Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA)

Matusi si sehemu ya malezi niliyokulia, mauji si sehemu ya mikakati yetu ya kisiasa, Unaweza kusoma hapa: Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012 kuhusu hayo masuala ya Iramba utapata ukweli.

Nadhani sasa nikubaliane na ushauri wa Aweda nitumie muda vizuri kujadili masuala ya taarifa ya kazi za maendeleo jimbo la Ubungo kama alivyoshauri.

JJ

mkuu mnyika naomba umpatie aweda kazi awe katibu wa mbunge naona anakuwakilisha vizuri sana apa.
 
Mbunge wangu John Mnyika,
Naelewa una dhamira ya dhati kabisa kuyatatua matatizo yetu,tatizo kuna baadhi ya watu wapo hapa kwa ajili ya kukupinga tu(kwa ajili wewe ni John Mnyika na sio kama mbunge......kwa sababu najiuliza tu,Ina maana hayo matatizo yapo jimboni kwetu pekee katika jiji zima?
Ni ahadi ngapi zilizotolewa na wabunge wa CCM wa Dar Es Salaam na hazijatekelezwa mpaka leo? mbona wao hawaanzishiwi uzi na kujadiliwa? Ama kweli nimeamini mti wa matunda ndio unaopigwa mawe....

Tupo pa1 sana Mh Mbunge,endelea kukaza buti japokuwa kuna changamoto nyingi zinazokukabili....
The Magnificient
Ubungo-Msewe
 
Last edited by a moderator:
Mh Mbunge wa Ubungo,
Ah yote uliofanya ni mazuri sana lakini kwa mtu wa mtaa wa Kilimani haoni kwa sababu double standards wanazofanyiwa na DAWASA/DAWASCO. Mtaa wa Kilimani, kata ya manzese mabomba ya maji yametandazwa karibu na kila nyumba miaka mingi sana iliyopita lakini mabomba yanaozea ardhini bila kutoa huduma kisa bomba (main feed pipe) lilikatwa wakijenga daraja la "Kindu" karibu na ofisi ya serikali ya mtaa. Hakuna sababu kwa wote walio na infrastructure wasipate maji hata kama hayatoshi ni kote hayatoshi na hata kama hayatoshi ni nani awe na haki ya kupata na nani asipate, wote tunalipa kodi na zamani tulikuwa na mita mpaka walipoziondoa wakiahid kusubiriwa mradi wa maji ambao ndio umeisha miaka mingi sana huko nyuma. Tafadhali chunguza ukweli huu hata wewe mwenyewe utashangaa. Tunasubiri jibu la Mh Mbunge.
 
Ritz,

Nashukuru kwa ushauri huu kutoka kwa kada wa CCM, kauli zako lakini ni za ujumla sana ungetaja hayo maeneo ambayo ndoo moja ya maji inauzwa 2000, inawezekana unazungumzia katika majimbo mengine lakini si Ubungo.

Pamoja na kuwa naelewa sasa hivi Mkoa mzima wa Dar es salaam maeneo kadhaa yana matatizo ya maji kutokana na uharibifu wa baadhi ya mabomba na DAWASCO wameshatoa kauli.

Niliyoyasema kwenye kampeni niliyaweka kwenye maandishi hapa: JOHN MNYIKA: Ujumbe wa Mbunge: Shukrani, Twende Kazi!, na utekelezaji wake katika mwaka mmoja na nusu usome katika taarifa ya kwenye mjadala huu.

Naomba nami nikushauri umshauri Rais Kikwete kuwa ahadi za maji alizozitoa mwezi Mei 2010 Kimara Mavurunza/Bonyokwa bado hazijatekelezwa na anao wajibu kusimamia zitekelezwe, kwa sasa naendelea kufuatilia DAWASCO, DAWASA na Wizara ya Maji hatua za haraka zisipochukuliwa nitaongoza wananchi kupata majibu kutoka ikulu.

JJ

Mnyika,
Tatizo nyie wanasiasa uwa mnaabadilika sana leo hii watu wakihoji ahadi zako ulizo ahidi unawaonyesha makaratasi ndio maana nakuambia achana na siasa za kwenye mitandao, maeneo ambayo ndoo ya maji 2000 ni Ubungo Maziwa, Kimara Temboni, Kimara Bonyokwa, Kibamba, Mnyika hayo mabomba ya Dawasco yamealibika lini, kabla ya kualibika ulipeleka maji...Mnyika kwa hiyo kama Rais Kikwete ajatimiza ahadi yake huko Bonyokwa na wewe unapata Excuse...halafu walikupigia kura ni wana ubungo sio Pro-Chadema JF kumbuka mungu akikupa uhai utarudi tena kuomba kura sijui utawaonyesha wana ubungo makaratasi au utawambia wakangalie maendeleo yao kwenye mitandao...Mnyika mwananchi Manzese Tandale, Bonyokwa, Kimara Temboni, Mahakama ya Ndizi, hajui habari ya JF anachotaka kuona maji yanatoka.
 
Mimi nadhani Kutoa hongera sana si msaada. kumsaidia mtu ni pamoja na kumwonesha changamoto zilizopo. Wana Ubungo, bado mna changamoto nyingi sana ambazo mngetumia muda huu kuzitoa kwa mbunge wenu. badala yake, mnapongeza tu. Msaada si kupongezana sana. "ILI NIFANIKIWE, NAHITAJI MARAFIKI. ILI NIFANIKIWE ZAIDI, NAHITAJI MAADUI" Ili kuharakisha maendeleo tunahitaji kupongezana, ILI KUHARAKISHA MAENDELEO ZAIDI TUNAHITAJI CHALLENGES"
 
Salute kwako John Mnyika maana uliingia madarakani kwa kuainisha majukumu manne ya wabunge na ni kweli kabisa kama ulivyosema wabunge wengi wamejikita kwenye kipengele cha kutoa huduma na kusahau majukumu mengine na ndio maana ukisikiliza wabunge wengi utakuta wanajisifu katika uongozi wake ameleta madawati, maji yanapatikana na vitu kibao mwisho wa siku wanatuharibu wananchi kwa kuamini kwamba mbunge ni mambo yote kumbe kuna wadau wengine kama madiwani na halmashauri kwa ujumla nao kwa nafasi yao wamechangia katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

My take: ENDELEA NA UTARATIBU WAKO KAMA KAWAIDA MAMBO MENGINE UNAWEZA KUYAPATA KUPITIA MADIWANI AU BARAZA LA MADIWANI AMBALO KILA BAADA YA MIEZI MITATU LINAKUTANA KUJADILI KERO ZA WANANCHI HIVYO INAKUWA RAHISI KUPATA VITU AMBAVYO VIPO NJE YA UWEZO WA HALMASHAURI (NADHANI HII NDIO MBUNGE ANATAKIWA AFANYE HIVI SIO KUJIPA UJIKO KIBAO WAKATI KAZI YA MBUNGE NI KUTUUNGANISHA SIE WANANCHI ILI TUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO BADALA MBUNGE KUCHANGIA MADAWATI 50 NA KUTAMBA WAKATI ALITAKIWA AKAE NA WANANCHI NA KUAINISHA MATATIZO MWISHO WA SIKU WANANCHI NA MBUNGE WAO KWA PAMOJA HUENDA WAKATOA MADAWATI ZAIDI YA HATA 500 JAPO MBUNGE KUTOA VITU KAMA MWANANCHI WA KAWAIDA HAIZUILIWI.
 
Last edited by a moderator:
....Kila La Kheri MH.MNYIKA....

....Fanya kazi kwa uwajibikaji wa kuwakomboa Watanzania jimbo la UBUNGO kutoka kwenye huu UMASKINI.....

....Endelea kusimamia katika UKWELI daima!!!
 
Mnyika,
Tatizo nyie wanasiasa uwa mnaabadilika sana leo hii watu wakihoji ahadi zako ulizo ahidi unawaonyesha makaratasi ndio maana nakuambia achana na siasa za kwenye mitandao, maeneo ambayo ndoo ya maji 2000 ni Ubungo Maziwa, Kimara Temboni, Kimara Bonyokwa, Kibamba, Mnyika hayo mabomba ya Dawasco yamealibika lini, kabla ya kualibika ulipeleka maji...Mnyika kwa hiyo kama Rais Kikwete ajatimiza ahadi yake huko Bonyokwa na wewe unapata Excuse...halafu walikupigia kura ni wana ubungo sio Pro-Chadema JF kumbuka mungu akikupa uhai utarudi tena kuomba kura sijui utawaonyesha wana ubungo makaratasi au utawambia wakangalie maendeleo yao kwenye mitandao...Mnyika mwananchi Manzese Tandale, Bonyokwa, Kimara Temboni, Mahakama ya Ndizi, hajui habari ya JF anachotaka kuona maji yanatoka.

.....VIONGOZI wa CHADEMA ni Wafuatiliaji siyo WABABAISHAJI kama sera za kidumu chama.....
Via
Maslahi ya Taifa kwanza...
 
Ritz akili yako haikui pamoja na kuwepo hapa JF muda mrefu.
Nani kakudanganya kwamba hakuna mtu anayeifahamu JF huko manzese, tandale, mahakama ya ndizi, bonyokwa na kimara temboni??
Bure kabisa wewe kusoma hujui, hata kupapasa huwezi!?
 
Last edited by a moderator:
Mie Ritz naondoka nakupenda ndio maana nimekuambia ukweli kama utaamua kufanyia kazi ushauri wangu ni hiari yako na kama utaamua kuendelea kupokea pongezi humu JF ni hiari yako...
 
Last edited by a moderator:
Naomba kuunga mkono hoja hii kwa nguvu sana.
Nashauri ripoti hii uichapishe na kuisambaza ktk jimbo lote. Viongozi wote wa chama ktk ngzi kata na tawi waipate ili wawaeleze wananchi.Ofisi zote za chama iwe na nakala.

Pili, Ni ukweli kwamba wagombea watarajiwa wa vyama vyote wanaeneza taarifa za uwongo huko mtaani kuwa wewe ni mbunge wa magazeti na mjengoni. Ukisambaza taarifa hii utakuwa umekata mzizi wa fitina.

Tatu, si vibaya kama utawaambia wengine kupitia vyombo vya habari. Well, wako watakaosema unatafuta cheap popularity, lakini ndivyo walivyomsema mbowe na helikopta yake 2005 lakini baadaye nao wakamwiga.

michael umeona kamanda huyo wa ukweli?cyo kipindi kile wakati upo seminary ukiwa sambamba na baba mwinji ukiwa bweni la kujitegemea m4c
 
Katika kijana mwanasiasa ninayemjua na aliyepo kwenye siasa kwa sasa ambaye namfikiria anafaa kuwa ni wewe nimemaliza. Labda udanganyike badae na urafiki wa kinafiki baadae
 
Mnyika,
Tatizo nyie wanasiasa uwa mnaabadilika sana leo hii watu wakihoji ahadi zako ulizo ahidi unawaonyesha makaratasi ndio maana nakuambia achana na siasa za kwenye mitandao, maeneo ambayo ndoo ya maji 2000 ni Ubungo Maziwa, Kimara Temboni, Kimara Bonyokwa, Kibamba, Mnyika hayo mabomba ya Dawasco yamealibika lini, kabla ya kualibika ulipeleka maji...Mnyika kwa hiyo kama Rais Kikwete ajatimiza ahadi yake huko Bonyokwa na wewe unapata Excuse...halafu walikupigia kura ni wana ubungo sio Pro-Chadema JF kumbuka mungu akikupa uhai utarudi tena kuomba kura sijui utawaonyesha wana ubungo makaratasi au utawambia wakangalie maendeleo yao kwenye mitandao...Mnyika mwananchi Manzese Tandale, Bonyokwa, Kimara Temboni, Mahakama ya Ndizi, hajui habari ya JF anachotaka kuona maji yanatoka.

Acha Uongo wewe Ritz mimi ni Mkazi wa Ubungo Maziwa Maji huwa yanatoka karibu Mara tatu kwa wiki na yakikatika tunanunua Dumu kwa shilingi 200
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom