Swali la Ugomvi: Serikali isiyo na "fedha" inaweza vipi kwenda vitani?

Mzeemwanakijiji, hongera zako mie nimekwisha jitoa mhanga kutounga mkono vita hii ya kutajirisha mafisadi.Hii ni sawa na vita ya kutengeneza kupotezea mambo mengine au kama vile upepo upite.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, Kawawa na Chief Mhaiki walishawahi kukubali kuwa ziwa lote si letu. Hizi zilikuwa kauli zao za Bungeni miaka ya sitini. Kuna mtu alifanya research juu ya mgogoro huo miaka ya nyuma sana na iliwekwa hapa JF in Pdf formatt.

Hivi hap uliowa refer ndio maoni ya Tanzania?
 
MM,
Ningekuwa na madaraka ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ningeagiza ukamatwe mara moja na ufunguliwe kesi ya uhaini. Nchi inapokuwa kwenye hali tete namna hii hutakiwi kutoa habari yenye heading ya namna hii, bila kujali ina ukweli ama la.

Na, ashuming kweli hatuna hela, unataka adui sasa atuvamie akijua kuwa hatuna hela? Ningeomba hii mada ifutwe na tuendelee na mijadala mingine, na pia watu wawe waangalifu na watu popular ndani ya forum hii kwa sababu wakati mwingine huwa wanachemsha saaaana ila tunashindwa kuona sababu ya popularity iliyowafunika.
Kwa hili MM ningekuomba usiongee sana hapa, kama una nafasi ongea na hao viongozi na wana siasa ana kwa ana, au hata kwa simu, uwape duku duku lako na si kukaa unamwaga mwaga mambo yako hapa hadharani. Hili swala ni tete na tusilijadili sana hapa, tuviachieni vyombo vinavyohusika vitali-handle. This case is a unique one and very different fron RICHMOND, KAGODA or whichever. Tuliache tusikae tunapayuka payuka hapa. Mwenye hoja, akaongee na viongozi wetu wapo watamsikiliza, na siyo ku-publicize, tuna jeopardize usalama wa nchi yetu na tukiendelea hivi ipo siku itakuja kutugharimu, japo siyo sasa!

Wa kwanza kukamatwa unatakiwa kuwa wewe,unaejifanya huujui au unataka kuficha ukweli ambao uko wazi
kwani inapotikea migomo ya madaktari na walimu na hali duni ya maisha ya watanzania Tanzania inakuwa yai
kwamba taarifa hazitfiki nje ya mipaka yetu? Na je udhaifu wa hii serikali ni siri kweli? Tuache kujifariji kwenye
ukweli tuambizane bwana.
 
Asante kaka kwa kuwakumbusha historia yetu hawa viongozi wanaofikiri kusema hayo ndo kutarudisha heshima yao kwa nchi, na watuelewe vizuri hatusemi kwamba tusiilinde mipaka yetu dhidi ya wavamizi(japo kuwa mara kadhaa tumekuwa tukiwasikia kuwa mipaka yetu i salama salmini) la hasha bali vita iwe ni njia ya MWISHO KABISA, yaani ikibidi. Lakini sasa hivi kila mtu amekuwa amir jeshi mkuu hawa watu ni wale hasa wasiojua hali ya maisha ilivyo kwa mtanzania (wao ni watanzania wakoloni).
 
Mkuu vita haipiganwi kwa maneno bali ni vifaa na mbinu
Sasa mtawapiga kwa muda wa dakika 30 kwa kutumia zile helicopter zinazoanguka zenyewe alizoleta Sailesh Vathlani
Acha hizo watu tunazungumzia mustakbali wa taifa na sio ushabiki
mpaka sasa wamalawi wa meshachukua ziwa lote na exploration inaendelea kama kawaida
Isitoshe wana support ya USA nas UK labda nyie mupate support ya Iran kama mlivyowasaidia kuregister meli zao

Tell him the truth,maana naona anatoka mapovu tu na point zenyewe anatoa ni pointless,nina shaka
kama wanajeshi wenyewe ni aina ya huyu bwana "wakati ndio sasa" tusithubutu kuingia vitani.
 
Tell him the truth,maana naona anatoka mapovu tu na point zenyewe anatoa ni pointless,nina shaka
kama wanajeshi wenyewe ni aina ya huyu bwana "wakati ndio sasa" tusithubutu kuingia vitani.
Si muhamie Lilongwe tu ili wakianza kudundwa muwatetee vizuri!
 
KT0183.jpg

Mara zote wakiulizwa kuhusu mambo mbalimbali wanasema 'hawana fedha' na kuwa serikali ni maskini. Tumeona migomo ya madaktari, walimu na tishio la migomo ya wafanyakazi. Tumeona jinsi ambavyo wamekuwa wakilalamika kila kukicha kuwa "serikali haina fedha" -sikiliza kwa makini majibu ya mawaziri Bungeni wanavyorudia suala hili. Wanasema "serikali ikiwa na uwezo" au "tunaendelea kutafua fedha kwa ajili ya mradi huo; tena za ndani na za 'washirika wa maendeleo'".

Kila ukiwauliza mengi ambayo hayaendi vizuri jibu lao ni "serikali yetu haina fedha" au "hali ngumu". Sasa leo hii serikali hii hii ambayo "haina uwezo" inadai ati iko tayari kwenda vitani. Wale ambao tulikuwepo wakati wa vita vya Uganda tunakumbuka gharama kubwa (great toll) ya vita ile kwa maisha ya wananchi hadi vijijini. Hakuna ambaye kwa namna yake hakusikia maumivu (pinch) ya vita. Na vita ilipokwisha gharama yake kwenye uchumi wetu na maendeleo ya watu wetu haikuweza kurudishwa kwa urahisi. Kwa karibu miaka minne (miwili ya vita na ile ya reconstruction) ilisababisha nchi yetu kurudi nyuma zaidi ya ilipokuwepo. Ni kweli tulishinda vita lakini kwa gharama kubwa sana siyo tu ya fedha bali pia ya watu.

Kwa wanaokumbuka historia ya Uganda mojawapo ya matukio ya vita ni vita ya kuichukua Lukuya (Battle of Lukuya) ni hapa kiasi cha wanajeshi wetu kiliposhtukizwa na wanajeshi mamluki wa Libya na kujikuta kinarudishwa nyuma kabla ya Brigedi ya 201 na 208 kujipanga upya na kuwashambulia mamluki hao na kuwashinda na kusafisha njia ya kwenda Kampala (baada ya kuchukua Entebbe na Jinja). Gharama ya fedha tu serikali ya Museveni ndio iliweza kuilipa Tanzania mwaka 2007! Ikumbukwe kuwa vita ya Uganda inakadiriwa kuigharimu Tanzania dola milioni 1 kwa siku na hizo zilitoka mifukoni mwetu (hatukuwa na wajomba). Leo hii tumepiga kelele kulipa dola laki moja kwa Symbion kwa siku. Fikiria Wamarekani kwenye vita ya Iraq walikuwa wanaunguza dola bilioni 1 kwa siku!

Nikiangalia hali hiyo najiuliza; hivi kweli kina Lowassa na wengine wanaoshabikia vita wanafikiria kweli gharama yake? Hivi kuna mtu amewahi kuuliza Tanzania ilipoteza askari wangapi vita ya Uganda? Hivi watu wanajua kuwa ili jeshi letu liende vitani ni lazima wale wote waliokuwa reserve nao wawe reactivated? Yaani kabla ya kwenda Vitani itabidi kwanza tuongeze askari wote kutoka kama 30,000 waliopo sasa hivi na kufikia angalau 150,000 hivi kuweza kushinda vita. Hawa tutakaowachukua wengi ndio wasomi wenyewe na wafanyakazi maofisini watabadilishwa na nani? Ikumbukwe kwenye vita ya Uganda hawakwenda JWTZ tu bali Mgambo, Polisi, Magereza na wale waliopewa mafunzo ya haraka haraka. Je tuko tayari kuleta "draft" ya kulazimisha wanaume wote wenye miaka 18 na zaidi kuingia kambini? au watu wanafikiria ni "JWTZ" ndio litaenda vitani wakati wengine tunacheza ping pong na kuchat kwenye JF juu ya maendeleo ya vita?

Ninachopinga kabisa na ninaona ni mambo ya hatari ni kuzungumzia masuala ya vita bila kuonesha fikara na hekima. Kabla haujaamua kwenda vitani jipe nguvu kwanza. Na hakuna nguvu kubwa zaidi kama nguvu ya kiuchumi. Lakini jambo jingine ambalo labda wengine wameshafikiria ni vikosi vyetu vitakula nini? Au watu wanafikiria wanajeshi wakienda vitani wanapewa zile ration tu? Pamoja na gharama nyingine zote je bado tutaweza kulilisha taifa letu wakati wa vita? Wapo ambao hawajui kuwa njaa ya mwanzoni mwa miaka ya 1980 sehemu kubwa pia ni matokeo ya vita ya Uganda? Je tuko tayari kula dona na yanga tena na kurudishwa kwenye ration kwa taifa zima na mambo yale ya duka la kaya? au watu wanafikiria wataendelea kula nyama choma jioni wakati vita inaendelea?

Tusianze kupiga ngoma za vita (we shouldn't beat the drums of war) kama hatuko tayari kuingia vitani. Ni uzembe na reckless na binafsi naamini viongozi wote watatu (Lowassa, Membe na Sitta) wanatia shaka kama wana hekima na busara ya kuwa viongozi wa taifa letu. Kiongozi hata mwenye uwezo kiasi gani ni lazima asite linapokuja suala la vita na siyo kusita kwa sababu ya woga lakini kusita kwa sababu ya kujua analiita taifa lake kufanya nini. Na anapozungumza vita awe na uhakika kabisa (absolute confidence) kuwa hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuepuka vita hiyo.

Kwa mara nyingine nawasihi watu wanaoshabikia vita kama njia ya "kulinda mipaka yetu" wafikirie kwa hekima kuwa zipo njia nyingine nyingi zaidi za kufanya hivyo ikiwemo mazungumzo na mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa. NI LAZIMA TUMALIZE NJIA ZOTE ZA AMANI (siyo mazungumzo tu) kabla hatujasema "we have had enough, we are preparing for war) na binafsi naamini kama tutaonesha hekima ya kutumia njia zote na busara ya kuepuka vita siku ikiitwa vita kweli kabisa tunaweza kwenda siyo kujihami tu bali kuiona Malawi kama tishio na kuanzisha an offensive assault ili kuliondoa tishio hilo mara moja na daima.

Nashauri vichwa vilivyotulia vizungumza lugha ya amani sasa hivi na kutuliza hizi ngoma za vita na mbiu za mapigano. Maana kama sasa hivi tu wanahangaika kulipa mishahara na kulisha taifa letu, sijui itakuwaje WAKATI WA VITA!

MMM

MMM, soma japo uchumi kidogo utajuwa fedha za kwendea vitani zinapatikana vipi na ni kwanini nchi hata iwe masikini vipi bado inaweza kwenda vitani. Wachumi watakueleza kwamba, you fund the war by consuming the future a.k.a borrowing a.k.a printing and you can't go wrong with that.

Labda swali lako lingejikita kwenye kuuliza njia ipi ni bora kupata ela za vita? Hutasikia hata siku moja nchi imeingiliwa ikashindwa kwenda vitani kwa kukosa ela, labda nchi hiyo isiwe na serikali.
 
MMM nilikuwa ninakuheshimu kama mtu unayefikiri sana lakini katika hili nimukushusha, hivi wewe ukivamiwa kwako watu wanakuja hadi sebuleni kuchukua mali, utakaa tu useme huna pesa, huna chakula. Hoja yako ni dhaifu sana. Kwa kukusaidia, angalia filamu ya Spartacus, sehemu ya tatu, walipokuwa sieged na warumi kilimani wamebaki wachache, mmoja wao muoga kama wewe, alihoji 'tutawezaje kupigana hapa hatuna chakula wala maji, tutafia hapa ni vyema tu surrender'. Doctore, mshauri wao alijibu akamwambia, 'mwanaume anapokuwa vitani akipigana kuokoa mali yake, utu wake na uhai wake, mwili wake hautegemei nguvu za chakula wala pesa, bali ni hiari na hari ya moyo wa kupigana'. Tulipoenda vitani uganda, tulikuwa na hali mbaya ya kifedha na kuichumu vilevile, na hata uwiano wetu na uganda walikuwa wakituzidi kwa 1:6. Lakini tulienda kwa moyo mmoja na uzalendo tukawatwanga, wakiwa na silaha kali sana kutuzidi. Fuatilia tena histiroa ya kivita kati ya waajemi na wagiriki utajifunza zaidi. NASEMA VITA VYA KULINDA MALI YAKO, UTU WAKO, UHURU WAKO MIPAKA YAKO, SIO VITA YA FEDHA WALA CHAUKULA.
 
Tujiulize Maswali Kabla Hatujasogea Mbele zaidi!! Hawa waliotangaza Vita wananafasi Yoyote Katika katiba hii ya zamani / soryy iliyopo sasa kutangaza Hayo? Au ndio Ile kusema kwa sasa Nchi haina Msemaji? / Amiri Jeshi Mkuu? Hadi watu wanamsemea tu?
 
MMM nilikuwa ninakuheshimu kama mtu unayefikiri sana lakini katika hili nimukushusha, hivi wewe ukivamiwa kwako watu wanakuja hadi sebuleni kuchukua mali, utakaa tu useme huna pesa, huna chakula. Hoja yako ni dhaifu sana. Kwa kukusaidia, angalia filamu ya Spartacus, sehemu ya tatu, walipokuwa sieged na warumi kilimani wamebaki wachache, mmoja wao muoga kama wewe, alihoji 'tutawezaje kupigana hapa hatuna chakula wala maji, tutafia hapa ni vyema tu surrender'. Doctore, mshauri wao alijibu akamwambia, 'mwanaume anapokuwa vitani akipigana kuokoa mali yake, utu wake na uhai wake, mwili wake hautegemei nguvu za chakula wala pesa, bali ni hiari na hari ya moyo wa kupigana'. Tulipoenda vitani uganda, tulikuwa na hali mbaya ya kifedha na kuichumu vilevile, na hata uwiano wetu na uganda walikuwa wakituzidi kwa 1:6. Lakini tulienda kwa moyo mmoja na uzalendo tukawatwanga, wakiwa na silaha kali sana kutuzidi. Fuatilia tena histiroa ya kivita kati ya waajemi na wagiriki utajifunza zaidi. NASEMA VITA VYA KULINDA MALI YAKO, UTU WAKO, UHURU WAKO MIPAKA YAKO, SIO VITA YA FEDHA WALA CHAUKULA.
 
MMM nilikuwa ninakuheshimu kama mtu unayefikiri sana lakini katika hili nimukushusha, hivi wewe ukivamiwa kwako watu wanakuja hadi sebuleni kuchukua mali, utakaa tu useme huna pesa, huna chakula. Hoja yako ni dhaifu sana.

Mzee mwenzangu MMM msameheni kwa hili. Alikurupuka na kuvaa jezi ya washabiki badala ya ile aliyepangiwa na kocha! Yuko tayari atawaliwe ili aendelee kula ugali badala ya kuutupa ugali apigane ili arudi kula ugali akiwa huru!
 
Si Malawi wala Tanzania ambayo ipo tayari kwa vita. maneno ya 'vita' 'vita' ni kawaida kutolewa pale ambapo nchi mbili au zaidi zinapotofautiana. USA na USSR walitupiana maneno sana kwa miaka mingi (cold war) lakini hawajawahi kuanzisha vita tunayoisema hapa.Nadhani waziri wa mambo ya nje alisomeka vizuri tu. labda kama tuna yetu vichwani mwetu.
..Sababu kubwa ya USA na USSR kutopigana ni kwamba wote wana nuke, na nuke haikopeshi! Ndo maana India na Pakistan wataendelea na kelele lakini sio vita. Si Malawi wala Tanzania wenye nuke....... Hakuna nchi iliyo tayari kwa vita-hata USA hawako tayari kwa vita na Iran, ingawa wanapenda wawapige. So ishu sio kuwa tayari, bali ulazima wa kuanzisha vita.
 
Hakuna vita za kuzuka zuka tu karne hii,kumbuka UK wana interest zao kule na ndege na RIG zilizopo kule ni za UK.huwezi kupiga kule maana wakubwa wamekaa pale wanataka gesi na labda mafuta!pia sisi lazima twende tukapitishe bakuli usa au uk,watatupa masharti magumu sana na kuona tuna rasilimali kibao sana na tumeshindwa kuzitumia sababu(ufisadi) na mikataba mibovu kabisa kuwahi kutokea,watatubana hapo na kuacha UN waje waamue wakati wale wakiendelea na utafiti!!hakuna vita hata siku moja miaka hii!!

Umenena kweli. Tatizo la watawala wetu ni kujibu kitu bila kutafakari the bigger picture na kufanya consultations zakutosha. Nakumbuka nikiwa kijana wa darasa la kwanza wanakijiji walichangishwa ng'ombe kwa ajili ya vita ya Kagera. Sihitaji kuona mambo kama haya wakati njia za amani zipo. Kuhusu serikali kukosa pesa hili ni tatizo litokana na kukosa utawala bora (rushwa, kukosa vipau mbele) na kuendekeza kutandaza bakuli kwa watawala wa dunia.
 
hawakutakiwa kuzungumzia masuala ya vita at all. Siyo katika hatua hii hata kikao cha kwanza cha "njia nyingine" hakijafanyika! Si wamepanga kukutana Augusti 20? so haraka yao ya nini?

mimi hili la kuzungumzia vita sioni tatizo, ulitegemea wa fanye kipi wakati viongozi wa malawi wanasisitiza ziwa ni lao na kuendeleza utafiti. tatizo naliona pale inapotokea kiongozi anaye zungumzia vita jamii inamchukulia vipi katika matendo yake kama kiongozi wa hiyo jamii? maana mwingine jamii ikiona anazugumzia kuingia vitani, vita yenyewe iwe ya kutetea raslimali tayari ni tatizo.

ila hili la malawi tunaweza kulimaliza kwa sisi kuwapa watu mikakataba ya utafiti upande wetu, tuipe kampuni ya kichina basi. kwenda mahakamani tutashindwa hilo halina ubishi, lakini wakubwa hawa wataheshimiana na wataelewana tu, naambiwa marekani nao wanatembeza bakuli china (hata tukiita mkopo). b

usara inaonyesha kuwa hamna jinsi wamalawi wanaweza kutuzuia tusitumie hilo ziwa lakini huo mwaka 1890 inaonyesha maslahi ndiyo yalitumika kugawa hiyo mipaka wala si busara, na wamalawi nao wameonyesha wanaongozwa na maslahi wala si busara, tena maslahi yenyewe wameyaelekeza kwenye gas na mafuta wakasahau maji, samaki, usafiri na kikubwa kabisa uhai wa watu wanaozunguka ziwa hilo.
 
hawakutakiwa kuzungumzia masuala ya vita at all. Siyo katika hatua hii hata kikao cha kwanza cha "njia nyingine" hakijafanyika! Si wamepanga kukutana Augusti 20? so haraka yao ya nini?

mimi hili la kuzungumzia vita sioni tatizo, ulitegemea wa fanye kipi wakati viongozi wa malawi wanasisitiza ziwa ni lao na kuendeleza utafiti. tatizo naliona pale inapotokea kiongozi anaye zungumzia vita jamii inamchukulia vipi katika matendo yake kama kiongozi wa hiyo jamii? maana mwingine jamii ikiona anazugumzia kuingia vitani, vita yenyewe iwe ya kutetea raslimali tayari ni tatizo.

ila hili la malawi tunaweza kulimaliza kwa sisi kuwapa watu mikakataba ya utafiti upande wetu, tuipe kampuni ya kichina basi. kwenda mahakamani tutashindwa hilo halina ubishi, lakini wakubwa hawa wataheshimiana na wataelewana tu, naambiwa marekani nao wanatembeza bakuli china (hata tukiita mkopo).

busara inaonyesha kuwa hamna jinsi wamalawi wanaweza kutuzuia tusitumie hilo ziwa lakini huo mwaka 1890 inaonyesha maslahi ndiyo yalitumika kugawa hiyo mipaka wala si busara, na wamalawi nao wameonyesha wanaongozwa na maslahi wala si busara, tena maslahi yenyewe wameyaelekeza kwenye gas na mafuta wakasahau maji, samaki, usafiri na kikubwa kabisa uhai wa watu wanaozunguka ziwa hilo.
 
MMM nilikuwa ninakuheshimu kama mtu unayefikiri sana lakini katika hili nimukushusha, hivi wewe ukivamiwa kwako watu wanakuja hadi sebuleni kuchukua mali, utakaa tu useme huna pesa, huna chakula. Hoja yako ni dhaifu sana. Kwa kukusaidia, angalia filamu ya Spartacus, sehemu ya tatu, walipokuwa sieged na warumi kilimani wamebaki wachache, mmoja wao muoga kama wewe, alihoji 'tutawezaje kupigana hapa hatuna chakula wala maji, tutafia hapa ni vyema tu surrender'. Doctore, mshauri wao alijibu akamwambia, 'mwanaume anapokuwa vitani akipigana kuokoa mali yake, utu wake na uhai wake, mwili wake hautegemei nguvu za chakula wala pesa, bali ni hiari na hari ya moyo wa kupigana'. Tulipoenda vitani uganda, tulikuwa na hali mbaya ya kifedha na kuichumu vilevile, na hata uwiano wetu na uganda walikuwa wakituzidi kwa 1:6. Lakini tulienda kwa moyo mmoja na uzalendo tukawatwanga, wakiwa na silaha kali sana kutuzidi. Fuatilia tena histiroa ya kivita kati ya waajemi na wagiriki utajifunza zaidi. NASEMA VITA VYA KULINDA MALI YAKO, UTU WAKO, UHURU WAKO MIPAKA YAKO, SIO VITA YA FEDHA WALA CHAUKULA.
Bravo!
Could'nt have said it better!

Heshima ya mwanaume, mwanaume wa kweli, si kulalama bali kugangamala to any threat percived or real.
Mtu kutetea familia yako wakati wa wasi wasi na kuitia moyo familia hiyo ni ujasiri mtu azaliwayo nao.

Si wote , kama huyu mtoa mada, mwenye ujasiri kama huo. Visingizio na malalimishi mbele ya uchokozi wa dhahiri yanakufanya mtu udharaulike katika jamii.

Na ndio maana ninawaheshimu sana Israel, kwa hali yao na walivyozungukwa na maadui hilo taifa lingekuwa lime-cease kitambo.

Tanzania italindwa na wenye moyo, wenye wasi wasi waondoke tu kama wahindi wafanyavyo, mrudi nchi ikisha tulia.
 
Upotoshaji haufai jamani, tusitimie kila credit tuliyo nayo kupotosha kila jambo liwe dogo ama kubwa, jema ama baya na yote kuyafanya yawe mabaya. Kunakipindi cha kutofautiana na kipindi cha kuwa pamoja.
Wakowapi watanzania halisi? Wote tumebakia magoigoi? Wataalam wa kupiga porojo kwenye kila jambo?

Nilazima umwoonyeshe mwizi wako how far are u ready to go, hata kabla hajaja mezani ili asije mezani akidhani ataleta longolongo na mambo kuisha. Nahoa mabwana zao wanao wadanganya waone hatari ya Miradi yao kuingiza hasara kubwa wakiendelea kuwadanganya jirani zetu. Viongozi wetu katika hili wamecheza karata dume.
MMM ulilo lenga ni sahihi na nilazima linaangaliwa, lakini elewa kama nimekutapeli alafu unakuja kwangu na uso wenye woga na kunibembeleza unategemea jibu gani? Mmemsahau yule waziri wa Sadam Hussein?
Siungi Mkono hoja.
 
Back
Top Bottom