Swali la Shyrose kwa Sophia Simba lazua kasheshe katika Mkutano Mkuu UWT

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
attachment.php

Shyrose Banji mjumbe wa mkutano mkuu umoja wa wanawake Tanzania ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Mashariki amenusurika kufukuzwa kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo baada ya kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi.
Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."

Note:
Shyrose alielekeza swali gumu pia kwa Anne Kilango Malecela kabla ya kumwuliza Simba. Swali lilikuwa kama ifuatavyo:
"Nini kimekusukuma kugombea uenyekiti UWT."
Swali hilo lilikingiwa kifua na Mwenyekiti wa Uchaguzi profesa Tibaijuka kwa kulikataa. Shyrose alipopata tena nafasi ya kumwuliza Simba ndipo yakajilia haya tunayojadili.
 
Huyu dada nae kila kukicha anashindwa kupima upepo coz upeo wake mdogo, sasa akiendelea hivi hata miaka miwili mingi. Anachotakiwa aache kuchukua maneno ya bongo flava na kuingia nayo kwenye duru za kisiasa. Awemakini, SILIVYO HATA UKUU WA WILAYA WANAO PEWAGWA MARA KWA MARA NA DHAIFU ATAUKOSA.
 
Shyrose nadhani ''she is in wrong place at wrong time'
Swali lake ni la msingi kabisa kwasababu alitaka kujua nini Sophia Simba amekifanya kutaka nafasi tena.

Swali hili halikulenga kumuumiza Sophia pengine lingemjenga sana. Kama kuna alichokifanya huu ndio ulikuwa wasaa wa yeye kuueleza mkutano mkuu kwa ufasaha. Nafasi hiyo adhimu akaitumia kutuonyesha aina ya viongozi tulio nao.

Mwenyekiti wa UWT ni mjumbe wa vikao muhimu vinavyotoa maamuzi ya nchi.
Jibu la kuwa yeye amejiimarisha katika matawi na hicho ndicho alichokifanya kwa umma wa wanawake wa Tanzania.
Kwanini tusiendelee kuwa masikini, tuzizongwe na ujinga na maradhi?

Tunatakiwa tufanye maamuzi yenye busara na hekima 2015. Kinyume chake tutaendelea kushudia uzezeta ukiwa ni sehemu ya tamaduni zetu.
 
na lile sekeseke alilofanya? ITV na Star TV walionyesha live huyu hafai!
 
Wanasiasa wengi wa miaka hii hapa nchini kwetu, wana historia ya uhuni, ama bado ni wahuni, hayo ndio madhara yake.
 
Kama kuna mtu amebebwa na mbeleko kuubwa na hajui kujishikilia ni SS,baada ya JK kubebwa na KK na wakati huo akiwa SS kama kimada wake aliezaa nae,kuanzia hapo JK analipa fadhila sana na hawezi kumuacha hata iweje!maana ni mzee wa fadhila na visasi!(+,-) zote anazo,mzee wa upepo...
 
Sofia Simba "...Muuliza swali hajakomaa kujua siasa za nchi hii.."

hao ndio watawa-wala
 
Mipasho,rushwa,ufisadi,usenge nyaji n.k ni utamaduni wa nyinyiem!!!amkeni wananchi tumkatae huyu ibilisi.
 
“Shyrose hajakomaa tumempa ubunge juzi juzi tu,hachaneni nae mama zangu”nanukuu
 
images
images

Shyrose Banji mjumbe wa mkutano mkuu umoja wa wanawake Tanzania ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Mashariki amenusurika kufukuzwa kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo baada ya kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi.
Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."

huyu chotara nae si atafute mume amuoe.....anashundana na mapapa ? haya yangu masikio
 
Back
Top Bottom