Taarifa kwa Umma-Tamko la J.Nassari kuhusu Tamko la NMC

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,086
103,316
*TAARIFA KWA UMMA*

Ninalazimika kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani... hotuba yangu niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Arusha siku ya jumamosi Tarehe 5, Mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga CHADEMA kutokea vyama mbalimbali vya siasa hususani chama tawala CCM.

Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa CHADEMA, Chama ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema Mwenyekiti ndio msimamo wangu japokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano. Lengo la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake

Joshua Nassari (MB)
Mei 09, 2012.
 
Wawepo vijana kama ishirini hivi wawe mawaziri mtaone Tanzania itakavyobadilika...tunapelekeshwa na hawa wazee kazi kulala tuu bungeni...bravo Nasari nakukubali kweli...kwa kweli ni kijana jasiri anayejali maisha ya watanzania...
 
dogo umedhihirisha ule msemo wa kiswahil unaukwel ndan yake.
"MASIKIN AKIPATA TA** ULIA MBWATA"
 
Duh wasemaji wa Nassari mko wengi angalia msijeshikana mashati na Mkuu Crashwise ha ha ha ha.
 
punguza jazba wakati mwingine jazba hupoteza busara. Muungwana siku zote huungama kama ulivyoamua wewe.
 
Umefanya vyema kufafanua kwa Maandishi, kitu ambacho si rahisi mtu awaye yote kupotosha. Maana Magamba walishachukulia Upotoshaji wao kama ndio subject kubwa na waliikomalia utadhani sasa wamepata solution ya Matatizo ya Mtanzania. AIBU YAO MAGAMBA
 
Mbona umetoa ufafanuzi haraka haraka kama vile ikulu inapohusishwa na biashara za waarabu?
 
... afadhali mkuu umetoa UFAFANUZI MURUA kihivi na sasa kila mtu ameelewa upotoshaji uliokua unafanyika kuhusu hotuba ya NMC sasa wakose kabisa pa kutokea.

Big up sana, siasa za CDM siku zote ni siasa za umoja wa kitaifa lakini BILA MCHANGANYIKO WA MFUMO FISADI.
 
Hii ndiyo aina ya Viongozi na Wanasiasa tunaohitaji... Mbona ZNZ kuna watu kwa sababu kama hizi za Nasari wameamua kuandamana ili kujitenga na Tanganyika na Bado wanapeta? mbona sijawahi kusikia Ismail Jusa akihojiwa na Polisi? Lakini amekuwa Mstari wa Mbele kutoa kauli kama hizi za watanzania.

mimi nafikiri tafsiri halisi ya alichokisema Nasari ni kwamba watu wako kwenye Dimbwi la matatizo si serikali wala Viongozi wake wanajishughulisha kuyatatua.. Imefika mahali watu wanauawa serikali inapiga blah blah... Sasa hivi Arusha Mjini si haina Madiwani, Meya, wala Mbunge na watu wanauawa kila kukicha jeshi la polisi liko kimya CCM ndiyo watuhumiwa hakuna hatua inayochukuliwa kwa hiyo kilichobaki ni kutoa shinikizo ambalo litawaamsha polisi na viongozi wa CCM..

Nasari hakuwa na maana ya kuwagawa watanzania hata kidogo. Ila waTZ tushagawanyika siku nyingi kati ya CCM na CDM hili si la kuuliza.

Wasitake kuwavuruga wananchi, M4C itawamaliza mwaka huu.

Kwanza JK hana mpango wa kutembelea Arumeru Mashariki wala A town tunajua yeye misele yake ni Nje ya Nchi tu
 
Nassari ni kijana mpambanaji, mwenye uchungu na nchi yake.
Ninachoamini ni kwamba he always goes through.
Yapo mambo anayotakiwa ajifunze, ni jinsi gani anatakiwa alikabili jukwaa. Naamini amejifunza na anaendelea kujifunza mengi
 
Back
Top Bottom