Taifa letu la kesho linaandaliwa hapa

Lakini hata hivyo si unacheki matofali hapo!?? watu wako shughulini kwa hiyo kimsingi kwa upande wao naona wanataka ku upgrade kutoka miti na tope kuwa matofali tena naona ya kuchoma hayo.
Anyway lets see 2010 is so closer

What does 2010 got to do with this?
 
Najuuuuta kuzaliwa nchi moja na EL, RA et al!! Haya yote nisingekuwa nayapitia, Jesus Christ!!
 
pamoja na hali hii Meneja wa TRA analipwa 18,000,000Tsh kwa mwezi akale yeye na awapandao, pia Meneja wa TBC, Meneja wa Tanroads, Wabunge, Waziri wa elimu nk .

Huku Spika 6 akikodishiwa nyumba ya million 10 kwa mwezi.
 
Wakuu taifa letu kuandaliwa hapo haisumbui wala haliumizi vichwa vya viongozi wetu wa sasa so long as viongozi wetu wa kesho hawandaliwi hapo! Viongozi wetu wa kesho ( soma keshokutwa maana tulionao sasa wengi wao ni wa tangu uhuru 1961 mmoja wapo kingunge!) ambao ni watoto wa viongozi wa sasa wanaandaliwa nje ya nchi halafu wakirudi wanaingizwa kwenye siasa ili kuja kurithi viti vya wazazi wao baadaye!
 
Mtoto
Yani mkuu, at times huwezi kuelewa kuwa wote hawa wanaishi nchi moja. Na cha kuudhi zaidi ni mmoja anakula pesa ya mwenzake. Kweli Mungu awalipe mara 100.

Shapu
Huku Spika 6 akikodishiwa nyumba ya million 10 kwa mwezi.

ndo maana kunawakati wizi unaitwa distribution of wealth. Wala siungi mkono wizi, lakini ni kitu kisichoweza kuepukwa kama pengo la masikini na matajiri litakuwa kubwa kupita kiasi.

Pia huwezi kutegemea amani ya kudumu kama gap ktk jamii linakuwa kubwa la kutisha. Let say, mshahara wa mwezi mmoja wa meneja wa Tanroads ni 18Mil. Gharama za kujenga darasa moja ni sh 5 - 7 Mil. Hivyo, huyu jamaa anaweza akawa analipwa 8Mil na kiasi kinachobaki kikajenga madarasa mawili kila mwezi.
 
WANAFUNZI12.jpg


Kazi ipo!

Na wakati huo huo, serikali ya Kikwete inataka kutoa bilioni 21 kwa makampuni nchini on top of trilion zaidi ya moja atakazopewa fisadi Noni kwa ajili ya TIB.

Kikwete anaipeleka hii nchi kuzimu.
 
meneja wa TRA na TBC wa tanzania nk wana mshahara mkubwa kuliko waziri mkuu wa Uingereza - Brown, huu ni wizi wa ukufuru. Hiwi viongozi wa Tanzania hawana hata aibu jamani? mimi hapa nilipo niko hoi
 
Hapa silaumu mafisadi.

Yaani wameshindwa kwenda kukata fito na miti kadhaa na kuja kujenga hizo kuta?

Sehemu za madirisha zingeachwa wazi ila vijana wawe ndani. Yaani hata udongo na fito nayo ni kazi? Hicho kijiji ni cha kuchapa viboko. Hiki ni kilema cha kutegemea serikali ije itufanyie kila kitu. Kijiji kizima kingelifanya hiyo kazi siku moja tu.

Inabidi kupata jina la Mbunge wa eneo hilo, mkuu wa wilya, mkoa, katibu kata, katibu tarafa, mwenyekiti wa kijiji....... Huu ni ukiwete mbaya kabisa duniani --KILEMA CHA MAWAZO.

Ningelaani kama kusingelikuwa na madawati na mabati juu. Hii shule ni BOMBA sana sana ukilinganisha na wengine tulizosomea. Masanilo, kama umetembea Sikonge nafikiri ulijionea mwenyewe shule za huku kwetu kama Iyombakuzova, Mibono, Pangale, Ipole, Tumbili, Utawambogo nk.

Hebu tuache kulaani kila kitu MAFISADI. Wananchi inabidi tubebe lawama ya asilimia 40 ya hali hii kwa ujumla. Yaani hakuna MWALIMU Juma wa kutibu magonjwa ya namna hii? Ningelimpeleka huko akatibu UTINDIA UBONGO wa Kijiji kizima. Mengine nakubali lawama ila hili mwenzenu SINUNUI.

Samahani sana kama hujui maana ya public goods uliza kwanza. Nini kazi ya kodi ya wazazi wa hao watoto kama wao wanatakiwa pamoja na kulipa kodi wajenge madarasa? Ni kwa siasa hizi hizi za kuwakandamiza raia na kutokuwaeleza nini haki yao katika serikali ndo maana rushwa haitaisha maana haki na favour hazitofautishwi nchini mwetu. Kwa mtu yeyote anaejali asingethubutu kutamka hayo maneno. Kama una moral standards jaribu kuona GDP ya tanzania inachangiwa na akina nani na je bila wao primary producers of goods je hizo jeuri zingetoka wapi? Wakati mwingine kua mstaarabu, bila kumumunya maneno MAFISADI NDO CHANZO cha halii hiyo no less no more.
 
Hiyo picha mbona haina tatizo lolote? unajua ninyi mnaoishi ng'ambo mmezoea sana kuangalia movies na maisha ya huko mlipo..hamna idea ya mambo yanayoendelea nchini kwenu.
 
Hiyo picha mbona haina tatizo lolote? unajua ninyi mnaoishi ng'ambo mmezoea sana kuangalia movies na maisha ya huko mlipo..hamna idea ya mambo yanayoendelea nchini kwenu.

Haina tatizo? Basi wewe umeridhika na hali iliyopo....kaazi kweli kweli
 
Inasikitisha sana nenda kainchi kama Rwanda wametupiku mbali mno tatizo letu hapa kinacho tuuumiza sisi ni kukumbatiana na mafisadi,
 
Kwa maoni yangu binafsi hapo ndipo tunavyoonyesha tulivyo. Ukiangalia picha unaona madawati, mabati, udongo mzuri tu wa kutengeneza matofari ya kuchoma au ya vumbi.

Ni kitu gani kinachoshindikana kutumia materials ya ujenzi vizuri? Mambo mengine sio watu kukaa nje au rocket science, it's just a common sense.
 
Ni kitu gani kinachoshindikana kutumia materials ya ujenzi vizuri? Mambo mengine sio watu kukaa nje au rocket science, it's just a common sense.

Kinachoshindikana au kinachokosekana ni akili. Watu wenye akili hawawezi kuishi ktk mazingira kama hayo. Kama unabisha, hebu observe hata hapo ulipo. Uki observe vizuri utagundua kuwa watu wenye akili kwa 'ujumla' huwa wana maisha mazuri zaidi kushinda wale wasio na akili.
 
Serikali haipo serious kuwekeza kwenye elimu...! Kwani ikiacha kuwanunulia wabunge mashangingi just kwa miaka kumi tu, na badala yake wapewe pikipiki... kisha hizo pesa zikatumika kuwekeza kwenye elimu si tutakuwa tumepiga japo hatua chache kwenye kuboresha mazingira ya watoto wetu!?
 
Kinachoshindikana au kinachokosekana ni akili. Watu wenye akili hawawezi kuishi ktk mazingira kama hayo. Kama unabisha, hebu observe hata hapo ulipo. Uki observe vizuri utagundua kuwa watu wenye akili kwa 'ujumla' huwa wana maisha mazuri zaidi kushinda wale wasio na akili.

Mkuu,

Kuwa na akili au kutokuwa nazo si tatizo, tatizo ni kuwa na akili na kushindwa kutumia akili hizo.
 
WANAFUNZI12.jpg


Haya na endeleeni kubisha kuwa Miafrika Sivyo Tulivyo! Watu wenye akili na ubunifu wangetumia akili na ubunifu wao kuboresha hayo mazingira ya kujifunzia. But guess what...wanasubiri lidude liitwalo serikali kuja na kuwaboreshea mazingira yao. Wanachosahau ni kwamba hata hilo lidude liitwalo serikali limejaa mijitu mijinga isiyo na akili kama wao. I guess unapokuwa mjinga hata kumtambua mjinga mwenzako inakuwa kaaazi kweli kweli.

haya ni maeneo ya pwani, wanapata upepo mzuri hasa ukizingatia hili joto.
darasa kama hili haliwezi kuwekwa sehemu yenye baridi kama Njombe, Mufindi, Arusha ama baadhi ya maeneo ya kilimanjaro tehetehetehe
 
Back
Top Bottom