Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,283
- 2,043
Wadau nawasabahi. Naomba niingie kwenye madam moja kwa moja. Hoja yangu ni juu ya utekelezaji wa hukumu za mahakama. Kumekuwa na utaratibu wa kupuuza utekelezaji wa hukumu zilizotolewa na mahakama zetu kwa baadhi ya taasisi mashirika na halmashauri zetu.
Kitendo hicho kimekuwa kero kubwa kwa walioshinda kesi na kupata usumbufu mkubwa kudai utekelezaji wa hukumu zao mpaka inafikia hatua ya mhusika kukata tamaa licha ya ushindi aliopewa na mahakama.
Taasisi na halmashauri mbalimbali zimekuwa kwa makusudi kabisa hazitaki kutekeleza hukumu za mahakama.
Ushauri: mahakama zetu ziwe na kitengo maalum kitakachokuwa kinafuatilia hukumu zake kwa kupewa taarifa ya utekelezaji na mhusika au taasisi au halmashauri iliyotakiwa kutekeleza hukumu hizo.Kufanya hivyo kutazifanya hizo taasisi na halmashauri kutekeleza kwa wakati hukumu hizo kwa wakati na kuwaondolea wananchi kero na usumbufu waliokuwa wanaupata.
Ikumbukwe kuwa uamuzi wa mahakama ni wa mwisho kama kuna mtu taasisi au halmashauri inaupinga basi ifungue kesi mahakamani badala ya kuwasumbua wananchi kwa kutokutekeleza hukumu.
Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app