Swali la Shyrose kwa Sophia Simba lazua kasheshe katika Mkutano Mkuu UWT

Katika mintaarafu hiyo, hata hoja ni swali, kwa maana inatolewa kuhoji (ona hoja na swali vinapoingiliana katika kuhoji) uhalali na uwezo wa mgombea.

Mtu anaweza kutoa statement (siyo question, statement) inayoweza kuhoji uwezo wa uongozi wa mgombea.

Ndicho alichofanya Shyrose hapa.

Ametoa statement inayo impeach na kuhoji uwezo wa Sophia Simba kuongoza. Kuhoji si lazima uulize swali, hata statement ya kuonyesha vinginevyo (kwamba Simba hawezi uongozi) inahoji uwezo wake kuongoza kwa maana ya kuwapa waliofikiri ana uwezo wa kuongoza tambo.

Rhetoric is an art best consumed slowly.

Umefanya wengi tufundishike hapa, maana kuna baadhi hapa ni kusoma muundo wa sentensi wa kidarasa bila kuangalia maana na maudhui ya nadharia ya kifalsafa. Mara nyingi tunapata taabu kuvielewa vyombo vya habari au watu wa kimataifa hasa nchi za magharibi tukifikiria wanatusifia kumbe hatuelewi madharia ya wanachokiongelea kuhusu sisi kifalsafa.

Ukifuatilia presidential debate inayoendelea Marekani, watanzania wengi kwa mwono huu tutaona kama hawaulizwi maswali ila wanaletewa statement waichambue namna wanavyoielewa na namna wakakavyoielekeza kwenye majukumu wanayoyatazamia katika kuongoza taifa. Tuko bado kupima mambo kwa mtazamo wa kishule badala ya kifalsafa.
 
Shyrose anaweza asiwe mkamilifu lakini ameuliza swali la msingi sana na ni ajabu sana kama wanawake wa CCM wameridhika na majibu ya Sophia Simba! Infact I would go as far as saying ni fedheha kwa wanawake wa Tanzania kama wanaongozwa na fikra za namna hiyo.

TAMWA wamesaidia/wanasaidia wanawake kuliko Wizara ya wanawake inayoongozwa na Sophia Simba. Na chini ya Sophia Simba wanawake wa CCM wamekuwa na sifa mbaya sana mbele ya jamii. Sijui Prof Tibaijuka anafanya huko?

siasa ni mnyama gani kwani?
 
Umefanya wengi tufundishike hapa, maana kuna baadhi hapa ni kusoma muundo wa sentensi wa kidarasa bila kuangalia maana na maudhui ya nadharia ya kifalsafa. Mara nyingi tunapata taabu kuvielewa vyombo vya habari au watu wa kimataifa hasa nchi za magharibi tukifikiria wanatusifia kumbe hatuelewi madharia ya wanachokiongelea kuhusu sisi kifalsafa.

Ukifuatilia presidential debate inayoendelea Marekani, watanzania wengi kwa mwono huu tutaona kama hawaulizwi maswali ila wanaletewa statement waichambue namna wanavyoielewa na namna wakakavyoielekeza kwenye majukumu wanayoyatazamia katika kuongoza taifa. Tuko bado kupima mambo kwa mtazamo wa kishule badala ya kifalsafa.

There is such a thing as a statement that impeaches something, or in some context, invites a denial/ justification/ clarification, and in so being framed, the statement questions.
 
'Rehema za uongozi'????

Sio kwamba hapa unachukua neno 'grace' na kulitumia visivyo?

Kiswahili kwa kuwa kiko influenced sana na kiarabu,na kiarabu kiko influenced na kiislam..

kuna baadhi ya maneno kwa kiswahili huwa ni kama hayatafsiriki..

mfano.....create....ukisema ni kuumba..

kuumba kwa kiswahili hutumika kwa ku refer Mungu only...

tofauti na create linavyotumika..

so swali langu hapa ni ulivyotumia hili neno 'rehema za uongozi'..

unaweza fafanua?

Rehema ni nini? Mwanadamu hawezi kuwa na rehema? Hakuna binadamu wanaoitwa "Rehema" hata katika Kiswahili?

Una hakika hulazimishi matumizi yako finyu ya maneno ya kiswahili yafanye kwamba maneno kama "rehema" yaonekane hayafai kutumika kwa binadamu?
 
Shyrose Banji mjumbe wa mkutano mkuu umoja wa wanawake Tanzania ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Mashariki amenusurika kufukuzwa kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo baada ya kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi.
Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."
attachment.php

CCM ipo kwenye risk, kuna dalili nyingi za split elemets hii ikiwa moja wapo. Jibu la Sophia simba si jibu la kumjibu mpiga kura anayetazamia kwamba she is going to cast in ballot for her favor. Inadhihirishwa wako tofauti ingawa mwuliza swali hakuzamilia kumwuliza swali Simba tu, kabla yake alielekeza mkuki mkali kama huo kwa Kilango Malecela kwa kumwuliza kama ifuatavyo:
Awali Bhanj alimuuliza mgombea Anne Kilango Malecela nini kimekusukuma kugombea uenyekiti wa UWT.
Swali hilo lilikataliwa na mwenyekiti wa Uchaguzi Profesa Tibaijuka kwa maana iliyotafsirika kama kumkingia kifua Anne Kilango Malecela.

Kwa vyo vyote haikuonyesha wazi Shyrose Bhanji kuelekeza swali kwa mgombea mmoja tu ila kwa wote.

Ni upepo unaovuma na nini kinachoendelea ndio kile ambacho hakikutazamia kuona wajumbe wanaomwunga mkono Simba hawakupinga swali ambalo Shyrose alilielekeza kwa Kilango, ila alipoelekeza shwali kwa Simba hapo moto ndipo ulipofuka.

Kwa hali ilivyo hawa wanaonyamazishwa hata wanapotaka kujua nini mwenyekiti wao atawafanyia wana nafasi gani ndani ya chama chao? Huu ufa unaozidi kujengeka wenyewe wanaufahamu au hawauoni kama ni risk kwa chama cha Mapinduzi kuipa faraja kambi ya upinzani kuzoa wanaowaita oil chafu ya CCM? Oil chafu ya CCM kadiri ya Nape ndio aina ya hawa akina Shyrose wenye kukandamizwa na mfumo dume ndani ya chama tawala CCM. Ipo siku watajutia kutotumia busara mazingira kama haya ambayo yanazidisha ufa kati yao. Kuonyesha mabavu ya huyu mama simba hadharani kwa mpiga kura wake kwa kiwango hiki inaonyesha dalili wazi za mfumo dume ndani ya CCM unavyotawala.
 
Sasa kwa nini Tibaijuka kakataa swali hilo ambalo ni la msingi kabisa kutoka kwa Shyrose?

Hili ndilo swali "alif" kabisa kwa yeyote anayegombea uongozi.

Naondoa maksi zangu zote nilizotoa kwa Tibaijuka kwa kuruhusu swali la Shyrose kwa Sophia Simba.

You can't even say this question is too much of a softball question (unless there are known rules stipulating every question to have a certain level of bonafide bloodsport credentials) kwa sababu linampa nafasi mgombea kutoa mipango yake ya uongozi na kujieleza.
 
Sasa kwa nini Tibaijuka kakataa swali hilo ambalo ni la msingi kabisa kutoka kwa Shyrose?

Hili ndilo swali "alif" kabisa kwa yeyote anayegombea uongozi.

Ukiangalia hali ilivyokuwa na waliokuwepo wanasema ilikuwa kama movie vile, ni full mchezo wa kuigiza katika utendaji wa mambo makubwa nchini. Hali kama hii inalipeleka wapi taifa?

Manaume mzima mzima Ustaadhi Makamu wa Rais alifungua mkutano huo, je hakutoa dondoo muhimu za kuwatahadharisha nini kinatakiwa kustahimili na kuvumiliana wanapotofautiana katika masuala fulani fulani kwamba ndiyo nature ya uchaguzi?
 
Sasa kwa nini Tibaijuka kakataa swali hilo ambalo ni la msingi kabisa kutoka kwa Shyrose?

Hili ndilo swali "alif" kabisa kwa yeyote anayegombea uongozi.

Naondoa maksi zangu zote nilizotoa kwa Tibaijuka kwa kuruhusu swali la Shyrose kwa Sophia Simba.

You can't even say this question is too much of a softball question (unless there are known rules stipulating every question to have a certain level of bonafide bloodsport credentials) kwa sababu linampa nafasi mgombea kutoa mipango yake ya uongozi na kujieleza.

Kwa sababu hakukuwa na suali. Hata kwa tafsiri uliyotumia ya kuhoji, hapa haijatumika. Hapajahojiwa kitu, pametolewa hoja tu. Ni sawa na mtu aambiwe arembe chumba akaja na urembo wa kila aina akauweka burungutu kwenye meza. Atakuwa hajaremba kaweka urembo mezani. Sawa na mwanamke anaeambiwa ajipambe, akaamua kuchukua wanja akashika mkononi, akasema keshajipamba maana wanja ni pambio kazi yake kupamba!

Kwa mintarafu hiyo hiyo Shyrose hajauliza suali maana hajahoji, kaweka hoja. Angehoji kama angetaka kujua kwa nini hakukitetea chama au kwa nini achaguliwe wakati hakukitetea chama au jengine lolote litakalofungamana na hoja yake ili aweze kuitumia kuhoji

Shyrose hajauliza suali wala kuhoji chochote.
 
Nikitoa hoja kwamba Wakavirondo ni wachafu, hoja yangu itahoji na kuuwekea swali usafi wa Wakavirondo hata kwa walioamini kwamba Wakavirondo ni wasafi.
 
Kwa sababu hakukuwa na suali. Hata kwa tafsiri uliyotumia ya kuhoji, hapa haijatumika. Hapajahojiwa kitu, pametolewa hoja tu. Ni sawa na mtu aambiwe arembe chumba akaja na urembo wa kila aina akauweka burungutu kwenye meza. Atakuwa hajaremba kaweka urembo mezani. Sawa na mwanamke anaeambiwa ajipambe, akaamua kuchukua wanja akashika mkononi, akasema keshajipamba maana wanja ni pambio kazi yake kupamba!

Kwa mintarafu hiyo hiyo Shyrose hajauliza suali maana hajahoji, kaweka hoja. Angehoji kama angetaka kujua kwa nini hakukitetea chama au kwa nini achaguliwe wakati hakukitetea chama au jengine lolote litakalofungamana na hoja yake ili aweze kuitumia kuhoji

Shyrose hajauliza suali wala kuhoji chochote.

Naona unatuzingua wasomaji na semantics zako zisizokuwa na mshiko wowote kiuhalisia.

Hebu tafadhali utufahamishe na kutufafanulia tofauti (ikiwezekana kwa mifano) kati ya kauli zako zifuatazo hapo juu:

1. "kuhojiwa kitu" na "kuhoji"

2. "kuuliza swali" na "kuhoji"

3. "kuhoji" na "kuweka hoja"

4. "kuuliza swali" na "kweka hoja"

5. "kuhoji" na "kutaka kujua"

6. Maana ya msemo "kuitumia [hoja] kuhoji"
 
Naona unatuzingua wasomaji na semantics zako zisizokuwa na mshiko wowote kiuhalisia.

Wewe nawe hujahoji, umetoa hoja kuwa wasomaji mnazinguliwa na semantics za Gaijin ambazo hazina mshiko wowote kiuhalisia

Kama Shyrose, nawe hujauliza suali lolote hapo
 
Wewe nawe hujahoji, umetoa hoja kuwa wasomaji mnazinguliwa na semantics za Gaijin ambazo hazina mshiko wowote kiuhalisia

Kama Shyrose, nawe hujauliza suali lolote hapo

Sikujua kama wewe ni mpuuzi namna hiyo. Kujifanya kote huko kuwa msomi wa lugha na unajua mambo kumbe ushuzi mtupu! Shame on you! Pambaaf!
 
Sikujua kama wewe ni mpuuzi namna hiyo. Kujifanya kote huko kuwa msomi wa lugha na unajua mambo kumbe ushuzi mtupu! Shame on you! Pambaaf!

Wewe umepewa mfano halisi baina ya kutoa hoja na kuhoji kwa kutumia maneno yako mwenyewe, ili iwe rahisi kuelewa ila inaonyesha juu ya yote hayo somo limekuwa gumu kwako

Pole sana
 
Wewe umepewa mfano halisi baina ya kutoa hoja na kuhoji kwa kutumia maneno yako mwenyewe, ili iwe rahisi kuelewa ila inaonyesha juu ya yote hayo somo limekuwa gumu kwako

Pole sana

Kigumu hapa ni kitu gani jamani? Tafadhali hebu jibu maswali yote niliyokuuliza pale juu (moja baada ya lingine) ikiwezekana utupatie mifano halisia.

Usitegemee kila mtu ataelewa analogies aka mifano yako mbuzi ya "mapambo" na "urembo".

Jibu maswali yangu yote kwanza kabla ya yoyote, ok?
 
Hapa siongezi kitu zaidi ya kukuhongea like umeusemea moyo wangu. Asante Mkuu najua Wadau wame note your words.

Shyrose nadhani ''she is in wrong place at wrong time'
Swali lake ni la msingi kabisa kwasababu alitaka kujua nini Sophia Simba amekifanya kutaka nafasi tena.

Swali hili halikulenga kumuumiza Sophia pengine lingemjenga sana. Kama kuna alichokifanya huu ndio ulikuwa wasaa wa yeye kuueleza mkutano mkuu kwa ufasaha. Nafasi hiyo adhimu akaitumia kutuonyesha aina ya viongozi tulio nao.

Mwenyekiti wa UWT ni mjumbe wa vikao muhimu vinavyotoa maamuzi ya nchi.
Jibu la kuwa yeye amejiimarisha katika matawi na hicho ndicho alichokifanya kwa umma wa wanawake wa Tanzania.
Kwanini tusiendelee kuwa masikini, tuzizongwe na ujinga na maradhi?

Tunatakiwa tufanye maamuzi yenye busara na hekima 2015. Kinyume chake tutaendelea kushudia uzezeta ukiwa ni sehemu ya tamaduni zetu.
 
Usitegemee kila mtu ataelewa analogies aka mifano yako mbuzi ya "mapambo" na "urembo".

Hapa tena hapana kuhoji, kuna hoja kuwa mifano aliyotoa Gaijin ni mifano mbuzi.

Kwa mtu anaedhani mifano ya "mapambo" na "urembo" si mifano halisia, kila kitu lazima kiwe kigumu maana sijui yupo katika ulimwengu gani ambapo mapambo na urembo si uhalisia
 
Kwa sababu hakukuwa na suali. Hata kwa tafsiri uliyotumia ya kuhoji, hapa haijatumika. Hapajahojiwa kitu, pametolewa hoja tu. Ni sawa na mtu aambiwe arembe chumba akaja na urembo wa kila aina akauweka burungutu kwenye meza. Atakuwa hajaremba kaweka urembo mezani. Sawa na mwanamke anaeambiwa ajipambe, akaamua kuchukua wanja akashika mkononi, akasema keshajipamba maana wanja ni pambio kazi yake kupamba!

Kwa mintarafu hiyo hiyo Shyrose hajauliza suali maana hajahoji, kaweka hoja. Angehoji kama angetaka kujua kwa nini hakukitetea chama au kwa nini achaguliwe wakati hakukitetea chama au jengine lolote litakalofungamana na hoja yake ili aweze kuitumia kuhoji

Shyrose hajauliza suali wala kuhoji chochote.

Mtu mzima tena Dr mwenye kuvaa suruali na ana wake wake wawili ambaye anamkaimu Kikwete akiwa na wadhifa wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye aliyepewa heshima ya kufungua mkutano huo na kutoa wasia kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT ambao yaliyojilia ndiyo hayo.
 
Hapa tena hapana kuhoji, kuna hoja kuwa mifano aliyotoa Gaijin ni mifano mbuzi.

Kwa mtu anaedhani mifano ya "mapambo" na "urembo" si mifano halisia, kila kitu lazima kiwe kigumu maana sijui yupo katika ulimwengu gani ambapo mapambo na urembo si uhalisia

Jibu maswali niliyouliza, eboo?

Usitake kuzingua watu aloo.

Wee kaa nani bana hadi ujitaje in third person?

Jibu maswali yangu pale juu, siyo kutuletea viroja dada!
 
Mie mpaka leo nashindwa kuelewa wanaume wote wa mjini hakuna hata mmoja aliyemzalisha huyu Shyrose?

MTOTO LAINIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII KA PAPAI VILE....
 
Back
Top Bottom