hawakutakiwa kuzungumzia masuala ya vita at all. Siyo katika hatua hii hata kikao cha kwanza cha "njia nyingine" hakijafanyika! Si wamepanga kukutana Augusti 20? so haraka yao ya nini?
Hilo andiko limekaa ki-fifth columnist.
No proud Tanzania will swallow that!
You may be.
Tujiulize Maswali Kabla Hatujasogea Mbele zaidi!! Hawa waliotangaza Vita wananafasi Yoyote Katika katiba hii ya zamani / soryy iliyopo sasa kutangaza Hayo? Au ndio Ile kusema kwa sasa Nchi haina Msemaji? / Amiri Jeshi Mkuu? Hadi watu wanamsemea tu?
Kaka nakubaliana na wewe 100%. Ki ukweli pamoja na heshima zoote za MMM, hili andiko lake halina mashiko kabisa, labda mtu ambae hawezi kung'amua kwa jicho la tatu. Siyo kila kitu arukie tu na kutoa maoni yake, hili andiko lake liko shallow sana, na halima mwangaza wowote kwa Taifa zaidi ya kupinga pinga tu!
RIGHT. Alafu kwa nini kauli nzito namna hii itolewe na mawiziri, eti hadi lowasa na yeye anajichomeka na kuelezea uwezo wa majeshi yetu? au mimi ndio sielewi chain of Command ilivyo. wen't MR President supposed to say if there were in need a need to say anything about our readness to deproy the armied forces? au wametake advantage ya Udhaifu wa rais?
Mara zote wakiulizwa kuhusu mambo mbalimbali wanasema 'hawana fedha' na kuwa serikali ni maskini. Tumeona migomo ya madaktari, walimu na tishio la migomo ya wafanyakazi. Tumeona jinsi ambavyo wamekuwa wakilalamika kila kukicha kuwa "serikali haina fedha" -sikiliza kwa makini majibu ya mawaziri Bungeni wanavyorudia suala hili. Wanasema "serikali ikiwa na uwezo" au "tunaendelea kutafua fedha kwa ajili ya mradi huo; tena za ndani na za 'washirika wa maendeleo'".
Kila ukiwauliza mengi ambayo hayaendi vizuri jibu lao ni "serikali yetu haina fedha" au "hali ngumu". Sasa leo hii serikali hii hii ambayo "haina uwezo" inadai ati iko tayari kwenda vitani. Wale ambao tulikuwepo wakati wa vita vya Uganda tunakumbuka gharama kubwa (great toll) ya vita ile kwa maisha ya wananchi hadi vijijini. Hakuna ambaye kwa namna yake hakusikia maumivu (pinch) ya vita. Na vita ilipokwisha gharama yake kwenye uchumi wetu na maendeleo ya watu wetu haikuweza kurudishwa kwa urahisi. Kwa karibu miaka minne (miwili ya vita na ile ya reconstruction) ilisababisha nchi yetu kurudi nyuma zaidi ya ilipokuwepo. Ni kweli tulishinda vita lakini kwa gharama kubwa sana siyo tu ya fedha bali pia ya watu.
Kwa wanaokumbuka historia ya Uganda mojawapo ya matukio ya vita ni vita ya kuichukua Lukuya (Battle of Lukuya) ni hapa kiasi cha wanajeshi wetu kiliposhtukizwa na wanajeshi mamluki wa Libya na kujikuta kinarudishwa nyuma kabla ya Brigedi ya 201 na 208 kujipanga upya na kuwashambulia mamluki hao na kuwashinda na kusafisha njia ya kwenda Kampala (baada ya kuchukua Entebbe na Jinja). Gharama ya fedha tu serikali ya Museveni ndio iliweza kuilipa Tanzania mwaka 2007! Ikumbukwe kuwa vita ya Uganda inakadiriwa kuigharimu Tanzania dola milioni 1 kwa siku na hizo zilitoka mifukoni mwetu (hatukuwa na wajomba). Leo hii tumepiga kelele kulipa dola laki moja kwa Symbion kwa siku. Fikiria Wamarekani kwenye vita ya Iraq walikuwa wanaunguza dola bilioni 1 kwa siku!
Nikiangalia hali hiyo najiuliza; hivi kweli kina Lowassa na wengine wanaoshabikia vita wanafikiria kweli gharama yake? Hivi kuna mtu amewahi kuuliza Tanzania ilipoteza askari wangapi vita ya Uganda? Hivi watu wanajua kuwa ili jeshi letu liende vitani ni lazima wale wote waliokuwa reserve nao wawe reactivated? Yaani kabla ya kwenda Vitani itabidi kwanza tuongeze askari wote kutoka kama 30,000 waliopo sasa hivi na kufikia angalau 150,000 hivi kuweza kushinda vita. Hawa tutakaowachukua wengi ndio wasomi wenyewe na wafanyakazi maofisini watabadilishwa na nani? Ikumbukwe kwenye vita ya Uganda hawakwenda JWTZ tu bali Mgambo, Polisi, Magereza na wale waliopewa mafunzo ya haraka haraka. Je tuko tayari kuleta "draft" ya kulazimisha wanaume wote wenye miaka 18 na zaidi kuingia kambini? au watu wanafikiria ni "JWTZ" ndio litaenda vitani wakati wengine tunacheza ping pong na kuchat kwenye JF juu ya maendeleo ya vita?
Ninachopinga kabisa na ninaona ni mambo ya hatari ni kuzungumzia masuala ya vita bila kuonesha fikara na hekima. Kabla haujaamua kwenda vitani jipe nguvu kwanza. Na hakuna nguvu kubwa zaidi kama nguvu ya kiuchumi. Lakini jambo jingine ambalo labda wengine wameshafikiria ni vikosi vyetu vitakula nini? Au watu wanafikiria wanajeshi wakienda vitani wanapewa zile ration tu? Pamoja na gharama nyingine zote je bado tutaweza kulilisha taifa letu wakati wa vita? Wapo ambao hawajui kuwa njaa ya mwanzoni mwa miaka ya 1980 sehemu kubwa pia ni matokeo ya vita ya Uganda? Je tuko tayari kula dona na yanga tena na kurudishwa kwenye ration kwa taifa zima na mambo yale ya duka la kaya? au watu wanafikiria wataendelea kula nyama choma jioni wakati vita inaendelea?
Tusianze kupiga ngoma za vita (we shouldn't beat the drums of war) kama hatuko tayari kuingia vitani. Ni uzembe na reckless na binafsi naamini viongozi wote watatu (Lowassa, Membe na Sitta) wanatia shaka kama wana hekima na busara ya kuwa viongozi wa taifa letu. Kiongozi hata mwenye uwezo kiasi gani ni lazima asite linapokuja suala la vita na siyo kusita kwa sababu ya woga lakini kusita kwa sababu ya kujua analiita taifa lake kufanya nini. Na anapozungumza vita awe na uhakika kabisa (absolute confidence) kuwa hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuepuka vita hiyo.
Kwa mara nyingine nawasihi watu wanaoshabikia vita kama njia ya "kulinda mipaka yetu" wafikirie kwa hekima kuwa zipo njia nyingine nyingi zaidi za kufanya hivyo ikiwemo mazungumzo na mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa. NI LAZIMA TUMALIZE NJIA ZOTE ZA AMANI (siyo mazungumzo tu) kabla hatujasema "we have had enough, we are preparing for war) na binafsi naamini kama tutaonesha hekima ya kutumia njia zote na busara ya kuepuka vita siku ikiitwa vita kweli kabisa tunaweza kwenda siyo kujihami tu bali kuiona Malawi kama tishio na kuanzisha an offensive assault ili kuliondoa tishio hilo mara moja na daima.
Nashauri vichwa vilivyotulia vizungumza lugha ya amani sasa hivi na kutuliza hizi ngoma za vita na mbiu za mapigano. Maana kama sasa hivi tu wanahangaika kulipa mishahara na kulisha taifa letu, sijui itakuwaje WAKATI WA VITA!
MMM
Nadhani hukuwasikia vizuri viongozi we2. Wamesema kama itabidi kufika huko itabidi kuingia vitani. Sasa jiulize kama hizo njia zingine zimeshindikana unatemegea tukae kimya? Kuwa Mzalendo wewe.
Akamatwe kwa kosa lipi? Wa kututangazia nchi iko tayari kwa lolote ni Sitta au Lowasa? Waambie wanaSIASA wetu wasilikuze suala hili kwa malengo yao kijinga.
Noana watu ameshindwa kuelewa, wamesema ikibidi tutaenda vitani. Mnajua maana ya ikibidi? Na kama unavamiwa na na eti huna pesa na inadidi uende vitani utakataa, acheni kupotosha kwani njia za majadiliano bado zinaendelea!
Mimi ni kunguru mwoga, ningependa kukimbiza mabawa yangu. Mimi kwa hii issue kimyaa,.... nawasikiliza wenyewe watakavyoamua, ila si kuendelea kujadili katika forum kama hii!
mkuu mmm definetly uko sahihi,kwa uchumi wa sasa wa tz wa kila kiongozi anawaza kujichotea kila
anachoona kiko karibu yake,na kupiga kelele kuwa serikali haina pesa kwa kila jambo la muhimu, je
tunawezaje kuingiza nchi vitani ktk mazingira ya ufisadi uliokithiri?kitakachotokea hata pesa itakayotengwa
kwa ajili ya hiyo vita itachakachuliwa.ilivyo ni kwamba joyce banda amesoma udhaifu wa serikali yetu na
uongozi uliopo sasa.ili kuiponya nchi yetu tusithubutu kuingia vitani tuwaachie malawi ziwa lao.
Hao wazalendo unaowaona wewe ndo hao wanaotangaza vita vya kumpiga Malawi kwa sababu ya ziwa?? mbona hao hao wameshindwa vita vya ufisadi wanajiumauma tu na kuinamisha nyuso chini kila wakiguswa??? mabilioni ya uswisi yaliyosemwa juzi kati ulimuona kidume gani ambaye alionesha DHATI kuyafuatilia???? Jamani watanzania tuweni makini na hawa kina EL, kwanza basi tu kwa sababu watanzania tumefungwa na blanket fulani hivi machoni na nyoyoni kiasi tunashinwa hata kuona na kufikiria mambo ya msingi mchana kweupe.
Ilitakiwa mpaka sasa tuwe tumeshaanza kuchapana VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE HAPA NCHINI KATI YA WANANCHI NA MAFISADI. POTELEA MBALI. LIWALO NA LIWE
Wa kwanza kukamatwa unatakiwa kuwa wewe,unaejifanya huujui au unataka kuficha ukweli ambao uko wazi
kwani inapotikea migomo ya madaktari na walimu na hali duni ya maisha ya watanzania Tanzania inakuwa yai
kwamba taarifa hazitfiki nje ya mipaka yetu? Na je udhaifu wa hii serikali ni siri kweli? Tuache kujifariji kwenye
ukweli tuambizane bwana.
Kweli kabisa mkuu!Kaka nakubaliana na wewe 100%. Ki ukweli pamoja na heshima zoote za MMM, hili andiko lake halina mashiko kabisa, labda mtu ambae hawezi kung'amua kwa jicho la tatu. Siyo kila kitu arukie tu na kutoa maoni yake, hili andiko lake liko shallow sana, na halima mwangaza wowote kwa Taifa zaidi ya kupinga pinga tu!