Vijana wanaosajili laini mitaani za mitandao ya simu wengi ni wezi

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,196
Hii nimeithibitisha kwa watu zaidi ya wawili mtaani kuna dogo alikuwa akisajili laini za Tigo basi akamwambia jamaa amboreshee laini yake ili aweze kupata mb na dakika nyingi kwa elfu moja tu.

Basi jamaa akaona kama kuna hiyo ofa bora aboroshewe laini yake na huyo wakala wa Tigo alikuwa akimwambia jamaa lazima ktk simu yake kuwe na shilingi 100 jamaa akanunua vocha na kuweka ndipo wakala wa tigo akamwambia jamaa atoe lain yake ktk simu yake kisha iwekwe kwenye simu ya wakala wa Tigo akidai kuna program ya ku boresha laini ya mteja.

Kitendo cha kuweka lain ktk simu ya wakala hela yote ilikombwa kwenye simu ya jamaa basi wakala akamwambia jamaa naona mtandao upo chini hivyo zoezi litakuwa gumu wakala akasepa jamaa kuangalia masalio pesa hakuna

Hivyo basi msisajili laini mitaani nendeni kwenye maduka ya watoa huduma ni hatar sana kesi imefunguliwa tatatibu za ufuatiliaji jamaa anaendelea nazo kwani laini iliyohamishiwa pesa ni ya mtandao wa Airtel ambao jamaa alipewa na wahudumu wa mtandao na taarifa zote za muhimu kapatiwa.

Na kibaya zaidi jina la wakala msajili laini linasoma la kike wakati wakala ni wa kiume kivyovyote kasajiliwa au wanashirikiana ntaweka hapa majina (Mariamu Sozi) hii ina maana kama mwanamke hausiki basi jamaa ka mchoma atawajibika bado kumsajilia mtu laini ni hatari.

Nawaza hao mawakala watakuwa wamewaibia sana watu na jeshi letu la polisi walivyo wazito ktk kesi hizi za wizi wa mitandao hadi uwape rushwa ndipo wakufanyie kazi yako

Tukio limetokea Mbezi Malamba mawili kwa osama
 
Yaani ukichimama nchale, ukikaa nchale, ukikimbia nchale sijui tutaponaje hata!
 
Nakumbuka Nilikuwaga nashida na laini ya halotel haraka zangu nikakutana na hao jamaa nikasajili ,aisee baada ya kusajili nilikuwa napata wrong Kila siku na namba sikuwah kuigawa baadae usajili wa laini ukabadiliswa likaja jina la kike.

Mwisho nikaamua niititupilie mbali
 
Hatar sana mkuu
 
Pia wanatumia kitambulisho chako kusajilia lina zaidi ya moja unapo mpa namba yako ya Nida akianza kusajilia atakusajilia line yako....pia atasajili line zaidi ya moja kwa Namba yako ya Nida,atajifanya kama fingerprint hazisomi vizuri atakwambia urudie rudie kumbe ndio anasajili line zingine,Mimi nimesajiliwa line Tigo Moja,ila nikiangalia usajili wa line kwa namba yangu ya Nida kuna namba mbili za Tigo Moja siitambui,Airtel nilisajili Moja ila zipo tatu mbili sizitambui.

Kuna Dogo alikuwa anasajili line anathibitisha ni kweli,Hapo inatakiwa uende kwenye maduka ya mitandao husika ukafute namba usizozitambua.

Hawa vijana ni wezi....jiulize zile line wanazoziuza zimeshasajiliwa vitambulisho au Namba za Nida huwa wanazitoa wapi?
 
Hii point kubwa sana mkuu hili sikulitanbua kabisa yaani
 
Back
Top Bottom