Swali kwa Jaji Mkuu: Je, mahakama zina kitengo cha kufuatilia utekelezaji wa hukumu zake kwa wahusika kama zimetekelezwa?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau nawasalimu.

Naomba nielekee kwenye hoja muhimu kuhusu Mhimili wa Mahakama.

Mahakama zetu zimekuwa zikipokea idadi kubwa ya mashauri kwa lengo la kutoa hukumu.

Hata hivyo, kumekuwa na tatizo la utekelezaji wa hukumu ambapo baadhi ya hukumu zinatekelezwa na nyingine hazitekelezwi na wahusika, hali ambayo inakwenda kinyume na agizo la mahakama. Kundi linalokabiliwa na changamoto hii ni pamoja na mashirika na halmashauri za jiji, miji, na wilaya.

Watendaji wa halmashauri hizi, wakiwa chini ya uongozi wa wakurugenzi wao, mara nyingi wamekuwa wakiukataa utekelezaji wa hukumu bila sababu za msingi. Hali hii imesababisha kucheleweshwa kwa wananchi kupata haki zao. Kesi nyingi ambazo wakurugenzi wa halmashauri hukaidi kwa makusudi utekelezaji wa hukumu za mahakama ni pamoja na kesi za migogoro ya ardhi na madai mbalimbali ya malipo dhidi ya halmashauri husika.

Swali kwa Jaji Mkuu ni: Je, ni lini mahakama zitaanzisha kitengo cha kufuatilia utekelezaji wa hukumu zake ili kuhakikisha kuwa zinatekelezwa kama ilivyokuwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi?

Kitengo hiki cha kufuatilia utekelezaji wa hukumu kitasaidia wananchi waliopata haki kuhakikishiwa utekelezaji wa hukumu zao kama ilivyoamuliwa na mahakama.
 
Si wapo probation services au na wao bado fofofo? nakumbuka mara ya mwisho ni Mrema alikuwa akiiongoza hii tasisi , sijui kwa sasa ni nani?
 
Ikitoka hukumu unaenda kukazia hukumu hapo madalali wanaweza kukamata hata vyombo vyao
KWANINI NA MAHAKAMA isiunde KITENGO CHAKE ILI KUHAKIKISHA HUKUMU ILIZIZITOA ZIMETEKELEZWA?LEO UKIMKURUPUSHA MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA UKIMUULIZA KTK HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA MAHAKAMA ZENU NI HUKUMU NGAPI ZIMETEKELEZWA NA NGAPI BADO HAWAJUI
 
Back
Top Bottom