Candela
JF-Expert Member
- Aug 12, 2021
- 638
- 1,686
Kama unasoma uzi huu basi u buheri, pole kwa wenye changamoto.
Hawa vijana wanaosajili laini za simu mitaani wamekuja na mbinu mpya kukuibia pesa.
Wanatumia app za kampuni husika, TIGO PESA APP AU MPESA APP n.k. Wanawahadaa wateja kuwaunga 5G wapate intaneti yenye kasi bure kama ofa.
Ukikubali anakwambia utoe laini uweke kwenye smartphone yake aiwezeshe, hapo anaunga namba yako na App kwenye simu yake.(Hizi app huwezi kuunga kama laini haipo kwenye simu).
Atakwambia uweke namba ya siri na anakuwa ameweka namna ya kurekodi screen touches so akitoka hapo namba yako ya siri anaijua.
Akimaliza anakupa laini yako anasepa, so anabaki na App akiwa na uwezo wa ku access akaunti yako ya TIGOPESA ama MPESA n.k.
Wamempiga mtu hapa 46,000 wakakopa na nivushe, ye anashangaa anaona meseji za TIGOPESA tu anakamilisha miamala.
Kuweni makini jamani, pia muelewe 5G ni hardware sio kitu cha kuwekewa kama kifaa chako hakina 5G support usidanganyike. Kama laini yako haina 5G basi nenda kabadilishe laini.
NINI CHA KUFANYA KAMA HILI LIMESHAKUKUTA.
Download App husika kwa mtandao wako(kama tayari ipo ifute u dowload upya), jisajili katika hiyo huduma then ukiwa ndani ya app nenda kwenye sehemu ya Vifaa vyangu(jihudumie/Settings), ukikuta zaidi ya kifaa kimoja futa usichokitambua.
Nawasilisha.