Taifa letu la kesho linaandaliwa hapa

Lakini ieleweke kuwa Taifa letu bado ni changa ,Rais wetu anafanya jitihada za hali ya juu kuondowa matatizo yanayotukabili ,tuwe wenye ustahamilivu kwa kipindi hiki kigumu ,tumpeni muda angalau inatia moyo hao wanafunzi wapo juu ya mabenchi na kupatiwa elimu.

Changa? huyu mtoto ambaye hakui ana tatizo gani?

Tatizo kuna mashimo mengi mno yanayovujisha rasilimali zetu.Yakizibwa yote naona hili taifa likiruka na kukimbia tena mbio za ajabu badala ya kutambaa kwa kusuasua.
 
Samahani sana kama hujui maana ya public goods uliza kwanza. Nini kazi ya kodi ya wazazi wa hao watoto kama wao wanatakiwa pamoja na kulipa kodi wajenge madarasa? Ni kwa siasa hizi hizi za kuwakandamiza raia na kutokuwaeleza nini haki yao katika serikali ndo maana rushwa haitaisha maana haki na favour hazitofautishwi nchini mwetu. Kwa mtu yeyote anaejali asingethubutu kutamka hayo maneno. Kama una moral standards jaribu kuona GDP ya tanzania inachangiwa na akina nani na je bila wao primary producers of goods je hizo jeuri zingetoka wapi? Wakati mwingine kua mstaarabu, bila kumumunya maneno MAFISADI NDO CHANZO cha halii hiyo no less no more.

Shangazi baelezee hawa bandugu. KODI (TAX) kazi yake ni nini? Ni fisadi tu ndio atatoa mawazo ya mtu anayelipa kodi ajipatie huduma kama hizo. Kwenye ilani za uchaguzi si kuna vitu kama kuboresha Elimu, je hiyo humaanisha nini? Hata kama wakijenga madarasa baadaye si wataambiwa wafundishe walimu kwa ajili ya shule hizi? Wakimaliza hapo watambiwa wanunue vitabu!! Ni Tanzania tu haya yanawezekana.

Hiyo picha mbona haina tatizo lolote? unajua ninyi mnaoishi ng'ambo mmezoea sana kuangalia movies na maisha ya huko mlipo..hamna idea ya mambo yanayoendelea nchini kwenu.

I hope you were being sarcastic.

Kwa maoni yangu binafsi hapo ndipo tunavyoonyesha tulivyo. Ukiangalia picha unaona madawati, mabati, udongo mzuri tu wa kutengeneza matofari ya kuchoma au ya vumbi.

Ni kitu gani kinachoshindikana kutumia materials ya ujenzi vizuri? Mambo mengine sio watu kukaa nje au rocket science, it's just a common sense.
Shule siyo majengo tu. Jengo hafifu nalo ni hatari zaidi kwa usalama na afya za watoto. Halafu kusema wawekeze muda wao kujenga madarasa kuzalisha kwa ajili ya familia zao watafanya saa ngapi? Wakiumia katika ujenzi nani atawalipia matibabu?


Kinachoshindikana au kinachokosekana ni akili. Watu wenye akili hawawezi kuishi ktk mazingira kama hayo. Kama unabisha, hebu observe hata hapo ulipo. Uki observe vizuri utagundua kuwa watu wenye akili kwa 'ujumla' huwa wana maisha mazuri zaidi kushinda wale wasio na akili.
Tunarudi kwenye suala la matumizi ya kodi zao. Hebu tueleze huko uliko kama watu wanajenga madarasa na kuchimba mitaro ya barabara. Kodi inakusanywa na inafanya kazi yake ipaswayo. Kwetu inakusanywa na ama kujenga mahekalu Msata, Mikocheni na nyingine kufichwa Jersey Island halafu mwananchi anaambiwa hana akili.
 
Hebu tueleze huko uliko kama watu wanajenga madarasa na kuchimba mitaro ya barabara. Kodi inakusanywa na inafanya kazi yake ipaswayo. Kwetu inakusanywa na ama kujenga mahekalu Msata, Mikocheni na nyingine kufichwa Jersey Island halafu mwananchi anaambiwa hana akili.

Wananchi hawana akili kwa sababu habari za hizo hela za kodi na misaada kuibwa zinajulikana na kila baada ya chaguzi wananchi wanachagua watu hao hao kuwaongoza.

Remember the definition of insanity given by Einstein...doing same thing (voting for CCM) over and over and expecting different results (progress)..
 
Sipati picha, mwanafunzi na haswa wa kike akihitaji kujisaidia huwa inakuwaje hapo???
 
jamani hata fito zinauzwa vijijini, siku hizi hamna vitu vya bure
matofali ya udongo yanahitaji labour nani atalipia hzio
hela zote zinazoliwa ni more than enough kwa wanafunzi wa TZ kusomea kwenye madarasa hauweni

hapo akili ni pesa tu na sio kitu kingine
 
Kwa wenzetu duniani watoto kama hao wana shule yaliokua well equipted, tena katika umri huo wanatumia computers. Imagine watoto hao pichani lini wana tamaa ya kuiona wacha kuitumia computer ? Na huko kwa wenzetu ninaozungumzia ni maskini ama kama au kushinda sisi, lakini wana well utilised their resourses. Far Eastern countries nyingi hazina natural resourses kama Tz, utalii na small industries ndio pato lao kubwa. Utasikia wana CCM kwenye mikutano yao hasa wakati wa kampeni za uchaguzi (hasa huko visiwani ) wakisema kua " Ona maendeleo karibu kila kilomita kumi utapata shule na zahanati " Yes I agree utaona lakini ni majengo tu bila ya chochote ndani, Zahanati ilokua haina hata karatasi ya daktari kukuandikia prescrition , If you are lucky huenda ukapata panadol 2 tab. God knows zime expire mwaka gani. Huu ndio Uhuru aliotuletea na aliotuachia Mwalimu. Imagine this country was ruled by Mwalimu who was graduate at Makerere at that time.
 
Watu wengi humu wanatoa majibu marahisirahisi tu kama ma-desktop researchers, hakuna substance..hiyo shule ninavyoiona iko poa tu..watoto wameketi kitako..wanapunga upepo na probably wanakula shule yetu ya kitanzania..

labda wale wazee wa kuchungulia mambo kwa angle ya kighaibuni mnadhani tatizo la picha hiyo ni nini?
 
Samahani sana kama hujui maana ya public goods uliza kwanza. Nini kazi ya kodi ya wazazi wa hao watoto kama wao wanatakiwa pamoja na kulipa kodi wajenge madarasa? Ni kwa siasa hizi hizi za kuwakandamiza raia na kutokuwaeleza nini haki yao katika serikali ndo maana rushwa haitaisha maana haki na favour hazitofautishwi nchini mwetu. Kwa mtu yeyote anaejali asingethubutu kutamka hayo maneno. Kama una moral standards jaribu kuona GDP ya tanzania inachangiwa na akina nani na je bila wao primary producers of goods je hizo jeuri zingetoka wapi? Wakati mwingine kua mstaarabu, bila kumumunya maneno MAFISADI NDO CHANZO cha halii hiyo no less no more.

Wee Felister,

Wala sipokei samahani yako. Naona na wewe uko katika kilema kilekile. Unafikiri ukishatoa kodi basi umemaliza kazi. Ndiyo maana tuna ukilema wa mawazo kwa kila kitu.

Kama ningeliupata ubunge wa eneo hilo, kabla sijapata fedha basi ningeliwahenyesha wanakijiji na mie mwenyewe siku nzima hadi tumalize hizo kuta na ndiyo niwaruhusu. Mie ningelifanya kazi bure na wao bure. Hayo ya hela za kodi ndiyo ningelifuatilia baadaye.

Mama, tafadhali sana. Nduguyo kijijini leo akianguka na kuzimia, utaita ambulance maana umetoa kodi. Isipofika, UTAKAA chini pwetee kusubiri hadi ifike. Kibaya zaidi unaweza kukuta ndiyo wanaisubiri ije kutoka German maana wametoa msaada. Na bandarini nako kitu hakitoki maana wafanyakazi wa TACT (Karamagi) wamegoma. Utasubiri sana hadi .......

Sijui kama umeshasafiri nchi wanazotoa kodi na kufuatilia hizo kodi. Siyo kweli kuwa kwa wazungu ukitoa kodi basi umemaliza kila kitu.
Nilishawahi kumtembelea Ngosha mmoja pale Stockholm (dr Sal. salamu zako) na akaniambia jambo lililonishangaza sana. Wakati wa winter, kwenye jengo lao (gorofa) ni kuwa ikianguka snow(barafu), ni kazi ya member wote kumwaga mchanga around hilo jengo na kuizoa hiyo snow. Mtu akipita hapo na akateleza na kuvunjika, basi member wote wanaoishi hapo, mtalipia gharama za matibabu. Na sweden gharama ya matibabu iko juu kinoma.
Kwa hiyo, hebu tupisheni na huu kupweteka kwenu kwa kusubiri kila kitu mje mfanyiwe na serikali ya matapeli na nyie wenyewe mnaKURA maraha. Watu wanakaa kwenye mitaro ya maji machafu, mvua ikinyesha watu wanatapisha vyoo, mifereji ya maji kila mwaka na hawawezi kujijengea kadaraja kadogo ili wasilowane. Mkisikia michango ya harusi, birthday, kitchen party na upupu mwingine, mnawahi ili MKARE BIA....... MIAFRICA.

Serikali ya KIFISADI ya Tanzania tumeshaisema sana. Kama tutaanza kubadilika na kufuatilia hali kama hizi, utakuwa mwanzo mzuri. Fisadi akija katika kijiji kama kile, anajua hapa ni ng'ombe na T-shirt, umechaguliwa. Akija na kukuta watu wamejitahidi kwa kutumia kila kilichopo ili kubadili maisha yao, basi hata FISADI atajua hapa kuna kazi kweli maana muamko uko juu.....

Sawa mama FISADI NDIYO CHANZO CHA KILA MATATIZO YA WATANZANIA. Nina amini kuwa TUKIUWA MAFISADI YOTE, basi TANZANIA ITAKUWA NI kama EUROPE. Kodi yetu itatupa kila kitu tunachotaka.
Is this not sounding like USSR era????? Ufanye kazi, usifanye kazi, UNALIPWA.
 
Serikali haipo serious kuwekeza kwenye elimu...! Kwani ikiacha kuwanunulia wabunge mashangingi just kwa miaka kumi tu, na badala yake wapewe pikipiki... kisha hizo pesa zikatumika kuwekeza kwenye elimu si tutakuwa tumepiga japo hatua chache kwenye kuboresha mazingira ya watoto wetu!?

nenda mwakani kagombee ubunge na usikubali kupewa shangingi utakuwa ume-make difference tatizo mnailaumu serikali bila kuelewa kuwa ni wabunge hao ndo wanataka hayo mashangingi.
 
Tumejaaliwa utajiri chungu nzima mbuga za wanyama za kuvutia ambazo karibu kila mwaka zinaingiza mabilioni ya shilingi. Tuna misitu ya kutosha ambayo inavunwa kila mwaka na kuingiza mabilioni ya shilingi. Tuna madini ya dhahabu, Tanzanite, Almasi ambayo mikataba yake ilisainiwa bila kuweka maslahi ya nchi mbele.

Kamwe hatustahili kuwa na shule ambayo iko katika hali mbaya kama hii katika sehemu yoyote ile Tanzania, lakini cha kusikitisha na kukatisha tama shule kama hizi ziko nyingi sana katika mikoa yetu mbali mbali nchini.

Nchi ina mabilionea kupitia ufisadi akina Rostam, Subhash, Chavda, Jeetu, Karamagi, Mkono, Mzindakaya na wengineo ambao wengi wao wanaona fahari kubwa kutoa michango ya mamilioni kumsaidia mgombea Urais badala ya kusaidia Watanzania kama hawa wanaoishi maisha ya dhiki kubwa na kusoma shule ambazo hazina hadhi hata ya kuitwa choo.

Sijui Kikwete au Pinda kama watakuwa katika ziara ya wilaya hiyo na kupelekwa kuitembelea shule hiyo watasema nini kuhusiana na hali mbaya ya shule hiyo.

Miezi michache ijayo tutasherehekea miaka 48 tangu Tanganyika ipate uhuru wake toka kwa wakoloni, lakini Watanzania walio wengi hawaoni manufaa yoyote ya kuishi katika nchi huru yenye utajiri wetu mkubwa tuliojaaliwa ambao unawafaidisha Mafisadi wachache na ‘viongozi' mafisadi na waroho wa utajiri wa haraka haraka akiwemo Mkapa, Chenge, Rostam, Mzindakaya, Mkono, Mramba, Chavda, Jeetu, Subhash, Manji na wengineo ambao mpaka sasa wameiba zaidi ya shilingi Trilioni na hakuna hata mmoja ambaye ameonekana na hatia hadi sasa.

Picha ya shule hii haiendani kabisa na ahadi za Kikwete katika kampeni zake za kuwania Urais 2005 alipowaahidi Watanzania "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Kikwete akiamua kupunguza bajeti yake ya safari za nje kwa asilimia 50 basi shule kama hizi nchini zinaweza kabisa kuwa na hadhi ya kuitwa shule kama hiyo 50% ya punguzo katika bajeti za safari za nje ambazo hazina tija zitaelekezwa katika shule hizi. "Mabilioni ya Kikwete" ambayo nayo hatujui yameishia wapi, si ajabu yalidakwa na mafisadi, kama yangeelekezwa katika ‘shule' kama hizi basi labda nyingi ya shule zetu zingekuwa katika hali ya kuridhisha.

Wabunge wote wanaotoka katika majimbo yenye shule zinazofanana na hii na Bungeni wanachapa usingizi bila ya kuyatetea majimbo yao kamwe hawastahili kuwa wawakilishi wa wananchi katika majimbo hayo maana wako bungeni kwa maslahi yao binafsi na si ya wapiga kura wa majimbo yao. Wabunge wengi Wanapiga kelele za unafiki kwenye vikao vya Bunge lakini mwisho madudu yotem ufisadi na maudhi yanabaki kama yalivyo miaka nenda miaka rudi huku maisha ya Watanzania walio wengi yakizidi kuwa ya kuhuzunisha.

Kuna haja ya kuwashinikiza viongozi wa mikoa yote Tanzania kuacha unafiki wao na kuhakikisha Kikwete na Pinda wanapokuwa katika ziara za mikoa hiyo kuwaonyesha hali halisi katika mikoa yao badala ya kuwapeleka katika shule chache ambazo zina hali nzuri.

Mungu ibariki Tanzania
 
Mkuu wazazi wanachangia sana ujenzi wa madarasa, vyoo na madawati, tena kwa lazima na hiari, labda tujiulize hivi viongozi wanakaa umbali gani na shule?

Umeona wajamaa wenzako hao wakila shule....kwikwikwikwi....
 
Back
Top Bottom