Swali la Shyrose kwa Sophia Simba lazua kasheshe katika Mkutano Mkuu UWT

Personal attacks, unaacha hoja unaenda kwenye viroja, argumentum ad hominem.

It is just a figment of your imagination, there is no personal attack in there except an illustration of the lineage of how she ended up in the Killango camp!! Strangely, Shy-Rose was helped greatly by EL in her quest to become an East African legislator but in this UWT saga she was against EL's prominent protege!!
 
hapo hela ndio inaongea, hata hao wazomeaji wamelipwa hela. hata huyo sophia kashinda kwa kuhonga hela. CCM kama hauna hela kushinda nafasi yeyote kichama ni ndoto za mchana!
 
I like women in high-boots..Shy-rose you have my vote.. unaongoza ligi kama Chelsea/
 
Mimi hadi sasa sijafahamu vizuri, je UWT ni umoja wa wanawake wa ccm au ni umoja wa wanawake kitaifa maana naona umekaa kiccm zaidi.

Je umuhimu wake ni upi, je wanawake wangapi ambao wamewezeshwa na huu umoja kimaisha? mathalan elimu, ufugaji, n.k. au ni wanapokea kwa kutuzuga kupokea donation na kuirudisha Chamwino kukiimarisha chama mama?
 
Hebu tupekeche akili zetu kidogo tu,kweli Sofia Simba ndiyo mwakilishi wa Wanawake wa Taifa hili?.
Kwanini uwakilishi wake usiishie tu pale Sinza Makabulini?.
 
Katika chaguzi za wenzetu, majibu ya mgombea huchangia sana kuchaguliwa kwake au la. Tatizo letu mgombea huchaguliwa mapema kabla hata ya kampeni. Kampeni hapa kwetu hazibadili chochcote kwa wapiga kura.

Majibu ya Sofia yalionyesha mafanikio ambayo ni aghalabu kuyapima kwa mizania iwayo yote. Kwa maneno mengine ni mafanikio ya kufikirika ambayo katika karne ya leo ya Sayansi na teknologia ni dhahiri kuwa hakuna alichofanya. Jibu hili linatoa nafasi kwa wapiga kura kufikiria kitu chochote kisichoonekana kama vile RUSHWA ya fedha na hatA NGONO. Mafanikio ya aina hii sio rahisi kuyaeleza kwenye kadamnasi lakini yanachangia kupata kura.
Pili kitendo cha kutaka kurushiana maneno baada ya kuuliza swali, ni tabia za mashangingi wa mitaani mabingwa wa kugombea wanaume. Kwamaba hata baada ya tukio hili kuonekana bado wajumbe wa mkutano huo wakampa kura nyingi inathibitisha ni kiasi gani wapiga kura wetu walivyo na upeo wa chini katika kuyachambua mambo. Huu ndiyo msingi mkubwa wa Tanzania kupata viongozi dhaifu kwa sababu wanachaguliwa na wapiga kura wenye mtazamo dhaifu wanowapima viongozi kwa mizania dhaifu kama rushwa na mipasho.
 
Hizo ndo siasa za magamba, Shyrose alishindwa kusoma upepo, na aliuliza swali ki-umbea na akajibiwa ki- umbea umbea, siasa za siku hizi bana!.
 
Nimefuatilia kwa karibu sana uchaguzi huu tangua hatua za awali na hotuba ya msaidizi wa KJ kama mfunguzi wa mkutano huu.Alichokisema Dr.B ni tofauti na kilicho tendeka hapo Dodoma jana.Nilicho baini kwa chama chetu kikubwa hapa nchini kwamba NO MONEY NO UONGOZI.Ndio kilichotokea jana.
 
Mpaka sasa najiuliza KOSA LA SWALI hilo ni nini? KWA NILIVYOONA MIPASHO ILE, UWT Haina tofauti na TAARABU...WANAWAKE BADO SANA KWA UONGOZI WA NCHI HII.WANABEBWA TU.NIMEWADHARAU SANA

mh taratibu wewee mbona sasa unatudharau na sisi??we sema hao waliogombana ndo hawafai bana!
 
kwenye huo umoja wao Sijawahi ona wamesimamishwa wagombea makini na wapo kibao,ni mashangingi ndio wagombeaji!,na huyo cheupe dawa watampa dawa na cha mama mwajuma chake!oo hoo!
 
images
images

Shyrose Banji mjumbe wa mkutano mkuu umoja wa wanawake Tanzania ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Mashariki amenusurika kufukuzwa kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo baada ya kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi.
Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."
Candid Scope hizo picha zinamaanisha nini? Au ndivyo walivyokuwa wakati wa maswali na majibu?
 
It is just a figment of your imagination, there is no personal attack in there except an illustration of the lineage of how she ended up in the Killango camp!! Strangely, Shy-Rose was helped greatly by EL in her quest to become an East African legislator but in this UWT saga she was against EL's prominent protege!!

My Take in this argument is that " Politics is a very dirty game full of Hypocricy these women are behaving like teenagers I don't know where this country is heading to!!?? But all in all EL is trying to kill this Country"
 
Back
Top Bottom