Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mzee Mwanakijiji,
Acha kujikanyaga kanyaga mkuu wangu., Kuna nchi ambayo haikuwepo kabla?... Hata Tanganyika ilikuwepo kabla hatujapata Uhuru na Hata Ukerewe ipo zamani tukija pata uhuru wetu ndipo tunaanza kuhesabu Ukerewe kama nchi..Sikuelewi unazungumzia kitu gani kwani ubishi wote wa madai ya Vatican kuwa nchi yanaanzia siku ilipotambulika na kukubalika kama nchi..na ndicho tunachochambua hapa.
Pengine mpe mtu mwingine ayasome maandishi yangu hapo juu na akutafsirie upate kuelewa tofauti niloizungumzia ya kwamba Vatican sio nchi. Nchi ni Vatican City na links zao nimekuwekea, zisome na upate kuelewa nachozungumza. Hakuna mahala nimekubali ulosema wewe, na hakuna mahala nimeandika ya kwamba vitu hivi havihusiani! isipokuwa swala ni nani tumeingia naye mkataba..Kisha hakuna Mtanzania anayetumia neno Holy see katika mazungumzo ya ku address Vatican.
Vatican represent Holy see na hata huyo Rugambwa anawakilisha Holy see kama balozi wa Papa..Maadam unakubali kuna tofauti baina ya nchi na Taasisi, pamoja na kwamba ni zinaunda utawala mzima bado ni tofauti na ktk utofauti huo ndipo tunapogoingana nikisema ni uwakilishi wa Taasisi ndiyo tumeingia nayo mkataba...Sasa huu ubishi unakwenda wapi?..
Mkuu wangu, kama kuna mkataba baina ya CCM na mtu yeyote kitaifa mathlan jengo la Vijana. Mtu yeyote anaweza kusema ni serikali ya Tanzania imeingia mkataba wa huyo mdosi..Tunaweza tumia jina la utawala wa CCM kuzungumza mkataba wa nchi kutokana na wao watawala lakini ipo tofauti kubwa sana..
Nimekupata vizuri kabisa, kwa vile tumeshakubaliana kuwa Vatican City ni nchi halali na inayotambulika kimataifa na kuwa Mkuu wake ni Papa na kuwa Holy See ni hakimiya ya utawala wa Papa tunaweza kuelewa basi ni kwanini Tanzania ina uhusiano wa kibalozi na Vatican (papa) kwa sababu yeye ni absolute monarch wa nchi ya Vatican City. Na kwa vile tumekubaliana kuwa OIC siyo nchi moja bali ni jumuiya ya nchi mbalimbali basi ni wazi kuwa uhusiano nayo unawezekana kama vile tulivyo na uhusiano na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa au taasisi zake mbalimbali.
Nashukuru kwamba hatimaye tumeumaliza mjadala wa Vaticani ni nchi au si nchi na kama kuna uraia au hakuna. Mchango wako kwa kweli umesaidia sana kuwaelewesha wengine ambao wamekuwa wakiuliza kwanini Tanzania ina balozi Vatican na kwanini kuna mwakilishi wa Holy See Tanzania. Natumaini maswali haya hayatakuwa yanarudiwa rudiwa tena.
Sasa tumebakiwa na swali la kuuliza ni uhusiano gani uwepo kati ya Tanzania na OIC? Uhusiano ambao utaheshimu Katiba ya OIC na katiba yetu na kuhakikisha kuwa una manufaa kwa pande zote mbili?
Binafsi napendekeza Rais Kikwete amteue Balozi wetu awe mwakilishi wa Tanzania kwenye OIC - hilo pendekezo la kwanza.
Napendekeza vile vile kama hilo la Ubalozi (ambalo naamini ni bora zaidi) tujiunge na OIC kwa masharti ya kutosimamia baadhi ya malengo ambayo yanahusiana na dini ya Kiislamu ya OIC ili kuhakikisha kuwa tunakuwa neutral. Kwa vile hoja kubwa inayotolewa ya kwanini tujiunga ni kuwa kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi basi OIC na Tanzania zikae chini na kuandika makubaliano ya kujiunga ambayo yatatufanya tujiunge kwa misingi ya uchumi tu na si kingine. Unasemaje?