Tamko la Pamoja la Jumuiya za Vijana Vyama Pinzani nchini kuhusu Miswada.

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Sisi viongozi wa Jumuiya ya vijana kutoka vyama pinzani vitatu nchini Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Jumuiya ya vijana CUF (JUVICUF) na Jumuiya ya vijana -NCCR Mageuzi ambapo awali tulikuwa pamoja na viongozi wenzetu kutoka Baraza la vijana Chadema (BAVICHA) kuanzia hatua ya vikao hadi hatua ya mwisho ya maandalizi ya tamko hili la pamoja kabla ya wenzetu kuomba udhuru wa kutoshiriki katika tamko hili kwa sasa lakini bado tunaamini kama vijana tutaendelea kushirikiana pamoja huko mbele kwenye mambo mengi .

Kwaniaba ya vijana wenzetu nchini tunatoa tamko la pamoja kuweka msimamo wetu kupinga miswada mitatu ambayo ni muswada wa mabadiliko ya sheria uchaguzi, muswada wa sheria mpya ya Tume ya uchaguzi na muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa iliyowasilishwa na kusomwa na serikali kwa mara ya kwanza Bungeni tarehe 10/11/2023.

Sisi viongozi wa Jumuiya za vijana vyama pinzani nchini, tunaamini ya kwamba wajibu wetu mkubwa ni kulinda na kutetea maslahi na ustawi wa vijana nchini, kulinda ustawi wa demokrasia yetu nchini ili kuongeza hamasa na ushiriki wa vijana katika masuala ya kisiasa ,kijamii na kiuchumi ili kuleta uwajibikaji madhubuti, kupigania haki na usawa ili kudumisha amani ya nchi yetu. Sababu tunaamini ya kwamba matatizo yeyote aidha ya kisiasa ,kiuchumi au kijamii yanayoikumba nchi yetu waathirika wakubwa ni vijana kwa sababu vijana ndio kundi kubwa 70% ya idadi ya watu nchini ni vijana.

Sisi viongozi wa Jumuiya za vijana vyama pinzani tunaipinga miswada hii sababu ina kasoro na madhaifu makubwa, miswada hii haijabeba hoja zenye ustawi kwa vijana nchini, vifungu vingi vya miswada hii vimekinzana na katiba ya JMT 1977,miswada hii haitaleta usawa na haki nchini,miswada hii haitaimarisha demokrasia nchini na kupanua ushiriki wa kisiasa wa wananchi ,vijana na makundi mengine ,miswada hii haitaleta uwajibikaji kwa viongozi sababu ya kutokuwa na chaguzi huru na haki na hivyo kuendelea kuwa na mazingira hatarishi ya amani yetu kutoweka nchini kipindi cha chaguzi (Post Election Violence).

Athari zote zitakazojitokeza sababu ya kasoro na madhaifu ya miswada hii waathirika wakubwa ni sisi vijana sababu sisi ndio kundi kubwa nchini. Hivyo tumeainisha maeneo kadhaa 10 yenye mapungufu kwenye miswada hii kuonesha uhai wa hoja zetu hapo juu.

1. Tunapinga Wakurugenzi wa Jiji, Manispaa, Miji na Halmashauri pamoja na watumishi wa umma kuendelea kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Kifungu cha 6(1) cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinatoa fursa kwa wakurugenzi wa Jiji, Manispaa, Miji na Halmashauri na watumishi wa umma katika kifungu cha 6(2) kuwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo na kata. Tunapinga vikali kifungu hiki sababu wakurugenzi hawa hawana uhalali wa kusimamia chaguzi zetu sababu wengi wao ni wanachama wa CCM. Hawawezi kutenda haki na usawa sababu wamekuwa wakiegemea na kupendelea chama chao cha CCM na mifano dhahiri ni uchaguzi wa 2020 na chaguzi zingine za nyuma na chaguzi za marudio.

➢ Ni hoja dhaifu iliyo katika kifungu cha 6(6) cha muswada wa sheria ya uchaguzi inayosema msimamizi wa uchaguzi atatoa tamko la kujitoa au kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa, mbele ya Hakimu kwa kutumia fomu itakayoainishwa. Kifungu hiki kimekuwa kikitumiwa makusudi kudhoofisha ibara ya 74(14) ya katiba ya JMT inayokataza afisa yeyote wa uchaguzi kujiunga au kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

➢ Pia ni hoja dhaifu iliyo kwenye kifungu cha 21(1) cha muswada wa sheria mpya ya Tume ya uchaguzi inayosema, Mtumishi aliyeteuliwa au aliyeazimwa na Tume katika kipindi cha kutekeleza majukumu yake atachukuliwa kama mtumishi wa Tume. Hiki kifungu kinadanganya umma au kinapotosha sababu watumishi wanaozimwa na Tume ikiwemo wakurugenzi wa Halmashauri hawawajibiki kwa Tume ya uchaguzi bali kwa mamlaka yao ya uteuzi na nidhamu ambapo kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma Sura 298(Toleo la 2019) kifungu cha 5(1)(a) na (2) mamlaka ya uteuzi kwa wakurugenzi wa Halmashauri ni Rais wa JMT ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa.

Hivyo Wakurugenzi hawajawahi kuwajibika kwa Tume ya uchaguzi bali kwa Rais na chama chao cha CCM.

➢ Pia ni suala la kushangaza serikali kuendelea kung’ang’ania kuwatumia wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia chaguzi ikiwa tayari Mahakama ya Afrika imetoa hukumu mwezi Juni 2023 katika kesi iliyofunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe (Application No.011/2020), Mahakama ilizuia wakurugenzi kusimamia uchaguzi na kutoa miezi 12 (Mwaka mmoja) kwa serikali ya Tanzania kufanya marekebisho ya sheria. Kitendo cha Serikali kuendelea kuwakumbatia wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia chaguzi katika miswada hii inaashiria kiburi cha serikali kutoheshimu mahakama ya Afrika,mikataba ya kikanda na kimataifa.

➢ Pia inashangaza sana serikali kupuuza na kutoheshimu mapendekezo ya Tume ya uchaguzi yaliyotolewa tarehe 21/Agosti/2021 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan na Tume ya Taifa ya uchaguzi katika Ripoti yake ya uchaguzi wa Rais, wabunge na Madiwani ya mwaka 2020.Ili kuboresha mfumo wa chaguzi zetu Tume ya uchaguzi yenyewe katika kurasa wa 108 wa ripoti yake ya uchaguzi wa 2020 ilitoa mapendekezo makuu matano. Pendekezo namba 2 Tume ilipendekeza iwe na watendaji wake yenyewe hadi ngazi ya Halmashauri.

Mapendekezo

Vifungu hivi 6(1) na 6(2) katika muswada wa sheria ya uchaguzi vinavyohusu kutumia wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma vifutwe vyote na hivyo kutoa fursa kwa Tume ya uchaguzi kuajiri watendaji wake yenyewe ,wenye sifa zitakazoainishwa kuanzia ngazi ya Mkoa ,Wilaya hadi Halmashauri kwa ajira za kudumu na za muda. Watu waombe kwa sifa,wafanyiwe usaili wa wazi badala ya Tume kutumia wakurugenzi wa Halmashauri.

2. Tunapinga namna ya upatikanaji wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Muundo wa Tume ya uchaguzi na Sifa za wajumbe wa Tume.

➢ Kamati ya usaili yenye jukumu la kuchakata na kusimamia mchakato wa usaili,mamlaka yake yanaishia kwa wajumbe wa Tume ya uchaguzi tuu kama ilivoainishwa kwenye muswada wa sheria mpya ya Tume ya uchaguzi kifungu cha 9(1)(5)(6)(7)(8) kwamba wanao omba nafasi ya kuwa wajumbe wa Tume ndio wanapita kwenye mchakato wa kuomba na kufanyiwa usaili na kamati ya usaili. Ila kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha muswada wa sheria mpya ya Tume ya uchaguzi Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi bado wanateuliwa na Rais moja kwa moja bila kupitia mchakato wa kuomba na kufanyiwa usaili na kamati ya usaili.

Mapendekezo

•Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Tume na wao wanapaswa kupita kwenye mchakato wa kuomba na kufanyiwa usaili na kamati ya usaili kama wajumbe wengine wa Tume.

➢ Muundo wa Tume ya uchaguzi bado haueleweki, Katika kifungu cha 5(4) na 20 (1) cha muswada wa Tume ya uchaguzi ametajwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atakuwa Katibu na Mtendaji Mkuu wa Tume ya uchaguzi ambaye kwa mujibu wa muswada wa Tume ya uchaguzi kifungu cha 18(1) atateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya uchaguzi. Lakini kifungu cha 9(3) cha muswada wa sheria ya Tume ya uchaguzi kinasema Mkurugenzi wa uchaguzi atakuwa katibu wa kamati ya usaili yenye jukumu la kusimamia mchakato na usaili wa upatikanaji wa Tume ya uchaguzi. Muundo huu unapoteza dhana ya uwajibikaji na usimamizi.

Mapendekezo

• Kifungu cha 18(2) kirekebishwe ,Muundo wa Tume ya uchaguzi ugawike sehemu mbili yaani Bodi na Menejimenti , ambapo Bodi iwe chini ya Mwenyekiti wa Tume ambapo Bodi hii ndio inapaswa kufanya mchakato wa kuajiri Mkurugenzi wa uchaguzi kwa sifa zitakazo ainishwa na kwa uwazi .Mkurugenzi wa uchaguzi ndio atakuwa mtendaji Mkuu wa Tume ya uchaguzi na ataongoza Menejimenti katika utendaji wa kila siku. • Kifungu cha 9(3) kifutwe kumuondoa Mkurugenzi wa uchaguzi kuwa katibu wa kamati ya usaili na badala yake katibu wa kamati ya usaili awe Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

➢ Sifa za wajumbe na viongozi wa Tume ya uchaguzi bado hazikidhi.

Sifa za viongozi wa Tume na wajumbe wa Tume zilizoainishwa katika muswada wa sheria mpya ya Tume ya uchaguzi katika kifungu cha 7(1) na (2) bado sifa hizi hazikidhi kwani sifa ya kutokuwa mwanachama au kujihusisha na chama cha siasa hazijawekwa jambo ambalo ni kinyume na ibara ya 74(14) ya katiba ya JMT 1977 inayokataza afisa yeyote wa uchaguzi kujiunga au kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Pia kifungu cha 18(2)(d) cha muswada wa sheria ya Tume ya uchaguzi kifutwe ili kuondoa sifa ya Mkurugenzi wa uchaguzi kuwa Afisa muandamizi katika utumishi wa umma.

Mapendekezo

• Sifa ya kutokuwa mwanachama au kujihusisha na chama cha siasa inapaswa iongezwe kwenye kifungu cha 7(1) na (2) cha muswada wa sheria ya Tume ya uchaguzi ili iendane na ibara ya 74(14) ya katiba ya JMT 1977.

• kifungu cha 18(2)(d) cha muswada wa sheria ya Tume ya uchaguzi kifutwe ili kuondoa sifa ya Mkurugenzi wa uchaguzi kuwa Afisa muandamizi katika utumishi wa umma. Mchakato wa kumpata mkurugenzi ufanywe na Tume ya uchaguzi kwa uwazi kuruhusu mtu yeyote kuomba kulingana na sifa zingine zitakazoainishwa.

• Sifa za wajumbe wa Tume katika kifungu cha 7(2) cha muswada wa sheria mpya ya Tume ya uchaguzi uzingatie vijana. Kifungu kitamke angalau wajumbe wawili kati ya watano wawe vijana.

3. Tunapinga dhamana ya fedha inayowekwa na mgombea kwa msimamizi wa uchaguzi

Kifungu cha 35(1)(2) na 51(1) cha muswada wa sheria ya uchaguzi katika uchaguzi kinahitaji mgombea wa udiwani,Ubunge au Urais kuweka dhamana ya fedha baada ya uteuzi na fedha hizo zitataifishwa ikiwa mgombea atapata chini ya moja ya kumi ya kura zote halali zilizopigwa au kama mgombea atajitoa kugombea baada ya siku ya uteuzi.Tunaamini kifungu hiki kinalenga kuzuia ushiriki wa vijana katika kutumia haki yetu ya kushiriki katika masuala ya kiuongozi na maamuzi kama ilivyoainishwa katika katiba ya JMT 1977 ibara ya 21(1)(2), sababu vijana ndio tutakaoathirika zaidi na kifungu hiki sababu ya uwezo wetu mdogo wa kifedha na kiuchumi.

Mapendekezo

• Kifungu cha 35(1)(2) na 51(1) katika muswada wa sheria ya uchaguzi vifutwe sababu vipo kinyume na katiba JMT 1977 ibara ya 21(1)(2) inayoruhusu uhuru wa mtu kushiriki katika masuala ya kiuongozi na maamuzi. Pia kifungu hiki kinazuia ushiriki wa vijana, hivyo hakuna haja ya mgombea kuweka dhamana kwa msimamizi wa uchaguzi ni jambo ambalo halina mantiki, ikiwa mgombea amepitishwa na chama chake inatosha kumuamini badala ya kuweka vikwazo vya dhamana ya fedha.

4. Tunapinga zuio kwa asiyeridhika na maamuzi ya Tume kutokwenda mahakamani. (Ouster Clauses/Finality Clauses/Exclusionary Clauses)

Katika miswada hii bado kuna vifungu ambavyo vinaipa nguvu Tume ya uchaguzi na kupokonya mamlaka na wajibu wa mahakama kwamba maamuzi ya Tume ndio ya Mwisho.

Kifungu cha 37(6) cha muswada wa sheria ya uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea wa urais na mapingamizi kwamba uamuzi wa Tume ya uchaguzi wa kutomteua mgombea kiti cha urais utakuwa wa mwisho, kifungu cha 53(6) kwa uteuzi wa mgombea wa ubunge uamuzi wa Tume ndio wa mwisho na kifungu cha 65(7) kwa uteuzi wa mgombea udiwani maamuzi ya Tume ndio yatakuwa ya mwisho. Maamuzi hayo ya Tume hayata katiwa rufaa katika mahakama yeyote. Pia kifungu cha 137 cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinazuia matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani isipokuwa matokeo ya ubunge na udiwani tuu.

Mapendekezo

• Tunapendekeza mgombea apewe haki kwa mujibu wa katiba JMT 1977 ibara ya 13(6)(a) kama hajaridhika na maamuzi ya Tume ya uchaguzi kukata rufaa na kupinga maamuzi hayo mahakama kuu. Kitendo cha kuzuia kukata rufaa ni kinyume pia na ibara ya 107(A) ya katiba ya JMT 1977 inayotoa mamlaka kwa mahakama kama chombo cha maamuzi ya mwisho katika utoaji haki ndani ya JMT.

Pia kuzuia watu kukata rufaa kupitia mahakama ambayo ndiyo njia ya amani na usawa katika kutafuta haki tafsiri yake ni kuwatengenezea mazingira wananchi kutafuta haki yao kwa njia nyingine aidha barabarani au msituni jambo ambalo sio sahihi kwa ustawi na mustakabali wa nchi yetu.

5. Tunasikitika namna ambavyo miswada hii haijajumuisha hoja za vijana na masuala ya vijana ya muda mrefu ili kupanua wigo wa ushiriki wa vijana kisiasa

Ikiwa tunaamini ya kwamba 70% ya idadi ya watu nchini ni vijana,ni sahihi ya kwamba changamoto nyingi zinazokumba jamii kwa ujumla kundi linaloathirika zaidi ni kundi la vijana ,hivyo basi kundi la vijana ni kundi ambalo linapaswa kuangaliwa kwa jicho nyeti katika masuala yote ya kisera na kisheria ili kupanua wigo wa ushiriki wetu vijana katika masuala ya kisiasa , uongozi,uwajibikaji na maamuzi kwa mustakabali wetu vijana na ustawi wa taifa letu. Ila tunasikitika hoja zetu nyingi vijana hazijazingatiwa na kuingizwa katika miswada hii kama ifuatavyo.

➢ Muswada wa sheria ya vyama vya siasa haujazingatia hoja ya kulazimisha vyama vyetu vya siasa kuwa na asilimia kadhaa ya vijana katika hatua ya uteuzi wa wagombea wa ngazi ya udiwani na ubunge.Muswada utamke wazi kuwa 40% ya wagombea ndani ya vyama ngazi udiwani na ubunge wawe vijana.

➢ Muswada wa sheria ya vyama vya siasa unapaswa kulazimisha vyama vyetu kutenga asilimia kadhaa ya ruzuku inayotolewa kwenye chama itumike kuwezesha na kuhamasisha ushiriki wa vijana kwenye siasa kupitia shughuli na majukumu ya Jumuiya za vijana katika vyama.

➢ Muswada wa sheria ya uchaguzi na mabadiliko ya katiba ya 1977 inapaswa kuweka ukomo wa muda fulani katika kutumikia nafasi moja ya uongozi, ngazi ya udiwani na ubunge kama ilivyo nafasi ya urais.Muswada uweke ukomo wa miaka 10 wa mtu kutumikia au kugombea nafasi moja.

➢ Muswada wa vyama vya siasa na gharama ya uchaguzi unapaswa uweke kifungu cha kuilazimisha serikali kugharamia fedha za kampeni (Ruzuku)kwa wagombea wote vijana ili kupanua wigo wa ushiriki wa vijana.Katika uchaguzi wa 1995 iliwezekana wagombea kupewa ruzuku na Tume ya uchaguzi.

➢ Sifa za wajumbe wa Tume katika kifungu cha 7(2) cha muswada wa sheria mpya ya Tume ya uchaguzi izingatie vijana. Kifungu kitamke angalau wajumbe wawili kati ya watano wawe vijana. Pia asilimia kadhaa ya watendaji wa tume wawe vijana.

➢ Marekebisho ya muswada wa sheria ya uchaguzi na mabadiliko ya katiba ya 1977 ibara ya 67(1)(a) yafanyike kutoa fursa kwa kijana wa miaka 18 anayeruhusiwa kupiga kura pia awe na sifa ya kugombea nafasi ya udiwani hata ubunge na isiwe hadi umri wa miaka 21.

➢ Marekebisho ya muswada wa sheria ya uchaguzi na mabadiliko ya katiba ya 1977 ibara ya 39(1)(b) yafanyike ili kupunguza umri wa kugombea urais na makamu wa urais kutoka miaka 40 hadi 35 ili kutoa fursa kwa vijana wenye uwezo kutoa mchango wao wa maarifa katika kuongoza nchi kwa maendeleo na ustawi wa Taifa.

➢ Marekebisho ya muswada wa sheria ya uchaguzi na mabadiliko ya katiba ya 1977 ibara ya 66(1)(e) yafanyike ili uteuzi wa wabunge 10 wanaoteuliwa na Rais uzingatie vijana,sheria na katiba itamke wazi kwamba kati ya wabunge 10 angalau 4 wawe vijana jinsia ya kiume na kike.

➢ Muswada wa sheria ya vyama vya siasa upanue wigo kwa kuweka masharti kuvilazimisha vyama vyetu asilimia kadhaa ya wajumbe katika vikao vikubwa vya chama kama kamati kuu na Halmshauri kuu wawe vijana ili kupanua wigo wa ushiriki wa vijana.

➢ Marekebisho ya muswada wa sheria ya uchaguzi na mabadiliko ya katiba ya 1977 yafanyike kuruhusu mgombea binafsi na kuondoa sifa ya kuwa mwanachama tuu ili kugombea, hii itaongeza sana ushiriki wa vijana.

➢ Marekebisho yafanyike katika muswada wa sheria ya uchaguzi kifungu cha 85(1) na 14(1) kuruhusu wananchi kupiga kura ya Udiwani,Ubungen na Urais popote walipo hata kama ni tofauti na maeneo waliyojiandkishia ,hili linawezekana kupitia matumizi ya Tehama na Teknolojia katika chaguzi. Na itasaidia vijana wengi nchini hasa wanafunzi na walio nje ya nchi (Diaspora )wenye sifa ambao mara zote wanapoteza haki ya kupiga kura sababu wapo mbali na maeneo waliyoandikishwa kupiga kura.

6. Tunapinga muswada wa sheria ya uchaguzi kutojumuisha uchaguzi wa serikali ya mitaa,vijiji na vitongoji

Muswada huu wa sheria ya uchaguzi unajumuisha uchaguzi wa Rais, Wabunge na madiwani tuu ambapo sheria hii inakwenda kufuta sheria ya uchaguzi wa madiwani sura 292 na sheria ya Taifa ya uchaguzi sura 343. Sheria hii haijajumuisha uchaguzi wa serikali ya mitaa (Neighborhood Election).

Na hii ni kwasababu uchaguzi wa serikali ya mtaa Tanzania (Neighborhood Election) hauna sheria yake (Legislation/act of parliament) inayongoza na kusimamia uchaguzi huu bali unaongozwa kwa kanuni ambazo waziri wa TAMISEMI amepewa mamlaka kuzitunga chini ya sheria ya serikali ya mitaa (Mamlaka ya wilaya) Sura 287 (Toleo la 2019) kifungu cha 56(3) na Sheria ya serikali ya mitaa (Mamlaka ya Miji) sura 288 (Toleo la 2019).Pia uchaguzi huu wa serikali ya mitaa,vijiji na vitongoji unasimamiwa na waziri wa TAMISEMI na sio Tume ya uchaguzi.

Mapendekezo

• Muswada wa sheria ya uchaguzi ujumuishe pia chaguzi za serikali ya mtaa(Neighborhood Elections) na uitwe Muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais,wabunge ,madiwani na viongozi wa serikali ya mitaa,vijiji na vitongoji.

• Uchaguzi wa viongozi wa serikali ya mitaa,vijiji na vitongoji usimamiwe na Tume ya uchaguzi na sio Waziri wa TAMISEMI, hii ni kwa sababu Waziri wa TAMISEMI ni mwanachama wa CCM hivyo hana uhalali na utaalamu wa kusimamia uchaguzi na hawezi kuzingatia usawa kwa vyama vingine vinavyoshindana na chama chake cha CCM. Na mfano halisi ni uchaguzi wa serikali ya mitaa, vijiji na vitongoji wa 2019 na chaguzi zingine za nyuma.

7. Tunapinga kifungu kinachozuia wafungwa kutumia haki yao ya kupiga kura

Kifungu cha 10(1)C cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinazuia mtu aliyetiwa hatiani kwa kifungo kinachozidi miezi 6 na kifungo cha Maisha kupiga kura .

➢ Kifungu hiki kipo kinyume na ibara ya 5(1) na 21 ya katiba ya JMT 1977. Ibara inatoa fursa mtu aliyefikisha umri wa miaka 18 kupiga kura.

➢ Kifungu hiki tayari kimebatilishwa na hukumu ya Mahakama kuu Tanzania katika kesi No.3 ya 2022 iliyofunguliwa na mwanaharakati ndug.Tito Magoti chini ya Jaji Elinaza Luvanda. Hukumu ya kesi hii ilibatilisha kifungu kinachozuia wafungwa kupiga kura katika sheria ya uchaguzi sura 343 kwamba kinakinzana na katiba ya JMT ibara ya 5(1).

Mapendekezo

• Kifungu cha 10(1)C cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinachozuia wafungwa kupiga kura kinapaswa kifutwe sababu kina kinzana na ibara ya 5(1) ya katiba ya JMT 1977, pia kina kinzana na hukumu ya mahakamu kuu katika kesi No.3 ya 2022 ya Tito Magoti.

Lakini pia ulimwengu umebadilika sasa nchi nyingi duniani zinaruhusu wafungwa kupiga kura bila kikwazo. Miongoni mwa nchi hizo baadhi ni,Kenya,Denmark,Finland,France,Zimbabwe,Japan,Poland,Peru,Norway,Netherlan ds,Ireland,Latvia,Lithunia,Spain,Sweden,Switzerland,CzechRepublic,Macedonia, Romania ,Cyprus na Ukraine.

8. Tunapinga fedha za uendeshaji wa shughuli za Tume ya uchaguzi kutoka katika bajeti ya serikali

Katika kifungu cha 22 cha muswada wa sheria ya Tume ya uchaguzi kinazungumzia fedha za uendeshaji wa shughuli za Tume zitatoka katika bajeti ya serikali, yaani chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tume ya uchaguzi itapangiwa waipe shilingi ngapi na lini .Hiki kifungu hakifai kwani kinadhoofisha uhuru wa Tume katika kutekeleza shughuli na majukumu yake.

Mapendekezo

• Tunapendekeza fedha za kuendesha shughuli za Tume zitoke kwenye mfuko mkuu wa serikali (Consolidated Fund) ambazo ni fedha za uhakika,zenye utaratibu mzuri na ambazo haziguswi zikiingizwa huko ,hii itaongeza uhuru na ufanisi wa Tume katika kutekeleza majukumu yake tofauti na sasa hivi Tume ya uchaguzi inatengewa na kupewa fedha kama hisani kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

9. Tunapinga Tume ya uchaguzi kulipisha wananchi fedha kwa kadi ya kupigia kura iliyoharibika ,kufutika au kupotea ili kupewa kadi mpya

Katika muswada wa sheria ya uchaguzi kifungu cha 20(1)(2) na 21(2) kinasema ikiwa mtu atapoteza kadi ya kupigia kura au kadi hiyo kufutika au kuharibika, basi ikithibitishwa na afisa mwandikishaji ,mtu huyo atapewa kadi mpya baada ya kulipia ada. Kifungu hiki hakifai na kina lengo la kuzuia vijana wengi wasipige kura (informal disfranchisement) sababu vijana ndio asilimia kubwa hawana kipato ,hivyo ada ya fedha itazuia vijana wengi kupata kadi na hivyo kunyimwa haki yetu ya kupiga kura kwa mujibu wa ibara ya 5(1) na 21 ya katiba ya JMT 1977.

Mapendekezo

• Tunapendekeza kuondoa gharama za kupata kadi /kitambulisho kipya cha mpiga kura.Tunapendekeza maneno “ada” yafutwe na kuondolewa ili kuongeza hamasa ya wananchi na vijana kupiga kura na pia ili kiende sambamba na matakwa ya katiba ya JMT 1977 ibara ya 5(1) na 21.

10. Tunapinga mamlaka makubwa aliyopewa Msajili wa vyama vya siasa na Mwanasheria Mkuu wa serikali katika kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea

Katika muswada wa sheria ya uchaguzi kifungu cha 37(3) ngazi ya urais, kifungu cha 53(3) ngazi ya ubunge na kifungu cha 65(3) ngazi ya udiwani ,vifungu hivi vinawapa uzito na mamlaka makubwa ya kupitiliza watendaji wa serikali kama Msajili wa Vyama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea ngazi zote urais,ubunge na udiwani jambo ambalo linaibua hisia za njama dhidi ya vyama pinzani na pia hisia ya matumizi mabaya ya mapingamizi .

Mapendekezo

• Tunapendekeza kuondoa mamlaka za serikali (Msajili wa vyama vya siasa na Mwanasheria Mkuu wa serikali) katika kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea.Kifungu kiruhusu mtu yeyote kuweka pingamizi na sio Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa au Mwanasheria Mkuu wa serikali.

MAAZIMIO

1.Tunaitaka serikali ,kamati za bunge na wabunge wote kusikia na kuheshimu sauti na maoni ya wananchi,vijana, vyama vya siasa ,Asasi za kiraia, wanaharakati,viongozi wa dini na wadau wote juu ya mapungufu na kasoro katika miswada hii ili mapungufu na kasoro zote ziondolewe kukidhi matarajio ya wananchi kwa mustakabali wa Demokrasia ,amani ,uwajibikaji na maendeleo ya nchi yetu.

2.Tunaitaka serikali ipeleke muswada wa marekebisho madogo ya katiba ya JMT ya 1977 katika vipengele ambavyo vinahusu chaguzi sambamba na miswada hii. Kupeleka miswada hii mitatu bila mabadiliko madogo ya katiba ya 1977 haita akisi maana halisi ya mabadiliko ya kisiasa yanayodhamiriwa kufanywa nchini.

3. Tunaitaka serikali iweke wazi ratiba ya mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya ili matukio yote yanayohusu mabadiliko ya katiba mpya yawe kwenye ratiba na kujua nani ana husika katika utekelezaji na kwa muda gani.

4. Tunawasihi vijana wenzetu wenye vyama na wasio na vyama, Asasi za kiraia ,wanaharakati ,waandishi wa Habari,viongozi wa dini na wananchi wote kusimama madhubuti kupaza sauti na kushinikiza na kupinga mapungufu na kasoro zote katika miswada hii,pamoja na kujitokeza kutoa maoni katika kamati za Bunge kuanzia tar.6 ,8 na 10 Januari 2024 Dodoma.

5. Ikiwa miswada hii itapitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais kama ilivyo bila kufanyia marekebisho katika maeneo yenye kasoro na mapungufu,sisi viongozi wa Jumuiya za vijana vyama pinzani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tutaenda mahakamani kupinga Sheria zote zitakazopitishwa katika vifungu vyote vinavyokinzana na katiba ya JMT 1977.

Imetolewa kwa pamoja leo Jumanne Januari 2,2024. Dar es Salaam.

Tunawatakia wote heri ya mwaka mpya 2024.

Abdul Omary Nondo. Mwenyekiti wa Ngome ya vijana-ACT Wazalendo Taifa.

Iddi Mkanza.
Katibu wa Vijana CUF Taifa.

Elisante Ngoma.
Katibu wa vijana NCCR-Mageuzi Taifa.
1083978315.jpg
222318546.jpg
75775265.jpg
 
Katibu wa vijana NCCR-Mageuzi Taifa.View attachment 2860273View attachment 2860274View attachment 2860275
Tunaunga mkono
 
Back
Top Bottom