Taarifa kwa Umma-Tamko la J.Nassari kuhusu Tamko la NMC

Better late than never, na heri nusu shari kuliko shari kamili.

Hii statement imeanza vizuri lakini naona kama imeishia njiani. Bado alitakiwa atoa paragraph ya mwisho (hitimisho) inayo - withdraw maneno yake na kuwataka watanzania wasikwazike.

Nassari kama unapitia hapa, anayekushitaki ni Nape na wapambe wake, na wanakushitaki kwa umma wa Tanzania. Hivyo wewe ulitakiwa uandike statement inawayotaka watanzania kutokwazika na maneno yako na uoneshe 'sincerity' kwamba umeyaondoa. Usizunguke kusema 'watu wanataka kupotosha' maana kutoposha maneno ya CHADEMA is what Nape does for a living. Wewe focus on what you have to do, and that is, to withdraw maneno 'tata'

Hata hivyo, ni mwanzo mzuri na inatia moyo kuona mwanasiasa anakubali udhaifu. Hili ndilo tumekosa kwa ccm. So next (I hope there won't be next) deal with the shortfall regardless mpinzani wako anasemama nini. Tusonge mbele.
 
Ulichokisema ni kipi bwana mdogo? Hicho ndo kitaweka bayana nini watanzania tufahamu/tutafsiri kuhusu kauli yako.
Hapa hujafunguka. Nadhani ni bora hata mwenye CD ya mkutano wa NMC basi atupostie humu ili tumsikilize huyu kijana kama ambavyo ya LUSINDE yalivyowekwa bayana.
Asante.
 
Nassari siyo kichaa. Hayo aliyoyasema ndiyo aliyokuwa anafikiria. Hata mlevi ukiona ametamka neno ujuwe kuwa ni kitu ambacho kilikuwa moyoni mwake alikuwa anshindwa tu kukitoa hadharani.

Binafsi nadhani Chadema wana fursa kubwa ya kupambana na CCM na ikiwezekana kuchukua nchi lakini kauli kama za akina Nassari zinafanya Watanzania wafikiri tena. Watanzania siyo wajinga hata kidogo. Jana nimesoma kwenye Posting mmoja hapa JF mwandishi akiwaomba kuwa muache kupiga nyimbo za dini kwenye mikutano yenu. Hili nalo ni muhimu. Tungeni nyimbo zenu kama CCM walivyofanya.

Chadema pamoja na matatizo mengi wanayoyapata kutoka Polisi na chama tawala ni lazima kabisa wajifunze kuwa wanasiasa makini. Neno au tendo moja tu linaweza kuvuruga mambo.
 
" Lengo
la hotuba yangu lilikuwa kuweka
msisitizo ili serikali na jeshi la
polisi lishughulikie matatizo
makubwa ya muda mrefu
mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi
mpaka kupelekea baadhi ya
watu kupoteza maisha, "

Mh mbunge kama nilivyokunukuu hapo juu, unaposema lengo la uloyasema ni namna ya kuweka msisitizo ili mamlaka zishughulikie matatizo. Je huoni kwamba namna ya uwasilishaji wa agizo lako lilizua hiyo sintofahamu...
Mi naamini binadamu sio malaika kuna wakati tunateleza hata katika matamshi na jambo la msingi kwako Mh ungeomba msamaha japo indirect,..
Nawasilisha.!
 
Naona sasa itabidi wapotoshaji wote waome msamaha. Maana wamepotosha sana lakini wamekwama.
Ukweli ndio huo.
Watu wengi sana huwa wananaswa kirahisi sana na mitego ya CCM.
Jamaa kadhaa humu JF wako 'kikazi' zaidi, wako busy kuanzisha thread ambazo information zake zimepotoshwa.
Halafu wachangiaji wanaingia kichwa-kichwa kwenye mtego wa kuchangia thread yenye contents zilizopotoshwa.
Mimi nilijiuliza sana, mbona wachangiaji wanasema Nasari aombe msamaha? Aome msamaha kwa lipi ???

Haya tena wapotoshaji, katika hili mmekwama, jaribuni tena baadaye !!!
 
Hii ndiyo aina ya Viongozi na Wanasiasa tunaohitaji... Mbona ZNZ kuna watu kwa sababu kama hizi za Nasari wameamua kuandamana ili kujitenga na Tanganyika na Bado wanapeta? mbona sijawahi kusikia Ismail Jusa akihojiwa na Polisi? Lakini amekuwa Mstari wa Mbele kutoa kauli kama hizi za watanzania.

mimi nafikiri tafsiri halisi ya alichokisema Nasari ni kwamba watu wako kwenye Dimbwi la matatizo si serikali wala Viongozi wake wanajishughulisha kuyatatua.. Imefika mahali watu wanauawa serikali inapiga blah blah... Sasa hivi Arusha Mjini si haina Madiwani, Meya, wala Mbunge na watu wanauawa kila kukicha jeshi la polisi liko kimya CCM ndiyo watuhumiwa hakuna hatua inayochukuliwa kwa hiyo kilichobaki ni kutoa shinikizo ambalo litawaamsha polisi na viongozi wa CCM..

Nasari hakuwa na maana ya kuwagawa watanzania hata kidogo. Ila waTZ tushagawanyika siku nyingi kati ya CCM na CDM hili si la kuuliza.

Wasitake kuwavuruga wananchi, M4C itawamaliza mwaka huu.

Kwanza JK hana mpango wa kutembelea Arumeru Mashariki wala A town tunajua yeye misele yake ni Nje ya Nchi tu

Red......wanajua sababu ya kunyamazia hiyo kitu maana watafumua makubwa zaidi kuhusu muungano ndo maana hawadandii hoja hiyo, cjasikia Magamba wakitao matamko ya wazi.
 
Hii ndiyo aina ya Viongozi na Wanasiasa tunaohitaji... Mbona ZNZ kuna watu kwa sababu kama hizi za Nasari wameamua kuandamana ili kujitenga na Tanganyika na Bado wanapeta? mbona sijawahi kusikia Ismail Jusa akihojiwa na Polisi? Lakini amekuwa Mstari wa Mbele kutoa kauli kama hizi za watanzania.

mimi nafikiri tafsiri halisi ya alichokisema Nasari ni kwamba watu wako kwenye Dimbwi la matatizo si serikali wala Viongozi wake wanajishughulisha kuyatatua.. Imefika mahali watu wanauawa serikali inapiga blah blah... Sasa hivi Arusha Mjini si haina Madiwani, Meya, wala Mbunge na watu wanauawa kila kukicha jeshi la polisi liko kimya CCM ndiyo watuhumiwa hakuna hatua inayochukuliwa kwa hiyo kilichobaki ni kutoa shinikizo ambalo litawaamsha polisi na viongozi wa CCM..

Nasari hakuwa na maana ya kuwagawa watanzania hata kidogo. Ila waTZ tushagawanyika siku nyingi kati ya CCM na CDM hili si la kuuliza.

Wasitake kuwavuruga wananchi, M4C itawamaliza mwaka huu.

Kwanza JK hana mpango wa kutembelea Arumeru Mashariki wala A town tunajua yeye misele yake ni Nje ya Nchi tu

Kasome katiba ya zanzibar!
 
Mbona kama ni APOLOGY Kwa watanzania lakini haiko wazi. Si afunguke tu aseme he was wrong.

Kweli mkuu anajificha nyuma ya Mbowe utafikiri ndio anamfikiria cha kuongea na jinsi ya kumsahihisha.
Hata hivyo nampongeza kwa kutambua ukweli kuwa AMEWAKOSEA WATANZANIA na siyo CCM kwa matamshi yake.
Kuelewa vile tu ni toba tosha kabisa.
 
Kimsingi, Nassari ameelezea nia ya maneno yake lakini hakuomba msamaha. Nimependa jinsi alivyoonyesha kwa sababu kuomba omba msamaha kunonyesha utoto
 
Wale wanaomwita Nassari kinda anayehitaji kufundishwa kuvaa kaptula baada ya kuwa mbunge wakiwemo gazeti la Mwananchi waseme sasa.
Walisema hana busara waseme pia
 
*taarifa kwa umma*

ninalazimika kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani... Hotuba yangu niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya nmc arusha siku ya jumamosi tarehe 5, mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga chadema kutokea vyama mbalimbali vya siasa hususani chama tawala ccm.

Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa chadema, chama ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa watanzania wote katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala dhamira ya kuwagawa watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa.

Hata hivyo, mwenyekiti wangu wa taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema mwenyekiti ndio msimamo wangu japokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano. Lengo la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au kumzuia rais kutekeleza wajibu wake

joshua nassari (mb)
mei 09, 2012.

hajaomba radhi kwa wale waliomuelewa vibaya, arudi atubu
 
haiwezekani mkuu, hii ni kamanda nyingine kabisa born in singida kwa mwingulu mchemba, ila nipo kwa ajili ya kuwakilisha mawazo mazuri ya chadema na wananchi wake

mshauri huyu kijana mwenzetu tena sociologist asiwe mwoga kusema samahani kwa wote mlioudhika na mtamshi yangu. Halafu anaweza pia kufungua akaunti nyingine na kutangaza waziwazi kuwa ndiye yeye ili baadhi ya mambo awe anayatolea ufafanuzi kupitia linki hii
 
Wale wanaomwita Nassari kinda anayehitaji kufundishwa kuvaa kaptula baada ya kuwa mbunge wakiwemo gazeti la Mwananchi waseme sasa.
Walisema hana busara waseme pia

Watoke wapi kaka, CCM wana tabia mbaya sana, wawe wanakuja na kauli za kutupongeza basi tunapofanya makubwa katika kutoa elimu kwa ya uraia, mambo ya kutuvizia ymepitwa na wakati
 
Naona sasa itabidi wapotoshaji wote waome msamaha. Maana wamepotosha sana lakini wamekwama.
Ukweli ndio huo.
Watu wengi sana huwa wananaswa kirahisi sana na mitego ya CCM.
Jamaa kadhaa humu JF wako 'kikazi' zaidi, wako busy kuanzisha thread ambazo information zake zimepotoshwa.
Halafu wachangiaji wanaingia kichwa-kichwa kwenye mtego wa kuchangia thread yenye contents zilizopotoshwa.
Mimi nilijiuliza sana, mbona wachangiaji wanasema Nasari aombe msamaha? Aome msamaha kwa lipi ???

Haya tena wapotoshaji, katika hili mmekwama, jaribuni tena baadaye !!!

Wewe nini wewe,
We si yule mmoja aliyesema Nassari hatakiwi kuomba msamaha kwa waTanzania?
Sasa busara imetawala na dogo janja a.k.a ze totoz amekwisha omba msamaha . Na sisi waTanzania hatuna noma tunaikubali kwa vile hakutegemea matokeo hayo.
Nyie ndo mnapotosha hata masuala nyeti ya Utaifa na kufikiri every thing is on the table.
Utaifa na kuuchezea is a no-go-area.
Uelewe hivyo!
Umenukuliwa vizuri sana hapa chini:
Hii mentality ya kujikomba kwa chama tawala na kutaka 'kuomba msamaha' kwa kila jambo unalolifanya imeenea sana hapa JF.
Kwa mwendo huu, mimi naona itafika wakati Chadema wataambiwa waombe 'msamaha' kwa kuongea maneno, au kufanya mambo ambayo si mazuri masikioni mwa CCM. Mathalani, Nasari itabidi aombe 'msamaha' kwa kushinda kiti cha ubunge Arumeru Mashariki, maana ushindi huo si mzuri machoni mwa CCM na polisi !!!!!
Mimi sijaona jambo lolote la kuombea msamaha katika hotuba ua Nasari.
Watu wengi wanasema tu 'aombe msamaha'. Ila hawasemi aombe msamaha kwa lipi ???
Watu wasichangie hapa kama watoto wadogo. Ukisema 'aombe msamaha', toa nukuu ya kipande cha hutoba husika ambacho anatakiwa 'akiombee msamaha'.
Yaani watu wengi sana hapa JF wamenasa kwenye mtego wa CCM wa kutumia vyombo vya dola kutishia watu ili waombe msamaha.

If anything you have proven that HUNA BUSARA!
 
Wale wanaomwita Nassari kinda anayehitaji kufundishwa kuvaa kaptula baada ya kuwa mbunge wakiwemo gazeti la Mwananchi waseme sasa.
Walisema hana busara waseme pia

Mkuu hausomeki kabisa, na sijui kama ulisoma japo mara mbili hicho kilichoitwa tarifa kwa umma!
 
Back
Top Bottom