Ushauri unahitajika: Niko njia panda, kila maamuzi ninayotaka kufanya naona yana athari

seludao85

New Member
Feb 19, 2024
1
23
Wasalamu wana MMU

Mimi ni member wa jukwaa hili wa muda mrefu. Nimeamua kuja na ID hii mpya kwa ajili ya hili suala.

Mimi ni kijana chini ya miaka 38. Nimeo ila ndoa yangu imeingia kwenye mgogoro mkubwa. Niko njia panda, kila maamuzi ninayotaka kufanya naona yana athari.

Kwa ufupi ndoa yangu ina zaidi ya miaka 10 na tumejaliwa kupata watoto watatu. Ndoa yangu imekua na migogoro tangia mwaka wa kwanza lakini naona sasa mambo yamekua magumu. Tatizo kubwa ambalo limekua linasumbua ni kuwa mwanamke ana dharau, ni jeuri, hasikii. Yaani hawezi kabisa kunisikiliza kwa jambo lolote. Hata akifanya kosa ukimuuliza yeye ndio anakufokea.

Hivi karibuni nilipata safari ya kwenda nje ya nchi na nimekaa huko mwaka mzima. Wakati niko huko ndio hali ya dharau iliongezeka. Wote sisi ni waajiriwa. Lakini ili kuongeza kipato tuliamua kufungua mradi. Sasa wakati niko huko akawa hataki nijue chochote kuhusu mradi. Yaani anajibu kabisa hawezi kunipa taarifa zozote za maendeleo ya mradi. Nikawa naishi lakini sijui tunaingiza nini kwenye mradi. Tulikopa bank mkopo wa biashara ili tuweze kupata na mtaji mkubwa.

Sasa nikiwa huko akawa ananiambia tu kuwa rejesho halitoshi, ukimuuliza kuwa mmeingiza kiasi gani na matumizi yakoje mpaka pesa yote iishe, anakujibu tu kuwa wewe unatakiwa ujue kuwa pesa haitoshi. Anasema hawezi kunipa mahesabu. Anasema niko nje ya Tanzania na yeye ndio yuko na mradi kwahiyo hawezi kunipa mahesabu. Anakwambia kuwa hujaniajiri kwahiyo siwezi kukupa raarifa yoyote. Hata ukimwambia pesa fulani ufanyie kitu fulani anakujibu kuwa atafanya lakini baadae hafanyi na anafanya matumizi yake anavyoona yeye. Ukimuuliza anakujibu kuwa hakujisikia kuniambi.

Kuna mambo yalijitokeza ila siwezi kueleza yote lakini baada ya mgogoro kuwa mkubwa nikawajulisha wazazi na kuomba kufanya kikao pindi nikirudi Tanzania. Nilirudi Tanzania mwanzonu mwa mwaka huu. Tukakaa kikao cha wazazi wote pamoja na baadhi ya ndugu. Kwenye kikao akaahidi kuwa atabadilika. Lakini baada ya kikao hakubadilika. Kelele zikawa ni za kila siku. Tunagombana kila siku.

Lakini kubwa ambalo limenileta hapa ni jambo ambalo ameniambia ambalo niseme kuwa linanitafuna sana. Kwenye malumbano akaniambia kuwa mimi nina maumbile madogo na hayamtoshi, anasema maumbile haya sio size yake. Na pia kazi siiwezi. Kwakweli suala hili limekua kaa la moto kwangu. Anasema wazi kuwa ameshanitoa moyoni mwake.

Kutokana na hii migogoro imefikia hatua naona suluhisho ni kuachana na hii ndoa. Yeye anasema hana mpango wa kuomba talaka ila anataka mimi ndio niende mahakamani kuomba talaka. Nilikuja kugundua anataka tuachane lakini hataki kuomba talaka kwasababu ya nyumba tuliyojenga.

Mimi nitaondoka hivi karibuni kwenda tena nje ya Tanzania. Lakini nimekua napata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali. Wapo wanaoniambia kuwa niachane na ndoa hii. Wapo wanaonisihi nisiachane naye kwa maslahi ya watoto. Mimi nilikua tayari kumsamehe kwenye migogoro ya nyuma ila hili ya kuniambia kuwa maumbile yangu sio size yake linanipa mtihani mzito sana. Najiuliza nitaweza kweli kuishi na yeye katika hali hii. Kibaya zaidi hata tendo la ndoa hataki kabisa kushiriki na mimi. Naombeni ushauri wenu kwenye suala hili. Je hali hii haiwezi kuniathiri?

Jambo lingine ni kuwa biashara ile imekufa, kwahiyo nitalazimika kulipa deni la bank kutokea vyanzo vingine. Tuliweka nyumba tunayoishi dhamana. Najiuliza je niendelee kulipa hili rejesho na wakati hakuna matumaini ya ndoa. Najiuliza kuwa nijitese huku wanaume wengine wanamtumia. Kuna muda napata hasira na kuwaza kuacha kuhangaika na hili deni kama bank watauza nyumba wauze.

Naombeni ushauri wenu. Nimechanganyikiwa sijui uamuzi gani nichukue.
 
Kabla ya kupewa ushauri inabidi utandikwe makofi ya kelbu kwanza ujinga ukutoke.

Mwanaume unaendeshwaje na mwanamke?

Uko nje ya nchi unatuma tu hela halafu ukiuliza maendeleo hupewi jibu, ila hela unatuma tu???

Sasa inabidi utandikwe makofi kwanza ili ujinga ukutoke huko kichwani mwako.
 
Kwa mtizamo wangu wewe ndio unakuza tatizo sababu mwanamke inaonekana anakutawala na anajua hauwezi kumuacha ndio maana anakuonesha dharau na kukujibu anavyotaka.

Katika maisha kipaumbele cha kwanza inatakiwa kuwa furaha na amani kwako kabla ya mtu mwingine. Kukaa kwenye ndoa ya aina hiyo ni kujitafutia stress na magonjwa yasiyoambukiza.

Kama yeye hataki kutoka, toka wewe ukaanze upya maisha muachie yeye nyumba na watoto
 
Keshapata bwana na si ajabu pesa ya biashara yenu ndo ilikuwa inaweka chumba na sebule cha yule boda wake mwenye guu la mtoto....na pia anahisi kazi yake ndo kila kitu jifanye kama mjinga enda inje ya inji jifanye kama umesahau kila kilichotokea endelea kuwasliana naye ukisalimia watoto ili ayakoroge mwenyewe aende zake atakuja kurudi
 
Wasalamu wana MMU

Mimi ni member wa jukwaa hili wa muda mrefu. Nimeamua kuja na ID hii mpya kwa ajili ya hili suala.

Mimi ni kijana chini ya miaka 38. Nimeo ila ndoa yangu imeingia kwenye mgogoro mkubwa. Niko njia panda, kila maamuzi ninayotaka kufanya naona yana athari.

Kwa ufupi ndoa yangu ina zaidi ya miaka 10 na tumejaliwa kupata watoto watatu. Ndoa yangu imekua na migogoro tangia mwaka wa kwanza lakini naona sasa mambo yamekua magumu. Tatizo kubwa ambalo limekua linasumbua ni kuwa mwanamke ana dharau, ni jeuri, hasikii. Yaani hawezi kabisa kunisikiliza kwa jambo lolote. Hata akifanya kosa ukimuuliza yeye ndio anakufokea.

Hivi karibuni nilipata safari ya kwenda nje ya nchi na nimekaa huko mwaka mzima. Wakati niko huko ndio hali ya dharau iliongezeka. Wote sisi ni waajiriwa. Lakini ili kuongeza kipato tuliamua kufungua mradi. Sasa wakati niko huko akawa hataki nijue chochote kuhusu mradi. Yaani anajibu kabisa hawezi kunipa taarifa zozote za maendeleo ya mradi. Nikawa naishi lakini sijui tunaingiza nini kwenye mradi. Tulikopa bank mkopo wa biashara ili tuweze kupata na mtaji mkubwa. Sasa nikiwa huko akawa ananiambia tu kuwa rejesho halitoshi, ukimuuliza kuwa mmeingiza kiasi gani na matumizi yakoje mpaka pesa yote iishe, anakujibu tu kuwa wewe unatakiwa ujue kuwa pesa haitoshi. Anasema hawezi kunipa mahesabu. Anasema niko nje ya Tanzania na yeye ndio yuko na mradi kwahiyo hawezi kunipa mahesabu. Anakwambia kuwa hujaniajiri kwahiyo siwezi kukupa raarifa yoyote. Hata ukimwambia pesa fulani ufanyie kitu fulani anakujibu kuwa atafanya lakini baadae hafanyi na anafanya matumizi yake anavyoona yeye. Ukimuuliza anakujibu kuwa hakujisikia kuniambi.

Kuna mambo yalijitokeza ila siwezi kueleza yote lakini baada ya mgogoro kuwa mkubwa nikawajulisha wazazi na kuomba kufanya kikao pindi nikirudi Tanzania. Nilirudi Tanzania mwanzonu mwa mwaka huu. Tukakaa kikao cha wazazi wote pamoja na baadhi ya ndugu. Kwenye kikao akaahidi kuwa atabadilika. Lakini baada ya kikao hakubadilika. Kelele zikawa ni za kila siku. Tunagombana kila siku.

Lakini kubwa ambalo limenileta hapa ni jambo ambalo ameniambia ambalo niseme kuwa linanitafuna sana. Kwenye malumbano akaniambia kuwa mimi nina maumbile madogo na hayamtoshi, anasema maumbile haya sio size yake. Na pia kazi siiwezi. Kwakweli suala hili limekua kaa la moto kwangu. Anasema wazi kuwa ameshanitoa moyoni mwake.

Kutokana na hii migogoro imefikia hatua naona suluhisho ni kuachana na hii ndoa. Yeye anasema hana mpango wa kuomba talaka ila anataka mimi ndio niende mahakamani kuomba talaka. Nilikuja kugundua anataka tuachane lakini hataki kuomba talaka kwasababu ya nyumba tuliyojenga.

Mimi nitaondoka hivi karibuni kwenda tena nje ya Tanzania. Lakini nimekua napata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali. Wapo wanaoniambia kuwa niachane na ndoa hii. Wapo wanaonisihi nisiachane naye kwa maslahi ya watoto. Mimi nilikua tayari kumsamehe kwenye migogoro ya nyuma ila hili ya kuniambia kuwa maumbile yangu sio size yake linanipa mtihani mzito sana. Najiuliza nitaweza kweli kuishi na yeye katika hali hii. Kibaya zaidi hata tendo la ndoa hataki kabisa kushiriki na mimi. Naombeni ushauri wenu kwenye suala hili. Je hali hii haiwezi kuniathiri?

Jambo lingine ni kuwa biashara ile imekufa, kwahiyo nitalazimika kulipa deni la bank kutokea vyanzo vingine. Tuliweka nyumba tunayoishi dhamana. Najiuliza je niendelee kulipa hili rejesho na wakati hakuna matumaini ya ndoa. Najiuliza kuwa nijitese huku wanaume wengine wanamtumia. Kuna muda napata hasira na kuwaza kuacha kuhangaika na hili deni kama bank watauza nyumba wauze.

Naombeni ushauri wenu. Nimechanganyikiwa sijui uamuzi gani nichukue.
Aisee. Hilo la kukuambia kuwa Abdala wako ni mdogo, ni kutaka tu kuumiza moyo wako. Wanawake wanajua sana vitu vinavyofanya wanaume waumie ni kudharaulika kwenye ile shughuli. Anyways, Timu kataa ndoa inapata bao jingine la penalti....
 
Back
Top Bottom