Uko sawa mkuu ila uhuru bila moderation ni tohu wa bohu manake ni chaos tupu! Utashangaa hata mambo ya wakubwa yanaletwa hapa hata mada nyingine zisizoendana na Ugreat thinker bado zinaletwa hapa. I support!Niko negatv kidooogo mkuu wangu
Mkuu, MMU ina mambo mengi ikiwa ni pamoja na chit chat, majibu ya mzaha na raha ili mradi watu wana relax. Ina topic muhimu sana na za mchanganyiko.Niko negatv kidooogo mkuu wangu ,nahisi hii itapunguza uhuru wa mchangiaji na kutokuwa tena sehemu ya new ideal ,kwanza ni criteria gani zinatumika kuijaji post kuwa ni upuuz inabidi mzidefine na ziwe specific,pili ukisha edit post ya mchangiaji nadhani ipost kwa jina lako kwa maana inakuwa yako si yake ni ya editor. USHAURI: Iwapo mtaset hizo criteria sasa then ikionekana haifai isipostiwe kabisa sio kuituma ukiiedit hiyo ni kuingilia right to identity ni crime
Kutokana na hali ambayo imekuwa ikiendelea humu kwenye Jukwaa la MMU kwa muda mrefu napenda kuwafahamisha members wote kuwa kuanzia sasa thread zote ambazo zitakuwa posted hapa MMU zitakuwa under MODERATION kabla hazijawa approved tumeamua kufanya hivi kwa sababu kumekuwa na mlolongo wa TOPIC zisizokuwa na maana yoyote au TOPIC ambazo kimsingi hazina mantiki yoyote ndani ya Jukwaa hili.
Halikuwa lengo letu kufanya hivi ila kwasababu hali hii imeendelea kwa muda mrefu bila watu kujirekebisha hivyo basi tumeona itakuwa ni busara tukaliweka Jukwaa hili under MODERATION kama tulivyofanya kwenye Jukwaa la Siasa, topic ambazo tunaona zinafaa kukaa hapa zitawekwa hapa na ambazo tutaona hapa sio mahala pake zitahamishwa na kupelekwa Jukwaa husika. Lengo hasa ni kufanya maboresho kwenye Jukwaa hili na kuiweka JF katika hatua nyingine tofauti na sasa hivyo tunaomba sana ushirikiano wenu.
Poleni kwa usumbufu, na wale ambao watakwazika tunawataka radhi.
Uwamuzi mzuri, watu wajipange kabla ya kuleta topic wakati mwingine zinakuwa marudio na za kukosa busara kabisa kama mlevi fulani wa gongo.