Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA)

Matusi si sehemu ya malezi niliyokulia, mauji si sehemu ya mikakati yetu ya kisiasa, Unaweza kusoma hapa: Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012 kuhusu hayo masuala ya Iramba utapata ukweli.

Nadhani sasa nikubaliane na ushauri wa Aweda nitumie muda vizuri kujadili masuala ya taarifa ya kazi za maendeleo jimbo la Ubungo kama alivyoshauri.

JJ

Mnyika nakuaminia kwa hizi reference zako...Kila wakitaka kuleta ngebe mwendo ni soma hapa...safi sana.
 
Mnyika yale yote ulioahidi hujatekeleza hata moja, ila kwa kupiga domo bungeni hilo umefanikiwa, nia yetu ya wakazi wa ubungo ni kutekeleza uliyotuahidi vinginevyo 2015 ukae mguu sawa ukalime.

Wewe si mpiga kura wa ubungo. Hongera Mnyika na twakutakia kila raheli.
 
Ritz akili yako haikui pamoja na kuwepo hapa JF muda mrefu.
Nani kakudanganya kwamba hakuna mtu anayeifahamu JF huko manzese, tandale, mahakama ya ndizi, bonyokwa na kimara temboni??
Bure kabisa wewe kusoma hujui, hata kupapasa huwezi!?

Mwita Maranya,
Wakati mwingine uwa nakuchokonoa makusudi nikupime kama kweli unafaa kuwa kiongozi lakini jinsi anavyokurupuka kujibu napata wasiwasi na ufahamu wako...kama kweli unataka kuwa kiongozi jifunze kutumia lugha nzuri sio kujibu kama vile mnywa mapuya...JF kuna members zaidi ya 90,000 na kuna Multiple ID's zaidi ya 10,000 members hai wa JF kama 70,000...na wapiga kura wa Jimbo la Ubungo wapo zaidi ya 400,000 ndio maana nimemwambia Mnyika watu wa Ubungo hawaijui JF asiangaike na siasa za kwenye mitandao, na wewe ukivyokuwa na akili kama za Zwizi akakurupuka kujibu.
 
Last edited by a moderator:
Sijaweza kuzifungua links nyingi kwa sababu natumia simu ila naomba utusaidie yafuatayo sisi wapiga kura wa Kibamba:
- Maji sasa yamekatwa bila sababu za msingi diwani wetu wa Kwembe alikuwa shuhuda siku ile wananchi walipotaka kum lynch mtumishi wa Dawasco kwa kukata mabomba yaliyokuwa yanatuletea maji, aliahidi(diwani) kulifikisha tatizo hili kwa Mkuu wa Wilaya lakini mpaka leo hatujapata mrejesho na maji ndo hivyo tena.
- Barabara, sisi tunaweza kuchanga ila tunachohitaji ni leadership na coordination. Binafsi mpaka leo sijui kama na sisi tuna viongozi wa serikali za mitaa kwani sijawahi kuwaona na mabarabara yanazidi kuvamiwa kwa ujenzi holela licha ya serikali kupima eneo hili mwaka 2008
 
Raisi Kenedy wa marekani alianza na ujasiri kama wa mnyika na akaishia kuwa raisi bora dunia haijwahi kuona. kitu kikubwa ni kujua mwananchi anataka kuboreshwa namna gani halafu unaingia katika brain power na kufanyia kazi. Hongera sana mnyika ila la muhimu pia angalia sana unemployment rate inavyotesa watu hapo jinboni ubungo. Halafu kitu bora kupita chochote ni huduma za maktaba. ukifanikiwa kujenga maktaba inayochukua watu hamsini kwa wakati mmoja hapo umejenga nchi kwa akiri za kuzaliwa. nakutakia kila la heri Jean baptist Mnyika!
 
kuna neno moja huwa nalipenda sana, nalo ni "get out of the box and then think" au "think out of the box" Jimbo ni kama box, Mbunge akiamua kufanya kazi kwa mtazamo wa jimbo kwangu sio tatizo kwa kuwa ana-think within the box na uwezo wake wa utendaji kazi unamipaka ambayo ni vibambazi/kuta za box.

Mimi kama mmoja wa watanzania milioni takribani arobani, ninaamini pasipo shaka kuwa uwezo wetu wa kufikiri ni tofauti, katika swala la wabunge, mimi mbunge ninayemchagua ni yule ambaye anashughulikia maswala ya kitaifa. kwa kuwa, taifa ni ultimate, jimbo ni sehemu ndogo sana ya taifa, kama jimbo linafanikiwa wakati taifa limeprove failure, obviously kufanikiwa kwa jimbo hilo sio sustainable kwa kuwa litakwama ndani ya muda mfupi.

Mheshimiwa Mnyika, mimi ni mmoja wa wakazi wa jimbo lako, mambo unayoyafanya 'in the interest of the nation' yamenifurahisha sana kiasi kwamba hata usipofanya chochote katika level ya jimbo bado kura yangu unayo.

Guys, let's think out of the box
 
Kimbunga mnyika yupo online sasa hivi

Mkuu Narubongo ndio kwanza naingia kwenye mtandao muda huu. Gari iliniharibikia maeneo ya Kimara Kilungule kwa kuwa iko chini na barabara ni mbovu mno. Ndio nimepata msaada nimeiacha garage kesho waichomee hivyo nimeingia nyumbani mida hii. Ngoja nisome ujimbe wa Mnyika japo naona anaturejesha kwenye blog. Ila kitu kimoja nisema kwamba Mnyika si muoga, anathubutu kuja mtandaoni na kutolea ufafanuzi mambo ambayo huwa yanaongelewa hapa iwe kwa kumsifia, kumuonya ama kumrekebisha. Ngoja nijielekeze kwenye kusoma hizo blog.
 
Last edited by a moderator:
Narubongo nimesoma yooote lakini ni yaleyale ya kila siku. Barabara ya Korogwe-Kilungule-external iko taaabani! Barabara ya baruti-kilungule iko taabani, barabara ya kiwanjani-kibanda cha mkaa-kibangu iko hoi, barabara ya Kimara mwisho - vyumba vinane -kwa beka iko hoi, barabara ya makoka kwa mama mzaire-kwa kichwa ipo oama haipo!Barabara ya maramba mawili kuelekea Kinyerezi hoi, mitaa ya Ubungo national housing iko taabani maji taka yanatiririka kila mahala. Maji safi hakuna.

Ndugu Mnyika ungana na Madiwani wako mhamasishe maendeleo. Hivi grader la manispaa liko wapi siku hizi. Wewe ni mbunge una sauti kwenye council omba grader hamasisha wananchi wachangie mafuta wape grader lichonge barabara za kimara zipitike utakuwa umeua tembo kwa ubua. Wewe ng'ang'ania tu blog uone mwisho wake manake watu hawaangalii blog wala JF watu wanataka maeneo yapitike. Kwa sababu ya barabara mbovu wananchi wa jimbo lako wanaamka saa kumi usiku kwenda kujikusanya morogoro road ili wapate usafiri.
 
Last edited by a moderator:
Kuwa karibu na Wananchi ni Jambo Jema

555496_10151087737259042_542450835_n.jpg
 
Mwita Maranya,
Wakati mwingine uwa nakuchokonoa makusudi nikupime kama kweli unafaa kuwa kiongozi lakini jinsi anavyokurupuka kujibu napata wasiwasi na ufahamu wako...kama kweli unataka kuwa kiongozi jifunze kutumia lugha nzuri sio kujibu kama vile mnywa mapuya...JF kuna members zaidi ya 90,000 na kuna Multiple ID's zaidi ya 10,000 members hai wa JF kama 70,000...na wapiga kura wa Jimbo la Ubungo wapo zaidi ya 400,000 ndio maana nimemwambia Mnyika watu wa Ubungo hawaijui JF asiangaike na siasa za kwenye mitandao, na wewe ukivyokuwa na akili kama za Zwizi akakurupuka kujibu.

Wewe lazima Utakuwa ni Mpare...Harikaaa! Namnani Havae! urewedi!

Puya hiyo Pombe ya Miwa oi`Miguva1
 
Wana ubungo ndo tunaona alichofanya huyu bw. mdogo,
walio nje ya ubungo tupeni nanyie kazi walizofanya hao watu wenu walioko huko mjengoni.
 
Mwita Maranya,
Wakati mwingine uwa nakuchokonoa makusudi nikupime kama kweli unafaa kuwa kiongozi lakini jinsi anavyokurupuka kujibu napata wasiwasi na ufahamu wako...kama kweli unataka kuwa kiongozi jifunze kutumia lugha nzuri sio kujibu kama vile mnywa mapuya...JF kuna members zaidi ya 90,000 na kuna Multiple ID's zaidi ya 10,000 members hai wa JF kama 70,000...na wapiga kura wa Jimbo la Ubungo wapo zaidi ya 400,000 ndio maana nimemwambia Mnyika watu wa Ubungo hawaijui JF asiangaike na siasa za kwenye mitandao, na wewe ukivyokuwa na akili kama za Zwizi akakurupuka kujibu.....

Ritz Mambo ya multiple IDs yanakuhusu sana wewe na wenzako kwakuwa mnajua mnatekeleza majukumu mliyopewa na Lumumba, mimi nipo hapa kwa ID hii hii usiku, mchana, asubuhi, jioni na adhuhuri.

Pointi ya msingi hapa ni wewe kutaka kuwadhalilisha wananchi wa Manzese, Tandale, mahakama ya ndizi, Bonyokwa na Kimara kwamba hawaijui JF, tena huo ni uchizi unakusumbua kwakuwa hapa tunapoandika JF hakuna anayefahamu kwa uhakika ni nani yuko wapi.

Inawezekana kabisa na ndio ukweli wenyewe kwamba hayo maeneo unayodhani hawaijui JF kuna members wengi tu tokea pande hizo.

Btw, mimi sipimwi na ritz kama nafaa kuwa kiongozi ama vinginevyo, kwani tayari hadi hapa nilipo ni kiongozi sasa sijui wewe unadhani kuwa kiongozi hadi niwe cha mabwepande?

John Mnyika amefanya kazi nzuri sana tangu awe mbunge tena kwa kipindi kifupi sana, mambo aliyoyafanya hayajawahi kufanywa na mbunge yeyote wa CCM tangu nchi ipate uhuru.

Ndani ya miaka miwili ameweza kufanya mambo makubwa na bado anaendelea kujitahidi kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, kwahiyo hadi anamaliza miaka yake mitano nina uhakika wananchi wa Ubungo watakuwa wamepiga hatua kubwa sana ya kimaendeleo na hawatoweza kumkumbuka mbunge yeyote wa CCM.
 
Narubongo nimesoma yooote lakini ni yaleyale ya kila siku. Barabara ya Korogwe-Kilungule-external iko taaabani! Barabara ya baruti-kilungule iko taabani, barabara ya kiwanjani-kibanda cha mkaa-kibangu iko hoi, barabara ya Kimara mwisho - vyumba vinane -kwa beka iko hoi, barabara ya makoka kwa mama mzaire-kwa kichwa ipo oama haipo!Barabara ya maramba mawili kuelekea Kinyerezi hoi, mitaa ya Ubungo national housing iko taabani maji taka yanatiririka kila mahala. Maji safi hakuna.

Ndugu Mnyika ungana na Madiwani wako mhamasishe maendeleo. Hivi grader la manispaa liko wapi siku hizi. Wewe ni mbunge una sauti kwenye council omba grader hamasisha wananchi wachangie mafuta wape grader lichonge barabara za kimara zipitike utakuwa umeua tembo kwa ubua. Wewe ng'ang'ania tu blog uone mwisho wake manake watu hawaangalii blog wala JF watu wanataka maeneo yapitike. Kwa sababu ya barabara mbovu wananchi wa jimbo lako wanaamka saa kumi usiku kwenda kujikusanya morogoro road ili wapate usafiri.

Mkuu,
analysis yako ni nzuri sana, lakini tatizo dogo hujasoma ripoti yake yote kwa undani. Baadhi ya maeneo au barabara ulizotaja ameelezea kwa urefu kuhusu hatua ambazo zimefikiwa ktk ufuatiliaji wake na nini kinategewa kufanyika lini.
 
Mh. Mnyika,
Wewe ni mbunge wangu, kura yangu ya pekee,I mean PEKEE iliyolipa tangu nilipotimiza umri wa kupiga kura. Lakini tangu siku nyingi nilishakutoa SADAKA uwe mbunge wa TAIFA. Yes. Ubungo nini bwana wakati tuna uhaba wa resources za kuweza kuwafikia babu na bibi zangu kule kidabaga, kachanchabuseta, tandahimba, kyabakari n.k. Go Mnyika go!

Mpaka asilimia walau 50 ya Tanzania itakapopata wabunge wa aina yako,ndipo nitaanza kukupima kwa uwajibikaji wako kwa ubungo.
 
Ritz Mambo ya multiple IDs yanakuhusu sana wewe na wenzako kwakuwa mnajua mnatekeleza majukumu mliyopewa na Lumumba, mimi nipo hapa kwa ID hii hii usiku, mchana, asubuhi, jioni na adhuhuri.

Pointi ya msingi hapa ni wewe kutaka kuwadhalilisha wananchi wa Manzese, Tandale, mahakama ya ndizi, Bonyokwa na Kimara kwamba hawaijui JF, tena huo ni uchizi unakusumbua kwakuwa hapa tunapoandika JF hakuna anayefahamu kwa uhakika ni nani yuko wapi.

Inawezekana kabisa na ndio ukweli wenyewe kwamba hayo maeneo unayodhani hawaijui JF kuna members wengi tu tokea pande hizo.

Btw, mimi sipimwi na ritz kama nafaa kuwa kiongozi ama vinginevyo, kwani tayari hadi hapa nilipo ni kiongozi sasa sijui wewe unadhani kuwa kiongozi hadi niwe cha mabwepande?

John Mnyika amefanya kazi nzuri sana tangu awe mbunge tena kwa kipindi kifupi sana, mambo aliyoyafanya hayajawahi kufanywa na mbunge yeyote wa CCM tangu nchi ipate uhuru.

Ndani ya miaka miwili ameweza kufanya mambo makubwa na bado anaendelea kujitahidi kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, kwahiyo hadi anamaliza miaka yake mitano nina uhakika wananchi wa Ubungo watakuwa wamepiga hatua kubwa sana ya kimaendeleo na hawatoweza kumkumbuka mbunge yeyote wa CCM.

Mwita Maranya,
Wapi nimewadhalilisha wakazi wa Manzese, Ubungo, Tandale, nilichosema mie ni kumfahamisha Mnyika kuwa aachane na siasa za mitandaoni, hawafuate wapiga kura wake, watu wa Tandale, Manzese, Ubungo, wanaitaji maji na barabara sio kuwawekea maendeleo yao kwenye mitandao hawajui mambo ya mitandao.

Nimekuambia kama unataka kuwa kiongozi ongea kama kiongozi tumia lugha nzuri watu watajenga imani na wewe huu ni ushauri nakupa, kama unataka kuwa mpiga debe endelea na kauli zako na kudharau watu.
 
Last edited by a moderator:
Mh mnyika,kwanini mliua kijana asiekuwa na hatia pale iramba mkk,huoni hiyo dhambi itakutafuna sana wewe kitila na mwikwabe hadi siku ya kufa kwenu?

Hapa unamtoa Mnyika kwenye lengo kwa makusudi na ndio maana amekugomea, siyo kwamba hana majibu. Ngoja nikusaidie kidogo.
Mosi, Mnyika na Dr Kitila Mkumbo walipata taarifa kuwa ccm wameandaa vurugu ili mkutano wa Chadema usifanyike. Wakatoa taarifa polisi ili walindwe vizuri na polisi wengi. Kwa mshangao wao, vurugu hizo zilitokea na mauaji hayo yakatokea.
Maswali ya kujiuliza;
Kwa nini waliomba polisi waje kwenye mkutano ambao wao wamepanga kuua mwanaccm?
Pili, kwa nini ccm walizima bungeni hoja hii ya mauaji ya kisiasa wakati msemaji wao aliipeleka bungeni?.
Lazima mimi nimekosea kujiunga na Chama ambacho kinaua watu tena kwa kuwaalika polisi ili waone watakavyoua. Kisha wanapeleka mjadala huo bungeni, halafu unakwamishwa na ccm.
Hii inanikumbusha wabunge 2 wa Chadema waliokatwa mapanga huko mwanza mbele ya polisi kwa mujibu wa wabunge wenyewe. Dr Kitila yuko humu kwa maelezo zaidi pm

Mnyika yale yote ulioahidi hujatekeleza hata moja, ila kwa kupiga domo bungeni hilo umefanikiwa, nia yetu ya wakazi wa ubungo ni kutekeleza uliyotuahidi vinginevyo 2015 ukae mguu sawa ukalime.

Duh! umenikwaza Mkingoma. Kwani kulima ni dhambi? Kosa? au adhabu? TAFAKARI hayo ni mawazo finyu
 
Back
Top Bottom