TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie!

Mbona TAKUKURU wanataka kutufanya sie Watanzania mazoba? Kupokea posho mara 2 ni rushwa? Kwani kazi hasa ya TAKUKURU ni nini? Hawa wabunge wamepokea rushwa au wamepokea posho mara 2? Mnaacha wanao kula rushwa nene mnafuatilia wanao kula posho mara 2 tuwaeleweje? Au ndo ukomo wenu ulipo fikia?
 
Ninyi ambao hamko kwenye AJIRA za TAASISI hizi za UMMA mnadhani posho hizi ni posho za kawaida. Ni mamilioni ya mapesa. Ni kila MBUNGE aliyeko kamati fulani anapojisikia kukamata milioni moja au zaidi anamwendea mkuu wa taasisi husika, anamwandikia kimemo au anapiga simu pesa inatafutwa haraka.
Kwa mtindo huu tunapoteza billions kwa mwaka zaidi ya zile za EPA. Kwa MAWAZIRI husika ndio USIPIME kabisa. Niambieni sasa kwa staili hii ni lini WABUNGE na BUNGE letu litafanya kazi ya kuisimamia SERIKALI?
Wabunge wanakuwa wakali pale tu wanapokosa MGAO wao. Nimekubaliana sana na kauli ya Polycarp Cardinal Pengo aliposema kwamba wanaopigia kelele ufisadi ni kwa kuwa wao wamezikosa nafasi hizo.
Jana Mh Zitto alijaribu kupeleka hoja kuwaondoa WABUNGE na WANASIASA kwenye bodi za TAASISI za UMMA. Hakuungwa mkono na Mbunge yeyote hata wale upinzani!
 
Let us agree in principle that TAKUKURU is one of the many failed CCM polocies. The Chief Executive Officer of the corrupted body Hosea severally sexed the Richmond corruption report and aliyemteua akatabasamu na kwa kua the President(JAKAYA MRISHO KIKWETE) na Maswahiba wake wamegubikwa na rushwa you can't note the difference. Kwa staili ya CCM kuwakingia kifua watu mpaka wastaafu we are just wasting our time tutambue imekula kwetu. Hivi hamshangai Rais kuamrisha Mitambo YA IPTL iwashwe at any cost do you Know why? Go back to history wakati serikali ilipoasaini makataba huo nani alikuwa waziri wa fedha baada ya akina Malecela kupigwa paranja na Mwl. JKNyerere obviously alikuwa ni huyu Mkwere!

Kama lila na fila hazitengamani vivyo hivyo Kikwete na mikataba hovyo ya IPTL na RICHMOND/BUZWAGI na Madini in general haitengamani! Go an extra mile huo utajiri wa Ridhwan Kikwete wa kuporomosha majumba akiwa na akina Mosha umetoka wapi!!! Labda tuunde tume!!! Nawasislisha...teee kalakabaho
 
Ugomvi uliopo kati ya dola na bunge uko wazi kabisa na hilo ndilo tatizo linalotokea sasa hivi. Bunge lililopita lilionyesha meno kwa serikali na kusahau kuwa serikali nayo ina namna ya kuwasulubu wabunge mmoja mmoja. Kinachotokea sasa hivi ni kama serikali inajibu mapigo kwa suluba iliyopata kwenye kikao kilichopita na kuzuia kipigo kipya kwenye kikao cha sasa.

Sipingani na hatua ya PCCB, lakini hatua hii inaleta utata kwani kiongozi wake mkuu alipendekezwa na kamati ya Bunge kuwa aondolewe kwenye nafasi yake. Iweje leo kabla mapendekezo hayajafanyiwa kazi yeye aongoze kuhoji wabunge? Inaonekana JK anataka kulisulubu bunge kwa nguvu ya dola aliyonayo.Anataka kunyamazisha wabunge ili serikali ifanye maamuzi bila kuhojiwahojiwa.

PCCB ina nguvu ya kikatiba, lakini kwanini utekelezaje wa majukumu yake unakuwa selective? Kuna watu kama akina Lowassa mpaka wamejiuzuru hatujawahi kusikia kama wamehojiwa na PCCB,wakati matatizo wanayodaiwa kusababisha yako wazi kwenye jamii yetu.

ZITTO ZUBERI KABWE

Naomba kutofautiana na wewe kaka. Kwanza suala la Mramba na yule mbunge wa Morogoro walifanya makosa tofauti na haya yanayosemekana yamefanywa na wabunge. Mramba alifanya makosa ambayo hayahusiani kabisa na kazi yake ya ubunge na ni hivyo hivyo kwa mbunge wa Mororgoro. Makosa aliyofanya Mramba aliyafanya akiwa anafanya kazi ya dola na ni dola hiyo hiyo iliyoamua kumpeleka mahakamani kupitia PCCB. Mbunge wa Morogoro alifanya kosa ambalo ni la jinai.Bunge najua lina kamati ya maadili ambayo ingeweza kuwahoji wabunge kwa kukosa maadili ya kazi.

Pili Zitto Kabwe ndugu yangu umepoa sana siku hizi. Kila unapotoa maoni kwenye mambo yanayotatiza jamii hii unaegemea sana kwenye upande wa uovu. Umekuwa tofauti na Zitto tunayemjua aliyekuwa mtetezi wa maslahi ya watanzania,Zitto aliyeibua suala la Buzwagi, Zitto aliyepokelewa kwa umati mkubwa na wakazi wa Dar es salaam baada ya kusimamishwa kuhudhururia vikao vya bunge. Niwe wazi kwako mkuu,kama ungesimamishwa leo kuhudhuria vikao vya bunge hakuna ambaye angeacha kazi zake kuja kukupokea kama ilivyokuwa wakati ule. Maoni yako yamekuwa ya utata sana. Kama una watu wanaokushauri,ujue wanakupoteza taratibu sana. Sijui umelishwa nini ndugu yangu,kila siku umaarufu wako unazidi kupotea. Mimi ushauri ninaotoa ni kutoka moyoni mwangu kabisa,jichunguze halafu chukua uelekeo sahihi.

Naomba nitoe mifano ya mambo ambayo yamekupotezea umaarufu sana kwenye jamii.
1. Kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya Dowans huku ukijua ina utata na ni uvunjaji wa sheria ya nchi.
2.Kukubali kuingia kwenye tume ya madini ya Rais (tume ya Bomani) ambayo ilikuwa "danganya toto" kwani tume nyingi zimepita hakuna mapendekezo yanayofanyiwa kazi.
3.Kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chadema halafu KUJITOA KWENYE HATUA ZA MWISHO.
4.Kutoa mapendekezo ya kutaifisha mitambo ya Dowans huku ukijua huo nu uvunjaji wa sheria na haki


Zitto Kabwe jichunguze,kama ndiyo mambo yale yale ya kupewa kitu kidogo ili uwe hivyo ulivyo ni hatari sana. Au umejengewa kale kaghorofa pale makongo juu?





 
Usipotoshe. Uchunguji ni wa muda mrefu. Umekuwa public hivi karibuni tu. TAKUKURU kimsingi chombo cha dola chini ya Ofisi ya Rais (Head of State). Head of State yupo juu ya mihimili yote mitatu. Rais kama Head of the Executive ndio mhimili mmoja. Lakini kama Mkuu wa Nchi ni mlinzi wa Katiba na sheria zilizotungwa kwa mujibu wa Katiba. Mbona Tume ya Maadili ya Viongozi inaendesha zoezi la kuchunguza mali za wabunge kwa kutuita na kutuhoji hamna kelele.

Msitetee uhalifu. Acheni tuhojiwe na kama tuna makosa tuwajibike. Hakuna visasi hapa!

Hapa zito sikuelewi. Hivi huu utaratibu umeanza awamu ya nne? Je huko nyuma hawakuwa wakipokea posho mara mbili? na kama imejulikana wamepokea posho mara mbili, kuna haja gani ya kuchunguza yaliyo wazi? Si mhalifu apelekwe mahakamni ndo akajitetee? Halafu, hiyo kesi inakuwa ni ya nini: kwani mbunge ameomba apewe hizo posho au ni bajeti ya wizara husika? Na kama ni bajeti, si lazima ilipitishwa hapo hapo bungeni? Mbona haya mambo mi nayaona ya kitoto, kwani kama huu utaratibu wa posho hautakiwi, jambo moja ni kuwa ufutwe. hapo baada ya kupigwa marufuku , ndipo itakuwa kosa kupokea hizo posho mara mbili. Nadhani takukuru hapo siwaelewi, ni njia tu ya kutaka kusema: wote tu wachafu. Huu ndio ujinga uleule aliosema Edward Lowasa, kwamba tukinyoosheana vidole hapa habaki mtu. Maana yake ninini?
 
Kweli kweli kweli, Mambo si mazuri kwa selikali yetu. Timing ya TAKUKURU kuwahoji wabunge inawalakini kabla ya hata kuzungumzia mamlaka yao kisheria. Kung'ang'ania kuchunguza upokeaji wa posho mara mbili, kama kwamba kesi kubwwa na zenye maslahi zaid kwa taifa hazipo, kunaleta maswali mengi kuliko majibu kwwa janga la ufisadi lililoikaba koo taifa letu.

Serikali inapoonekana kushindwa au kukataa kutekeleza maazimio ya bunge, chombo muhimu kama TAKUKURU kuonekana Ku "majoring in minors and minoring in majors" ndipo kweli WM anapotakiwa kujiuzulu akifuatiwwa na Mkurugenzi wa TAKUKURU.
 
kumshambulia Zitto!, mlikuwa serikali ya Kayombo nini nyie??

Haya makundi yenu ndiyo yanawaaibisha, JF ni huru, na ukiwa huru wa mawazo utakuwa huru kusema kwa uhuru, makundi si mahali pake hapa, maana ubishi wa bila sababu haujaleta manufaa, urafiki huu ndiyo umewazaa akina JK kuwachagua washikaji kwenye position nyingi! yet we are blaming them bad leaders


ebu ona pumba hizi!

!
Hii siyo imeanza jana au leo amevutana na kamati ya Mwakyembe, TV zimeonyesha mivutano yote hiyo! na sasa ndo anakuja na hoja hizo hizo watu wanaelewa, watu wana akili, JF bado ni huru nivizuri kumwelimisha kama hajui.
 
Kweli sisi watanzania ni wadumavu wa fikra....yaani unamtetea Mwakyembe ambaye amepokea posho mbili mbili kwa kuwa aliongoza kamati teule???Hivi mnajua kuwa hivi fedha wanazolipwa wakitembelea Halmashauri zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kununulia madawa, kujenga zahanati, na shughuli nyingine za maendeleo??sasa Mwakyembe kala hela za madawa halafu sisi tunamtetea huku wananchi wanakufa kwa kukosa madawa, UPUUZI MTUPU!!
 
hivi Tanzania kuna Bunge teh teh ..mie naonaga tu wanakalia vile viti wanasinzia tu wanajitahidi kuongea pointless ambazo wananchi hatujawatuma ,wanachukua posho na kujimuvuzisha makwao kupimzika
Mimi nionanvyo
FL1
 
ndugu jibu hoja usilete vihoja tunakupa masaa kadhaa ukiendelea na tabia hizi za kushambulia watu binafsi utakuwa banned

USINITISHIE WEWE, kwani Hosea,Lowassa na wengine wote ambao huwa wanajadiliwa humu siyo watu binafsi? Hoja zinahusu watu hao, haiwezekani kutoa hoja bila kumuhusiha mtu kwani hoja zinawahusu watu. Kama imekuuma sana kumueleza Zitto Kabwe ukweli na kama una uwezo wa kuniban kama usemavyo, I had rather be banned other than shut my mouth.

Umeisoma post yangu vizuri?
Hoja gani unataka nijibu?
Au unataka nijibu unavyotaka wewe?
Kama unataka nifikiri unavyotaka wewe haitawezekana,kwani mimi ni tofauti na wewe,ndiyo maana unanitishia ukidhani mimi ni muoga kama wewe. Unaonyesha ni muoga sana usiyependa hoja zinazopingana nawe. Hebu elezea ni kioja kipi nimetoa hapo. Don't judge without a reason,give a reason for every judgment you make,Don't be a foolish judge.
 
"Naomba nitoe mifano ya mambo ambayo yamekupotezea umaarufu sana kwenye jamii.
1. Kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya dowans huku ukijua ina utata na ni uvunjaji wa sheria ya nchi.
2.kukubali kuingia kwenye tume ya madini ya rais (tume ya bomani) ambayo ilikuwa "danganya toto" kwani tume nyingi zimepita hakuna mapendekezo yanayofanyiwa kazi.
3.kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chadema halafu kujitoa kwenye hatua za mwisho.
4.kutoa mapendekezo ya kutaifisha mitambo ya dowans huku ukijua huo nu uvunjaji wa sheria na haki
zitto kabwe jichunguze,kama ndiyo mambo yale yale ya kupewa kitu kidogo ili uwe hivyo ulivyo ni hatari sana. Au umejengewa kale kaghorofa pale makongo juu?"


KWELI KABISA, ZITO ZUBERI KABWE AMEBADILIKA SANA! KUNA BAADHI WANADAI ALIKUWA MDOGO SASA AMEKUA!
 
Ninachoona hapa Wabunge wamelipwa posho kwa ridhaa ya watendaji wa makampuni au taasisi husika. Tathmini ya kiasi cha malipo ingefanywa na Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Serikali na kutolewa tamko la Serikali aidha pesa zirudishwe au mazoea hayo yasitishwe. Mikutano katika mashirika ya binafsi wakati wa kazi ni sehemu ya kazi hivyo hakuna posho, lakini kwa mashirika ya umma ni tofauti na mtu anaweza kuhudhuria vikao zaidi ya kimoja ndani ya muda wake wa kazi kisheria na akalipwa posho. Enzi zile za SCOPO hili lingethibitiwa kwa kutolewa mwongozo hata sasa mwongozo ni muhimu zaidi badala ya kuchunguza jambo ambalo liko wazi na bayana kwamba posho zinatolewa
 
Tatizo hapa ni hii selective application of justice.

Hakuna watu wanaoongoza kuchukua posho mara mbili kuliko mawaziri wa serikali.

Huu uchunguzi ukiutazama vizuri umelenga wabunge tu wasio mawaziri. TAKUKURU kama inafanya kazi kwa maslahi ya taifa, iwachunguze na mawaziri kuhusu kupokea posho lukuki kutoka kwenye mashirika yaliyo chini ya wizara zao. TAKUKURU haitakiwi kuwa chombo kinachofanya kazi kwa interests za kijikundi kidogo cha watu kama ilivyo sasa.

Wabunge msirudi nyuma kwenye maazimio ya RICHMOND, HOSEA....OOUT!
 
hivi Tanzania kuna Bunge teh teh ..mie naonaga tu wanakalia vile viti wanasinzia tu wanajitahidi kuongea pointless ambazo wananchi hatujawatuma ,wanachukua posho na kujimuvuzisha makwao kupimzika
Mimi nionanvyo
FL1

Kimsingi waTZ tuvumiliage tu matatizo yetu lakini hatuna cha bunge wala serikali ya maana. Wanaoitwa wabunge wa TZ ni watu wanaenda kukusanya posho na kuondoka kula chao na vimada wao basi.
 
99% ya wanasiasa wa tanzania ni njaa kali hivyo ni wezi tu nao zitto ukiwemo.
Zitto hajajitoa. Anataka na yeye achunguzwe. Kama ulimwangalia jana jioni wakati ule wa muswada wa bodi ya korosho utajua tu ni kiasi gani suala hili la WANASIASA kujichotea mapesa ya UMMA linavyomtenganisha Zitto na Wabunge wenzake.Linapunguza sana ile dhana ya Bunge kuwa MUHIMILI wa pili wa DOLA.
 
Kaka unajua Mramba alihojiwa na kufikishwa mahakamani akiwa Mbunge? Unajua stori ya yule mbunge wa Morogoro aliyeburuzwa na Landrover la Polisi kwa madai ya Maji? Hawa nani alikuja hapa kuwatetea na kusema tawi la utendaji lisiingilie Bunge?

Kuna tatizo la msingi katika Taifa letu na katika mfumo wa Bunge. Fanya tafiti zako, ni Bunge la Tanzania tu duniani ndilo halina utaratibu wa kudhibiti mienendo ya Wabunge. Nchi nyingine wana mtu anaitwa Kamishna wa mienendo (Office of the Commissioner for standards). Huyu huchunguza mienendo na ile ambayo ni ya kijinai huenda katika jinai na ile ya kimaadili (hili la posho ninadhani ni la kimaadili) linakwenda kamati ya Maadili na kisha Bunge kutoa adhabu.

Mwaka 2004 Sheria ya maadili ilirekebishwa ili Bunge lipitishe 'code of conduct' kwa wabunge. Mpaka leo hatujapitisha. Mwaka 2008 niliwasilisha muswada binafsi ili kuunda code na kisha kuunda ofisi ya Kamishna huyu. Mpaka leo Ofisi ya Spika imekalia muswada huu na kukataa kuupeleka kuwa gazzetted ili ujadiliwe Bungeni.

Hivi MwanaKijiji unajua wabunge wanasafiri kwa mabasi kutoka Dar kuja Dodoma na wanagushi risiti kuwa wanakuja kwa magari yao na wanalipwa. Unajua Wabunge wakiwa hawapo Bungeni au kwenye Kamati wanasainiana posho za vikao?

Tunafanya makosa, halafu hakuna code wala mamlaka ya kutuchunguza halafu tuachiwe. Hapana. Mwanakijiji wewe kwa heshima yako hupaswi kutetea uvunjifu wa maadili.

Waache TAKUKURU wafanye kazi yao. Lazima Wabunge tujue kuwa hatupo juu ya sheria na kwamba tupo accountable na answerable kwa vitendo vyetu (for actions and inactions).

Zitto,
TAKUKURU wako right kabisa, lakini wanachofanya hawafanyi at a right time, timing yao ndio inayoleta walakini na mvutano, baada ya Hosea kuona anajadililiwa yeye anafanya counter attack ili apunguze makali ya mumjadili. Muhimu Hosea awajibike kama maagizo ya bunge yanavyotaka na baadaye kuhojiwa kuenedelee kwa kufuata taratibu na ile wawe fair kwa kiasi kinachotakiwa waanze na mawaziri, manaibu, wabumbe, makatibu wakuu na washuke chini zaidi, natoa hoja.
 
Zitto,
TAKUKURU wako right kabisa, lakini wanachofanya hawafanyi at a right time, timing yao ndio inayoleta walakini na mvutano, baada ya Hosea kuona anajadililiwa yeye anafanya counter attack ili apunguze makali ya mumjadili. Muhimu Hosea awajibike kama maagizo ya bunge yanavyotaka na baadaye kuhojiwa kuenedelee kwa kufuata taratibu na ile wawe fair kwa kiasi kinachotakiwa waanze na mawaziri, manaibu, wabumbe, makatibu wakuu na washuke chini zaidi, natoa hoja.
Kwa nini tunahusisha hili suala la posho haramu za Wabunge na suala la Hosea/Richmond? Dr Hosea sio PCCB na wala taasisi hii haitafutika huyu bwana akiondoka!
 
Sio wabunge wetu peke yao wenye haka ka-mchezo. Tujifunze kwa wenzetu wa Uingereza.

http://www.accessinitiative.org/blog/2009/05/british-speaker-resigns-–-a-victory-transparency

http://www.telegraph.co.uk/news/new...Brown-criticises-gentlemens-club-Commons.html

http://www.nytimes.com/2009/05/20/world/europe/20britain.html?_r=2

Ninavyoona mimi Zitto yuko sahihi kuwa kuna haja ya kuwa na chombo ndani ya bunge kusimamia maadili yao. Wakati umefika kwa wabunge wetu kuonyesha kweli wanastahili kuitwa waheshimiwa.

Tunahitaji kuwa na sheria ya uhuru wa habari. Raia au mkazi yeyote (kama alivyofanya Heather Brookes) awe na haki ya kufuatilia matumizi ya wabunge na bunge pamoja na maofisa wengine wa serikali na mahakama.

Vyama vya siasa vichukue hatua ya kudhibiti wabunge wao wenye haka kamchezo maana inaelekea ni siri iliyo wazi.

Viongozi wetu wanapogundulika kuwa wamechukua posho kutoka kwa shirika lingine lolote ili watoe huduma fulani na wasipotimiza, waajiri wake wawachukulie hatua. Magazeti yahakikishe kuwa haki inatendeka. Mifano ni mingi ya waheshimiwa na viongozi wengine kukaribishwa kwenye makongamano, kulipiwa gharama zote na waliowaalika lakini pamioja na yote hayo wanahudhuria kwa saa kiduchu na kutokomea wanakojua wenyewe. Wenye tabia kama hizi wanatakiwa waanikwe mbele ya umma.

Wabunge wakumbushwe kuwa wao ni raia kabla ya kuwa wabunge. Kinga yao ni kwa vitendo watakavyofanya kama wabunge. Wakifanya vitendo ambavyo haviendani na wadhfa wao watachukuliwa hatua kama raia mwingine. Wakiiba, wakibaka, wakipokea au kutoa rushwa, wakiwapiga wafanya kazi wao, wakiwadhulumu wafanyakazi wao, raia wengine au mtu mwingine yeyote n.k. watafunguliwa mashtaka na kuburuzwa mahakamani kama raia yeyote. Mbona hata Marekani wabunge wengi tu wamefikishwa kwa pilato kwa kupokea hongo itakuwa sisi!

Lakini pamoja na hayo, makosa kama haya ambayo Takukuru wanayavalia njuga si mojawapo. Haya yako ndani ya uwezo wa bunge, vyama vyao na waliowapeleka bungeni kushughulikia. Kama kuna majina ya wenye kamchezo huu basi waanikwe kwa umma tuwajue ili tusiwachague tena safari ijayo.

Amandla.....
 
Back
Top Bottom