwe sasa hivi wakati Bunge linataka majibu toa Serikalini? Tuitendee haki nchi kwa kutokuwa wanafiki ndani na nje ya mioyo yetu. Kama ulijua hayo ya wabunge kugushi risiti, je uliishawahi kutoa taarifa ktk chombo chochote ili hatua madhubuti zichukuliwe?
 
Takukuru wanaweza kuwa sahihi lakini timing yao ndiyo inatia kichefuchefu - inaufanya uchunguzi mzima uwe ni ufisadi in its own right! Labda wasimamishe liishe hilo la Richmond ndio waanze uchukuzi makini kuanzia mwanzo wa ENZi sio juzi tu! Waanze na akina JK wakiwa wabunge ili na akina Pinda na wengine wasafishwe! Waende mpaka kwenye vikao ya ndani vya mashirikani (eg senates kule vyuoni) - ili tuone kwa nini mwalimu au mwanafunzi ahudhurie kikao halafu alipwe pesa - kama wataiona rationale basi tutafute muafaka wa kitaifa! La sivyo, tukikubali kufuata kila upepo, tutaishia kupoteza mwelekeo! Lazima tujue ku prioritise!
Hilo lipo wazi wazee Timing ndo zinazotuonesha kuwa wanalipiza kisasi. Ni sawa na visa vya Madenge "Katuni"
babaake anamuuliza "kwanini Umefeli Mtiani?"
Madenge naye anauliza kabla ya kujibu, "Mbona na wewe Baba Umefeli Ubunge?"
Halafu Kwamba lipo wazi Hosea alishasema kuwa tabia ya kuumbuana hakuna wa kupona na ndo ameanza hivyo.
 
It's all about finding a balance. Ki-sheria, "What happens in Bunge, stays in Bunge". Hivyo hii ishu ingepaswa kushughulikiwa na Kamati za huko huko bungeni. Na kama mnaona vipi, mnapeleka ripoti jimboni, mkihakikisha kuwa wananchi wanajua kuwa wamemchagua mwizi. Lakini kuruhusu uvamizi wa bunge kwa taasis kama PCCB na Polisi ni kosa. Bunge ni sauti HURU ya Wananchi. Wananchi katika Majimbo wapewe nguvu za kuondoa wabunge wao katika ya msimu. Na kazi ya waandishi kama MWJJ ni kuwapelekea hao wananchi taarifa za utendaji. Hivi ndo tutajenga system yenye ufanisi zaidi.

Ivi Dr Slaa si alikuwa na ile kampeni ya kuzunguka nchi nzima kuonyesha huu upuuzi unao-endelea bungeni? Alipigwa vita sana na wabunge wezi. Sasa sijui kaishia wapi.
 
Mhe. Zitto Kabwe, hivi ni kweli unaamini kwa dhati ya moyo wako kuwa posho zile zinatakiwa kuchunguzwa na TAKUKURU? Hivi ile ni RUSHWA kweli? Nani amehonga? Ili iwe nini? Je, hongo hiyo imefanikiwa kwa kiasi gani? Na imesababisha hasara ya ukubwa wa kiasi gani kwa Taifa hili? Inafananaje na ile ya Richmond, TRL, TICS n.k?
Zitto, usitoke ktk mstari wa kuwatetea wananchi, utakwisha kisiasa. Acha kujidharau, na usiwe dhaifu mbele ya maovu.
 
Kaka unajua Mramba alihojiwa na kufikishwa mahakamani akiwa Mbunge? Unajua stori ya yule mbunge wa Morogoro aliyeburuzwa na Landrover la Polisi kwa madai ya Maji? Hawa nani alikuja hapa kuwatetea na kusema tawi la utendaji lisiingilie Bunge?

Kuna tatizo la msingi katika Taifa letu na katika mfumo wa Bunge. Fanya tafiti zako, ni Bunge la Tanzania tu duniani ndilo halina utaratibu wa kudhibiti mienendo ya Wabunge. Nchi nyingine wana mtu anaitwa Kamishna wa mienendo (Office of the Commissioner for standards). Huyu huchunguza mienendo na ile ambayo ni ya kijinai huenda katika jinai na ile ya kimaadili (hili la posho ninadhani ni la kimaadili) linakwenda kamati ya Maadili na kisha Bunge kutoa adhabu.

Mwaka 2004 Sheria ya maadili ilirekebishwa ili Bunge lipitishe 'code of conduct' kwa wabunge. Mpaka leo hatujapitisha. Mwaka 2008 niliwasilisha muswada binafsi ili kuunda code na kisha kuunda ofisi ya Kamishna huyu. Mpaka leo Ofisi ya Spika imekalia muswada huu na kukataa kuupeleka kuwa gazzetted ili ujadiliwe Bungeni.

Hivi MwanaKijiji unajua wabunge wanasafiri kwa mabasi kutoka Dar kuja Dodoma na wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?

Tunafanya makosa, halafu hakuna code wala mamlaka ya kutuchunguza halafu tuachiwe. Hapana. Mwanakijiji wewe kwa heshima yako hupaswi kutetea uvunjifu wa maadili.

Waache TAKUKURU wafanye kazi yao. Lazima Wabunge tujue kuwa hatupo juu ya sheria na kwamba tupo accountable na answerable kwa vitendo vyetu (for actions and inactions).

Ahsante mheshimiwa kwa kutujuza haya! Nadhani tatizo si kuhojiwa na Takukuru, ni mfumo mzima wa namna wabunge wanavyohojiwa!
 
Back
Top Bottom