Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,902
- Thread starter
- #141
Katika mintaarafu hiyo, hata hoja ni swali, kwa maana inatolewa kuhoji (ona hoja na swali vinapoingiliana katika kuhoji) uhalali na uwezo wa mgombea.
Mtu anaweza kutoa statement (siyo question, statement) inayoweza kuhoji uwezo wa uongozi wa mgombea.
Ndicho alichofanya Shyrose hapa.
Ametoa statement inayo impeach na kuhoji uwezo wa Sophia Simba kuongoza. Kuhoji si lazima uulize swali, hata statement ya kuonyesha vinginevyo (kwamba Simba hawezi uongozi) inahoji uwezo wake kuongoza kwa maana ya kuwapa waliofikiri ana uwezo wa kuongoza tambo.
Rhetoric is an art best consumed slowly.
Umefanya wengi tufundishike hapa, maana kuna baadhi hapa ni kusoma muundo wa sentensi wa kidarasa bila kuangalia maana na maudhui ya nadharia ya kifalsafa. Mara nyingi tunapata taabu kuvielewa vyombo vya habari au watu wa kimataifa hasa nchi za magharibi tukifikiria wanatusifia kumbe hatuelewi madharia ya wanachokiongelea kuhusu sisi kifalsafa.
Ukifuatilia presidential debate inayoendelea Marekani, watanzania wengi kwa mwono huu tutaona kama hawaulizwi maswali ila wanaletewa statement waichambue namna wanavyoielewa na namna wakakavyoielekeza kwenye majukumu wanayoyatazamia katika kuongoza taifa. Tuko bado kupima mambo kwa mtazamo wa kishule badala ya kifalsafa.