Swali gumu. . . . . . .!!

Ulichokisema ndicho nilichosema jana, hadi nikagive up; naona MH, ameona akutolee mfano wewe! LOL

Babu DC anaeleweka zaidi kuliko wewe. Labda hujui jinsi ya kujieleza vizuri ukaeleweka.

Na hakuna anayetaka ku-deflect blame. Kilichosemwa jana na kinachosemwa leo ni kwamba wote wanastahili lawama ingawa uzito na portion ya lawama vinatofautiana. Same thing with being an accessory to a crime.

It's not rocket science or complicated logarithm. Dark City gets it.
 
Utakuwa umenikosea illa kosa lako kwangu siyo kubwa kama la mke wangu ambaye alikula kiapo cha kuwa mwaminifu kwangu hadi kifo. Kosa lako ni la kimaadili ila kosa la mke wangu ni la kuvunja kiapo/nadhiri.. Hayo makosa hayana uzito sawa hata kidogo!

Halafu kwenye hili tatizo, huyo dada hana obligation yoyote ya kutunza uaminifu wa mume kwa mke wake. Ila ona obligation kama mwanajamii mwingine la kutomtendea vibaya mwenye mume!

Babu DC!!

Umeeleweka na sasa tuko ukurasa mmoja.
 
DC unajua nini, some of us (cheaters hasa wanaume) huwa hatutaki kukubali na kuchukua kosa lote, lazima tutafute wa kumgaia lawama!

Au tutankaumu, wife kwa kuwa mchoyo/mchovu etc,
Au tatamlaumu huyo other woman kuwa alinitega (aliniona mimi si rijali etc)

So kuchukua mzigo wote wa makosa inakuwa ngumu, ref Adam alivyooulizwa na Mungu; akasema ni huyo mwanamke uliyenipa ..... (kipipi, nimejaa mistari.LOL)

Wanasema ukikosa wa kumblame, blame hata weather!

Ulichokisema ndicho nilichosema jana, hadi nikagive up; naona MH, ameona akutolee mfano wewe! LOL

Kaunga,

Ni bahati nzuri sijasome hiyo thread ya jana, so natoa mawazo yangu nikiwa naive...Nikipata muda nitaitafuta.

Hata hivyo ni makosa kukwepa lawama na kuwajibika kwa makosa tunayokuwa tumeyatenda kwa kutafuta mahali pa kusukumia lawama.

Nikiamua kucheat mie kama Babu DC, basi ni uamuzi wangu. Kama wife ananikera basi inabidi nihangaike naye kutafuta suluhu. Hilo haliwezi kuwa excuse ya makosa yangu pale ninapoamua kwenda kungonoka nje!

Huyo dada wa nje hatakiwi kubebeshwa lawama za mimi kukosa uaminifu kwa mke wangu...Alaumiwe kwa kosa la uasherati tena na mume wa mtu...Hana wajibu wa kutunza viapo vya ndoa yetu!

Babu DC!!
 
Huyo dada wa nje hatakiwi kubebeshwa lawama za mimi kukosa uaminifu kwa mke wangu...Alaumiwe kwa kosa la uasherati tena na mume wa mtu...Hana wajibu wa kutunza viapo vya ndoa yetu!

Babu DC!!

Sasa kuna wengine watakuambia eti huyo dada hastahili kabisa lawama! SMH.

Ndiyo maana jana baada ya kusikia hivyo nikazungumzia maadili halafu nikaulizwa eti maadil yanakujaje. Sasa mtu kutembea kwa makusudi na mke ama mume wa mtu huyo mtu ana maadili yanayokubalika na jamii kweli?

Wewe mwenyewe babu umesema mtu huyo anastahili lawama kwa kufanya uasherati na mume wa mtu. Kwa hiyo hata wewe unaona hilo tendo si sawa. Au nimekosea kuelewa ulichoandika?
 
MH
Nakubaliana nawe uwezo wangu wakujieleza, hauwezi kumfikia DC!

Lakini, NEMO alifafanua vizuri sana (DC, angalia the first 2 pages za Uzi ule wa Boflo wanaume wote wanacheat); lakini ulimjibu and l quote "Nonsense".

Nilicho learn na samahani unaweza kuwa umbumbu wangu pia, Nemo ni She, l am She and DC is a He. Na kwa mtu ambaye anataka kumpa lawama mwanamke wa nje kwa kosa la kumcheat mkewe; ni kawaida tu kama theluji kipindi cha Xmas huko Marekani Kaskazini na Ulaya!
 
Mnyama Hatari,

Kwa msimamo wangu, vyote uzinzi na uasherati ni makosa na wanaotenda hayo mambo hawawezi kukwepa lawama. Tofauti ni levels na uzito wa lawama!!

Babu DC!!
 
MH
Nakubaliana nawe uwezo wangu wakujieleza, hauwezi kumfikia DC!

Lakini, NEMO alifafanua vizuri sana (DC, angalia the first 2 pages za Uzi ule wa Boflo wanaume wote wanacheat); lakini ulimjibu and l quote "Nonsense".

Nilicho learn na samahani unaweza kuwa umbumbu wangu pia, Nemo ni She, l am She and DC is a He. Na kwa mtu ambaye anataka kumpa lawama mwanamke wa nje kwa kosa la kumcheat mkewe; ni kawaida tu kama theluji kipindi cha Xmas huko Marekani Kaskazini na Ulaya!

Hahahahahahah,

Huwa naogopa sana mijadala ya JF inajaribu kugeuka personal...!!!

Anyway...mwenye kufanya makosa hana budi kublawama zake zote zinazomhusu. Huyo aliyemsaidia kutenda makosa naye ana lawama kwa makosa yake ila zinatofautiana sana. Hakuna anayebeba mzigo wa mwenzie...!!

Babu DC!!
 
Ndio maana ukaitwa Babu (full mabusara).
Usiku mwema DC na Mnyama Hatari!
 
Ni sawa na mtuhumiwa na akomplesi wake?

Hapa hata sijue nijibu vipi,

Ila kwa imani yangu, makosa ya kufanya vitendo vya ngono yanahusisha maamuzi ya ndani kabisa ya mtu. Habari za kusaidiwa au la sijui kama zina nafasi. Ila kwa sababu hilo kosa linahusisha watu 2 ndio maana anaingizwa mtu wa pili.

Huyo mtu wa 2 ana lawama zake za kukubali kufanya ngono kinyume na maadili ya jamii (kama ameyaridhia) au imani yake (kama ni muumini wa dini inayozuia uzinzi/uasherati). Hata hivyo, sidhani kama anakosa la kumshawishi au kumsaidia mtu wa kwanza (temporary partner) kufanya kosa la uzinzi au uasherati (unless proved beyond reasonable doubt)!!

Kwa watu wanaonfanya uzinzi na makahaba, hao makahaba wanakuwa sehemu ya makosa??

Babu DC!!
 
Adhabu za mtuhumiwa na akomplisi huwa ziko sawa?

Mie si mwanasheria ila sidhani kama hao watu wana makosa yanayolingana...

Na kama hayalingani basi hata hukumu zao zitalalia kwenye vifungu tofauti na adhabu zao haziwezi kuwa sawa...

Labda kama judge anayetoa hukumu ni kimeo kama yule wa Lema!!

Babu DC!!
 
Hapana haviko sawa..,

unaweza kucheat bila kuzini..., (kumpa mtu kitu ambacho kwa kawaida its meant only to be given to your partner, e.g. romance, kisses n.k. )...

Na unaweza Kuzini bila kucheat... (Kuzini mara nyingi inahusika na dini, kwamba huwezi kufanya tendo la ndoa na mtu yoyote bila kuwa kwenye ndoa)

Hivyo basi ni mambo mawili tofauti ambayo moja linaweza likatendeka bila lingine

mmmhhh kwanini mtu akizini anasema amecheat?
 
Ni sawa na mtuhumiwa na akomplesi wake?

Kuna makosa zaidi ya moja (cheating, kuzini, uasherati) na watuhumu pia ni zaidi ya mmoja (Mke aliye chitiwa na Mungu).

So akomplex wa kosa gani na alimsaidia nani?

Tuanzie hapo!
 
Kwa watu wanaonfanya uzinzi na makahaba, hao makahaba wanakuwa sehemu ya makosa??

Babu DC!!

Hapo kahaba anakuwa anajua marital status ya huyo anayemegana naye au anakuwa hajui?

Manake katika mjadala wa jana na by extension huu wale ni kwamba huyo mtu wa pili anakuwa analala na huyo mwanandoa huku "akijua" kuwa huyo mwanandoa yuko kwenye ndoa.

Sasa kahaba unayenunua mtaani naye anakuwa anajua marital status ya huyo mteja ama?
 
Kwa kosa la kuzini hakuna akomplesi hapo, kama ilivyo kwenye uasherati. Kila mtu ni mtuhumiwa mbele za Mungu!

Kwenye kuvunja ahadi hakuna akomplesi pia, mwenye kosa ni aliyevunja ahadi; ila yule mwingine hajatenda vyema kuumiza furaha ya ndoa ya mwenzie (na hiyo inategemea moral zake kama alivyosema RR)
 
Back
Top Bottom