Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,071
Rais Kikwete aliahidi ajira milioni moja kila mwaka, lazima tuwaondoe
...ndiyohiyo
Alikwenda Gorani, Jimbo la Ubungo mwaka juzi, wananchi wakamwambia wanataka maji, akaahidi kuwa ataitisha kikao cha wadauwa maji ikulu. Akawataja. wananchi wakapiga kelele lazima mbunge awepo. Kikwete akalazimika kukubali kuwa mbunge awepo maana yeye ndiye mwakilishi wa wananchi na mpiganaji wa suala la maji ndani na nje ya bunge.
Hiyo ilikuwa mwaka 2013, siku chache baada ya hoja ya Mnyika kuhusu tatizo la maji kuzua zogo ndani ya ukumbi wa bunge. Watu wengi hawajui suala hili; kwamba vurugu ndani ya bunge kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu zilitokea siku hiyo ambapo, serikali bungeni, uongozi wa bunge na wabunge wa CCM walikuwa wanazuia hoja ya Mnyika kuhusu tatizo la maji Ubungo, Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla isijadiliwe.
Eti ingewaumbua na kuanika ufisadi, uozo na udhaifu wa Serikali ya CCM katika tatizo hilo ambalo sasa linaanza kuwa sugu.
Hadi tunapoandika hapa ikulu haijawahi kuitisha kikao hicho kama ambavyo Rais Kikwete aliahidi tena akasema hadi siku/tarehe. Hadharani. Mbele ya wananchi. Leo ni miaka mitatu. Kikao tu....