Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA)

Jembe Mnyika tunakufatilia live hapa JF,naomba baadhi ya post uziruke wanataka kukutoa kwenye mjadala wa maendeleo ya wana Ubungo.

Jamani tuwaache wanaubungo wa humu JF wawakilishe wenzao tusijaze thread hii siasa za akina Ritz!

Twende kazi kamanda JJ Mnyika a.k.a kiboko ya Dhaifu!
 
Tunawajua nyinyi kazi yenu kuvuruga mijadala ya viongozi wa Chadema! ptuuuuuuuuuuuuuu!

hakuna kinachovurugwa,mi mnyika nilimpigia kampeni 05 ht juzi nimempa kura ila ameudhi sana kututukana sisi watanzania wote kutuona ni mijusi.hakuna alichofanya cha maana zaidi ya mijisifa ya kijinga.aige utendaji wa rejia r.i.p hawaropoki lakini wanapiga mzigo balaa
 
Barabara katika jimbo zima la ubungo mbovu,tatizo la maji ubungo ndoo inauzwa hadi mia 700,hao wanaokupa sifa za kijnga hawakupendi.

Kanali Gadafi,

Asante kwa maoni yako, hata hivyo unatoa tu ujumbe wa ujumla na kwa mara nyingine unapotosha. Taja majina ya barabara na aina ya ubovu kwa kuwa huwezi kusema tu kwa ujumla tu barabara zote ni mbovu wakati wako wanaofurahia matengenezo ya barabara katika maeneo yao.

Kuhusu bei ya maji, ungesema ni eneo gani hasa ambapo maji ni 700; naelewa maeneo yenye ulanguzi wa maji mpaka 500. Na kama ukiingia kwenye hii taarifa na kusoma sehemu ya maji JOHN MNYIKA: Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA) unaweza kupata maelezo ya hatua ambazo tumechukua.

Ni maoni yangu na nilishawaeleza DAWASCO na DAWASA kwamba nao wanastahili kuingia katika kusambaza maji kwa malori katika kipindi hiki ambacho uwekaji wa mtandao wa mabomba au uchimbaji wa visima unasubiriwa ili kuweka ushindani katika biashara haramu ya maji ya sasa. Kwa kuwa hata EWURA itakapotoa bei elekezi ya kwenye sekta binafsi ya maji ikiwemo ya malori ili kudhibiti soko holela bado palipo na uhaba kutakuwa na bei ya kuruka ya kilanguzi (blacket market). Imefika wakati wananchi wa maene mnayolanguliwa maji katika mkoa wa Dar es salaam sio ya jimbo la Ubungo pekee kuunga mkono hizi jitihada ili lisiwe wazo la Mnyika bali la umma serikali itekeleze haraka zaidi.

JJ
 
hakuna kinachovurugwa,mi mnyika nilimpigia kampeni 05 ht juzi nimempa kura ila ameudhi sana kututukana sisi watanzania wote kutuona ni mijusi.hakuna alichofanya cha maana zaidi ya mijisifa ya kijinga.aige utendaji wa rejia r.i.p hawaropoki lakini wanapiga mzigo balaa

Ptuuuuuuuuuuuuuu! Khaa!
 
Naomba kuunga mkono hoja hii kwa nguvu sana.
Nashauri ripoti hii uichapishe na kuisambaza ktk jimbo lote. Viongozi wote wa chama ktk ngzi kata na tawi waipate ili wawaeleze wananchi.Ofisi zote za chama iwe na nakala.

Pili, Ni ukweli kwamba wagombea watarajiwa wa vyama vyote wanaeneza taarifa za uwongo huko mtaani kuwa wewe ni mbunge wa magazeti na mjengoni. Ukisambaza taarifa hii utakuwa umekata mzizi wa fitina.

Tatu, si vibaya kama utawaambia wengine kupitia vyombo vya habari. Well, wako watakaosema unatafuta cheap popularity, lakini ndivyo walivyomsema mbowe na helikopta yake 2005 lakini baadaye nao wakamwiga.

kuna kitu unabembelezea upate kwa mnyika sio bure.unajipisha pitisha mno,be careful mkuu mjini apa.
 
Kanali Gadafi,

Asante kwa maoni yako, hata hivyo unatoa tu ujumbe wa ujumla na kwa mara nyingine unapotosha. Taja majina ya barabara na aina ya ubovu kwa kuwa huwezi kusema tu kwa ujumla tu barabara zote ni mbovu wakati wako wanaofurahia matengenezo ya barabara katika maeneo yao.

Kuhusu bei ya maji, ungesema ni eneo gani hasa ambapo maji ni 700; naelewa maeneo yenye ulanguzi wa maji mpaka 500. Na kama ukiingia kwenye hii taarifa na kusoma sehemu ya maji JOHN MNYIKA: Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA) unaweza kupata maelezo ya hatua ambazo tumechukua.

Ni maoni yangu na nilishawaeleza DAWASCO na DAWASA kwamba nao wanastahili kuingia katika kusambaza maji kwa malori katika kipindi hiki ambacho uwekaji wa mtandao wa mabomba au uchimbaji wa visima unasubiriwa ili kuweka ushindani katika biashara haramu ya maji ya sasa. Kwa kuwa hata EWURA itakapotoa bei elekezi ya kwenye sekta binafsi ya maji ikiwemo ya malori ili kudhibiti soko holela bado palipo na uhaba kutakuwa na bei ya kuruka ya kilanguzi (blacket market). Imefika wakati wananchi wa maene mnayolanguliwa maji katika mkoa wa Dar es salaam sio ya jimbo la Ubungo pekee kuunga mkono hizi jitihada ili lisiwe wazo la Mnyika bali la umma serikali itekeleze haraka zaidi.

JJ

Halafu mh. Mnyika,
wapotoshaji wengine kama ulivyosema mwenyewe uwapotezee, sisi tutawajibu sawia. Maana wanadhani unakaa hapo kujibu hoja zao huna kazi nyingine za kichama za kufanya.
 
Mkuu Mnyika,
Kazi yako ni hakika kila mtu anaikubali labda awe kuadi wa UFISADI. Tunashukuru leo upo nasi hapa kwenye forum. Nina ombi kwako mkuu wangu. Kwa niaba ya wapigakura wako wa Msakuzi/Makabe ninaomba kwa heshima na taadhima sasa ututembelee tusaidiane kutatua baadi ya changamoto ambazo zinatishia ustawi wa jamii yetu. Mambo ambayo tunataka utusaidie kusukuma ni;
1. UMEME: Mh. ni kwamba tunaishi msakuzi, njia ya kuelekea Mpiji magoe. Kitongoji chetu kina nyumba zaidi ya mia moja. Pia kuna nyumba/makazi ya watawa wa Katoliki pamoja na shule ya chekechea. TANESCO waliplan kuleta umeme maeneo hayo na tayari walileta na nguzo, cha ajabu nguzo zimeanza kuoza huu mwaka wa pili sasa umeme haupo. Cha ajabu maeneo ya jirani kuna umeme na tunazuiliwa kuunganisha umeme kutoka maeneo hayo kwa kisingizio cha kuw tuko kweye mradi mkubwa. Hivyo mkuu tunaomba ututembelee ili tupange pamoja nawewe namna ya kutusaidia.
2. Maji. Tunaomba ufatilie kwa kwa nini maji ya Ruvu juu yanatoka mbombani kwa wiki mara moja tuu na tena kwa mgao. Angalia isije ikawa ni hujuma dhidi yako ili wananchi wakuchukie kuwa huwatetei. Nadhani njia nzuri ni kututemeblea ili upate kero za wananchi

Ahsante

Mpigakura wako

Asante sana, kabla ya mkutano wa bunge nilikuja Msakuzi eneo ambalo tatizo nililoelezwa ni umeme kuwa chini, eneo hilo na njia ya kwenda Mpiji Magohe sikujulishwa. Hata hiyo, ukirejea hotuba yangu bungeni utaona kwamba kati ya maeneo ambayo nilihoji bungeni kuwa baadhi hayana umeme ni pamoja na Msakuzi wakati na nikataka hatua ya Wizara ya Nishati na TANESCO kupitia Kasma 3154 (Rejea: JOHN MNYIKA: HOTUBA YA KAMBI RASMI YA UPINZANI; WIZARA YA NISHATI NA MADINI ). Sasa kabla ya kufanya ziara kwa kuwa umenieleza kwamba palikuwa na mradi tayari, naomba nakala ya nyaraka zozote za mawasiliano kati yenu na TANESCO ili nipate pa kuanzia. Mpatie Diwani Kajale 0655956551 hapo Mbezi ataniletea kabla ya kupanga ratiba ya mkutano ili nikija iwe nimeshafuatilia. Mueleze pia Diwani kuhusu maji kwa kuwa kuna tatizo limejitokeza Mbezi kwa ujumla katika siku za karibuni katika hatua za uwekaji wa mtandao wa ziada zinazoendelea. Ukikwama unijulishe kwa hatua zaidi.

JJ
 
safi sana mkuu tulianza na ww kwa kulinda kura na tutamaliza na ww katika kusaidiana kuleta maendeleo siyo ubungo tu bali tanzania kwa ujumla kwan ww ni mbuge wa kitaifa!

mbunge wa kitaifa ni mbatia na wenzake,huyu ni wa jimbo la ubungo.
 
anaongoza kwa matusi na mauaji ya vijana, mfano kule iramba.

Matusi si sehemu ya malezi niliyokulia, mauji si sehemu ya mikakati yetu ya kisiasa, Unaweza kusoma hapa: Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012 kuhusu hayo masuala ya Iramba utapata ukweli.

Nadhani sasa nikubaliane na ushauri wa Aweda nitumie muda vizuri kujadili masuala ya taarifa ya kazi za maendeleo jimbo la Ubungo kama alivyoshauri.

JJ
 
Kanali Gadafi,

Asante kwa maoni yako, hata hivyo unatoa tu ujumbe wa ujumla na kwa mara nyingine unapotosha. Taja majina ya barabara na aina ya ubovu kwa kuwa huwezi kusema tu kwa ujumla tu barabara zote ni mbovu wakati wako wanaofurahia matengenezo ya barabara katika maeneo yao.

Kuhusu bei ya maji, ungesema ni eneo gani hasa ambapo maji ni 700; naelewa maeneo yenye ulanguzi wa maji mpaka 500. Na kama ukiingia kwenye hii taarifa na kusoma sehemu ya maji JOHN MNYIKA: Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA) unaweza kupata maelezo ya hatua ambazo tumechukua.

Ni maoni yangu na nilishawaeleza DAWASCO na DAWASA kwamba nao wanastahili kuingia katika kusambaza maji kwa malori katika kipindi hiki ambacho uwekaji wa mtandao wa mabomba au uchimbaji wa visima unasubiriwa ili kuweka ushindani katika biashara haramu ya maji ya sasa. Kwa kuwa hata EWURA itakapotoa bei elekezi ya kwenye sekta binafsi ya maji ikiwemo ya malori ili kudhibiti soko holela bado palipo na uhaba kutakuwa na bei ya kuruka ya kilanguzi (blacket market). Imefika wakati wananchi wa maene mnayolanguliwa maji katika mkoa wa Dar es salaam sio ya jimbo la Ubungo pekee kuunga mkono hizi jitihada ili lisiwe wazo la Mnyika bali la umma serikali itekeleze haraka zaidi.

JJ

asante kwa maelezo, barabara inayoanzia apa external kupitia darajani pale hadi kukutana na ile ya mabibo ni muhimu sana lakini mbaya kweli kweli.pili feeder roads kuacha morogoro road kwenda kimara kilungule ni mbaya sana.
 
Mnyika yale yote ulioahidi hujatekeleza hata moja, ila kwa kupiga domo bungeni hilo umefanikiwa, nia yetu ya wakazi wa ubungo ni kutekeleza uliyotuahidi vinginevyo 2015 ukae mguu sawa ukalime.

Ni bora kuwa na mnyika bungeni, mtetea wanyonge kuliko kuwa na wanaolala bungeni kwa miaka 50 huku wakijaribu kuwahadaa watanzania kwamba nchi ni maskini wakati wao wanatoroshea mabilioni nje ya nchi . Ushauri kwa mnyika pls imarisha security yako hawa watu wa ccm hawapendi msema kweli
 
Daaah Gadafi umetoroka kutoka kwenye?
Kwani libya kuna jimbo la ubungo!

Usipo mshukuru mtu kwa kidogo hatutegemei umshukuru kwa makubwa atakayo fanya!

Jimbo la ubungo halijabadilika chochote,kero ziko pale pale.sawa tu utawala wa magamba,mh mnyika amebaki na lawama kwa ccm ambazo hazina msaada kwetu,tunataka maji na barabara sio porojo
 
John Mnyika,
Nakushauri achana na siasa za vijiweni na zile za kwenye mitandao ya kijamii zinazokutukuza na kujiona shujaa ukavimba kichwa, jikite zaidi jimboni kwako.

Sijui kama hunajua saizi ubungo saizi mabomba ya umma karibu yote hayatoi maji na kwa hiyo watu kwenye baadhi ya maeneo bei ya ndoo moja Sh2,000 sijui umefanya jitihada gani, wakati wa kampeni za kutafuta kura za wananchi Mnyika, ulisema mengi.

Ulisema wakikupa kura utakomesha tatizo sugu la maji na kuwapa ahueni wakazi wa ubungo, lakini sasa tatizo limegeuka sugu zaidi..

Mnyika, unasahau hekima ya Bwana Yesu aliyefundisha na kuonya wafuasi wake akisema wasiwe kama wanafiki ambaye anamwambia mwenzake, ngoja nikutoe kibanzi kilicho kwenye jicho lakini anasahau kuwa yeye ana boriti jichoni, ambalo ni kubwa kuliko kibanzi cha mwenzako.

Huu ni ushauri wangu kwako najua tapingwa lakini nimefikisha.

Ritz,

Nashukuru kwa ushauri huu kutoka kwa kada wa CCM, kauli zako lakini ni za ujumla sana ungetaja hayo maeneo ambayo ndoo moja ya maji inauzwa 2000, inawezekana unazungumzia katika majimbo mengine lakini si Ubungo.

Pamoja na kuwa naelewa sasa hivi Mkoa mzima wa Dar es salaam maeneo kadhaa yana matatizo ya maji kutokana na uharibifu wa baadhi ya mabomba na DAWASCO wameshatoa kauli.

Niliyoyasema kwenye kampeni niliyaweka kwenye maandishi hapa: JOHN MNYIKA: Ujumbe wa Mbunge: Shukrani, Twende Kazi!, na utekelezaji wake katika mwaka mmoja na nusu usome katika taarifa ya kwenye mjadala huu.

Naomba nami nikushauri umshauri Rais Kikwete kuwa ahadi za maji alizozitoa mwezi Mei 2010 Kimara Mavurunza/Bonyokwa bado hazijatekelezwa na anao wajibu kusimamia zitekelezwe, kwa sasa naendelea kufuatilia DAWASCO, DAWASA na Wizara ya Maji hatua za haraka zisipochukuliwa nitaongoza wananchi kupata majibu kutoka ikulu.

JJ
 
asante kwa maelezo, barabara inayoanzia apa external kupitia darajani pale hadi kukutana na ile ya mabibo ni muhimu sana lakini mbaya kweli kweli.pili feeder roads kuacha morogoro road kwenda kimara kilungule ni mbaya sana.

Asante, hiyo ni ya kutoka Ubungo Maziwa mpaka Mabibo External kupitia daraja la Kisiwani, tayari nimefuatilia sana na imetengewa fedha za kujengwa kwa kiwango cha lami na TANROADS kuanzia mwaka wa fedha 2012/2013. Aidha, maombi yamewasilishwa mfuko wa barabara kwa ajili ya kupanua daraja ambalo sasa karibu linaweza likavunjika kutokana na uwingi wa magari. Wakati hatua hizo zikisubiriwa unaweza kuwasiliana na Diwani wa Ubungo Boniface Jacob na kuchangia matengenezo ya mara kwa mara ambayo huwa vijana wanayafanya pale kwa kuwa Manispaa imeshindwa kwa sasa: JOHN MNYIKA: Michango kwa ajili ya Barabara ya Maziwa-External Mandela, kifusi sasa; lami itafuata

Feeder road Kilungule ilifanyiwe matengenezo ya awali, itafanyiwa mengine na TANROADS ukirejea kwenye JOHN MNYIKA: Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA) utaona ni kati ya barabara nilizoorodhesha. Nitaendelea kufuatilia hatua kwa hatua, nanyi naombeni mfuatilie kwa kushirikiana na madiwani wa kata za Kimara na Makuburi.

JJ
 
Mh mnyika,kwanini mliua kijana asiekuwa na hatia pale iramba mkk,huoni hiyo dhambi itakutafuna sana wewe kitila na mwikwabe hadi siku ya kufa kwenu?
 
Asante, hiyo ni ya kutoka Ubungo Maziwa mpaka Mabibo External kupitia daraja la Kisiwani, tayari nimefuatilia sana na imetengewa fedha za kujengwa kwa kiwango cha lami na TANROADS kuanzia mwaka wa fedha 2012/2013. Aidha, maombi yamewasilishwa mfuko wa barabara kwa ajili ya kupanua daraja ambalo sasa karibu linaweza likavunjika kutokana na uwingi wa magari. Wakati hatua hizo zikisubiriwa unaweza kuwasiliana na Diwani wa Ubungo Boniface Jacob na kuchangia matengenezo ya mara kwa mara ambayo huwa vijana wanayafanya pale kwa kuwa Manispaa imeshindwa kwa sasa: JOHN MNYIKA: Michango kwa ajili ya Barabara ya Maziwa-External Mandela, kifusi sasa; lami itafuata

Feeder road Kilungule ilifanyiwe matengenezo ya awali, itafanyiwa mengine na TANROADS ukirejea kwenye JOHN MNYIKA: Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA) utaona ni kati ya barabara nilizoorodhesha. Nitaendelea kufuatilia hatua kwa hatua, nanyi naombeni mfuatilie kwa kushirikiana na madiwani wa kata za Kimara na Makuburi.

JJ

mkuu hizi ni porojo tu hakuna lolote na 2015 ipo nyumba ya pili apo sijui utawadanganya nini tena watu wa ubungo
 
asante kwa maelezo, barabara inayoanzia apa external kupitia darajani pale hadi kukutana na ile ya mabibo ni muhimu sana lakini mbaya kweli kweli.pili feeder roads kuacha morogoro road kwenda kimara kilungule ni mbaya sana.

kama mlitegemea mnyika ndo atawaletea maendeleo andikeni maumivu,huyu dogo ni msanii mbaya kabisa
 
Matusi si sehemu ya malezi niliyokulia, mauji si sehemu ya mikakati yetu ya kisiasa, Unaweza kusoma hapa: Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012 kuhusu hayo masuala ya Iramba utapata ukweli.

Nadhani sasa nikubaliane na ushauri wa Aweda nitumie muda vizuri kujadili masuala ya taarifa ya kazi za maendeleo jimbo la Ubungo kama alivyoshauri.

JJ

mkuu hebu toa maelezo vizuri apo.pale kwenye mauaji ya iramba hutoki wewe,mana ulihamasisha vijana wako wamgonge yule kijana nao wakafanya kweli,mbona hakufa jana yake au mwaka jana bali ulipoenda wewe na vibaraka wako ndio mkamuua?kuhusu matusi na kauli za kitoto unabisha nini wakati bunge huwa linaonyeshwa live?umeshakua sasa,badilika.
 
Back
Top Bottom