Swali la Ugomvi: Serikali isiyo na "fedha" inaweza vipi kwenda vitani?

Muulize Nyerere aliyetufungisha mikanda mpaka anakufa. Sijui wako ulifunguliwa?
Alifia madarakani kama Atta Mills? Idd Amin hakuingia kijeshi ndani ya mipaka ya Tanzania? Unafanya vizuri sana Zomba kumtaja Mwalimu mara kwa mara.
 
MMKJ, hoja yako ni ya msingi sana kwa sasa. Ila kuna watu wa kizazi cha dot.com na washabiki wa siasa za kufuata mkumbo wamekushambulia wewe wakati hoja yako ni ya utetezi kwa manufaa ya taifa kwa sasa na raia wote.
Kama kweli Taifa halina fedha za kuweza kununua dawa,vifaa mahospitalini,vitabu na madawati,mikopo elimu ya juu na kadhalika, jee itaweza kuingia vitani hiyo?
Mimi sikatai kuwa kuna wakati hata kama huna chochote uko radhi upambane hata kwa mapanga kulinda kicho chako au heshima yako baada ya kukosekana njia nyingine yeyote.
Jee sisi tumeshafikia mahala njia zingine zote za majadiliano zimeshindwa? Hapana maana kuna tarehe ya mazungumzo iko huko mbeleni.
Mwanakijiji,hakuna cha kwenda vitani katika swala hili bali ni wanasiasa wenye uchu tuu ndio wamekurupuka na kuzungumza bila mamlaka ya juu kuruhusu.
Tatizo limeanzia juu, Bwana mkubwa ameshindwa kuwa kata makali hawa jamaa kwa kutamka hadharani kuwa Tanzania na Malawi bado ziko katika mazungumzo ya kidiplomasia hivyo minong'ono ya vita ingepotea. Ila kwenye hili kanyamaza kabisa bali kwenye suala la Rada kawa wa kwanza kumnyamazisha Membe kuhusu mafisadi wa Rada.
Chakaza;
Baunsa au mtu mwingine yeyote akija nyumbani kwako (na-assume wewe ni mwanamme) akakuambia kwamba kuanzia leo let's say, mtoto wako wa pili wa kiume ni wake na anataka kuja kumchukua siku moja aondoke naye akakae nyumbani kwake milele, ipo siku anakuja,..., utakaa kimya? Hutajiandaa kwa vita? na siku ikitokea kweli akaja amedhamiria kufanya kile alichosema, utaacha kupigana hata kama nyumbani kwako hamna upinde, wakati mikono unayo?
 
Back
Top Bottom