Isome vizuri heading ya thread hii kisha usome na bandiko lote jinsi lilivyo. Malawi wanatudharau sana kama kauli ile ya Lowasa imetoka kwa mtu mwenye uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa nchi yetu.Waandishi wengine wavumilieni bure tu maana wanaandika kwa kutaka sifa.
Miaka ya Mwalimu wakati kuna suala tete mobilisation ya kitaifa alikuwa anaandika mwenyewe tahriri ya habari ili jamii tuwe na msimamo mmoja.
Sasa hili la Mwanakijiji kutaka kuonekana kupinga kila kitu kinamwonesha in a different light.
Aidha ni mwoga, au ni fifth columnist au analipwa kufanya hivyo.
Kwa vyovyote vile hali ya kiuchumi ya Tanzania leo ni much better off kuliko 1978, na vile vile kama vita itazuka, wapenda nchi wataenda mbele.
Makala kama hizi za Mwanakijiji kwa kweli zinaonyesha mtu mwenye akili inayomfaa yeye mwenyewe na hali ikiwa mbaya zaidi mpakani, itachukuliwa kuwa inamsaidia adui.