Je mhimili wa mahakama una kitengo kinachofuatilia utekelezaji wa hukumu zake?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau nawasalimu.Mimi sina Ufahamu MKUBWA wa Masuala ya Sheria .Ninaomba kufahamishwa juu ya Suala mzima la UTEKELEZAJI wa HUKUMU zinazotolewa na MAHAKAMA zote.

Nimekuwa nafuatilia baadhi ya KESI na HUKUMU zake .MAHAKAMA nimekuwa zinazotoa HUKUMU mbalimbali zipo zinazotekelezwa na zipo zisizotekekezwa na Watu, Ofisi mbalimbali za Serikali na Mashirika Mbalimbali.Sababu za kutotekeleza Hukumu hizo nyingi zitakuwa ni KUTOKUTAKA TU kuzitekeleza ili Mhusika akate Tamaa.Nilikuwa naamini kama Mtekelezaji hataki au hakubaliano na Hukumu angekata Rufaa lakini hafanyi hivyo na matokeo yake Ni kumnyima HAKI mhusika kwa Makusudi.

Kutokana na hali hiyo ndio maana nimeuliza JE MAHAKAMA ina KITENGO Kinachofuatilia UTEKELEZAJI wa HUKUMU zake?
Umuhimu wa Kuwa na KITENGO hicho kutawasaidia WANANCHI kupata HAKI ZAO kama zilivyoamuliwa na MAHAKAMA tofauti na USUMBUFU unaofanywa na Wasio taka KUTEKELEZA HUKUMU za MAHAKAMA.

KITENGO hicho kitawasaidia Wananchi kwenda Kutoa MALALAMIKO yao kwenye Hicho KITENGO na HATUA za Haraka zitachukuliwa kwa wale Waliokataa Kutekeleza HUKUMU za MAHAKAMA.

OMBI kwa JAJI MKUU tunaomba Kuwe na CHOMBO cha Kufuatilia Utekelezaji wa HUKUMU zitolewazo na MAHAKAMA ili kuwaondolea USUMBUFU wananchi.
 
Utekelezaji wa Hukumu zilizoaamuliwa Mahakamani inategemea na mshinda tuzo, Kama mshinda tuzo uko vizuri Kiuchumi Hukumu yako itatekelezwa faster! Kama mshinda tuzo huna kitu, hiyo hukumu kutekelezwa ni kipengele kingine unaweza kataa tamaa!!
 
Ndio maana tunaishauri MAHAKAMA iwe na Kitengo ambacho kitakuwa kinahakiki iwapo Hukumu zake zinatekelezwa Kwani WASHINDA TUZO wengi kwa kukosa Pesa Wanazungushwa sana
 
Utekelezaji wa Hukumu zilizoaamuliwa Mahakamani inategemea na mshinda tuzo, Kama mshinda tuzo uko vizuri Kiuchumi Hukumu yako itatekelezwa faster! Kama mshinda tuzo huna kitu, hiyo hukumu kutekelezwa ni kipengele kingine unaweza kataa tamaa!!
Mwambie waziwazi kua awe na Mchele sio mkono mtupu
✍️
 
Mambo ya mahakama na sheria ukiwa huna hela ni magumu sana.
Picha linaanza utaanza kuliwa hela na wakili kila baada ya muda na hukumu ikishatoka inahama kwa watumishi wa mahakama nao wakumalize hela.
 
kama unataka hukumu yako itekelezwe fungua kesi ya pili ya kuomba kutekeleza (kukazia) hukumu (execution of a decree)

Sio unashinda kesi unapewa hukumu unaenda kuitunza ndani itakua ni pambo tu,

wewe si ndo unataka kulipwa, sasa kama hufatilii, Mahakama haina chombo cha kuja kukulazimisha kufatilia kulipwa wakati wewe mwenyewe hutaki au haufatilii!

Kwani wakati unafungua kesi kuna chombo gani cha Mahakama kilikuja kukufata?
 
Back
Top Bottom