Swali kwa kina dada, Tunavumilia ili iweje?

Da Pretty

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
3,059
1,148
Nimekua nikijiuliza sana kuhusu mahusiano.

1. Dada ana mpenzi wana miaka,sio mume wala mwanaume hana mpango wa kuoa,
wanafanya kazi mikoa tofauti, ajabu mwanaume anampa mwanamke masharti ya kufika kwa mwanaume.
Dada akienda lazima atoe taarifa kabla na hata ukitoa taarifa sio kwamba lazima atakuruhusu, anaweza kusema usije nina wageni wa ofisini. Dada akienda wageni hakuna na ananuniwa
inabidi aondoke tu. Akirudi kwake mwanaume ndio analeta mapenzi na dada anapata amani kua alimkosea laaziz,hivi huyu mwanamke hapa huwa anang'ang'ania nini?
Kama hamjaoana hakujali, ndani ya ndoa si itakua balaa?

2. wapenzi wqanaishi mikoa tofauti, mwanaume aakienda mkoa anaoishi mpenziwe hamjulishi, dada anaambiwa na wanaomjua huyu kaka kuwa tumemuona,kaka akiulizwa anajibu nipo ila nina mambo mengi nitakutafuta. Kaka anamaliza kilichomleta hadi anaondaoka bila kumtafuta mpenzi wake,bibie akipiga simu kumuulizia kaka anajibu nimeondoka ilikua ghafla!!
Dada anaandaa safari kwenda kwa kijana na zawadi kafungasha, wakiwa kwa mwanaume mapenzi kunoga lakini kaka akienda mkoa anaoishi mdada anajificha.
Mdada anavumilia eti kweli kazi nyingi,jamani kweli au ndio mapenzi upofu?

3. Utakuta dada ana mpenzi ambaye siyo mume, siyo mchumba wala siyo baba mtoto.
Mwanaume ana visa na mbaya zaidi ni mpigaji hadi dada tunakupeleka hospitali lakini ukipona umerudi na style ya maisha ni ile ile kupigana.
Hivi hapa kinachomfanya dada huyu kuvumilia mateso na aibu hii ni nini? Na anavumilia ili aolewe au ndio kupenda?

Kama kweli mapenzi Upofu mbona visa tunavyotendwa tunaviona, TUNALALAMIKA,tunalia tunafuta machozi halafu bado tunajipa moyo, Hivi huwa nini kinatufanya tuendelee kuvumilia?
 
ni kupenda nahisi hii ndo sababu kuu but kinachotucost zaid ni kusema wanaume wote wapo hivo hivo sio kweli, hata kidogo then na kuitaka ndoa kwa nguvu mi naona kama ndoa ipo ipo tuu kama hautaipata basi pia shukuru Mungu haina haja ya kua na mwanaume wa aina hizo hapo juu......huo sio uvumilivu ni mateso ya kujitakia mi ninachoomba kwa wanawake wenzangu WAJIAMINI TU iyo ndo itakua salama yetu sote hamna kuendekezana aisee..ni hayo tuuu Mungu wabariki wanawake wote uwaokoe na wanaume wasiojua wajibu wao,kuwapenda na kuwaheshimu wanawake zao AMEN
 
Da Prety huyu dada anahiaji kuamshwa usingizini.............................mwanaume ana 'mambo' yake so asitegemee kuwa na amani akiolewa naye..........huyu dada seems to be desparate kuolewa aikwae ile status ya society kuwa ni Mrs somebody..........mwambie ni bora akaiepuka dhambi ya kucheat mapema kabla hajajing'ang'aniza asipopendwa.

Karibu
 
Pole zake/zako bi dada...sina hakika na status yako kimahusiano bt nikuhakikishie jibu la maswali yako utalipata tu muda si mrefu...
 
Mie hata sielewi yaani. Lkn kuna mawili eidha mapenzi au huyo dada amekuwa na mahusiano mengine mengi kaamua kutulia hata kuamua kuvumilia
 
Mie hata sielewi yaani. Lkn kuna mawili eidha mapenzi au huyo dada amekuwa na mahusiano mengine mengi kaamua kutulia hata kuamua kuvumilia
Umeona eh Dena jamani mapenzi ni kizungumkuti

Afu wewe nilishikika but am longing to see you babygal.
 
Tatizo ni mlio sensitive kushauri mtakavyokua wanyonge yakiwafika...well...tukubaliane kwamba Mapenzi ni bahati nasibu simply coz whom atakuja kuishi nawe hukudream kua naye..kwa phenomena hiyo hiyo tukubaliane kua unaweza kuibuka na kimeo au bahati ikawa upande wako!
 
naweza kusema hajiamini................... haamini kama ataweza kupata mwingine ambaye atamwambia nakupenda. Inawezekana hata huyo ilitokea bahati nzuri ndo maana anang'ang'ania. hapo mimi sioni hata chembe ya mapenzi, I mean, hata huyo dada wala hampendi huyo kaka, anakaa tu sababu hana jinsi............
 
Sijatbisha,
Hayajanifika ndio maana huwa najiuliza
Labda yakinifika, Mungu aniepushie...
 
Huyo dada ni mjinga (samahani kama ni nimetumia lugha nzito. Hivi anahitaji mtu kumwambia kuwa huyo jamaa anamtumia tu, tena kama taili la spea?

watu wengine bwana (awe KE au ME) nadhani wana matatizo ya akili....

Nimemchukia sana huyu binti...Kwani asipokuwa na mwanamume ndo atakuwa ame..R.I.P??

Nimechoka mwenzeni na hawa watoto... Mzee DC!!
 
Anampenda huyo mwanaume sijui nielezeje
Na ratiba ya mpenzi wake kuwepo Dar anaipata ofisini kwa huyo kaka
kuna dada anafanya kazi na huyo kaka ni rafiki yetu.
wala hajakosa ndio ninapomshangaa mimi
Naogopa kuelezea sana isije akasoma humu akaona nimemuanika.
Kweli mapenzi kizungumkuti ila nakataa mapenzi sio Upofu maana anaona sana
anavyotendwa na huwa analalamika sana tu na kufikia kusema sasa basi!!!
Ghafla shost kasafiri eti kaombwa msamaha.
Tatizo jamaa huwa anarudia ni tabia yake
 
NENO LAKO NIMELIPENDA!
Kumshauri mtu amuache mpenzi wake ni ngumu jamani yataka hekima ya Suleimani!
Kwa sababu kama hakuna mapenzi ya nini kuwa nae?
 
Kwa huyo wa namba 2 my dia,acha!!
Anampenda huyo mwanaume sijui nielezeje
Na ratiba ya mpenzi wake kuwepo Dar anaipata ofisini kwa huyo kaka
kuna dada anafanya kazi na huyo kaka ni rafiki yetu.
wala hajakosa ndio ninapomshangaa mimi
Naogopa kuelezea sana isije akasoma humu akaona nimemuanika.
Kweli mapenzi kizungumkuti ila nakataa mapenzi sio Upofu maana anaona sana
anavyotendwa na huwa analalamika sana tu na kufikia kusema sasa basi!!!
Ghafla shost kasafiri eti kaombwa msamaha.
Tatizo jamaa huwa anarudia ni tabia yake

Kumbe unaongelea wasichana tofauti...Hilo ndo naliona. Hata hivyo haibadili mtazamo wangu kwao..Wana matatizo makubwa vichwani mwao. Kwa ufupi ni wangonjwa na wanahitaji ushauri nasaha haraka. Wasaidieni kwani watakuwa tayari ni vituko huko mtaani kwao!

Kwani hao wanaume ndo Mungu wao?
 
Huwezi amini ni wengi wamenaswa ndani ya upuuzi kama huo! Vitu vingi huchangia ikiwa ni pampoja na:-
-low self esteem
-naiveness
-jamii (kuolewa ni heshima)
-ushauri (vumilia ndoa ndivyo zilivyo)
-kikubwa kuliko vyote ni UJINGA wa mwanamke, hajui anachotaka kwenye relationship!

I was there l know what l am talking about! Unajitahidi hoping mapenzi yako yatambadilisha mwanaume awe caring n understanding kidogo; kumbe u r creating a monster ambaye anaona bila yeye huwezi ishi!
 
Nimekua nikijiuliza sana kuhusu mahusiano.

1. Dada ana mpenzi wana miaka,sio mume wala mwanaume hana mpango wa kuoa,
wanafanya kazi mikoa tofauti, ajabu mwanaume anampa mwanamke masharti ya kufika kwa mwanaume.
Dada akienda lazima atoe taarifa kabla na hata ukitoa taarifa sio kwamba lazima atakuruhusu, anaweza kusema usije nina wageni wa ofisini. Dada akienda wageni hakuna na ananuniwa
inabidi aondoke tu. Akirudi kwake mwanaume ndio analeta mapenzi na dada anapata amani kua alimkosea laaziz,hivi huyu mwanamke hapa huwa anang'ang'ania nini?
Kama hamjaoana hakujali, ndani ya ndoa si itakua balaa?

2. wapenzi wqanaishi mikoa tofauti, mwanaume aakienda mkoa anaoishi mpenziwe hamjulishi, dada anaambiwa na wanaomjua huyu kaka kuwa tumemuona,kaka akiulizwa anajibu nipo ila nina mambo mengi nitakutafuta. Kaka anamaliza kilichomleta hadi anaondaoka bila kumtafuta mpenzi wake,bibie akipiga simu kumuulizia kaka anajibu nimeondoka ilikua ghafla!!
Dada anaandaa safari kwenda kwa kijana na zawadi kafungasha, wakiwa kwa mwanaume mapenzi kunoga lakini kaka akienda mkoa anaoishi mdada anajificha.
Mdada anavumilia eti kweli kazi nyingi,jamani kweli au ndio mapenzi upofu?

3. Utakuta dada ana mpenzi ambaye siyo mume, siyo mchumba wala siyo baba mtoto.
Mwanaume ana visa na mbaya zaidi ni mpigaji hadi dada tunakupeleka hospitali lakini ukipona umerudi na style ya maisha ni ile ile kupigana.
Hivi hapa kinachomfanya dada huyu kuvumilia mateso na aibu hii ni nini? Na anavumilia ili aolewe au ndio kupenda?

Kama kweli mapenzi Upofu mbona visa tunavyotendwa tunaviona, TUNALALAMIKA,tunalia tunafuta machozi halafu bado tunajipa moyo, Hivi huwa nini kinatufanya tuendelee kuvumilia?

Da Pretty,

Habari ya masiku mpendwa, nimefurahi kukuona uwanjani, kuhusu hii thread mie naona kwenye bold hapo ndo kuna matatizo sana!

Unajua tatizo akina dada wengi nao sio wakweli katka mahusiano ya kimapenzi, hivyo huenda huyo dada historia yake ya siku za nyuma anaijua jinsi alivyochanganya wanaume na hatimaye akaachwa, hivyo anaona ni bora ashikilie hapo hapo mpaka kieleweke (NDOA).

Huwezi mtoto wa kike ukakaa miaka na miaka na mtu ambaye sio mchumba, sio mume au sio mpenzi kivilee so unatafuta nini? basi kama hivyo wote ni wahuni tu kama tuliozoea kuwaona mitaani coz is not clicking in mind hata kidogo!

Ok, kifupi hapo hakuna mapenzi kwa wote sio mwanaume au mwanamke ila wote huwa wanatamaniana tu kimwili basi.

By the way nakupa hi sana!!
 
Dah haya mapenzi jamani. Dah tuweni na akili jamani wanawake, tunaweza kuishi bila hawa viumbe ni uamuzi tu. Wakati ukifika kama kuna kuolewa tutaolewa tu, kwa nini kuizika nafsi na roho kwa mtu asiyekupenda wala kujali? Dah hebu tufungukeni. Kama mtu ni sababu ya huzuni yako why unamganda? Wanaume wapo kibao wazee kwa vijana kama shida ni mapenzi, but kwani tumekosa nini hadi kujitesa namna hio? Dah mi mtu wala sifikirii mara mbili. Kinachotakiwa ni furaha na amani bwana. Kama mtu akupi furaha we wa nin
 
Nimetafakari sana. Hapo nimeangalia pande zote. Kama wanaume wenye sifa tu wangekuwa wanapata wenza, basi wengine wangedoda. Jibu ni kuwa hata wanaume wa hovyo wanapata wapenzi. Na huyo kajipatia mdada mvumilivu. That's life. Kila mtu ana chaguo lake ambalo ni ngumu kwa third part kujua kigezo cha chaguo hilo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom